Wanawake. . . .

CM siwezi kataa kwamba wanaume hamna wenye tabia hizo, wapo hata mimi nimewaona ila bado sio wengi ukilinganisha na wanawake.

Ya wanawake nimeona kwa wengine, ndugu jamaa na marafiki zangu wa karibu na mie mara moja nilijionea namna watu walivyo na vituko. Kama mambo mengine yote mazuri kwa mabaya, kila kundi lina watu wanaojishughulisha nao. Ila tofauti ya wingi ipo kutegemeana na jambo pia kundi la watu. Ndio maana vitu kama roho mbaya/wivu/umbea hua vinahusishwa na wanawake. . .Sio kama wanaume hamna wenye hayo, ila wanaoongoza ni wanawake na ndio maana hua tunahusishwa nayo hata kama sio wote tuko hivyo.

Your highness my newly crowned queen,hapo kwenye blue ni hisia zako ndio zinakutuma kufikiri hivyo,au sbb imezoeleka kusemwa hivyo au kuna research ulifanya ukaibuka na takwimu zinazoonesha kwamba wanawake ndio tumewazidi wanaume kwa hiyo tabia au kuna source yeyote inayoaminika iliyofanya research ikaibuka na hiyo fact au ni kitu gani unatumia kudhibitisha hilo?.Tafadhali naomba unieleweshe kwa mifano na takwimu zinazoeleweka kutoka ktk vyanzo vinavyoaminika.
 
Nimeona kwa walionizunguka, nimesikia kwa walionizunguka na nimesikia na kuona hata kwa wale ambao hawajanizunguka bali nagongana nao.
 
Tabia ya wanawake kuchukiana ni sijui tuseme ni nini,mfano mdogo tu hata hapa jf
kwenye segment ya 'love connect' we angalia mwanamke anapokuwa anatafuta partner na pengine ana umri mkubwa labda 30+,wengi watakao mvunja moyo ni wanawake
utaona mara,siku zote ulikuwa wapi,mara kwa umri huo labda aliyefiwa na mke wake,mara kwa umri huo huna hata mchumba si bure.

Badala wao ndio wangekuwa wa kwanza kumuelekeza na kumuinua.

Sijui kama wanawake tutaja badilika.
 
Soraya....
 
Lizzy
Hakukujibu kwa sababu alichukia wewe kumgonga! Yule mkaka hakimgonga si ndio? Wa kwanza alikuomba msamaha coz aliassume yeye ndio kakigonga. Hayo ni maoni yangu tu!

About wanawake kuchukiana.
Yes n No.
Ukiwa na nyodo sana, na kuonesha dharau kwa wengine kuna watu women included watakuchukia tu!

Wanawake huonesha hisia zao kwa nje kuliko wanaume!

Wanawake wanahitaji friendship toka kwako na si zaidi, wanaume hutamani kile kilochofichwa na nguo zako, so wanaweza au kukuvumilia au kukuvisha sifa fake na ukaona wanakupenda kuliko wanawake!

Wanaume wanaweza share mwanamke na kuendelea kuwa buddies (coz it was just a fling, love was not in the picture), but wanawake ni wachache (labda sex workers tu); pamoja na hayo, mwanaume ampendaye mkewe au GF wake akimkuta na mtu mwingine, kumuua huyo mwizi si jambo la ajabu (nao hawapendani???)

Mwisho mimi namchukia mtu kwa tabia zake na si kwa nini alichonacho btn miguu yake! Na zaidi yule nimpendae akiniudhi namhate zaidi, asiyenihusu namuignore tu; sipotezi nguvu zangu kumhate!
 
Yani mm sijui nisemeje wanawake hatupendani kabisa, mm imeshanitokea nilienda crdb bank
nikamuomba dada mmoja ambae anafanya kazi pale anipatie deposit slip zilikuwa zimeisha jamani alinijibu vibaya
kwa kweli nilijisikia vibaya sana nikasema hii ni slip tu naomba, ingekuwa ni kitu cha kunielekeza kweli angenielekeza? hatupendani hata kidogo niwa chache sana ambao kweli hatupo hivyo.

Ukifanyia na mtu mmoja kidogo, unaconclude? Je utasemaje ukisikia mdada mwingine akirefer kitu ulichofanya na akaconclude kuwa wanawake hampendani?
Kila mtu analalamika kafanyiwa ubaya, mfanya ubaya ni nani?
 
Tabia ya wanawake kuchukiana ni sijui tuseme ni nini,mfano mdogo tu hata hapa jf
kwenye segment ya 'love connect'
we angalia mwanamke anapokuwa anatafuta partner na pengine ana umri mkubwa labda 30+,wengi watakao mvunja moyo ni wanawake
utaona mara,siku zote ulikuwa wapi,mara kwa umri huo labda aliyefiwa na mke wake,mara kwa umri huo huna hata mchumba si bure.

Badala wao ndio wangekuwa wa kwanza kumuelekeza na kumuinua.

Sijui kama wanawake tutaja badilika.

soraya my dear unataka kunambia hujawahi kuona jinsi wanaume wanavyowashambulia wenzao humu wanaokuja kutafuta wachumba?lol
Kwa uzoefu wangu mim,mtu akija kutafuta mchumba watu humchukulia kimasihara na wanawake kwa wanaume humuuliza maswali ya kejeli.
Naombeni mnisamehe kwa kutokubaliana na msemo wenu wa kuwa wanawake hatupendani sbb mim mwenzenu nimesaidiwa sana na wanawake wenzangu.
Nadhani mtu unachukiwa sbb ya jinsi ulivyo kwa wenzako,kama una nyodo,show off nyingi,dharau,ukipata kitu kidogo tu kazi kuwaambia wenzio mtajibeba lazima utaishia kuamini kuwa wanawake hatupendani hadi siku ya kuingia kaburini.
Tujichunguze sisi wenyewe kwanza,kwanini hatupendwi na wenzetu,ukishajua kasoro yako na ukajirekebisha na tukajifunza kuishi vizuri na wanawake wenzetu,na kujifunza kupuuza mapungufu madogo madogo ya wenzetu tukiamini kwamba hata sisi hatujakamilika na kuacha imani kuwa hatupendani lazima tutagundua kuwa kuna wanawake wenye wivu mbaya kama ilivyo kwa wanaume na kuna wanawake wenye roho ya kupenda kuona na kusaidia wenzao wasonge mbele.

Inaaminika wanaume ndio wanaochukiana zaidi wao kwa wao kuliko wanawake kwa wanawake sbb idadi ya mauaji ya mwanaume kwa mwanaume ni makubwa zaidi ya idadi ya mauaji kati ya wanawake kwa wanawake.

Pia inaaminika kwamba wanaume wanachukiana zaidi wao kwa wao zaidi ya mwanamke kwa mwanamke sbb wanaume wana sifa kama za wanyama za kuamini kwamba wanaume wengine wanaweza kuingilia territory zao wakati wowote,hivyo wanaogopana na kuchukiana.
 
nina wasiwasi women celebrations kama hii inaweza leta yae yaliyokusudiwa kwa kulaumiana na kuzodoana.

Kwa mawazo yangu nahisi kama tumedandia treni kwa mbele ndio kwa mfano, kupewa vyeo, kupewa siku ya kusherehekea etc kwa vile hili jambo tumelidaka toka kwa waliolianzisha na kulitekeleza lilivyo bila kuliasili kwanza. Kwa mfano tungestudy tamaduni zetu, dini zetu, makabila yetu, etc ili kuweza kupata hitimisho na pendekezo la pamoja on way forward na issues za wanawake hapa Tanzania ili tuweze kuwa na kauli moja, mtizamo na imani moja na wanawake wenzetu duniani.
 
Back
Top Bottom