Wanawake wengi wasomi au wenye kipato kizuri hawadumu kwenye mahusiano!

Heshima kwenu wakuu,kwangu mimi sioni kama tatizo liko kwa wanawake,maana tukumbuke kuwa dunia inabadilika na wanaume (baadhi)hawakubali kwenda na mabadiliko ya dunia.Zamani ilikuwa shughuli zote za ndani ni kazi ya mwanamke na mwanaume yeye anakuwa mtafutaji,lakini leo hii sote tunashirikiana katika utafutaji bila kujali kama ni msomi au la.Hivyo basi linapokuja suala la majukumu ya ndani si vibaya tukasaidiana maana nashindwa kuelewa inakuwaje mwanaume unarudi umechoka na mwanamke anarudi amechoka lakini mkifika nyumbani mwanamke ndio aanze kuingia jikoni sijui wapi wakati mwanaume kanyoosha miguu na gazeti mezani,mbona ulivyokuwa bachelor ulifanya yote?Kwangu mimi mke nitakayemuoa sitamchukua ili sijui anipikie,anifulie,anisafishie nyumba na mengineyo mengi kwa kuwa nayaweza yote hayo.Nitaoa ili mke wangu anisaidie kazi moja tu ambayo mimi siiwezi na wote mnaijua ni kazi gani, hayo mengine tutashirikiana.
 
Hivi kwanini wanawake wengi hasa wa kitanzania waliosoma ni wasumbufu katika ndoa. Wakisha olewa nao wanakuwa kama wanaume!!! Tabutupu hii!!!!

we ndo mbovu! Si uende kijijini kwenu sitimbi ukaoe ambaye hajahudhulia hata darasa moja? Kwani hulilazimishwa kumwoa. Tuondolee ukuda hapa kama umemchoka nae kakuchoka pia mwache atapata mwingine wa kumpenda. Kila siku mkiamka ni post kuhusu wanawake tuu! Fikiria kujenga taifa si upupu usio na maana
 
Hii ni tabia ya mtu hata kama asome, asisome kama aliumbwa na Kiburi atakua nacho tu.....

Ebwana hii ni kweli kabisa mtu wangu, nishaona jamaa ana mke ambaye kwao masikini, elimu hana lakini hizo nyodo uspime, ukimkuta anavompandia mumewe huweze amini
 
Heshima kwenu wakuu,kwangu mimi sioni kama tatizo liko kwa wanawake,maana tukumbuke kuwa dunia inabadilika na wanaume (baadhi)hawakubali kwenda na mabadiliko ya dunia.Zamani ilikuwa shughuli zote za ndani ni kazi ya mwanamke na mwanaume yeye anakuwa mtafutaji,lakini leo hii sote tunashirikiana katika utafutaji bila kujali kama ni msomi au la.Hivyo basi linapokuja suala la majukumu ya ndani si vibaya tukasaidiana maana nashindwa kuelewa inakuwaje mwanaume unarudi umechoka na mwanamke anarudi amechoka lakini mkifika nyumbani mwanamke ndio aanze kuingia jikoni sijui wapi wakati mwanaume kanyoosha miguu na gazeti mezani,mbona ulivyokuwa bachelor ulifanya yote?Kwangu mimi mke nitakayemuoa sitamchukua ili sijui anipikie,anifulie,anisafishie nyumba na mengineyo mengi kwa kuwa nayaweza yote hayo.Nitaoa ili mke wangu anisaidie kazi moja tu ambayo mimi siiwezi na wote mnaijua ni kazi gani, hayo mengine tutashirikiana.

Kama hayo yote yametoka moyoni basi Babu DC anakutabilia kuwa utakuwa mume mwema. Kwa wale wanaotafuta..you are true husband material!

Wengine hayo yote tunayafanya practically na ndio maana tunawashangaa baadhi ya wanaume wanaofikiria kama vile ni mwaka 1960 wakati tunaelekea mwaka 2011!

Mungu atakuwa na nawe na familia yako itakuwa na baraka tele...!!!!!
 
Nakubaliana na wewe, nafahamu wanawake wasomi wengi tu na wengine wana vyeo vikubwa, lakini wanafahamu sana responsibilities zao as wives. Kikubwa ni kwamba ndoa ni pande mbili, inahitaji uelewa wa pande mbili na kulingana kwa maadili na utamaduni wa pande mbili za ndoa.

kama wewe ni mchaga unaoa mswahili basi ujue wazi kuwa dunia itakuwa chugu kwako. Kama wewe ni mtu wa Ungija unaolewa na Mkurya au mjita, basi ujue kuwa ndoa itakuwa mgogoro.

Kuna wanaume wanaona kuwa mwanamke ni a possesion na sio binadamu, na kuna wanawake wengine wanaona kama mwanaume ni money spitting machine, wengine wanaona easytu ku-rent miili yao na kuwaita wanaume mbuzi (buzi), hii ni utamaduni. Watu kama hawa hata wasome vipi ni tatizo elimu kwao ni wastage of time. Cha muhimu ni kwamba kama wewe ni mstaarabu na unaheshimu utu wako na wa mtu mwingine ni kuepuka watu kama hawa, jaribu kuangalia mnayendana.

So i would say that it is not entirely true that educated women are problematic and can not make good wives. Those women who are hard headed like mules, are born that way, and they will behave the same way regardless of whether they are educated or not

Huu ni ukabila tu, ukaburu mtupu hakuna jingine! Kwa mawazo yako mkurya au mjita na hao wengine uliotaja hawawezi kuwa kwenye ndoa na watu wa kabila tofauti, umechemsha bro, uongo mtupu huu na tena ni uzandiki uliojaa ubaguzi wa kikabila. Una maana kila mtu akaoe kabila yao tu ndio atapata ndoa nzuri? Watu kama nyie ndio hamtakiwi katika nchi hii, kutwa kuwaza ukabila tuuuu, yaani this is so primitive!
 
we ndo mbovu! Si uende kijijini kwenu sitimbi ukaoe ambaye hajahudhulia hata darasa moja? Kwani hulilazimishwa kumwoa. Tuondolee ukuda hapa kama umemchoka nae kakuchoka pia mwache atapata mwingine wa kumpenda. Kila siku mkiamka ni post kuhusu wanawake tuu! Fikiria kujenga taifa si upupu usio na maana

Kuberwa...hebu nenda mdogo mdogo..hata kama watu wengine wanakera vipi, jitahidi na kuwavutia pumzi. Wanahitaji msaada kuliko wanavyodhani na labda kuamini!
 
Huu ni ukabila tu, ukaburu mtupu hakuna jingine! Kwa mawazo yako mkurya au mjita na hao wengine uliotaja hawawezi kuwa kwenye ndoa na watu wa kabila tofauti, umechemsha bro, uongo mtupu huu na tena ni uzandiki uliojaa ubaguzi wa kikabila. Una maana kila mtu akaoe kabila yao tu ndio atapata ndoa nzuri? Watu kama nyie ndio hamtakiwi katika nchi hii, kutwa kuwaza ukabila tuuuu, yaani this is so primitive!

Mkuu, mpotezee jamaa. Inaonekana kapotea long time. Tribal barriers zilishavunjwa siku nyingi sana. Kama hana taarifa aendelee kusubiri kidogo tu atasoma namba!
 
Kama hayo yote yametoka moyoni basi Babu DC anakutabilia kuwa utakuwa mume mwema. Kwa wale wanaotafuta..you are true husband material!

Wengine hayo yote tunayafanya practically na ndio maana tunawashangaa baadhi ya wanaume wanaofikiria kama vile ni mwaka 1960 wakati tunaelekea mwaka 2011!

Mungu atakuwa na nawe na familia yako itakuwa na baraka tele...!!!!!

Nashukuru babu kwa utabiri mwema na ninakuhakikishia tena babu kuwa hayo yote uliyoyasoma ndio ukweli wa moyo wangu.
 
Kila la heri PM, hakuna kitu kinachoshinda determination.

I prayed to be married to my best friend, the best of the best and God answered my prayers. Why not you?

Acahana na wanaume wnaang'ang'ani mambo ya past. Usipotee wala kupotezwa na kitu chochote na amini usiamini ndoto zako zitatimia walau over 90% kama siyo 110%

DC
 
Heshima kwenu wakuu,kwangu mimi sioni kama tatizo liko kwa wanawake,maana tukumbuke kuwa dunia inabadilika na wanaume (baadhi)hawakubali kwenda na mabadiliko ya dunia.Zamani ilikuwa shughuli zote za ndani ni kazi ya mwanamke na mwanaume yeye anakuwa mtafutaji,lakini leo hii sote tunashirikiana katika utafutaji bila kujali kama ni msomi au la.Hivyo basi linapokuja suala la majukumu ya ndani si vibaya tukasaidiana maana nashindwa kuelewa inakuwaje mwanaume unarudi umechoka na mwanamke anarudi amechoka lakini mkifika nyumbani mwanamke ndio aanze kuingia jikoni sijui wapi wakati mwanaume kanyoosha miguu na gazeti mezani,mbona ulivyokuwa bachelor ulifanya yote?Kwangu mimi mke nitakayemuoa sitamchukua ili sijui anipikie,anifulie,anisafishie nyumba na mengineyo mengi kwa kuwa nayaweza yote hayo.Nitaoa ili mke wangu anisaidie kazi moja tu ambayo mimi siiwezi na wote mnaijua ni kazi gani, hayo mengine tutashirikiana.

salute you paka! Midume jifunze toka hapa... Haya yote ni matunda ya wanaume kuacha majukumu yao
 
Women have been empowered these days. Our men ego should shift otherwise we would think the women we have are no wives material. The problem could not be women... the problem might be how men think about women. Just note that gone are days when women were just for cooking and raising kids.
Now days they can as well finance our household budgets.

Your very wrong and idiot. Do you think ur married to fince the family? It seem u do no the meaning of marriage
 
Mkuu,

Katika issue kama hizi hakuna haja ya kutukanana. Tunatakiwa kukubali kwamba kazi ya kubadilisha mitizamo ambayo mtu kaijenga kwa miongo mingi na kwa msaada wa jamii yake si ndogo hata kidogo. Tupeane muda na kuvumiliana ila tulipofika sasa hakuna kurudi nyuma. Wanawake hawaonekana tena kama mitambo ya kutotoa watoto na kufurahisha wanaume. Watazidi ku-prove kuwa ni wabia muhimu sana wa maisha bora, yenye furaha, raha na amani! Anayezidi kupingana na haya asubiri kiama kimfike!

DC
 
Huwa ni inferiority complex kama mzee hujapiga kitabu!! Kama na wewe umepiga kitabu, una kazi nzuri hakuwezi kuwa na shida.
Problem ni pale mama atakapo anza kulipa fadhila ya kupewa uwaziri, ukurugenzi kwa kutoa uroda kwa waheshimiwa, hapo shida ita anza. Na kama ukifanya utafiti wako utagundua wengi wenye kiburi huko nyumbani ujue wazee wamesha anza kumega.

Na hiyo pia ni inferiority complex, kwani lazima kwa mwanamke kupata uwaziri atoe uroda? Na wanaume wanaopewa uwaziri wanatoa nini kama shukurani?

Mungu ameumba akili sawa kwa wanawake na wanaume, tatizo lilikuwa wanaume wanajiona wao ndiyo wenye mamlaka ya kuamua kila kitu na opportunities zote walijipa wao. Leo mambo yamebadilika wanaanza kusema ooooooh wanawake wasomi wako hivi na vile....

Kama unaona shida nenda ukaoe kijijini wako wa kila aina hata wale ambao hawajaenda shule hata siku moja kajichukulie tu uje umwamrishe unavyopenda.
 
C'mon guys....kwanini hatupendi kutumia lugha yetu ya taifa ili tuelewane?

Nilimjibu mtu aliye post kwa lugha ya kigeni, yawezekana hajui kiswahili.
Hakuna usawa kati ya m and f , hata dini zote zinaeleza hivyo. Hii dhambi ya kujifanya tupo sawa inatumaliza. Ndoa hazidumu hata mwaka mmoja. Watoto wengi kwa sasa wanalelewa na single parent. Na ndio maana watoto wengi ni majuha siku hizi.
Lazima kuwe na kiongozi katika familia.
 
Kweli mkuu dini zote zina mambo ambayo mengine kwa mtazamo wetu ni kandamizi kwa wanawake. Hata kama wewe unaona ni sawa, je kipi ni bora kwako..ndoa kuvunjika kila mtu akaishi kwa amani na kuanza upya au kuishi katika utumwa maisha yako yote?
 
we ndo mbovu! Si uende kijijini kwenu sitimbi ukaoe ambaye hajahudhulia hata darasa moja? Kwani hulilazimishwa kumwoa. Tuondolee ukuda hapa kama umemchoka nae kakuchoka pia mwache atapata mwingine wa kumpenda. Kila siku mkiamka ni post kuhusu wanawake tuu! Fikiria kujenga taifa si upupu usio na maana

It seems wewe ni mmoja wao hata kauli zako zinadhihirisha hayo. Utani tu ila sijapenda kauli zako
 
Kweli mkuu dini zote zina mambo ambayo mengine kwa mtazamo wetu ni kandamizi kwa wanawake. Hata kama wewe unaona ni sawa, je kipi ni bora kwako..ndoa kuvunjika kila mtu akaishi kwa amani na kuanza upya au kuishi katika utumwa maisha yako yote?

kwa nini ndoa iwe utumwa? Ni kwa sababu ya huu usawa. Kama wazazi wako wangeachana kama unavyoshauri wewe sidhani kama tungekuona hapa jf. Ungekuwa juha fulani huko.
Kila mtu atimize wajibu wake katika ndoa. Watoto wana haki ya kunyonya maziwa ya mama, sio ya ngombe. Wao sio ndama
 
Ni kweli ndoa nyingi zina matatizo sana, na mara nyingi sana wanawake ndio chanzo mara anasema ohh mi nafanya kazi kama wewe sasa usiniambie habari ya chakula,maji wala nguo zako haki sawa, lakini kibaka akija ukimwambia hebu toka nje uangalie mbwa wanabweka sana, si haki sawa?!! hataki na anakuambia mwanaume gani!!

Wengine wanatukana waume zao kwamba mimi nina masters wewe na ka degree kako huna maana hayo yapo ni suala lao kujirekebeisha ama la hawatadumu kwenye ndoa.watabaki wanapiga majungu ohh mwanaume malaya ooh hanipendi..nani apende mwanamke anaemtukana?!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom