Wapendwa nimfanyaje huyu X husband

sisi wa baba hovyo kabisa!mtoto akifanikiwa ktk maisha, utasikia ni mtoto wangu huyu
 
pole sana kwa matatizo yaliyokupata...

kwenye namba za simu uliandaka ya baba wa mtoto ina maana hukuweka na yako???

je mahusiano yako na ya mzazi mwenzako yakoje??

nini kiliwatenganisha?
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Baba wa mtoto hana kosa wewe ndo una makosa huwez tu kukurupuka kwenda kutoa details zake bila kumjulisha na kuona utayari wake. Mmmh mara nying akina mama mmeharibu maisha ya watoto kwa kuleta mambo yenu/maugomvi kwa watoto...
alikuwa na taarifa usihukumu jambo usilolijua, yeye ndio mtu wa visasi na nisingeweka detail zake pia ni yale yale
 
pole sana kwa matatizo yaliyokupata...

kwenye namba za simu uliandaka ya baba wa mtoto ina maana hukuweka na yako???

je mahusiano yako na ya mzazi mwenzako yakoje??
niliandika namba zangu mbili na ya ofisini moja, jumla namba tatu na ya baba mtu nashaaa mimi kutokupigiwa simu hata moja, mawsiliano sio mazuri,ni mtu wa shari huwezi kujadiliana nae jambo lolote, kiufupi ni haeleweki kabisa ni mtu wa shari mud wote
 
alikuwa na taarifa usihukumu jambo usilolijua, yeye ndio mtu wa visasi na nisingeweka detail zake pia ni yale yale

Siwez kuhukumu wewe wala huyo baba maana kama mliwasiliana je mlikubaliana nin? Maana unaweza kuwa unataka tumwone huyu jamaa ni katili asiye jali kumbe kuna mambo mengi mazito... Na baki pale pale lazima kushilikishana na kukubaliana maana nimeona maisha ya watoto weng yakiharibiwa kisa baba na mama wameachana, na mara nyingi akina mama ngao ni watoto. Mara anaumwa mara cijui nn?
 
Hahaha, mwisho wa article, baba aliyemzaa Steve Jobs na kumtelekeza bila aibu anasema "They produced the best" "Steve Jobs was a genius". Masikini mwanawe mwenyewe hata kumuona ukubwani hajawahi.

Kutelekeza mtoto kunamfanya binadamu kuwa hana tofauti na mnyama. Hata wanyama wengine hawafanyi hivyo.
 
Du!! hii kali, kuna wanaume wengine ni disgrace kwetu wanaume-sijui hawa tuwaite nani?! Nakosa hata jina linalomstahili
 
pole sana dada. Ila huyo baba anaupeo mdogo sana,manake alichofanya ni cha kijinga sana. Atakuja kujuta mbeleni dogo mambo yake yakimyookea,hawa ndio baadae wanakuja kupiga magoti kwa watoto wao,shame on him
 
Asanteni sana kwa ushauri wenu mmenitia moyo sana, nawashukuru wote, mungu awabariki sana, nawatakia jioni njema
 
Du!! hii kali, kuna wanaume wengine ni disgrace kwetu wanaume-sijui hawa tuwaite nani?! Nakosa hata jina linalomstahili

unajua watu hawajadadavua vizuri ndugu zangu mimi simlaumu huyo baba hata kidogo kwani mmejua ni nini kiliwafanya waachane? Acheni jamani mambo mengine tuna-commet tu ila undani hatuujui.
 
Pole sana, mtafutie mtoto shule nyingine na uliache hilo libaba liendelee na maisha yake.
 
nyie wanawake wa siku hizi mnajitahidi sana kuonyesha ubabe kwa baba za watoto wenu
kama unaishi na mtoto je mna makubaliano yoyote kuhusu mtoto??
je anapenda kuishi na mtoto na unamkatalia????
 
unajua watu hawajadadavua vizuri ndugu zangu mimi simlaumu huyo baba hata kidogo kwani mmejua ni nini kiliwafanya waachane? Acheni jamani mambo mengine tuna-commet tu ila undani hatuujui.

hata kama hatuujui undani huyo jibaba hakupaswa kumuharibia mtoto kihivyo. Hebu imagine mmama kahangaika apate shule halafu mtu analeta habari za kizushi. Ugomvi wa wazazi usihamishiwe kwa watoto.
 
kwani ulimpa taarifa kuwa unampeleka shule mwanae?
Kutokumpa taarifa ilikuwa DHARAU!.
 
kwani ulimpa taarifa kuwa unampeleka shule mwanae?
Kutokumpa taarifa ilikuwa DHARAU!.

Mkuu Fm haya matatizo hata sisi tunayo
hawa mama wa watoto zetu ni madharau kwa kwenda mbele,hasa akipata mtu mwenye vihela kidogo utapata tabu kweli kweli
 
Baba wa mtoto hana kosa wewe ndo una makosa huwez tu kukurupuka kwenda kutoa details zake bila kumjulisha na kuona utayari wake. Mmmh mara nying akina mama mmeharibu maisha ya watoto kwa kuleta mambo yenu/maugomvi kwa watoto...

Baba wa mtoto yeyote yule ambaye hata kama ndoa imevunjika atafurahia kuhusishwa na elimu ya mtoto wake hata kama hakupewa taarifa za awali. Wanaume wengine pale ndoa inapovunjika hutaka kuwaadhibu pia watoto waliopatikana ndani ya ndoa, kitu ambacho si sawa hata kidogo.
 
unajua watu hawajadadavua vizuri ndugu zangu mimi simlaumu huyo baba hata kidogo kwani mmejua ni nini kiliwafanya waachane? Acheni jamani mambo mengine tuna-commet tu ila undani hatuujui.
kuachana sio sababu ya kumtesa mtoto ugomvi wetu sisi usingemwingiza mtoto ambaye hana hatia wala hakuomba azaliwe, huwezi ukasema kila kitu maana sindano inavyouma anajua uchungu wake yule aliyechomwa nayo
 
  • Thanks
Reactions: BAK

unaonekana unamdharau baba wa watoto wako,,mwache akukomeshe hata angekuwa ndugu yangu ningemwambia anyamaze kimya kama hayupo duniani
 
Baba wa mtoto yeyote yule ambaye hata kama ndoa imevunjika atafurahia kuhusishwa na elimu ya mtoto wake hata kama hakupewa taarifa za awali. Wanaume wengine pale ndoa inapovunjika hutaka kuwaadhibu pia watoto waliopatikana ndani ya ndoa, kitu ambacho si sawa hata kidogo.

ndio ndio ndio.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom