Wakaka: Ukiona nyani mjini ujue kaletwa

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,561
2,857
I greet you my elders!

Huo ni ujumbe mahsusi niliopatwa kupewa na kimwana mmoja mzuri, niliyedumu naye kwa kipindi cha miaka miwili katika mahusiano bila kujua kuna mwanaume mwenzangu alikuwa anaingia gharama juu yake nyuma ya pazia! Maneno hayo mazito mithili ya makontena yaliyo potea Bandarini yalipenya kwenye ngome za masikio yangu na kutua moyoni na kuniachia jakamoyo.

Huyu dada tulijuana kupitia kampuni yao iliyokuwa inafanya biashara na kampuni yetu kwa miaka kadhaa alikuwa na mtoto mmoja, aliniambia aliyezaa naye hayupo nchini, waliachana kabla ya kufunga ndoa, pia huyu mwanaume sio mtanzania hatarudi Tanzania.Baada ya mda mdada huyu aliacha kazi kampuni yao akafungia biashara yake mjini hapahapa jijini Dar.

Mda wote nipo naye tulikuwa wote maeneo tofauti ndani ya nchi hata nje ya nchi sikuwahi kufikiria kama ana mtu zaidi yangu, nilikuwa huru nyumbani kwake na baadhi ya ndugu zake.Hakuwahi kukubali wala kuomba hela toka kwangu zaidi kukubali zawadi
hela marafuku kote tulikokuwa tunaenda kwenye mitoko mimi ndo mlipaji kwa hela zangu pia sikuwa namtegemea kwa fedha.

Hatimae nikaja kugundua kuwa alizaa na boss wake katika kampuni alikokuwa anafanyakazi!Na ile biashara kafunguliwa na boss ndo anayehudumia
hata nyumbani kwa mdada huwa anaenda, mimi sikuwa napenda kwenda kwake.

Nilivyomuuliza kwanini hakuniambia ukweli akaniambia nilipaswa kutumia akili na kuelewa kuwa ''ukiona nyani mjini jua kaletwa, anamwenyewe''!Ngachoka
funzo ukiona dada anapendeza, hahitaji hela yako na anaendesha maisha yake bila msaada wako baadhi yao kunakuwana mwanaume mwenzio anawajibika.

Nilikaa pembeni, kumpisha boss aendelee na kuhudumia na kula mzigo.

Ushauri sio ibada wote mseme ameni, mengine niachie mwenyewe.
 
Siku moja tulikuwa tunataniana na mke wangu ndoa mbichi kabisa namwambia siku hizi baby wanawake wananitamani sijui nimebadirika nini? Au kwa sababu unanipikia vzr na kuning'arisha"
Alinijibu, wambie ukiona ngedere mjini ujue ana mwenyewe
Hahhhaaaaaa
 
La una roho ngumu ingawa bure aghali lakini kutelekeza mahusiano yasiyo gharama wala madhara naona kama umefanya dhambi. Akikutafuta usimzingue pakua mzigo. Kupenda hakuna hiari.
 
Vijana wengi wakigundua mwanamke anajiweza na yupo na mtu anamfinance hugeuza mapenzi hayo kuwa fursa ya ajira yaani atafanya kila wawako faragha kuakikisha jimama achomoki ..na baada ya mda sound zinakuja kama mvua...
 
Bob Luse; naona una experience ya kutosha kwa haya maisha..........
 
Bob Luse; naona una experience ya kutosha kwa haya maisha..........
I have seen it all Jerrytz.sionagi jipya siku hizi.ndo maana natoa ushauri kwa wale ambao hawajapitia huko na ikiwa wanamasikio wakamate darasa!
 
Siku moja tulikuwa tunataniana na mke wangu ndoa mbichi kabisa namwambia siku hizi baby wanawake wananitamani sijui nimebadirika nini? Au kwa sababu unanipikia vzr na kuning'arisha"
Alinijibu, wambie ukiona ngedere mjini ujue ana mwenyewe
Hahhhaaaaaa
vilivyotunzwa vina tbs lazima vipendwe.
 
La una roho ngumu ingawa bure aghali lakini kutelekeza mahusiano yasiyo gharama wala madhara naona kama umefanya dhambi. Akikutafuta usimzingue pakua mzigo. Kupenda hakuna hiari.
Siwezi kula sahani moja na mwanaume mwenzangu huku najua yupo! vimwana wa viwango mbona wapo!.nafuu niwe napigwa mizinga najua niko peke yangu.kuliko bure kumbe kuna mwenza.
 
Back
Top Bottom