Waliotandikwa viboko Ikulu hawa hapa

Mkuu najua Ben is not popular, hasa ukiangalia jinsi alivyoendesha privatization(na kujiuzia mgodi) na alivyo-foresee ufisadi, ana madoa mawili matatu ambayo ni makubwa sana kwenye rekodi yake, ambacho wengi tunakubaliana. Kitu ambacho ninamlaumu sana ni kuwa mwaka wa mwisho wa urais wake ni kama aliwazira watu aliokuwa anawaongoza. He looked like he was really looking forward to leaving the office, na kusema ngoja niachana na wajinga hawa. Alikuwa amezongwa sana na pressure ya mtandao kiasi kwamba akabaki na donge moyoni na akatuzira watanzania. He did not use the powers vested in him (kwenye chama na Serikali) kuandaa mwelekeo mzuri baada ya yeye kuondoka ofisini. That is why we are where we are now, and only God knows how we are going to get out of this quagmire.

Lakini ukiangalia performance yake in general utaona kuwa he was much much better than awamu ya pili na awamu ya tatu, in many respects. Hatuwezi kumlinganisha na awamu ya kwanza kwa kuwa it was different era and different politics. He was no saint, and some of us would be happy to see him in court, but that does not change the fact he had a better team and provided better leadership than the current one.
Sijui sifa za kiongozi kwa wadanganyiika lakini pengine hiyo much much better inasimamia mtu alopata F na point 24 badala ya 26..
 
Aliyechapwa viboko alikuwa ni Mwabulambo (RIP) Yeye alichapwa kwa kukaidi amri ya Mwalimu Nyerere ya kuwataka wanafunzi waombe msamaha ubalozi wa Uholanzi baada ya maandamano yao na kupindua na kupiga mawe motakaa ya ubalozi. Mwalimu aliwaita Ikulu kuwataka waombe msamaha. Kuna baadhi walikataa. Alipowauliza ni nani asiyetaka kuomba msamaha Mwabulambo akanyoosha mkono. Akaitwa na akamwamuru poliisi amchape viboko. I know this because the late Mabulambo was my friend.

Kuna mahali Blueray kasema Nyerere aliua mamilioni. Naomba atutajie hata watano tu kati ya mamilioni waliouawa na Nyerere.
halafu baadaye akampa madaraka kwenye serikali!!
 
halafu baadaye akampa madaraka kwenye serikali!!
Kuna mchapo alinipa marehemu Mwabulambo. Siku moja Julius ameenda ziara ya kikazi mkoani na miongoni mwa waliokwenda
kumpokea alikuwa ni Mwabulambo. Akamuuliza " na wewe uko hapa?" Wote wakaangua vicheko. Mwabulambo was funny (rip)
 
Kwako Bluray nakuelewa lakini jua hata mzazi kumchapa mtoto kwa nia nzuri ya kumrudi wengine watasema ni sawa wengine kama huko USA watasema huna haki mzazi mueleze tu zuri na baya yeye ataamua badala ya kumlazimisha kwa kumpa adhabu. Matokeo ya USA tunayajua.

La muhimu hapa ni kujiuliza kwa ujumla JKT ni kitu kizuri (yaani kwa maoni ya wengi siyo ya mtu mmoja, kama wewe pekee utasema ni kitu kibaya na wengi wanafikiri hivyo?). Shuleni masomo ni pamoja na malezi ya tabia na maadili mema. Kama wengi wanasema JKT ni kitu kizuri au hata kuwa si kitu kibaya basi tusimulaumu Nyerere maana alikuwa na anafanya kitu kizuri kwa nia nzuri.

Pia kumbuka ubaya wa tendo uko katika nia ya mtendaji.
 
-Kassim Hanga
-Sheikh Othman Sharif
-Dk. Kleruu

-Many of the villagization process victims where the bulk of this accusation is stemming from.Nyerere may not have killed a significant number of people directly, but his policies and mediocrity resulted in the deaths of so many, probably in the million range if not hundred of thousands. We may never know for sure the exact figure due to the nature of the secrecy of the era.

See Pratt, Cranford (1999). "Julius Nyerere: Reflections on the Legacy of his Socialism". Canadian Journal of African Studies 33 (1): 137 – 52. doi:10.2307/486390

acha kutudanganya dr kleruu aliuliwa na mkulima wa kawaida tu!tena akiwa nyumbani kwake na baada ya huyo mkulima kumuua dr kleruu alimpakia kwenye land rover akaburuza mwili mpaka kituo cha polisi na kujitaja mwenyewe kuwa amemuua dr kleruu!uliza wanaojua historia ya mji wa iringa watakwambia.
 
By Masatu
Hapana bana, binafsi nimeenda JKT 1990's utawala wa Mkapa. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!





Asante Mkuu (Keil) Uko makini sana nashukuru umeweka Sawa hapo chini....uongo wa masatu umeishia hapo...



Masatu punguza ushabiki kwa Mkapa ndugu yangu. Mkapa kaingia madarakani December 1995, wakati huo JKT kwa mujibu wa sheria hawakuwa wanaenda tena.

Nadhani intake ya mwisho iliyotumikia mwaka mzima ilikuwa ni 1992, baada ya hapo wakabadilisha mfumo wakasema sasa itakuwa miezi 6 badala ya mwaka mzima. Zilienda intake 2 au 3 za miezi sita sita na baada ya hapo hakuna intake yoyote iliyoenda.

Mwaka 1994 kulikuwa na tetesi kwamba mfumo wa mwaka mzima, lakini haikuwa hivyo na badala yake hawakwenda kabisa. Waliomaliza vyuo vya ngazi ya cheti na waliomaliza Form 6 baada ya mwaka 1994 hakuna aliyekwenda JKT kwa mujibu wa sheria.

Kwa hiyo utawala wa Mkapa (Dec 1995 - Dec 2005) hakukuwa na intake hata moja ya JKT. Labda kama unaongelea JKT ya kujitolea, lakini siyo ya mujibu wa sheria.

Kama ulienda JKT enzi za utawala wa Mkapa ilikuwa ni mwaka gani (specific year) siyo useme in 1990s, which is a general statement ili kutudanganya. Hata Mwinyi alikuwa madarakani mpaka 1990s, wewe unaongelea 1990s ya lini?

Wewe huwa unapenda watu waje facts, ninaomba niku-challenge uje na facts, sema ni mwaka gani ulienda, ulikuwa operation gani na ulikuwa kambi gani?
 
Nasikiaga hiyo JKT inaongezaga uzalendo eti. Hili huwa lina ukweli wajameni???

Aah wapi! hawa mafisadi wote wanaotusumbua sasa hivi wamepitia JKT. Na kama kuna mtu leo hii anaamini kuwa wanafunzi wakilazimishwa kwenda JKT basi tatizo la ukosefu wa uzalendo litaisha basi atakuwa ana matatizo makubwa sana kwenye uwezo wake wa kufikiri na kutafakari.
 
Hivi mtu aliecharazwa bakora na nyerere anakua amelaniwa au ujumbe gani tunaupata na somo gani? Je,nyerere was an angel?

Kwa inavyoonekana watanzania wengi tunasumbulia na suala la kiitikadi,kila anachofanya wa itikadi/kundi tofauti kiwe kizuri wengine wataona yaleyale, akifanya kitu kibaya wa itikadi/kundi lake utaona kinavyopambwa na wafuasi ili tu kionekane kizuri.

Kitu mhimu ni kupata uhuru wa kufikiri kila mmoja na si kufikiri kwa kupitia mtu fulani
By kilaza fulani.
 
I can equally say ukitaka kufahamu jinsi Mwalimu alivyokuwa dikteta wa one man show aliyeshindwa kuandaa leadership ya kuja kuchukua uongozi baada yake angalia uongozi wote baada yake.

Makosa ya Mwalimu ni kwamba aliondoka madarakani bila ya kutengeneza Taasisi Imara na Huru kimfumo ambazo zingetusaidia kuwadhibiti watawala wahuni na wezi ambao wamejaa ktk utawala wa sasa.
 
nimewasikia majina ya waliotandikwa viboko na mwalimu JKNyerere nao ni wawili mimi ninaowafahamu:-
Samuel Sitta.
Wilfred Mwabulambo.

I STAND TO BE CORRECTED.
 
Wanabodi naomba tu kufahahamishwa mpaka post no 92 kuna wachangiaji ambao kwa kweli ukisoma hoja zao kwa unafurahi lakini jamvini siku hizi hawaonekani apart from Mkandari, Nyani Ngabu, Jasusi and very few others. Nyie wakongwe hawa watu wameenda wapi? i really miss these guys kwenye hoja
 
Hii maneno niliwahi kusikia kitambo kidogo watu walikula viboko kwa kwenda mbele.Niliambiwa Samwel Sitta na Mark Bomani walikuwemo.
Sitta alikuwepo kati ya waliogoma,hizi ni habari za kuaminika;habari za kuaminika pia kuwa yeye alikuwa particularly stubborn. Kwa hiyo kama mtu yoyote alipigwa viboko,labda itakuwa ni Sitta. Lakini hii habari ya viboko bado sijaisikia hata siku moja.
 
Hapana. Mark Bomani hakuwemo. Wakati huo tayari alikuwa Attorney General.
Namfahamu mmoja tu, marehemu Mwabulambo. JKT iliuliwa enzi za Mwinyi.

Marehemu W.James Panjinga Mwabulambo hakucharazwa bakola kwa sababu ya kugomea National service yeye kweli akipata adhabu hiyo lakini kwa kushusha bendera ya muingereza[ Union Jack] wakati wa maanadamano ya wanafunzi kupinga UDI ya Rhodesia!!
 
Hapana bana, binafsi nimeenda JKT 1990's utawala wa Mkapa. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!

Kumbukumbu zangu za uhakika ni kuwa kweli JKT iliuliwa wakati wa Mwinyi maana mimi nilikuwa intake ya Pili kutoenda JKT mwaka Juni 1995 nikiwa Milambo High School. Wa kwanza kutoenda ni intake ya Nehemia Mchechu - Director wa NHC na wenzake kama Myenzi Mkurugenzi wa Haki za Binadamu. Kwa hiyo si wakati wa Utawala wa Mkapa!
 
Dah, kweli kizazi kipya kinajifunza sana kupitia hizi thread za kipindi hicho. Shukrani wanajamvi!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom