Mchungaji Mgogo "Ukiona Mwanaume Hachepuki Basi ujue kuna Mawili"

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,495
99,293
Mchungaji maarufu kutoka Tanzania, Daniel Mgogo ameorodhesha sababu mbili kuu ambazo zinaweza kumfanya mwanaume asimsaliti mpenzi wake katika ndoa na kuchepuka.

Katika video ambayo Mgogo alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, alielezea sababu kuu ambazo zinawafanya wanaume wengi kutulia kwenye ndoa na wake zao.


Moja ya sababu ambayo Mchungaji Mgogo alitaja ni kuwa na hofu ya Mungu au wale ambao hawana pesa, aghalabu huwa watulivu sana kwenye ndoa zao na uaminifu kwa wake zao huwa katika kiwango cha haiba iliyotukuka.


“Ukiona mwanamume ana mke mmoja na ametulia naye, ni mambo mawili tu yamemfanya kutulia; moja dini imemuingia sana kiasi kwamba anaogopa kukengeuka na sababu ya pili ni hana hela,” Mgogo alisema.


Mchungaji huyo alisema mwammume yoyote anaweza kupitia changamoto za kujaribiwa na wanawake, wakiwemo wachungaji kanisani pia.


“Hata sisi wachungaji hupitia majaribu kama hayo kwa sababu mle kanisani kuna mabinti wengi ambao hawajaolewa, kwa hiyo usipokuwa na kujihimili mwenyewe, unaenda na maji. Dhambi hii haijali wewe ni mchungaji wewe ni mshirika, almaradi wewe ni kiumbe itakupata tu,” mchungaji huyo alieleza.


Mchungaji huyo alimaliza akisema kwamba kwa kawaida mwanamume ni kiumbe kisichoridhika.


Wiki chache zilizopita, mchungaji huyo pia alisema kuwa wanawake wengi wanaishi maisha marefu kuliko wanaume kwa sababu wao ni viumbe wanaopenda kuzungumza sana.


Mgogo alisema kuwa kitendo cha wanawake kuongea hutoa sumu miilini mwao wakati wanaume wengi hujinyamazia na shida zao na hilo huzaa sumu miilini kusababisho vifo vyao mapema

NINI MAONI YAKO?, Nawasilisha
 
Naunga mkono hoja

Yani kama mimi nimetulizana kisa sina hela tu
Nikizipata.......... 😁😁
 
“Ukiona mwanamume ana mke mmoja na ametulia naye, ni mambo mawili tu yamemfanya kutulia; moja dini imemuingia sana kiasi kwamba anaogopa kukengeuka na sababu ya pili ni hana hela,” Mgogo alisema.
Mkuu, Mchungaji amesahaua mambo mengine yanayofanya mwanaume atulie.

Kuna Wanaume wana ugonjwa wa Sunk-cost fallacy. hawa ni wale wanabakia na kutulia na Mwanamke mmoja wakiteseka na kushindwa kumuacha kwasababu ya kuogopa kupoteza vitu walivyowekeza. Aina hii ya Wanaume jamii husema WAMELOGWA.

Na Mchungaji amesahau pia kuna Wanaume ambao wao ni One at a Time. Yaani wanatulia na mwanamke mmoja hadi pale watakaposhindwana ndio wanatafuta Mwingine. Hawa wanafocus na maisha na sio Mapenzi.

KUKOSA HELA hili napingana nae. Ukiwa huna hela utawakosa MALAYA tu wa mjini, ila Wanawake utawapata.
 
I mean no malice to nobody
FB_IMG_17083680782606174.jpg
 
Back
Top Bottom