cheusimangala
JF-Expert Member
- Feb 27, 2010
- 2,585
- 497
Hehehe ahsante CM
Uko sahihi kwa kiasi kikubwa. . .Na mawazo yako hayako mbali sana na yangu ila wanaume wanaochukia wanaune wenzao kwakua tu wanaume waliofanikiwa kwa hili au lile ni wachache sana. Ni rare sana kukuta mwanaume amekaa chini anamsema mwanaume mwenzie kama wanawake. Yani maneno kama "muone anavyoringa na huyo bwanake. . .angejua sio wake mwenyewe mbona angejibeba" sio maneno yaliyozoeleka kwenye makundi ya wanaume. Wao ni mwendo wa "demu wa fulani mkali kweli. . .Au hajatulia" ila hawahangaiki kumkashifu huyo fulani hata kama wanatamani wangekuwepo kwenye nafasi yake.
Yani hata hako kachuki kakiwepo hakaonyeshwi kwa matendo. Kama ni huduma itatolewa, maongezi yatakuwepo na vicheko juu. Sio mtu ghafla anavuta mdomo kuleeee. . .utadhani unachangia matatizo binafsi aliyonayo.
Kuhusu kuhisi "kuchukiwa" huko nako kupo kwa kiasi fulani. Ni kama wale wanaohisi kuonewa. . .hua siku zote wanaonewa, ila sio wengi wenye hulka hiyo.
ni kweli lugha zetu zimetofautiana lkn kitu ni kile kile.Labda ww uhang sana na wanaume lkn wanaume wenye wivu,roho ya kwa nini na majungu wamejaa tele.Kinachofanya sisi tuonekana haka katabia ni ketu ni sbb sisi wanawake tuko wengi kuliko wao hivyo ni rahisi hii tabia kuonekana kwa wingi kwetu zaidi yao na sbb nyingine ni kwamba sisi tumejaliwa maneno mengi hivyo mahali pakiwa na wivu tu hautajificha sbb ya maneno na vijembe vyetu na makelele mengi, mtu akiuliza nini tatizo hakuna sbb ya maana atakayopata zaidi ya huyu ana nyodo huyu ananionea wivu.
Narudia tena kusema tofauti yetu na wanaume ni ktk lugha tu wkt sisi tukioneana wivu tutasema "anaringa angejua huyo bwana ana mwanamke kila kona" wanaume wao wanasema"jamaa limbukeni kweli tokea apate shori mkali hata hatoi hi kwa washikaji maskani".Pia sisi kitu kidogo tunakivalia sana njuga kuliko wanaume ndo mana sisi tunaonekana sana kuliko wao ktk hili.
Pia nataka kuongezea kwenye kuhisi kuchukiwa.Unakuta mtu kafanikiwa,nyie wala hamumuonei wivu lkn kumbe yeye rohon mwake anahisi kawivu kanawamaliza,yeye mwenyewe sbb anadhani mnamuonea wivu anaanza vitu vya ajabu,mfano anaweza kuanza kutoa vijembe kama....kama ipo ipo tu,mwenye wivu ajinyonge...bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi..na pia anaweza yeye mwenyewe akawakatia mawasiliano.Nyie mnaopigwa vijembe mtaona yeye aliyefanikiwa anawafanyia nyodo,lazima mtajisikia vibaya na ni vigumu kumuombea mema na hata akiporomoka mtamcheka na kufurahia sbb nani anapenda kuona maendeleo ya mtu mwenye dharau na nyodo?
Mim naomba tu ujiulize,je ni kweli kwamba sisi wanawake tukiwa na maendeleo kushinda waume au boyfriend zetu lazima tu tutawadharau?
Kama utajibu hapana,sio wote ni baadhi ,basi jiulize kwa nini wanaume kwa kiasi kikubwa sana huwa hawafurahii mwanamke awe na kipato kikubwa kumshinda yeye kama sio wivu?
Kama ni wivu jiulize kauli hizi umezisikia kwa wingi kiasi gani.