Wapendwa nimfanyaje huyu X husband

je ulimshirikisha toka mwanza kuhusu kutafuta shule na kwamba mwanao akipata nafasi wanaweza kuwasiliana nae??? je huwa mnakutana au kuwasiliana kuhusu maendeleo ya mtoto???

Thanks umemuuliza. Nilitaka kuuliza hilo pia. Kama waliachana miaka sita iliyopita ina maana mtoto atakuwa alikuwa darasa la pili or so. Je wakati mtoto akiwa shule ya msingi mama alikuwa anamshirikisha baba katika maendeleo ya mtoto kielimu? Au amesubiri mpaka mtoto anaenda sekondari ndio anataka sasa kumshirikisha baba mzazi?

Uhusiano wa mtoto na baba ukoje? Mtoto ana fikra kama za mama yake kuwa mawasiliano na baba sio mazuri, ni mtu wa shari huwezi kujadiliana na mtoto jambo lolote, ni baba msumbufu, mtesaji mnyanyasaji hajawi kuona?
 
Wapendwa, Salaam poleni na majukumu, tatizo langu ni kwamba nimeachana na mume wangu takribani miaka sita sasa, mtoto wangu wa kawnza ndio alimaliza darasa la saba mwaka huu, katika kuhangaika kumtafutia shule ili ajiunge na kidato cha kwanza nilimchukulia fomu Marian Boys ya Bagamoyo.

Kwenye fomu niliandika jina la baba na namba ya simu kwa kutambua kwamba ni baba wa mtoto, alifanya mtihani na akafaulu, tatizo illilonisikitisha sana ni kitendo cha huyu baba mtu pindi alipopigiwa simu ili atambue hilo aliwajibu kwamba, huyo mtoto yupo kwa mama yake mimi hanihusu hiyo nafasi itoelewe kwa mtu mwingine.

Nilipata maelezo hayo baada ya kupiga simu shuleni ili nijue utaratibu unakuaje na kuambiwa nafasi yake ilishatolewa baada ya baba mtu kuwajibu vile. Je baba kama huyu nimfanyaje kwa hili, mtoto amejua na amekosa amani, naombeni ushauri wenu sijawahi kuumia kama nilivyoumia kwa hili.

Asanteni nakaribisha ushauri wenu

We ndiye mwenye matatizo, tena nahisi una mapepo ... Umeniudhi sana sio siri.
 
hakuna kitu kizuri kama mipangilio na mahusiano (kuhusishwa) hata kama mtu hajiwezi kiuchumi ..
BMP baba amehusishwa na anajiweza kiuchumi sana, tatizo liko ananikomoa na kutafuta kuniumiza kupitia mtoto, ana uwezo mara 100 yangu
 
hata nikielezea chanzo utasema unataka kusikia kutoka upande wa pili naomba ushauri kwa hili kwanza lililojitokeza

Mkuu nafikiri ushauri wa hekima na busara unatokana na kusikilizwa kwa pande zote mbili. Bahati mbaya inakuwa vigumu kwa forum kama hii unless huyo ex wako ajitokeze. Kuna mwanaume mmoja alikuja hapa akaeleza matatizo yake dhidi ya mkewe watu wakamwonea huruma. Baadae mke nae akaja hapa kutoa maelezo ya upande wa pili mbona watu waliwithdraw ushauri wao wa mwanzo.

Kama walivyosema wengine the best thing you can do ni to do best for your child. Nenda kwenye shule yenyewe waulize kwa nini hawakukupigia simu wewe? Who knows inawezekana walipiga lakini hukupatikana ndio wakaamua kupiga kwa baba mzazi? Kama hawakupiga then walelezee exactly uhusiano wako na huyo ex na kwa nini amefanya kama alivyofanya.

Lakini kama shule ni ya kidini sana na uliweka contact details za ex wako ili kuleta impression that mnaishi kama familia moja ili mtoto apate nafasi inaweza ku backfire. Pia huwezi kujua ex alisema nini zaidi au aliambiwa nini alipopigiwa simu. Inawezekana kuna kitu aliambiwa na kwa hasira akafikia maamuzi aliyofikia. Siwezi kumhukumu. He is entitled to be heard as well.

Lakini cha msingi ni kumtafutia mtoto shule nyingine unless labda ulikuwa unategemea ex wako amlipie karo. Kama hakupata nafasi hapo shuleni, that is not the end of it. Kwani alifanya mtihani kwenye shule hiyo tuu? Au hakufaulu kwenye shule nyingine alizifanya mitihani?
 
We ndiye mwenye matatizo, tena nahisi una mapepo ... Umeniudhi sana sio siri.
unaelewa nilichokiongea au unaanza tu mashambulizi nimekuudhi na nini, una ona raha mtoto kukosa nafasi ya kusoma kwa ajili ya tu baba ana chuki dhidi ya mama?
 
umeongea ukweli kaka wewe gt
 
  • Thanks
Reactions: EMT
unaelewa nilichokiongea au unaanza tu mashambulizi nimekuudhi na nini, una ona raha mtoto kukosa nafasi ya kusoma kwa ajili ya tu baba ana chuki dhidi ya mama?

wewe mwanamke utakuwa una matatizo kwa sababu hujitambui na narudia tena inaelekea una stress ile mbaya za maisha kwa sababu kama ulishaachana nae unatoa namba zake za nini ? Ni sawa na ukutane na rafiki yako akuambia naomba namba zako za simu umpe za mmeo alafu umwambie lakini tumeachana Si wehu huo
 
  • Thanks
Reactions: EMT
BMP baba amehusishwa na anajiweza kiuchumi sana, tatizo liko ananikomoa na kutafuta kuniumiza kupitia mtoto, ana uwezo mara 100 yangu

wewe dada uwezo siyo tatizo linakuja je mwenzako ananini rohoni mwake? Na ni jambo gani linamsukuma kufanya hivyo?
 
  • Thanks
Reactions: EMT
wewe liweke wazi tatizo hasa ili uweze kupata ushauri zaidi..
  1. je ndoa ilikuwaje??
  2. mliishi kwa muda gani pamoja ???
  3. nini kilipelekea mtengani
  4. je alikuwa na upendo na mtoto wakati mnaishi pamoja??

BPM huyu tumpe mwaliko aje kwenye ofisi zetu bure
 
Vin D, Baba alikuwa anaelewa kila kitu, hata mtoto alipofaulu nilimweleza, ila nadhani yeye ndio anaamua kumwumiza mwanae kupitia mimi akijua ananikomoa mimi, suala la mtoto kujua alifatilia mwenyewe pale msimbazi na kuambiwa hivyo baada ya kuona mimi namchenga kumwambia ukweli, tatizo hapo sio utoto tunatofautiana uelewa
Kyelli .....pole sana but mh unanitisha kuachana miaka sita bado mmewekeana vinyongo?? Sio afya mnajua?

Tatizo nadhani kwa kuwa hamkukaa chini kama wazazi mkazungumzia suala ya watoto. Wewe hukutoa nafasi ya kujadiliana bali ulikuwa UNATOA TAARIFA tu kitu ambacho mwenzio anawezakuwa amekichukulia kama dharau (na hasa ukizingatia mna kinyongo). Ulitakiwa alipofaulu umweleze tu adhma yako ya kumsomesha mtoto shule flani na ungemwomba akupe mawazo yake yeye kama baba mtu. Wanaume wengine huwa wako hivyo hivyo

I had the same experience, wakati nataka kumwamzisha wa kwangu shule...nikajifanya kuja na hadithi za oh nimempatia shule ya karibu, ni nzuri, ya masista bla bla kibao. Nashukuru MUNGU kuwa hakunifanyia ulichofanyiwa wewe, ila tu nilishtukizwa keshatafuta shule yake (pampja na kuwa mwanzo alikuwa anasuasua) na mtoto anakujachukuliwa kwenda shule.

So sometimes wazazi tunatakiwa kujishusha, weka hacra, feelings, chuki, wivu pembeni, shughulikia issue ya mtoto/watoto. Ukifanikiwa na mkija kwenye yenu, tafuta joho lako lenye mahacra, chuki, jeuri, madharau you name it, vaa.
 
acha nitulie kwanza isije kuwa kama ile story ya theone na mke wake!

make waliumbuana humu watu wakakosa upande wakutetea!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mhh, ingawa x wako atakuja jutia ujinga wake, amefanya mbaya sana. Kuna mambo ma2 hapa: inaonekana ulimnyima haki ya kuwa karibu na mwanae kwa muda mrefu; hali hii imemfanya asione umuhimu wa yeye kuwajibika kwa 'kid' wake. Ktk hali hiyo akasema vile akidhani anakukomoa wewe, kumbe anajikomoa mwenyewe. Ushauri: jaribu kumjengea mwanao ukaribu na babake kama unamtakia mwanao amani na babake hata kama nyie mko kama paka na panya. Kila mtoto needs his/her father or mother kwa makuzi bora!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
BPM huyu tumpe mwaliko aje kwenye ofisi zetu bure

hapa hataki kuweka tatizo wazi maana ni heli tatizo likawekwa wazi watu wakakushauri ilivyo sahihi kuliko kuficha tatizo maana ushauri utakuwa kwa upande mmoja na hautakuwa msaada kwako zaidi ya kuzidi kukupotosha ..
usijisikie vibaya ila kama tatizo linaweza likawa kwako pia si mbaya kwani tutakupa mwongozo la msingi ni kukubali tatizo na kubadilika kwa ajili ya mtoto
 
  • Thanks
Reactions: EMT
BMP baba amehusishwa na anajiweza kiuchumi sana, tatizo liko ananikomoa na kutafuta kuniumiza kupitia mtoto, ana uwezo mara 100 yangu

kuna aina nyingi katika ushirikishwaji isije ukawa ulikuwa ni mtu wa kupeleka taarifa tu kwa mhusika (baba) na maamuzi ukawa nayo wewe na si maamuzi ya wote .. lakini bado dada yangu nalia na wewe hebu tuweke wazi hasa tatizo lenu la kutengana ni nini maana athari kama hizi ndo zinakuja kuangukia kwa watoto .. pls dada yangu nakuomba sana tueleze chanzo cha tatizo siamini mtu anaweza kuwa na roho ngumu bila sababu
 
  • Thanks
Reactions: EMT
wewe liweke wazi tatizo hasa ili uweze kupata ushauri zaidi..
  1. je ndoa ilikuwaje??
  2. mliishi kwa muda gani pamoja ???
  3. nini kilipelekea mtengani
  4. je alikuwa na upendo na mtoto wakati mnaishi pamoja??

mkuu mbona naona hizo information kwa sasa ni irrelevant. Huyo mzee hata kama huyo mtoto asingekuwa amemzaa yeye kiungwana sio vizuri kabisa alichokifanya.
 
mkuu mbona naona hizo information kwa sasa ni irrelevant. Huyo mzee hata kama huyo mtoto asingekuwa amemzaa yeye kiungwana sio vizuri kabisa alichokifanya.

husn bado zina umuhimu kwani tatizo limejitokea kwa sasa ndo tunaelezwa na bado mtoto ana safari ndefu kielimu naamini kuna mabadiliko yanahitajika ili mtoto atengenezewe njia katika safari yake kimasomo
 
  • Thanks
Reactions: EMT
wewe mwanamke utakuwa una matatizo kwa sababu hujitambui na narudia tena inaelekea una stress ile mbaya za maisha kwa sababu kama ulishaachana nae unatoa namba zake za nini ? Ni sawa na ukutane na rafiki yako akuambia naomba namba zako za simu umpe za mmeo alafu umwambie lakini tumeachana Si wehu huo

kwani watu wakiachana hawatakiwi kushirikiana kwenye maswala ya watoto?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
husn bado zina umuhimu kwani tatizo limejitokea kwa sasa ndo tunaelezwa na bado mtoto ana safari ndefu kielimu naamini kuna mabadiliko yanahitajika ili mtoto atengenezewe njia katika safari yake kimasomo

hebu niambie akikwambia ndoa ilidumu miaka 6 au 20 itasaidia nini katika kumfanya huyu mama aweze kumake decision?
 
usilolijua ni sawa na usiku wa giza, alishawahi kuwachukua watoto na kuwapeleka nisikokujua miaka miwili, nilipeleleza nikajua wanakosoma nikaenda ile shule HM akaniambia wale watoto hawana mama yule bwana alimweleza mama yao alishakufa, baadaye watoto walimsumbua alinifuata akanikabidhi watoto hapo ndipo longolongo za matunzo zilipoanzia jamani nina mengi siwezi kusimulia kila kitui
 
mamii mungu atakupigania utaishinda hii mitihani. Jitahidi kujibu maswali ya huyo baba erick na bmp ingawa mengine nayaona ni CRAP ila huwezi jua labda wanataka kukushauri jambo la maana.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom