Msaada tutani; Nina hali ngumu sana, nisaidieni kazi niweze kujikwamua

ngungwangungwa

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
642
554
Ndugu zangu,

Wanajamvi, umofia kwenu,

Ndugu zangu me ndugu yenu nimezingirwa nipo katikati ya maisha na mbinguni.

Naomba nijieleze kidogo.

Ndugu zangu me member hapa tangu mwaka 2013, ni zaidi ya miaka 10 sasa. Tangu niwe hapa sijawahi kulumbana na mtu, kugombana, kumfanyia fitina au kumtapeli mtu yeyote. Kama kuna yeyote niliwahi kumfanyia chochote kibaya iwe hapa au kwingineko anaweza kuniumbua hapa.

Ndugu zangu me nilioa tangu mwaka 1998 nikiwa mkoani.. Baadae mwaka 2007 nikahamia dar kutafuta maisha zaidi na wakati huo tayari tulikuwa tumejaaliwa watoto 3. Mambo hayakuwa km nilivyotarajia, mambo yalikuwa magumu haswa lkn km mwanaume nilipambana kuhakikisha maisha yanaendelea.

Nilijtafuta mpakaa kufikia mwaka 2010 mambo ndo yakaanza kukaa vyema..! Biashara niliyokuwa nafanya wakati huo iliniendea vizuri sana! Kiufupi kuanzia huo mwaka 2010 mpaka 2017. Nilikuwa nimefanikiwa kwa kiasi ukilinganisha na nilikotoka...mwaka 2014 nilifanikiwa kununua sehemu iliyokuwa na slop mbili.. Moja ya vyumba 3 na nyingine ya vyumba 2. Kwa milioni 14 na bank nilikuwa na zaidi ya milioni 30.

Mwaka 2015 nikaibomoa ile slop ya vyumba 3 nikaanza kujenga nyumba kubwa.. Ile slop ya vyumba 2 nikaiacha.. Nilinyanyua nyumba ya vyumba 3 vya kulala.. Nyumba ilikamilika ujenzi wake mwaka 2017...lkn iliniacha nikiwa nimefilisika.. Pesa zilikata na biashara nikafunga.

Baadae mwaka 2018 kuna tajiri mmoja akaniajiri kusimamia maduka yake.. Posho yake haikuwa kubwa lkn ilikuwa inatosha kuhudumia familia.. Biashara ile nilijtahidi kui-manage vizuri na kusema kweli ilikuwa inaendelea vizuri na tajiri nilikuwa naelewana naye sana! Tatizo lilikuwa watoto wake, walianza kuniingilia sana kwenye majukumu yangu.. Wanachukua vitu hawalipi, wanawanyanyasa wauzaji.. Kwa ustaarabu na heshima niliyokuwa nayo na Yule mzee nikaamua kuacha kazi..

Mwaka 2019 mwishoni akanibembeleza yule tajiri akanipeleka mkoani kwenda kusimamia ujenzi. Nikaenda, kule nikasimamia majengo matatu ya nyumba za kulala wageni na jengo moja la kupangisha. Nilisimamia mpaka kuanzisha hizo biashara mpaka zilipoanza ndo nikarudi kwangu mwaka 2021. Kipindi chote nikiwa huko pesa yote nilikuwa namtumia mke wangu atunze na zingine afanye matumizi...yaani nilikuwa hata nikipata laki 4 me ntabaki na elf 40 nyingine yote natuma nyumbani ili watoto wangu na mke wangu wasiteseke.

Niliporudi nyumbani kulikuwa na mabadiliko makubwa kwa mke wangu.. Kuanzia nidhamu, na hakukuwa na akiba ya pesa hata 500. Nilivyoona hayo mabadiliko nikaanza kufanya uchunguzi, nikagundua mke wangu ana uhusiano usiofaa na mwanaume mwingine.

Nikambana akakubali na kukiri nilimsamehe ingawa nilikuwa na maumivu makali Sana! Lkn msamaha wangu haukuwa na maana kwake, ndo kwanza alijiimarisha huko kwa huyo kijana.. Kumbuka wakati huo tulikuwa na watoto 5.

Nikaanza kuwindwa mm either nipotezwe au nitafutiwe kesi nikafungwe.. Na jaribio la kutaka kufungwa likafanyika kwa kusingiziwa kuiba hela za mke wangu.. Nikapelekwa police nikalazwa mahabusu kwa siku 6 baadae mahakamani.. Nashukuru mahakamani haki ilisimama upande wangu nikashinda.

Baada ya kesi ile sikutaka tena kuendelea kuishi hapo nyumbani.. Nikabeba suruali zangu na hati yangu ya nyumba nikaondoka nikaanza mchakato mpya kabisaa wa maisha km kijana anayebalehe. Tangu niondoke hapo kwangu mwezi October mwaka 2021, sijawahi kukanyaga hapo nyumbani kwangu wala kuongea na huyo mwanamke. Watoto huwa nawafuata shuleni kwenda kuwaona na kuwasaidia nnachoweza.

Nimekaa single tangu wakati huo.. Mwaka jana nilipata shida ya kuumwa jicho na madaktari walihisi ule uvimbe unaweza kuwa saratani.. Kwa kuogopa saratani kuna mdada nilikuwa nadate naye.. Nikamuomba aje tuishi pamoja..nikihofia naweza kufa kibudu.. Mwezi wa 11 mwaka jana akaja tukaanza kuishi pamoja..!

Baadae baada ya vipimo sikuwa na saratani nilikuwa tu na kidonda katikati ya jicho.. Siku ya tarehe 12 mwezi huu yaani jtatu iliyopita. Niliitwa shuleni kwa mtoto wangu anayesoma kigamboni..! Nimeondoka nyumbani tukiongea vizuri tu na mwenzangu...wakati nashuka kwenye gari kuelekea shule kwa mtoto kuna dogo pale nnapoishi akanitext akaandika tu father.. Me nikampigia. Akaniuliza mbona umehama kimyakimyaa..!? Nikashangaa kuhama ki-vp!? Akaniambia huyu mama mbona ameleta toyo hapa na amepakia vitu na kuondoka!?

Nikamwambia mwizi huyo chukua bodaboda umzuie. Dogo hakufanikiwa.. Nikajaribu kumpigia yeye yule mwanamke hakupokea na baadae akazima kabisaa simu mpaka leo.. Me nikaenda shule kuongea na mkuu wa shule akaniruhusu nirudi Kwanzaa kupambana na hili.. Maana kichwa hakikuwa sawa.

Niliporudi nyumbani alikuwa amebeba kila kitu cha maana.. Hela yote ya akiba tuliyokuwa nayo ndani.. Vyombo, kitanda na godoro, gas, TV mpaka na king'amuzi. Yaani aliacha kabati tu la nguo..!!

Ndugu zangu nimekuja hapa kwa dhati kabisaa ya Moyo wangu mnisaidie nisidhalilike. Hivi nnavyoandika tangu asbh sijakula chochote nimejikuta mpaka natamani kujiua kwa magumu na mawazo niliyopitia hizi siku chache kuanzia Jumatatu.

Nisaidieni kibarua japo nipate vyombo na gas pamoja na chakula wakati nikijaribu kujitafuta tena! Nina hali ngumu sana na ninajichukia!

Naomba atakayewiwa anaweza kunisaidia kibarua kwa number 0755385918.

Natanguliza shukrani.
 
Pole sana ndugu yangu nakupa pole huku na mm nikiwa napitia changamoto za kimaisha lkn ulifanya makosa kukimbia nyumba km kweli uliijenga kwa jasho lako mwenyew.

Kama hati iko na jina lako fukuza huyo mwanamke,mwanamke msaliti msamehe lkn hafai ht kuishi pamoja kwamaan mwanamke akishaonjeshwa dudu huko tena ww ukiwa labd sio mtundu wa mambo ni ngumu sana kuvunja hayo mahusiano dudu ilishamkolea.

Yan kile kile kipind ungerud om na kufukuza huyo bibi hapo om aondoke usiangalie umezaa nae watoto wangp hiyo sio tija bali kumbuka hakuw na nia nzur juu yk au km vipi ungemchapa matukio mpk yeye akimbie

Bado una nafas kubw katika maisha usikate tamaa na usiombee kufa mm nakuelewa vyema hizo mambo tumeyapitia mkuu najua yanaumiza sana najua kiumri umenizid ila nina jambo la kukushaur km mwanaume mwenzio PAMBANA KAKA MM SINA CHA KUKUPA KIFEDHA ILA NTAKUOMBA MOLA AKUFANYIE WEPESI ILA USIPENDE KUISHI KIUNYUMBA NA WANAWKE WA KUOKOTA MATOKEO YAKE NI HAYO KUKUIBIA NA KUSEPA

POLE SANA YATAISHA YOTE AMIN MUNGU NA UMTEGEMEE PIA FANYA SANA IBADA WW NI MUISLAM AU KM MKRISTO BHS HUDHURIA MAKANISA YA KWEL NA UWE NA IMANI MOYON NAKUHAKIKISHIA YATAISHA
 
Wewe ni karibia ningekuita baba lakini najikuta nakudharau kwa mambo fulani.

Unampaje mwanamke hela zote au nyingi akutunzie?

Uliporudi nyumbani ukakuta mabadiliko ya kipumbavu uliyavumiliaje badala ya kuchukua hatua nzitonzito?

Ulipokimbia nyumbani wakati huohuo mke wako mliyeishi miaka mingi kakupotezea hela nyingi na kaanzisha mahusiano na kijana ulikuwa na maana gani?

Unataka tukuonee huruma wakati unatia hasira kulikoni?

Yani wewe mzee hata ukiwaeleza watoto wako wanaokupendahali halisi watapandwa na hasira na kujiuliza huyu ni baba gani?

Yani unakomaa huko kwenye kazi za kuajiriwa unamtumia mama mshahara wote alafu urudi nyumbani ukute mauzauza tena anagawa nje alafu badala utumie mamlaka yako unaamua kukimbia nyumbani, serious tena anaenda kutafuta mwanamke mwingine uishi nae?

Pumbav
 
Nadhani hata wewe mwenyewe huelewi ulichoandika.. Umewafikiria watoto wangu 3 ambao walikuwa bado wadogo na wapo shule!? Unadhani ningemfukuza mama yao angeondoka tu na kuridhika kufukuzwa kwake!? Niliangalia sana maisha ya wanangu.. Mwanamke hata akiwa Malaya lkn atajali kuhusu watoto wake.

Nilimuacha hapo ili kuweka utulivu wa wanangu.. Na wanaendelea vyema! Lkn nashukuru kwa maoni yako.
 
Mwanaume ndiyo mtawala ila sasa hivi wanawake wanataka kuwa watawala.
Ulipo ondoka pale nyumbani ulimuacha mkeo atawale sababu alipanga kutawala na wewe ukawa rahisi sana kumuacha atawale kwahiyo akaona ame win game.
Rudi nyumbani aisee umekosea kuondoka na kumuachia nyumba.
Ukisha jua adhma ya adui yako usi muache ashinde vita kirahisi rahisi kwa kususa.
Rudi nyumbani ndugu tena kwa hasira zote,anzisha vurumai mpaka alielewe somo.
Huku nje maisha magumu ndugu.
Pole sana mkuu.
 
Ndugu zangu,

Wanajamvi, umofia kwenu,

Ndugu zangu me ndugu yenu nimezingirwa nipo katikati ya maisha na mbinguni.

Naomba nijieleze kidogo.

Ndugu zangu me member hapa tangu mwaka 2013, ni zaidi ya miaka 10 sasa. Tangu niwe hapa sijawahi kulumbana na mtu, kugombana, kumfanyia fitina au kumtapeli mtu yeyote. Kama kuna yeyote niliwahi kumfanyia chochote kibaya iwe hapa au kwingineko anaweza kuniumbua hapa.

Ndugu zangu me nilioa tangu mwaka 1998 nikiwa mkoani.. Baadae mwaka 2007 nikahamia dar kutafuta maisha zaidi na wakati huo tayari tulikuwa tumejaaliwa watoto 3. Mambo hayakuwa km nilivyotarajia, mambo yalikuwa magumu haswa lkn km mwanaume nilipambana kuhakikisha maisha yanaendelea.

Nilijtafuta mpakaa kufikia mwaka 2010 mambo ndo yakaanza kukaa vyema..! Biashara niliyokuwa nafanya wakati huo iliniendea vizuri sana! Kiufupi kuanzia huo mwaka 2010 mpaka 2017. Nilikuwa nimefanikiwa kwa kiasi ukilinganisha na nilikotoka...mwaka 2014 nilifanikiwa kununua sehemu iliyokuwa na slop mbili.. Moja ya vyumba 3 na nyingine ya vyumba 2. Kwa milioni 14 na bank nilikuwa na zaidi ya milioni 30.

Mwaka 2015 nikaibomoa ile slop ya vyumba 3 nikaanza kujenga nyumba kubwa.. Ile slop ya vyumba 2 nikaiacha.. Nilinyanyua nyumba ya vyumba 3 vya kulala.. Nyumba ilikamilika ujenzi wake mwaka 2017...lkn iliniacha nikiwa nimefilisika.. Pesa zilikata na biashara nikafunga.

Baadae mwaka 2018 kuna tajiri mmoja akaniajiri kusimamia maduka yake.. Posho yake haikuwa kubwa lkn ilikuwa inatosha kuhudumia familia.. Biashara ile nilijtahidi kui-manage vizuri na kusema kweli ilikuwa inaendelea vizuri na tajiri nilikuwa naelewana naye sana! Tatizo lilikuwa watoto wake, walianza kuniingilia sana kwenye majukumu yangu.. Wanachukua vitu hawalipi, wanawanyanyasa wauzaji.. Kwa ustaarabu na heshima niliyokuwa nayo na Yule mzee nikaamua kuacha kazi..

Mwaka 2019 mwishoni akanibembeleza yule tajiri akanipeleka mkoani kwenda kusimamia ujenzi. Nikaenda, kule nikasimamia majengo matatu ya nyumba za kulala wageni na jengo moja la kupangisha. Nilisimamia mpaka kuanzisha hizo biashara mpaka zilipoanza ndo nikarudi kwangu mwaka 2021. Kipindi chote nikiwa huko pesa yote nilikuwa namtumia mke wangu atunze na zingine afanye matumizi...yaani nilikuwa hata nikipata laki 4 me ntabaki na elf 40 nyingine yote natuma nyumbani ili watoto wangu na mke wangu wasiteseke.

Niliporudi nyumbani kulikuwa na mabadiliko makubwa kwa mke wangu.. Kuanzia nidhamu, na hakukuwa na akiba ya pesa hata 500. Nilivyoona hayo mabadiliko nikaanza kufanya uchunguzi, nikagundua mke wangu ana uhusiano usiofaa na mwanaume mwingine.

Nikambana akakubali na kukiri nilimsamehe ingawa nilikuwa na maumivu makali Sana! Lkn msamaha wangu haukuwa na maana kwake, ndo kwanza alijiimarisha huko kwa huyo kijana.. Kumbuka wakati huo tulikuwa na watoto 5.

Nikaanza kuwindwa mm either nipotezwe au nitafutiwe kesi nikafungwe.. Na jaribio la kutaka kufungwa likafanyika kwa kusingiziwa kuiba hela za mke wangu.. Nikapelekwa police nikalazwa mahabusu kwa siku 6 baadae mahakamani.. Nashukuru mahakamani haki ilisimama upande wangu nikashinda.

Baada ya kesi ile sikutaka tena kuendelea kuishi hapo nyumbani.. Nikabeba suruali zangu na hati yangu ya nyumba nikaondoka nikaanza mchakato mpya kabisaa wa maisha km kijana anayebalehe. Tangu niondoke hapo kwangu mwezi October mwaka 2021, sijawahi kukanyaga hapo nyumbani kwangu wala kuongea na huyo mwanamke. Watoto huwa nawafuata shuleni kwenda kuwaona na kuwasaidia nnachoweza.

Nimekaa single tangu wakati huo.. Mwaka jana nilipata shida ya kuumwa jicho na madaktari walihisi ule uvimbe unaweza kuwa saratani.. Kwa kuogopa saratani kuna mdada nilikuwa nadate naye.. Nikamuomba aje tuishi pamoja..nikihofia naweza kufa kibudu.. Mwezi wa 11 mwaka jana akaja tukaanza kuishi pamoja..!

Baadae baada ya vipimo sikuwa na saratani nilikuwa tu na kidonda katikati ya jicho.. Siku ya tarehe 12 mwezi huu yaani jtatu iliyopita. Niliitwa shuleni kwa mtoto wangu anayesoma kigamboni..! Nimeondoka nyumbani tukiongea vizuri tu na mwenzangu...wakati nashuka kwenye gari kuelekea shule kwa mtoto kuna dogo pale nnapoishi akanitext akaandika tu father.. Me nikampigia. Akaniuliza mbona umehama kimyakimyaa..!? Nikashangaa kuhama ki-vp!? Akaniambia huyu mama mbona ameleta toyo hapa na amepakia vitu na kuondoka!?

Nikamwambia mwizi huyo chukua bodaboda umzuie. Dogo hakufanikiwa.. Nikajaribu kumpigia yeye yule mwanamke hakupokea na baadae akazima kabisaa simu mpaka leo.. Me nikaenda shule kuongea na mkuu wa shule akaniruhusu nirudi Kwanzaa kupambana na hili.. Maana kichwa hakikuwa sawa.

Niliporudi nyumbani alikuwa amebeba kila kitu cha maana.. Hela yote ya akiba tuliyokuwa nayo ndani.. Vyombo, kitanda na godoro, gas, TV mpaka na king'amuzi. Yaani aliacha kabati tu la nguo..!!

Ndugu zangu nimekuja hapa kwa dhati kabisaa ya Moyo wangu mnisaidie nisidhalilike. Hivi nnavyoandika tangu asbh sijakula chochote nimejikuta mpaka natamani kujiua kwa magumu na mawazo niliyopitia hizi siku chache kuanzia Jumatatu.

Nisaidieni kibarua japo nipate vyombo na gas pamoja na chakula wakati nikijaribu kujitafuta tena! Nina hali ngumu sana na ninajichukia!

Naomba atakayewiwa anaweza kunisaidia kibarua kwa number 0755385918.

Natanguliza shukrani.
Pole Sana ndugu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom