Wapendwa nimfanyaje huyu X husband

unaonekana unamdharau baba wa watoto wako,,mwache akukomeshe hata angekuwa ndugu yangu ningemwambia anyamaze kimya kama hayupo duniani
hanikomeshi mimi anamkomesha mwanae, taarifa alikuwa nazo sijamdharau wala kuacha kumshirikisha jambo ila ni yeye ndio anadharau,
 
hanikomeshi mimi anamkomesha mwanae, taarifa alikuwa nazo sijamdharau wala kuacha kumshirikisha jambo ila ni yeye ndio anadharau,

kama ulikuwa unampa heshima yake kama baba wa mtoto sidhani kama angefanya vile
umeshapata bwana mwingine mwenye vihela uchwara sasa unajaribu kumwonyesha madharau
mapenzi ya miafrica ndivyo hivyo!!!!!!!!!!!!!!!
 
Pole sana kwa matatizo dada yangu..
Nyote naona mmechangia kwenye hili tatizo.
kwanza ulitakuwa kumjulisha ex mumeo kuwa umejaza namba zake kwenye form za shule ya mtoto.kwa kufanya hivyo msingefikia hapo.
Pia hata kama mmeachana mlitakiwa kukaa chini na kujipanga namna ya kulea watoto...ina kwa kuendekeza ugomvi wenu mmemuumiza mtoto na kakosa fursa ya kwenda shule...nyie mna akili gani...nadhani utakuwa umemweleza mwanao ukweli ndio maana umesema amejua ana amekosa amani...sio yote twawaeleza watoto..
Fanyeni yote ila watoto wasiwe wahanga na 'utoto' wenu.
Tafakari chukua hatua...

sioni kama kulikua na sababu ya baba kuambiwa kua eti namba yake imetumika kwa mtoto wake mwenyewe. huyu baba naona uwezo wake mdogo na sidhani kama pesa ya school fees anayo, hivyo kwa kukwepa hili akaona akane mapema asije akaambiwa amlipie mtoto school fees. wako wengi wa aina hii siki hizi wanaosahau majukumu yao na kutumia ubabe usiokua na maana kama kinga. pole sana mpendwa lakini kutoa namba ya baba kwa swala la mtoto wenu hukufanya kosa na hakuna sababu ya kumwambia baba maana mtoto ni wake pia.
kama anadhani amekukomoa anakosea maana mwisho wa siku mwenye kuathirika na mtoto. Next time usimhusishe kwenye lolote linalohusiana na mtoto maana in a way amemkana. ningekua ni mimi, hata sir name ya mtoto ningempa ya baba yangu mzazi, stupid husband no wonder ndoa ilivunjika. hafai hata kwa kulumangia.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Asante sana mpendwa nitazingatia ushauri wako
 
kama ulikuwa unampa heshima yake kama baba wa mtoto sidhani kama angefanya vile
umeshapata bwana mwingine mwenye vihela uchwara sasa unajaribu kumwonyesha madharau
mapenzi ya miafrica ndivyo hivyo!!!!!!!!!!!!!!!

Wewe wasema, but nafikiri baba mtu angemjali mwanae na si mama mtu!!
 
kuachana sio sababu ya kumtesa mtoto ugomvi wetu sisi usingemwingiza mtoto ambaye hana hatia wala hakuomba azaliwe, huwezi ukasema kila kitu maana sindano inavyouma anajua uchungu wake yule aliyechomwa nayo
Wewe ndiye unamakosa mumy kwani umetoa personal contacts bila idhini ya muhusika pia hukumshirikisha muhusika. Pia we umemweleza mwanao ya nini sasa. Inaonyesha una-depression
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Wapendwa, Salaam poleni na majukumu, tatizo langu ni kwamba nimeachana na mume wangu takribani miaka sita sasa, mtoto wangu wa kawnza ndio alimaliza darasa la saba mwaka huu, katika kuhangaika kumtafutia shule ili ajiunge na kidato cha kwanza nilimchukulia fomu Marian Boys ya Bagamoyo.

Kwenye fomu niliandika jina la baba na namba ya simu kwa kutambua kwamba ni baba wa mtoto, alifanya mtihani na akafaulu, tatizo illilonisikitisha sana ni kitendo cha huyu baba mtu pindi alipopigiwa simu ili atambue hilo aliwajibu kwamba, huyo mtoto yupo kwa mama yake mimi hanihusu hiyo nafasi itoelewe kwa mtu mwingine.

Nilipata maelezo hayo baada ya kupiga simu shuleni ili nijue utaratibu unakuaje na kuambiwa nafasi yake ilishatolewa baada ya baba mtu kuwajibu vile. Je baba kama huyu nimfanyaje kwa hili, mtoto amejua na amekosa amani, naombeni ushauri wenu sijawahi kuumia kama nilivyoumia kwa hili.

Asanteni nakaribisha ushauri wenu
kama ni kufanya kitu basi jifanye wewe mwenyewe. haiwezekani wewe ukae upange mipango halafy utake mtu mwingine ambaye hamna uhusiano wa kihivyo aitekeleze bila kushauriwa. Si ajabu hata hauna habari huyo bwana anapataje mkate wake wa kila siku halafu bila kumshauri unamshushia bili kama hiyo. Hivi ingekwua wewe ndo umefanyiwa hivyo, ungejisikiaje... na yeye ni mtu kama wewe
 
hata kama hatuujui undani huyo jibaba hakupaswa kumuharibia mtoto kihivyo. Hebu imagine mmama kahangaika apate shule halafu mtu analeta habari za kizushi. Ugomvi wa wazazi usihamishiwe kwa watoto.

Unajua Husn hata mie namshangaa sana baba Erick! Hata kama ukweli hatuujui still huyo baba hakupaswa kuhamishia hasira zake kwa mtoto. Hata kama alikuwa hataki/anakwepa kulipa ada alichokifanya ni kibaya sana, bora hata angewapiga kalenda then baadae akamwambia mama mtu kuwa halipi na ajipange yeye kama mama amlipie mwanae kuliko kumpotezea mtoto chance ya kusoma! Yaani majukumu hataki alafu bado anataka kuharibu hadi kwa watoto? ........................
 
  • Thanks
Reactions: BAK
mijanaume mingine hovyo. Lea mwanao tupa kule. Janaume gani lisilojali maendeleo ya mwanae? Halifai na shukuru haupo nae
 
Wewe ndiye unamakosa mumy kwani umetoa personal contacts bila idhini ya muhusika pia hukumshirikisha muhusika. Pia we umemweleza mwanao ya nini sasa. Inaonyesha una-depression

Unfortunately, am pressed with time, ningekutolea uvivu nakwambia!
 
hata kama hatuujui undani huyo jibaba hakupaswa kumuharibia mtoto kihivyo. Hebu imagine mmama kahangaika apate shule halafu mtu analeta habari za kizushi. Ugomvi wa wazazi usihamishiwe kwa watoto.

Ahsante sana Husninyo. Nakuunga mkono kwenye hili.
 
Unajua Husn hata mie namshangaa sana baba Erick! Hata kama ukweli hatuujui still huyo baba hakupaswa kuhamishia hasira zake kwa mtoto. Hata kama alikuwa hataki/anakwepa kulipa ada alichokifanya ni kibaya sana, bora hata angewapiga kalenda then baadae akamwambia mama mtu kuwa halipi na ajipange yeye kama mama amlipie mwanae kuliko kumpotezea mtoto chance ya kusoma! Yaani majukumu hataki alafu bado anataka kuharibu hadi kwa watoto? ........................

isijekuwa baba eric ndio x husband mwenyewe.... Mmmmh!
 
MamaTuli Dada we acha maana nikisema niandike kila kitu watu watamaliza kusoma kesho, yaani ni mwanaume msumbufu, mtesaji mnyanyasaji sijawi kuonaona, huwa atoa hela kwa kusumbuana kwanza utadhani sio mwanae

ah,hii stor ya upande mmoja,nikipata maelezo ya upande wa pili,ntashauri kitu!
 
Back
Top Bottom