Tundu Lissu, lini umewahi kulisaidia taifa?

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
TUNDU LISSU,LINI UMEWAHI KULISAIDIA TAIFA?.

Leo 12:15pm 24/11/2019.

Kwa mwaka wa pili sasa, Lissu, amekuwa nje ya mipaka ya Tanzania akionekana na Diasporas kama akina Emmanuel Muganda,Haji Khamis,Ansbert Ngurumo,Evarist Chahali uko Marekani,Canada,Scotland na Ubelgiji.

Pengine Tundu Lissu bado mgonjwa na kama mgonjwa hajapona, ni wazi kuwa hawezi kukumbuka chochote, hawezi kurudi nchini kuwashukuru Watanzania na wananchi wake waliokuwa wakimwombea na kumtolea mchango.

Lakini pia ni wazi kuwa hakumbuki chochote kama alichangiwa na akapatiwa matibabu mjini Dodoma. Hawezi kukumbuka hata maombi aliyofanyiwa na viongozi wa dini na hata Serikali iliyopambana kuokoa uhai wake hospitali ya Dodoma baada ya kupigwa risasi.

Twit ya Lissu ya jana imenifanya nimfikirie na kumjengea hoja na kumhitimisha kutokana na hoja aliyoijenga yeye mwenyewe.Lissu anasema "Mh Rais ndege yako imekamatwa tena Canada,huyo Profesa uliyemuokota jalalani na wenzake hawakusaidii wewe na hawaisaidii nchi yetu,wanatumikia matumbo yao tu,watumbue"

Kama mtaalamu wa saikolojia naweza kusema, Lissu amefikia kilele, yaani anaweza kuunga mkono juhudi muda wowote ule kutokana na sentensi yake inayoonyesha kuitaka nafasi ya Profesa anayesema ametolewa jalalani au kwa namna nyingine baada ya kufika kileleni mwa harakati zake.

Sasa Lissu anaelekea kudata muda wowote kuamua "liwalo na liwe maana hana cha kupoteza" katika hali hii hatumtarajia Tundu Lissu aseme mema ya kutukuka yanayofanywa sasa na Serikali yetu ya Tanzania ya awamu ya tano,kwa hali aliyonayo sasa ni sawa na kusubiri meli katika Uwanja wa ndege mpya utakaojengwa Msalato,Jijini Dodoma.

Mwanzoni mwa mwaka huu 2019, Lissu alitoka nje ya Ubelgiji na kufanya mahojiano katika vituo vya televisheni vya kimataifa akianzia BBC katika kipindi maarufu cha Hard Talk na baadae Ujerumani katika telavisheni ya DW.

Huko kote, mwanasiasa huyo hakumung'unya maneno juu na kuishambulia vibaya nchi yake ya Tanzania.

Pengine Lissu alifanya makusudi kulichafua Taifa lake la Tanzania au pengine hakuweza kufahamu madhara yatakayoipata nchi yake kwa kile alichokizungumza alipokuwa mataifa mengine kwa kuwa bado hajapona vizuri.

Kwa alicho kiongea lissu akiwa BBC na DW niligundua kitu kimoja kwamba Lissu si Mzalendo tena kwa taifa la Tanzania,pengine sasa uzalendo ameuhamishia katika tumbo lake,kwa sababu

1.Amekuwa kama Morgan Tsvangirai aliyezunguka kwa wazungu akitaka wasitishe misaada kwa nchi ya Zimbabwe na sasa tumeona Zimbabwe ilivyo na wanaoteseka ni Wananchi wa Zimbabwe.

2.Lissu amekuwa kama kibaraka wa kutumiwa mabeberu kutatua matatizo yao.

3.Lissu hakujua faida na hasara ya maneno yasiyo takia mema nchi yake ya Tanzania.

5.Kwa ushuhuda wa lugha yake katika mazungumzo na maandishi,Lissu amekuwa ni mshangiliaji na shabiki wa mabeberu.

Bila kujali kuwa alichofanya Lissu ni sahihi au si sahihi. Bila kujali matamshi aliyotoa mbele ya kamera za televisheni kupitia vipindi mbalimbali, bado Tundu Lissu, anapita njia ambayo katika duru za kisiasa zimefanywa mara nyingi na wanaharakati wa vyama vya kiharakati katika nchi mbalimbali na ujumbe wake ndiyo matokeo yanayofikirisha zaidi na kuibua mijadala juu ya Uzalendo na utaifa wa Tundu Lissu.

Je Lissu ni mhaini hata aogope kurudi Tanzania?

Wazalendo wengi nchini Tanzania wanasema kwa utovu wa Uzalendo wa Tundu Lissu basi atakuwa msaliti wa nchi ya Tanzania na hivyo ni mhaini,kwa kutumia Ibara ya 28 kifungu cha 4 cha Katiba ya Tanzania ambayo inatamka "uhaini kama unavyofafanuliwa na sheria utakuwa ni kosa la juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Muungano."

Kama Tundu Lissu anaogopa kurudi Tanzania basi anaogopa kushtakiwa Mahakamani na kushikishwa adabu kwa maslahi ya wengi,hayo ni mawazo yake yeye Tundu Lissu lakini Mimi nimwambie kwamba Uhuru wa mawazo tunao na ndiyo maana Lissu ameyaongea mengi uko BBC na DW na bado akabaki kuwa mtu huru.

Sasa Uhuru gani zaidi unautaka Bwana Lissu!? Lakini nikutahadharishe uko kwa wazungu ulipo,husije kuanza kutia watu vidole machoni halafu ukafikiri wazungu watakuchekea,hapana Uhuru una mipaka na ukizidi ni tatizo rejea Malcom x.

Kama utakuwa Mzalendo na kuongea mema ya nchi yetu ya Tanzania basi endelea na ziara zako kwa kuwa zinasimamiwa na Ibara ya 18 (kifungu cha A hadi D) ya Katiba ambayo inampa uhuru na haki ya kutoa maoni juu ya jambo lolote bila kuvunja sheria nyingine.

Hata Ibara ya 16 (kifungu cha kwanza) itakusaidia kwani inatamka "kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi,".

Na hata ibara ya 17 kiufungu cha kwanza itakulinda ambayo inaeleza kila raia anayo haki ya kwenda kokote na kuingia, pamoja na kifungu cha 2(a) na (b)(i-iii).

Lakini pia Ibara ya 29 kifungu cha 2 inaelezwa "kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kupata hifadhi sawa chini ya sheria za Jamhuri ya Muungano,".

-Historia ya ukaidi wa Tundu Lissu.

Kama alivyowahi kusema yeye mwenyewe kwamba alizaliwa muasi yaani rebel kwa lugha ya beberu, na hivyo haikuwa ajabu hata kidogo Tundu Lissu kujiunga na chama cha upinzani cha NCCR-Mageuzi kikiwa kinaipinga Serikali ya Chama Cha Mapinduzi,ilikuwa ni hatua inayotegemewa kwa muasi yeyote.

Kwa muonekano maongezi yake miaka ya 1995 Tundu Lissu alionekana ni Mjamaa wa mrengo wa kushoto kabisa lakini hivi sasa ukimuona Tundu Lissu na maongezi yake ni dhairi shahiri bila wasi wasi Tundu Lissu ni bepari.

Kwa miaka saba ya shule yake ya msingi, Tundu Lissu hakuwahi kuwahi namba shuleni hata siku moja, Siku zote alikuwa mchelewaji na alichapwa viboko kweli kweli.

Lissu aliwahi kuhojiwa kuhusu tabia yake ya kuchelewa namba shule ya msingo,alisema tatizo ni kuamka alfajiri saa 11 ili saa 12 niwe shuleni. Kwa hilo alikuwa rebel (muasi).

Kwa uasi wa Tundu Lissu akiwa shuleni alikuwa akibishana na walimu toka primary school, secondary school, hadi chuo kikuu, siku zote imekuwa hivyo.

Wakati wa vita vya Nduli Iddi Amini Dada,Tundu Lissu akiwa mdogo mwanafunzi wa shule ya msingi alikataa kuchimbishwa handaki nje ya nyumba yao ili hali ikiwa tete yeye na familia yake wajifiche, sababu yake aliyoitoa alikataa kwa sababu mahandaki hayakuwa marefu.

-Tundu Lissu na tetesi za kuwa mtumwa wa Usalama wa Taifa.

Tundu Lissu akiwa Jkt kwa mujibu wa sheria kipindi iko alitofautiana na RPC Omary Mahita alipowatembelea makuruta katika kambi za jeshi akiwa kama Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa.

Lissu aliuliza kama rpc ni mjinga au Mwalimu ndiye mjinga kuhusu wao kushiriki kwa namna moja au nyingine katika Siasa za vyama vingi.

Ndipo dawati zima la makamanda wa polisi walipoinuka na kutaka kumshughulikia kuruta Tundu Lissu,shukrani kwa Kanali Shija aliyeingilia kati kuwapiga Siasa Makamanda na kumuokoa Tundu Lissu.

Baada ya tukio la kumjibu vibaya Rpc Mahita hakuna ofisa wa JKT aliyewahi kumgusa Tundu Lissu,Wengi baada ya hapo wakaamini Tundu Lissu ni usalama wa taifa.

Maisha yakamuwia mazuri kambini,Hakuna aliyemgusa kwa sababu kama alimtukana Rpc na kutetewa na kanali wa jeshi, kwa sababu mkuu wa kambi wakati huo hakuwa kanali, alikuwa luteni kanali, sasa Tundu Lissu alitetewa na Kanali Shija. Kwa hiyo alionekana dhahiri kuwa ni mtumwa wa Usalama wa Taifa.

-Mzalendo hasi Evarist Chahali.

Evarist Chahali amekuwa mtu mwenye uchungu na kilicho chake (mwenye mapenzi ya kweli na muwazi), si mwenye kuacha kilicho chake kipotee (atalinda), ila sidhani kama anajenga kila penye maendeleo mazuri na sidhani uko uzunguni alipo anafanya kila juhudi kuhakikisha,kudumisha na kulinda mema ya nchi yake ya Tanzania.

Evarist Chahali anasema hakuna atakayetaka kugusia utendaji kazi wake tangu alipokuwa "kitengo maalum" (pekee kilichowahi kuchanganya surveillance na field work) mara baada ya kutoka chuoni.

Hakuna atakayegusia utendaji kazi wake alipokuwa mwanafunzi chuo kikuu, akitumia vema kifuniko chake cha uandishi wa habari, akijulikana kama "Ustaadh Bonge" huku akiwa field officer wa "Kanda."

Hakuna atakayekwambia mchango wake katika kudhibiti "kunji" pale Mlimani.
Pia hakuna atakayekwambia kuhusu utendaji kazi wa Chahali kwenye dawati la CI (Counterintelligence).

Baada ya kupambana vilivyo na kila jasusi aliyetumwa kuifanyia ujasusi Tanzania,Evarist Chahali anasema hakuna atakayekwambia kuwa baada ya kufanya vizuri alipewa promosheni na kuwa Mkuu wa Kanda C.

Evarist Chahali anasema hakuna atakayekwambia kuwa maafisa waliokuwa chini ya "bosi Chahali" walitumia "Pajero yake ya ukuu wa Kanda na dereva wake vilikuwa kama vya kila afisa, kwani alithamini kila mtu." katika eneo la majimbo ya Temeke na Kigamboni yaliyokuwa maeneo yake ya Kanda, ili ujue alifanya kazi vipi na sources.

Evarist Chahali anasema hawatokwambia kuwa Chahali ndio mtumishi pekee katika historia ya Idara ya Usalama wa Taifa kuandika kitabu cha Kiswahili kuhusu taaluma hiyo, kitabu ambacho kimesaidia sana kuwafahamisha Watanzania umuhimu wa kazi akiwasaidia sana maafisa, kwani iliamriwa kila afisa kusoma kitabu iko.

Ndugu yangu Chahali Kila mzalendo ni mwananchi. Lakini si kila mwanachi ni mzalendo. Kuna wananchi ambao hawana uzalendo, yaani hawana upendo kwa nchi yao, na hawako tayari kuitumia nchi yao kwa moyo wote na kwa uadilifu kama alivyo Lissu hasa ukifuatilia historia yake tangu utotoni.

Uzalendo wa mtu (au ukosefu wa uzalendo) haupimwi kwa tendo moja au tukio moja. Kuwa mzalendo au kutokuwa mzalendo lazima iwe ni tabia ya kudumu inayojionesha nje.

-Mzalendo ni nani?

Uzalendo ni matokeo ya historia iliyotukuka ya mwanachi kutetea ukweli na haki kwa faida ya nchi yake, kusimamia rasilimali au kutumia uwezo wake, cheo chake kwa faida ya nchi yake kwanza kabla hata ya kufikiri kujinufaisha.

Mzalendo anatakiwa kuwa na msimamo katika maamuzi yake na hata kuhakikisha anawahamasisha watu wengine kuwa misimamo sahihi haswa katika suala ambalo anaona lina manufaa kwa kila raia,

Mwalimu Nyerere alipowakatalia wazungu kuchimba madini, na kuwaambia yatachimbwa na watanzania wenyewe watapokuwa na akili, Huyu alikuwa Mzalendo namba moja wa Taifa Mwalimu Nyerere alifanya hivi makusudi ili,kila mwananchi aweze kufaidika na madini, lakini leo Tundu Lissu anawasaidia wezi wa madini akitoa ushauri wa kushindwa kwa maamuzi ya Serikali ya Tanzania dhidi ya wezi wa Madini yetu na wahukumu wa uchimi wetu.

Kuna wakati Madaktari walikosa Uzalendo kwa kitendo chao cha kuitisha mgomo nchi nzima.

Kuwa mzalendo ni zaidi ya kuifia nchi yako. Kwa sababu aidha kwa uzembe au kwa ujinga au kwa imani yake mtu aweza kufa lakini kumbe hakuipenda nchi ila kwa matakwa yake binafsi.

Wito wa udaktari ulipaswa kuwa tunda la uaminifu, upendo kujitoa, kuwatumikia Wananchi katika nchi yako,huo ndio ulipaswa kuwa Uzalendo wa kwanza kwa Madaktari.

-Uzalendo ni kutetea na kulinda Maslani ya Nchi.

Uzalendo ni kusimama kwa nchi yako,Mfano mzuri ni waisraeli, nilikuwa nikifuatilia mgogoro wa Israel na Lebanon, Kila muisrael popote duaniani alipohojiwa alikuwa anatetea nchi yake na kuponda sana Hizbolah.

Vivyo hivy kwa wairan na Wasyria hata kama nchi yao ilikuwa inatumia nguvu kupindukia na kuua raia wasio na hatia. Wanajua nini matunda yake,bado waliomba mema na kuitakia mema siku moja pawe na amani,ile nchi ndio nyumbani na wakiamua kwenda wanakaribishwa na waziri mkuu wa nchi na kupewa almost mahitaji yote.

Huo ndio uzalendo ambao mimi na wewe tulitakiwa kuwa nao hata kuitetea nchi yetu katika saga ya mapanki katika jua na katika Mvua,lakini hivi sasa watu wanafurahia Mzungu anapokamata ndege ya Watanzania.

-Upinzani wanapinga hata waliyoyapigania kwa miaka 20.

Pengine Rais John Magufuli ndiye mtu aliyeyaona sana matatizo ya Watanzania kuliko wapinzani.

Mh Rais Magufuli ametatua matatizo yote yaliyokuwa yakipigiwa kelele na wapinzani kwa miaka 20 iliyopita.

Wapinzani walihubiri kupata mabadiliko tu kama tutapata kiongozi kwenye highest position yaani Urais ambaye hakutoka kwenye inner circle ya CCM (unfortunately opposition is still very weak) lakini tumempata Mh Rais Magufuli sawa sawa na maombi yao.

Tumeona Mh Rais akiwachukulia hatua vigogo wa chama na Serikali ambao ndio wamemlea kichama mpaka akafika hapo alipo, hili ndilo lilikuwa ombi la upinzani kupata mtu ambaye hatamuone haya yeyote atayetenda kinyume na maslahi ya Umma.

Kuna wakati John Mnyika alisema Rais Jk ni dhaifu na tulihitaji Rais mwenye kariba ya Fidel Castro ambaye aliidhinisha adhabu ya kifo kwa jamaa yake waliepigana naye bega kwa bega msituni kwa kuwa alitiwa hatiani kwa kushiriki biashara ya madawa ya kulevya ambayo inabeba adhabu ya Kifo.

Nimalizie kwa kuwatia moyo Wazalendo popote mlipo,pamoja na changamoto za hapa na pale bado naamini ninyi ndio tegemeo la Taifa la Tanzania nashukuru pia sera ya Ujamaa na kujitegemea inafuatwa kwani kwa wanaofahamu Ujamaa ni kujali utu na heshima na haki ya kila mtu na kwamba kila mtu aweze kupata elimu, afya, nafasi ya kuishi na usawa,kwa hakika tutaifikia Tanzania ya Viwanda.

Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kuibariki Tanzania,Tupe neema ya kutumia vyema baraka ulizotujaalia,Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kumbariki na kumlinda Rais wetu John Magufuli.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854.
 
Kwa wewe na wenzako wahitimu wa shule za kata katu na kamwe hamuwezi kuujua mchango wa Tundu Lissu kwa Tanzania.
Ukiwauliza watu wa Geita na Mara kwa uchache,waliozungukwa na migodi,utapata sehemu tu ya mchango wake kwa Tanzania.
 
Wenye Afya hawana haja na tabibu
Hata Yesu hakuja kwaajili ya Watakatifu ila wenye dhambi
Pia, mwemye shibe hamjui mwenye njaa
Usisahau, uzima wa mtu haumo ndani ya wingi wa mali alizonazo.
Kimsingi, heri wenye njaa na kiu ya haki maana hao watashinishwa.
Asante.
 
Maneno hayavunji mfupa hakuna kati yetu aliyepigwa risasi na watu wasiojulikana! Leo hii mtu kudidiki kwenye mitandao kirahisi tu kujifanya mzalendo kuliko wadiriki kufa ni kichekesho.
 
Muulize Makinda, Waulize wakurya wa nyamongo waliokuwa wamebambikiwa kesi na police na ccm kwenye mgodi alivyowatete na kumaliza kesi zao.

Magufuli alikuwa waziri aliwasaidia nini wananchi wa nyamongo wakati wanatililishiwa maji yeye sumu na mgodi wa nyamongo?.

Waulize wakina Melo uenda asingekuwa Lissu Usingepata hiyo platiform kuandika uo upuuzi wako kama asingemtetea Melo kwa kesi fake aliyopewa na ccm uko nyuma kiufupi uelewi chochote kuhusu Tundu Lissu.
 
Wakiwa Chadema mnawaita wasaliti siku wakiunga mkono juhudi za 'malaika' mnawaita mashujaa! Wote kina Kafulila, Mtatilo, Dr. Kitila, Kalist, Waitala hata Shonza kuna kipindi mliwaita wasaliti na leo ndio vichwa huko ccm! Wasaliti wa nchi wapo huko huko ccm!
 
Anza kuweka hapa kwanza msaada wako kwa taifa, mimi sina msaada wowote kwa taifa kwani si mwanachama wa CCM.
 
Unafahamu maumivu ya risasi?, unataka Lisu arudi ili iweje? Kama lisu hana msaada unaumia nini kuona harudi? Anawalalmikia watawala wa Tanzania au analilalamikia taifa la Tanzania?
Ni mtu mwenye afya njema ya akili pekee anaweza kujibu maswali yako
 
TUNDU LISSU,LINI UMEWAHI KULISAIDIA TAIFA?.

Leo 12:15pm 24/11/2019.

Kwa mwaka wa pili sasa, Lissu, amekuwa nje ya mipaka ya Tanzania akionekana na Diasporas kama akina Emmanuel Muganda,Haji Khamis,Ansbert Ngurumo,Evarist Chahali uko Marekani,Canada,Scotland na Ubelgiji.

Pengine Tundu Lissu bado mgonjwa na kama mgonjwa hajapona, ni wazi kuwa hawezi kukumbuka chochote, hawezi kurudi nchini kuwashukuru Watanzania na wananchi wake waliokuwa wakimwombea na kumtolea mchango.

Lakini pia ni wazi kuwa hakumbuki chochote kama alichangiwa na akapatiwa matibabu mjini Dodoma. Hawezi kukumbuka hata maombi aliyofanyiwa na viongozi wa dini na hata Serikali iliyopambana kuokoa uhai wake hospitali ya Dodoma baada ya kupigwa risasi.

Twit ya Lissu ya jana imenifanya nimfikirie na kumjengea hoja na kumhitimisha kutokana na hoja aliyoijenga yeye mwenyewe.Lissu anasema "Mh Rais ndege yako imekamatwa tena Canada,huyo Profesa uliyemuokota jalalani na wenzake hawakusaidii wewe na hawaisaidii nchi yetu,wanatumikia matumbo yao tu,watumbue"

Kama mtaalamu wa saikolojia naweza kusema, Lissu amefikia kilele, yaani anaweza kuunga mkono juhudi muda wowote ule kutokana na sentensi yake inayoonyesha kuitaka nafasi ya Profesa anayesema ametolewa jalalani au kwa namna nyingine baada ya kufika kileleni mwa harakati zake.

Sasa Lissu anaelekea kudata muda wowote kuamua "liwalo na liwe maana hana cha kupoteza" katika hali hii hatumtarajia Tundu Lissu aseme mema ya kutukuka yanayofanywa sasa na Serikali yetu ya Tanzania ya awamu ya tano,kwa hali aliyonayo sasa ni sawa na kusubiri meli katika Uwanja wa ndege mpya utakaojengwa Msalato,Jijini Dodoma.

Mwanzoni mwa mwaka huu 2019, Lissu alitoka nje ya Ubelgiji na kufanya mahojiano katika vituo vya televisheni vya kimataifa akianzia BBC katika kipindi maarufu cha Hard Talk na baadae Ujerumani katika telavisheni ya DW.

Huko kote, mwanasiasa huyo hakumung'unya maneno juu na kuishambulia vibaya nchi yake ya Tanzania.

Pengine Lissu alifanya makusudi kulichafua Taifa lake la Tanzania au pengine hakuweza kufahamu madhara yatakayoipata nchi yake kwa kile alichokizungumza alipokuwa mataifa mengine kwa kuwa bado hajapona vizuri.

Kwa alicho kiongea lissu akiwa BBC na DW niligundua kitu kimoja kwamba Lissu si Mzalendo tena kwa taifa la Tanzania,pengine sasa uzalendo ameuhamishia katika tumbo lake,kwa sababu

1.Amekuwa kama Morgan Tsvangirai aliyezunguka kwa wazungu akitaka wasitishe misaada kwa nchi ya Zimbabwe na sasa tumeona Zimbabwe ilivyo na wanaoteseka ni Wananchi wa Zimbabwe.

2.Lissu amekuwa kama kibaraka wa kutumiwa mabeberu kutatua matatizo yao.

3.Lissu hakujua faida na hasara ya maneno yasiyo takia mema nchi yake ya Tanzania.

5.Kwa ushuhuda wa lugha yake katika mazungumzo na maandishi,Lissu amekuwa ni mshangiliaji na shabiki wa mabeberu.

Bila kujali kuwa alichofanya Lissu ni sahihi au si sahihi. Bila kujali matamshi aliyotoa mbele ya kamera za televisheni kupitia vipindi mbalimbali, bado Tundu Lissu, anapita njia ambayo katika duru za kisiasa zimefanywa mara nyingi na wanaharakati wa vyama vya kiharakati katika nchi mbalimbali na ujumbe wake ndiyo matokeo yanayofikirisha zaidi na kuibua mijadala juu ya Uzalendo na utaifa wa Tundu Lissu.

Je Lissu ni mhaini hata aogope kurudi Tanzania?

Wazalendo wengi nchini Tanzania wanasema kwa utovu wa Uzalendo wa Tundu Lissu basi atakuwa msaliti wa nchi ya Tanzania na hivyo ni mhaini,kwa kutumia Ibara ya 28 kifungu cha 4 cha Katiba ya Tanzania ambayo inatamka "uhaini kama unavyofafanuliwa na sheria utakuwa ni kosa la juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Muungano."

Kama Tundu Lissu anaogopa kurudi Tanzania basi anaogopa kushtakiwa Mahakamani na kushikishwa adabu kwa maslahi ya wengi,hayo ni mawazo yake yeye Tundu Lissu lakini Mimi nimwambie kwamba Uhuru wa mawazo tunao na ndiyo maana Lissu ameyaongea mengi uko BBC na DW na bado akabaki kuwa mtu huru.

Sasa Uhuru gani zaidi unautaka Bwana Lissu!? Lakini nikutahadharishe uko kwa wazungu ulipo,husije kuanza kutia watu vidole machoni halafu ukafikiri wazungu watakuchekea,hapana Uhuru una mipaka na ukizidi ni tatizo rejea Malcom x.

Kama utakuwa Mzalendo na kuongea mema ya nchi yetu ya Tanzania basi endelea na ziara zako kwa kuwa zinasimamiwa na Ibara ya 18 (kifungu cha A hadi D) ya Katiba ambayo inampa uhuru na haki ya kutoa maoni juu ya jambo lolote bila kuvunja sheria nyingine.

Hata Ibara ya 16 (kifungu cha kwanza) itakusaidia kwani inatamka "kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi,".

Na hata ibara ya 17 kiufungu cha kwanza itakulinda ambayo inaeleza kila raia anayo haki ya kwenda kokote na kuingia, pamoja na kifungu cha 2(a) na (b)(i-iii).

Lakini pia Ibara ya 29 kifungu cha 2 inaelezwa "kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kupata hifadhi sawa chini ya sheria za Jamhuri ya Muungano,".

-Historia ya ukaidi wa Tundu Lissu.

Kama alivyowahi kusema yeye mwenyewe kwamba alizaliwa muasi yaani rebel kwa lugha ya beberu, na hivyo haikuwa ajabu hata kidogo Tundu Lissu kujiunga na chama cha upinzani cha NCCR-Mageuzi kikiwa kinaipinga Serikali ya Chama Cha Mapinduzi,ilikuwa ni hatua inayotegemewa kwa muasi yeyote.

Kwa muonekano maongezi yake miaka ya 1995 Tundu Lissu alionekana ni Mjamaa wa mrengo wa kushoto kabisa lakini hivi sasa ukimuona Tundu Lissu na maongezi yake ni dhairi shahiri bila wasi wasi Tundu Lissu ni bepari.

Kwa miaka saba ya shule yake ya msingi, Tundu Lissu hakuwahi kuwahi namba shuleni hata siku moja, Siku zote alikuwa mchelewaji na alichapwa viboko kweli kweli.

Lissu aliwahi kuhojiwa kuhusu tabia yake ya kuchelewa namba shule ya msingo,alisema tatizo ni kuamka alfajiri saa 11 ili saa 12 niwe shuleni. Kwa hilo alikuwa rebel (muasi).

Kwa uasi wa Tundu Lissu akiwa shuleni alikuwa akibishana na walimu toka primary school, secondary school, hadi chuo kikuu, siku zote imekuwa hivyo.

Wakati wa vita vya Nduli Iddi Amini Dada,Tundu Lissu akiwa mdogo mwanafunzi wa shule ya msingi alikataa kuchimbishwa handaki nje ya nyumba yao ili hali ikiwa tete yeye na familia yake wajifiche, sababu yake aliyoitoa alikataa kwa sababu mahandaki hayakuwa marefu.

-Tundu Lissu na tetesi za kuwa mtumwa wa Usalama wa Taifa.

Tundu Lissu akiwa Jkt kwa mujibu wa sheria kipindi iko alitofautiana na RPC Omary Mahita alipowatembelea makuruta katika kambi za jeshi akiwa kama Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa.

Lissu aliuliza kama rpc ni mjinga au Mwalimu ndiye mjinga kuhusu wao kushiriki kwa namna moja au nyingine katika Siasa za vyama vingi.

Ndipo dawati zima la makamanda wa polisi walipoinuka na kutaka kumshughulikia kuruta Tundu Lissu,shukrani kwa Kanali Shija aliyeingilia kati kuwapiga Siasa Makamanda na kumuokoa Tundu Lissu.

Baada ya tukio la kumjibu vibaya Rpc Mahita hakuna ofisa wa JKT aliyewahi kumgusa Tundu Lissu,Wengi baada ya hapo wakaamini Tundu Lissu ni usalama wa taifa.

Maisha yakamuwia mazuri kambini,Hakuna aliyemgusa kwa sababu kama alimtukana Rpc na kutetewa na kanali wa jeshi, kwa sababu mkuu wa kambi wakati huo hakuwa kanali, alikuwa luteni kanali, sasa Tundu Lissu alitetewa na Kanali Shija. Kwa hiyo alionekana dhahiri kuwa ni mtumwa wa Usalama wa Taifa.

-Mzalendo hasi Evarist Chahali.

Evarist Chahali amekuwa mtu mwenye uchungu na kilicho chake (mwenye mapenzi ya kweli na muwazi), si mwenye kuacha kilicho chake kipotee (atalinda), ila sidhani kama anajenga kila penye maendeleo mazuri na sidhani uko uzunguni alipo anafanya kila juhudi kuhakikisha,kudumisha na kulinda mema ya nchi yake ya Tanzania.

Evarist Chahali anasema hakuna atakayetaka kugusia utendaji kazi wake tangu alipokuwa "kitengo maalum" (pekee kilichowahi kuchanganya surveillance na field work) mara baada ya kutoka chuoni.

Hakuna atakayegusia utendaji kazi wake alipokuwa mwanafunzi chuo kikuu, akitumia vema kifuniko chake cha uandishi wa habari, akijulikana kama "Ustaadh Bonge" huku akiwa field officer wa "Kanda."

Hakuna atakayekwambia mchango wake katika kudhibiti "kunji" pale Mlimani.
Pia hakuna atakayekwambia kuhusu utendaji kazi wa Chahali kwenye dawati la CI (Counterintelligence).

Baada ya kupambana vilivyo na kila jasusi aliyetumwa kuifanyia ujasusi Tanzania,Evarist Chahali anasema hakuna atakayekwambia kuwa baada ya kufanya vizuri alipewa promosheni na kuwa Mkuu wa Kanda C.

Evarist Chahali anasema hakuna atakayekwambia kuwa maafisa waliokuwa chini ya "bosi Chahali" walitumia "Pajero yake ya ukuu wa Kanda na dereva wake vilikuwa kama vya kila afisa, kwani alithamini kila mtu." katika eneo la majimbo ya Temeke na Kigamboni yaliyokuwa maeneo yake ya Kanda, ili ujue alifanya kazi vipi na sources.

Evarist Chahali anasema hawatokwambia kuwa Chahali ndio mtumishi pekee katika historia ya Idara ya Usalama wa Taifa kuandika kitabu cha Kiswahili kuhusu taaluma hiyo, kitabu ambacho kimesaidia sana kuwafahamisha Watanzania umuhimu wa kazi akiwasaidia sana maafisa, kwani iliamriwa kila afisa kusoma kitabu iko.

Ndugu yangu Chahali Kila mzalendo ni mwananchi. Lakini si kila mwanachi ni mzalendo. Kuna wananchi ambao hawana uzalendo, yaani hawana upendo kwa nchi yao, na hawako tayari kuitumia nchi yao kwa moyo wote na kwa uadilifu kama alivyo Lissu hasa ukifuatilia historia yake tangu utotoni.

Uzalendo wa mtu (au ukosefu wa uzalendo) haupimwi kwa tendo moja au tukio moja. Kuwa mzalendo au kutokuwa mzalendo lazima iwe ni tabia ya kudumu inayojionesha nje.

-Mzalendo ni nani?

Uzalendo ni matokeo ya historia iliyotukuka ya mwanachi kutetea ukweli na haki kwa faida ya nchi yake, kusimamia rasilimali au kutumia uwezo wake, cheo chake kwa faida ya nchi yake kwanza kabla hata ya kufikiri kujinufaisha.

Mzalendo anatakiwa kuwa na msimamo katika maamuzi yake na hata kuhakikisha anawahamasisha watu wengine kuwa misimamo sahihi haswa katika suala ambalo anaona lina manufaa kwa kila raia,

Mwalimu Nyerere alipowakatalia wazungu kuchimba madini, na kuwaambia yatachimbwa na watanzania wenyewe watapokuwa na akili, Huyu alikuwa Mzalendo namba moja wa Taifa Mwalimu Nyerere alifanya hivi makusudi ili,kila mwananchi aweze kufaidika na madini, lakini leo Tundu Lissu anawasaidia wezi wa madini akitoa ushauri wa kushindwa kwa maamuzi ya Serikali ya Tanzania dhidi ya wezi wa Madini yetu na wahukumu wa uchimi wetu.

Kuna wakati Madaktari walikosa Uzalendo kwa kitendo chao cha kuitisha mgomo nchi nzima.

Kuwa mzalendo ni zaidi ya kuifia nchi yako. Kwa sababu aidha kwa uzembe au kwa ujinga au kwa imani yake mtu aweza kufa lakini kumbe hakuipenda nchi ila kwa matakwa yake binafsi.

Wito wa udaktari ulipaswa kuwa tunda la uaminifu, upendo kujitoa, kuwatumikia Wananchi katika nchi yako,huo ndio ulipaswa kuwa Uzalendo wa kwanza kwa Madaktari.

-Uzalendo ni kutetea na kulinda Maslani ya Nchi.

Uzalendo ni kusimama kwa nchi yako,Mfano mzuri ni waisraeli, nilikuwa nikifuatilia mgogoro wa Israel na Lebanon, Kila muisrael popote duaniani alipohojiwa alikuwa anatetea nchi yake na kuponda sana Hizbolah.

Vivyo hivy kwa wairan na Wasyria hata kama nchi yao ilikuwa inatumia nguvu kupindukia na kuua raia wasio na hatia. Wanajua nini matunda yake,bado waliomba mema na kuitakia mema siku moja pawe na amani,ile nchi ndio nyumbani na wakiamua kwenda wanakaribishwa na waziri mkuu wa nchi na kupewa almost mahitaji yote.

Huo ndio uzalendo ambao mimi na wewe tulitakiwa kuwa nao hata kuitetea nchi yetu katika saga ya mapanki katika jua na katika Mvua,lakini hivi sasa watu wanafurahia Mzungu anapokamata ndege ya Watanzania.

-Upinzani wanapinga hata waliyoyapigania kwa miaka 20.

Pengine Rais John Magufuli ndiye mtu aliyeyaona sana matatizo ya Watanzania kuliko wapinzani.

Mh Rais Magufuli ametatua matatizo yote yaliyokuwa yakipigiwa kelele na wapinzani kwa miaka 20 iliyopita.

Wapinzani walihubiri kupata mabadiliko tu kama tutapata kiongozi kwenye highest position yaani Urais ambaye hakutoka kwenye inner circle ya CCM (unfortunately opposition is still very weak) lakini tumempata Mh Rais Magufuli sawa sawa na maombi yao.

Tumeona Mh Rais akiwachukulia hatua vigogo wa chama na Serikali ambao ndio wamemlea kichama mpaka akafika hapo alipo, hili ndilo lilikuwa ombi la upinzani kupata mtu ambaye hatamuone haya yeyote atayetenda kinyume na maslahi ya Umma.

Kuna wakati John Mnyika alisema Rais Jk ni dhaifu na tulihitaji Rais mwenye kariba ya Fidel Castro ambaye aliidhinisha adhabu ya kifo kwa jamaa yake waliepigana naye bega kwa bega msituni kwa kuwa alitiwa hatiani kwa kushiriki biashara ya madawa ya kulevya ambayo inabeba adhabu ya Kifo.

Nimalizie kwa kuwatia moyo Wazalendo popote mlipo,pamoja na changamoto za hapa na pale bado naamini ninyi ndio tegemeo la Taifa la Tanzania nashukuru pia sera ya Ujamaa na kujitegemea inafuatwa kwani kwa wanaofahamu Ujamaa ni kujali utu na heshima na haki ya kila mtu na kwamba kila mtu aweze kupata elimu, afya, nafasi ya kuishi na usawa,kwa hakika tutaifikia Tanzania ya Viwanda.

Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kuibariki Tanzania,Tupe neema ya kutumia vyema baraka ulizotujaalia,Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kumbariki na kumlinda Rais wetu John Magufuli.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854.
Blablablah rubbish!
Mlivyomtwanga risasi hamkuja humu kuandika upupu wenu
Let the man live his life
Mmeshindwa kuendesha nchi kutwa Lissu Lissu
Huna wazazi wewe huna watoto wewe huna ndugu wewe?? Kwa alichofanyiwa Lissu jiweke wewe kwenye nafasi yake ndio uje uandike urojo wako hapa

You are disgusting!
 
Hadithi ndefu kumbe pumba tupu!

Nikuulize swali jepesi tu, hata kama umebaini kuwaTundu Lissu siyo mzakendo, je njia iliyotumika ya kutaka kutoa uhai wake kwa kumminia,risasi mfululizo zaidi ya 30 kwenye gari lake ndiyo ilikuwa njia sahihi kwenu??
 
Na mawasiliano umeweka kabisa ili uteuliwe. Nguruwe wa Lumumba mnahangaika sana.
 
Back
Top Bottom