St. Paka Mweusi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 7,639
- 4,527
Heshima kwenu wakuu,kwangu mimi sioni kama tatizo liko kwa wanawake,maana tukumbuke kuwa dunia inabadilika na wanaume (baadhi)hawakubali kwenda na mabadiliko ya dunia.Zamani ilikuwa shughuli zote za ndani ni kazi ya mwanamke na mwanaume yeye anakuwa mtafutaji,lakini leo hii sote tunashirikiana katika utafutaji bila kujali kama ni msomi au la.Hivyo basi linapokuja suala la majukumu ya ndani si vibaya tukasaidiana maana nashindwa kuelewa inakuwaje mwanaume unarudi umechoka na mwanamke anarudi amechoka lakini mkifika nyumbani mwanamke ndio aanze kuingia jikoni sijui wapi wakati mwanaume kanyoosha miguu na gazeti mezani,mbona ulivyokuwa bachelor ulifanya yote?Kwangu mimi mke nitakayemuoa sitamchukua ili sijui anipikie,anifulie,anisafishie nyumba na mengineyo mengi kwa kuwa nayaweza yote hayo.Nitaoa ili mke wangu anisaidie kazi moja tu ambayo mimi siiwezi na wote mnaijua ni kazi gani, hayo mengine tutashirikiana.