Waliotandikwa viboko Ikulu hawa hapa

Sasa kulikuwa na tofauti gani kati ya Nyerere na Karl Peter? Ndio maana watanzania wana mawazo finyu sana.
 
Hapana bana, binafsi nimeenda JKT 1990's utawala wa Mkapa. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!
Ulikuwa KJ gani, CO wako alikuwa nani na Ulikuwa Operesheni gani?

JKT ilikufa 1993. Huu ulikuwa utawala wa nani?
 
Nasikiaga hiyo JKT inaongezaga uzalendo eti. Hili huwa lina ukweli wajameni???
Mbona Lowassa alipita JKT na bado Mwizi mkubwa, Mbona JK nae nasikia alikua Kanali , bado hana uzalendo wowote, Kama Tunataka kusonga mbele kama Taifa imara lazima tujifunze kusimamia sheria bila kuoneana aibu.

Zakumi,
Nilikuwa huko mwezi uliopita. Kinachonipa hofu ni huu mfumuko wa maghorofa il hali sewage system yetu ikiwa taabani. Pitia pale Mikocheni karibu na ma apartments yanayomilikiwa na Mwinyi junior kuna harufu mbaya sana ya sewage. That's all.

Dr. Hussein Mwinyi anamiliki apartments ambazo ni adjacent na nyumba yetu ya Msasani. Hakuna harufu yoyote. Au maana Mwinyi jr. yupi?
 
-Kassim Hanga
-Sheikh Othman Sharif
-Dk. Kleruu

-Many of the villagization process victims where the bulk of this accusation is stemming from.Nyerere may not have killed a significant number of people directly, but his policies and mediocrity resulted in the deaths of so many, probably in the million range if not hundred of thousands. We may never know for sure the exact figure due to the nature of the secrecy of the era.

See Pratt, Cranford (1999). "Julius Nyerere: Reflections on the Legacy of his Socialism". Canadian Journal of African Studies 33 (1): 137 – 52. doi:10.2307/486390

Jasusi amekuomba utaje watano hao uliowataja ni watatu, Dr. Kleruu aliuliwa na Mwamwindi kwa mantiki hiyo umebakiwa na wawili; kama Nyerere angekuwa muuaji kama unavyodai ni wazi isingekupa tabu kuwataja aliowauwa hii inadhihirisha wazi hizi ni porojo za kuchafua jina la Mwalimu, nakukumbusha tu hazitafanikiwa laiti kama Mwalimu angekuwa muuaji umati ule uliojitokeza kumzika usingejitokeza. R.I.P Mwalimu!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
SITTA ni mnafiki sana naomba kuwasilisha kwamba huyu jamaa alipigwa viboko Ikulu na Nyerere kwa fitna zake ndio maana alikuwa kwenye political wilderness for a long time. If it was not for BWM kumuweka TIC he would have been a has been long time ago. Asilete za kuleta KAMA ANABISHA ALETE HOJA DATA TUNAZO! Habari hiyo naiwakilisha JF mtafakari!!! Opportunistic people hawatakiwi TZ

Fitina zipi? Hawa walikuwa wanalalamikia utendaji wa Serikali,na ile incident ikasababisha Mwalimu Nyerere ajipunguzie mshahara, kuonyesha dedication yake kwa wananchi. Na huyu Sitta nimesema alikuwa particularly stubborn. Lakini I must correct that.

Huyu alikuwa the most stubborn. Nilipata habari za uhakika[from the horses' mouth], kwamba,'' hata walipokuwa re-enstated wale wanafunzi Sitta ndiye alikuwa wa mwisho kurudishwa, kwa sababu, kwa sababu nadhani Mwalimu Nyerere alikuwa amekasirika sana''
 
Masatu punguza ushabiki kwa Mkapa ndugu yangu. Mkapa kaingia madarakani December 1995, wakati huo JKT kwa mujibu wa sheria hawakuwa wanaenda tena.

Nadhani intake ya mwisho iliyotumikia mwaka mzima ilikuwa ni 1992, baada ya hapo wakabadilisha mfumo wakasema sasa itakuwa miezi 6 badala ya mwaka mzima. Zilienda intake 2 au 3 za miezi sita sita na baada ya hapo hakuna intake yoyote iliyoenda.

Mwaka 1994 kulikuwa na tetesi kwamba mfumo wa mwaka mzima, lakini haikuwa hivyo na badala yake hawakwenda kabisa. Waliomaliza vyuo vya ngazi ya cheti na waliomaliza Form 6 baada ya mwaka 1994 hakuna aliyekwenda JKT kwa mujibu wa sheria.

Kwa hiyo utawala wa Mkapa (Dec 1995 - Dec 2005) hakukuwa na intake hata moja ya JKT. Labda kama unaongelea JKT ya kujitolea, lakini siyo ya mujibu wa sheria.

Kama ulienda JKT enzi za utawala wa Mkapa ilikuwa ni mwaka gani (specific year) siyo useme in 1990s, which is a general statement ili kutudanganya. Hata Mwinyi alikuwa madarakani mpaka 1990s, wewe unaongelea 1990s ya lini?

Wewe huwa unapenda watu waje facts, ninaomba niku-challenge uje na facts, sema ni mwaka gani ulienda, ulikuwa operation gani na ulikuwa kambi gani?

nA KWAKUKAZIA NI KWAMBA MWAKA 1994 mwezi June Nikiwa na Form yangu ya kujiunga JKT kambi ya Chitah Kule Ifakara , waziri wa Elimu , kama nakumbuka Charles Kabeho baada ya kupokea maagizo ya Ikulu ya Mwinyi akatutamgazia Umma kuwa JKT haitakuwepo katika mwaka huo kwahiyo Form six tuliokua tunajiandaa kwenda tukazuiwa, ILIKUA FURAHA SANA, KWAKUA UJINGA ULE SIKUUTAKA KABISA.
 
Hapana bana, binafsi nimeenda JKT 1990's utawala wa Mkapa. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!

Rejea vizuri historia yako. Mwinyi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1985 - 1995. Mkapa akawa rais kwa kipindi cha 1995-2005 na Kikwete alianza 2005 - nk.

Kwa suala la kifo cha JKT ni kuwa kilikufa June 1994 (kipindi ambacho rais akiwa Mwinyi). Kabla ya kifo chake kilitangulia vipindi viwili vya miezi sita sita (hapo kabla JKT ilikuwa ya mwaka moja moja). Ninakumbuka opereshini ya miezi sita (Juni - Desemba 1993) iliitwa opereshini miezi sita na Januari - Juni 1994 ilikuwa na jina la opereshini Oljoro (nasikia kuwa viongozi wa jeshi walifanya kikao cha kumpindua Mwinyi hapo - mpango ambao waliuacha).
 
..binafsi nadhani hiki kilikuwa kitendo cha aibu kwa Mwalimu kuwachapa viboko wanafunzi wa Chuo Kikuu.

..Mwalimu mwenyewe aliwahi kutuasu kwa ile kauli yake ya "nguvu za hoja na siyo hoja za nguvu."

..sasa hapa naona Mwalimu got his way kwa kutumia viboko na siyo hoja.

JokaKuu umechemsha,

Mwalimu aliamuru wanafunzi watandikwe bakora. Cha ajabu kipi hapo?

Nani alikwambia mwanafunzi wa chuo kikuu hachapwi bakora akichemsha? Basi hata jera asiswekwe akipatikana na hatia - maana yeye ni mwanafunzi wa choo kikuu.
 
Dr. Hussein Mwinyi anamiliki apartments ambazo ni adjacent na nyumba yetu ya Msasani. Hakuna harufu yoyote. Au maana Mwinyi jr. yupi?

Andrew,
Pale Mikocheni kuanzia TANESCO hadi mtaa wa Warioba kuna sewage mbaya na chafu sana. Halafu hata pale mbele ya TANESCO nasikia watu walijenga kwenye eneo la mkondo wa maji kuelekea baharini.
 
Makosa ya Mwalimu ni kwamba aliondoka madarakani bila ya kutengeneza Taasisi Imara na Huru kimfumo ambazo zingetusaidia kuwadhibiti watawala wahuni na wezi ambao wamejaa ktk utawala wa sasa.

thats very tru. Kama mwalimu angetengeneza mfumo thabit wakiutawala ungeweza kuwadhibit hawa mafisadi wa leo. Japo alijitahid kujenga taasisi ya usalama wa taifa. Leo hii ndio wamekua pet wa mafisad what a shame!
 
Charles Mwakitwile. Ni marehemu sasa. Alifia Mareheni miaka mitatu iliyopita na kuzikwa huko. A genius ambaye alinyimwa nafasi ya kurudi Mlimani kabisa akalazimika kumalizia masomo yake kwa njia za Kanisa la Baptist. Alifariki akiwa na Doctorate nadhani....

Rejea vizuri historia yako. Mwinyi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1985 - 1995. Mkapa akawa rais kwa kipindi cha 1995-2005 na Kikwete alianza 2005 - nk.

Kwa suala la kifo cha JKT ni kuwa kilikufa June 1994 (kipindi ambacho rais akiwa Mwinyi). Kabla ya kifo chake kilitangulia vipindi viwili vya miezi sita sita (hapo kabla JKT ilikuwa ya mwaka moja moja). Ninakumbuka opereshini ya miezi sita (Juni - Desemba 1993) iliitwa opereshini miezi sita na Januari - Juni 1994 ilikuwa na jina la opereshini Oljoro (nasikia kuwa viongozi wa jeshi walifanya kikao cha kumpindua Mwinyi hapo - mpango ambao waliuacha).
 
nA KWAKUKAZIA NI KWAMBA MWAKA 1994 mwezi June Nikiwa na Form yangu ya kujiunga JKT kambi ya Chitah Kule Ifakara , waziri wa Elimu , kama nakumbuka Charles Kabeho baada ya kupokea maagizo ya Ikulu ya Mwinyi akatutamgazia Umma kuwa JKT haitakuwepo katika mwaka huo kwahiyo Form six tuliokua tunajiandaa kwenda tukazuiwa, ILIKUA FURAHA SANA, KWAKUA UJINGA ULE SIKUUTAKA KABISA.

Kwa hiyo mpaka leo unaamini JKT ilikua ujinga fulani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom