Mgeja amchana Sitta, kumbe alishachapwa viboko na Nyerere kwa kuongoza maandamano!!!

eumb

Senior Member
Apr 2, 2012
149
70
SIKU moja baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa kumrushia kombora zito Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Hamis Mgeja amemtaka waziri huyo na wabunge wengine 55 wapime, watafakari na hatimaye wachukue hatua kwa kuondoka ndani ya CCM.
Mgeja ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, amesema tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi ya Sitta na wabunge hao, zinathibitisha jinsi kiongozi huyo na wenzake walivyo wasaliti ndani ya chama chao na serikali, na kwamba kitendo cha kuigeuza ofisi ya spika kuwa kijiwe cha kupanga uhaini na usaliti ndani ya CCM hakivumiliki hata kidogo.
Mgeja alitoa kauli hiyo jana jijini Mwanza, alipozungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kumpongeza Dk. Slaa kwa kufichua uozo wa Waziri Sitta na wenzake hao. Alisema Dk. Slaa ameisaidia CCM kutambua viongozi wake wanaokisaliti.
"Nianze kwa kumpongeza Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Slaa kwa kufichua madhambi ya Samuel Sitta. Huyu mtu (Sitta), ni hatari sana katika maendeleo ya chama chetu.
"Dk. Slaa ametueleza jinsi Sitta alivyotumia ofisi ya spika kama kijiwe cha kutaka kukisaliti chama chetu na kuanzisha CCJ. Huyu mtu ni hatari sana... tunaomba CCM imtose yeye na wabunge hao 55 maana uroho wao wa madaraka unaweza kuigharimu CCM.
"Kwa kashfa hii nzito dhidi yao, namshauri wapime, watafakari na hatimaye wachukuwe hatua. Pia nawashauri kwanza watubu na kuomba radhi chama na wana CCM wote, au wajiengue kwa hiari yao bila shuruti, ili walinde heshima yao. Wasingoje kuhukumiwa na wanachama," alisema.
Mjumbe huyo wa NEC na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga aliyejipambanua kupiga vita ufisadi na vitendo viovu ndani na nje ya CCM, alisema historia ya Waziri Sitta inajionesha wazi kwamba ni 'mkorofi na msaliti mkubwa', kwani mwaka 1966 akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alishiriki maandamano hadi Ikulu kupinga sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Alisema katika harakati zao hizo za kupinga sheria hiyo iliyotaka kila mwanafunzi wa Chuo Kikuu lazima ajiunge na Jeshi la Kujenga Taifa, Baba wa Taifa wakati huo akiwa Rais wa nchi na mkuu wa chuo hicho, alilazimika kumchapa viboko Sitta kutokana na usaliti wake huo kwa serikali.
Mgeja alisema mbali na kufanya maandamano hayo, Sitta na wenzake ambao wengine ni marehemu kwa sasa walikuwa na mabango yenye ujumbe mkali kwa serikali, ukiwemo uliosema 'Onyo kali na la mwisho kwa serikali', na kwamba alikuwa akiipinga pia Serikali ya Baba wa Taifa huku akiusifu uongozi wa kikoloni.
"Huyu Sitta ambaye leo hii anawadanganya watu, kipindi hicho akisoma Chuo Kikuu alikuwa akiipinga serikali na kudai afadhali serikali ya kikoloni. Tusipoamini leo usaliti wake huu tunasubiri hadi aje shetani atuambie usaliti wa Sitta ndipo tuamini?
"Za mwizi ni 40, ndiyo maana tumeambiwa toka mwaka 2005 hadi 2010 huyu Sitta amekuwa akikisaliti chama chetu kupitia Bunge alilokuwa akiliongoza. Tunataka chama kimtose na kisiwaonee haya wasaliti hawa wakubwa. Wasipoondoka kwa hiari yao wataondolewa kwa nguvu ya wanachama wa CCM,” alisema.
Alimtuhumu pia Waziri Sitta kwa kauli zake za kulalamikia serikali bila kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayolikumba taifa, na alimtaka ataje jinsi alivyoisaidia serikali kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, mfumuko wa bei, ufisadi na mambo mengine ndani ya chama na serikali.
Kwa mujibu wa Mgeja anayedaiwa kuanza kuundiwa mbinu chafu za kutaka kuangushwa katika kinyang'anyiro cha uenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga na kundi la kigogo mmoja anayetajwa kutaka kugombea urais mwaka 2010, tuhuma hizo dhidi ya Waziri Sitta zimekisaidia maradufu chama, kwani siyo Dk. Slaa pekee aliyewahi kumshutumu kiongozi huyo kwa usaliti ndani ya chama.
Alisema yupo tayari kusulubiwa, kutolewa kafara au kufukuzwa na chama kwa kusema ukweli daima, kwani anayasema hayo kwa kufuata kiapo cha katiba ya CCM

Sorce; Tanzania Daima
 
atatwangwa kotekote,..cdm wanapiga huku magamba yanapiga kule..huwezi kukibeza chama kilichochaguliwa na wananchi kuongoza nchi mwaka 2010..
 

6324088563257897474-4323692948903928007
na Betty Kangonga

BAADA ya bomoa bomoa, yameibuka madai kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wilayani Kinondoni, Anna Luvanda ‘Mama Makete' amekuwa akiwatumia wananchi wanyonge kwa maslahi yake binafsi kuvamia maeneo yaliyopo katika wilaya hiyo.

Agosti 22, mwaka huu Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na vyombo vya dola, ilibomoa nyumba zaidi ya 300 zilizojengwa katika Kata ya Mabwepande na Madale, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kwa madai ya kuvamia eneo hilo.

Pamoja na hilo, Mama Makete anadaiwa kuwapa pesa kinamama na watoto na kuwapakia katika magari binafsi na kisha kuwatelekeza karibu na ofisi ya Ikulu.

Akisoma taarifa ya umoja wa watu waliovamiwa maeneo yao jijini Dar es Salaam juzi, katika mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Kituo cha Polisi Kawe, Kaimu Mwenyekiti wa umoja huo, James Mramba, alidai Mama Makete amekuwa akitumia cheo chake kwa maslai binafsi.

Mramba alidai kuwa Mama Makete aliwakodisha kinamama na watoto wao na kuwalipa ujira mdogo ili wafike katika ofisi za Ikulu waonane na Rais Jakaya Kikwete.

"Huyu kigogo ndiye chanzo cha vurugu zote za uvamizi wa maeneo katika wilaya hii, amekuwa akiwatumia wanyonge na mbaya zaidi wakati wa bomoa bomoa aliwachukua wanawake na kuwapeleka karibu na Ikulu.

"Aliwafikisha hapo ili waende wakaeleze kuwa wameonewa na manispaa na waweze kupatiwa maeneo hayo," alidai Kaimu Mwenyekiti huyo.

Aidha, alidai Mama Makete amekuwa akifadhili wananchi waliovunjiwa maeneo hayo kwa sasa kwa kuwapatia hifadhi katika eneo la machimbo ya kokoto ambako wameweka kambi.

Alibainisha kuwa, anashindwa kujitokeza hadharani kwa kuwa anajua eneo analomiliki hakulipata kihalali.

Akichangia katika mkutano huo, Mbunge wa Viti Maalumu, Rita Mlaki (CCM), alisema serikali imeshafanya utafiti wa kina juu ya kuwepo kwa kigogo huyo na ripoti yake imeshafika mezani kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick.

"Hatuna haja ya kulalamika juu ya jambo hilo… ninajua Serikali ya CCM haiwezi kumkubatia mtu kama huyo," alisema.

Mlaki alidai kwa sasa kuna uhuni unafanywa na wavamizi hao ambapo wanajipanga na kuandaa nyaraka, ili ionekane wazi kuwa maeneo hayo
ni mali yao kihalali.

Huku akikitetea chama chake, Mlaki alidai kuwa CCM haiwezi kukubali kigogo huyo aendelee kukichafua chama hicho, hivyo anaamini hatua zaidi zitachukuliwa kukomesha vitendo hivyo vya kifisadi.

Hata hivyo, alisema ingawa wavamizi walikimbilia Tume ya Haki za Binadamu, bado wanayo nafasi ya kukutana na kiongozi wa tume hiyo ili kujua undani wa maeneo hayo.

"Nasi tusimame imara, Tume ya Haki za Binadamu ninawafahamu viongozi wake na tunaweza kwenda kule na tumevumilia vya kutosha kwa kuwa tunaiheshimu serikali maana nasi tulikuwa na uwezo wa kuwa Mungiki," alisema.

Naye Seif Magugu, alidai kigogo huyo anamiliki machimbo ya kokoto na ndiye mfadhili mkuu wa vijana wanaoendesha vitendo vya kibabe katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Akizungumzia tuhuma hizo, Mama Makete aliziita ni za kisiasa na zina lengo la kumchafua.

Alifananisha tuhuma hizo na methali ya ‘akutukanaye hakuchagulii tusi' na akasema hawezi kuitumia Ikulu kuendesha vitendo viovu.

"Mimi nina malori matano na hayo sikai nayo, sasa ni muda upi niliwabeba hao watu na kwenda kuwashusha Ikulu?" alihoji.

Alisema eneo analodaiwa kuvamia aliuziwa miaka nane iliyopita, hivyo kama kuna mtu ana umiliki halali wa eneo hilo, hana budi kujitokeza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema, Jeshi la Polisi litafuatilia juu ya kuwepo kwa kikundi cha wavamizi kuweka kambi katika eneo la mchimbo ya kokoto.

 
Hivi ukitaka kuhama chama ni usaliti au dhambi?
Just asking................
 
Ni haki ya kila mtu kutoa sauti juu ya lile aliaminili kua sahihi hasa kama kitekelezwacho si sahihi. Sitta kutumia bunge kuunda CCJ hakuna ushahidi ila kutumia Bunge kuwapa changamoto CCM ni sahihi na hakuna anaelipinga kwani bila yeeye mirija ya RICHMOND AND THE LIKE INGEKUA INAENDELEA. Sina la kuongeza ila SITTA hana pa kushika hasa baada ya mafisadi kuchukua idadi kubwa ya wanaCCM.

Kibao kimemgeukia ila upepo huu ni mbaya kwake ila shukrani kwa kutoa haki kipindi akihudumu kama SPIKA.
 
Hivi ukitaka kuhama chama ni usaliti au dhambi?
Just asking................

Unakuwa usaliti pale unapokuwa upo ndani ya chama CCM akili yako CCJ

Lowasa aliwahi kusema kwamba wakati wao wanapiga kampeni za CCM 2010 Sitta na wenzake walikuwa busy kusajili CCJ nadhani ndio maana kwenye uspika walimchomoa.
 
Sitta lazima wamshabulie,mafisadi wanataka apotee na CDM inatumika bila kujijua,wanamsafishia njia mpinzani wao wa 2015.

Duuuuuuh. mzee hakuweka exit door au fallback procedures.sasa kawapush CDM wamwanike,katengeneza uadui na hivyo kujipunguzia nafasi ya kuja pumzika CDM au hata kupata ulinzi wa upinzani mara mambo yatakavyokuwa magumu ktk vita kuu ndnai ya CCM.Upo wapi huo uzoefu?wenzake wana tread na CDM with care na hivyo kupata spillovers.


Kiongozi makini anaweza tread na CDM kwa upole hata pale wanapomlipua bila kudhurika sana na baadaye maisha kwenda mbele.somewhere wananchi wanaweza wanaweza piga kura kwa vigezo zingine.


CDM hawatumiki ila 6 ni common enemy yeyote atakayemwadhibu kuna faida kwa miwngine.Na hivyo kuifanya iwe coincidence.Ni 6 mwenyewe kachanga karata vibaya pengine alidhani kuwa akiifanya hivyo ataweza wabomoa CDM, halafu katik Chama angetumia karata ya ufisadi.Ila hakupiga mahesabu vizuri.Kwani sasa hata CCM wenyewe tayari wana file la longtime.Na pia mpashaji anawema kuwa mzee 6 analalama tuu halafu hajatoa majibu.Hii nayo ni blow nyingine mbaya.Kwani mtu huna haki ya kukataa kilichopo wakati huna jibu.maisha hayawezi simama bila sababu kwa vile mtu nasema kitu hakifai.
 
Sita alichapwa?ah!ah!ahaaaaaa! Yaani na kujifanya linajua kila kitu kumbe pumbavu mpaka likachapwa?....Dr.slaa sio saizi yake aangaike sofia simba ndo saoizi zake.....mwendawazimu kweli...
 
sitaaaaaaaaaaaaaaa umezeeeeeeeeeeeka...kapumzke kijijini.....jamani huyu mzee sita kashachoka arud kijijin akalime yeye,na mitume plus nn walianzsha ccj wakaprve wrnggggg....sasa anatapatapa
 
Back
Top Bottom