Nimepitia mengi toka 2013 kwa kufupisha fupisha story hii mpaka 2023

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
424
1,044
Mwaka 2013 nilipata kazi kwenye kampuni moja katika branch yake Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu, sasa basi maisha yalianza kwa kufanya kazi kwa sababu sikua najua chochote ilibidi nijifunze kupitia kwa yule niliyemkuta ndio alinipa uzoefu sababu yeye alikuwa kanitangulia na anajua vingi kuhusu kazi.

Nilianza na mshahara wa Tsh100,000/= hapo nile nivae ninunue viwalo vingine vya kubadilisha kazini na hela nyingine niweke kama akiba na nyingine nitume kama matumizi nyumbani maana kama unavyofahamu familia zetu hizi tumezaliwa tukakuta wazazi hawajajitafuta.

Nilikomaa kibishi bishi hivyo hivyo mshahara ukitoka naenda kutoa kama elf 70,000 naigawanisha nyingine natuma home elf 30 iliyobakia bank naiacha kama akiba matokeo yake kabla hata mwezi haujafika katikati nimeishiwa inabidi niifate ili inisaidie kumalizia mwezi au inaweza ikaisha kabisa nikawa naenda kukopa mshahara ukitoka narudisha mambo yanakaa vizuri.

Katika kufanya kazi kwangu kote sikuwahi kuwa na tamaa ingawa kampuni niliyokuwa nikifanya kazi ilikuwa ni kucheza na hela muda wote nikama bank unapokea na kutoa ila sikuwahi kuwa na vishawishi nidokoe au nisepe na hela kama wengine walinitangulia walivyokuwa wakifanya.

Niliendelea

kufanya kazi kwa miezi takribani 6 sikuongezewa Salary yaani mshahara haukuongezeka wala kupanda kulingana na pesa niliyokuwa nachukua haikuwa inatosheleza Maisha na life langu muda huo ni mimi tu ndio nalijua. Kuna muda nilitamani niache kazi nirudi kufanya vibarua vyangu nilivyozoea maana kabla hapo mimi nilikuwa fundi.
  1. Viatu yaani shoeshine
  2. Fundi seremala
  3. Fundi ujenzi na kupaua nyumba,
Pia nilikuwa mtu nisiyeacha kazi yeyote ikatize ilikuwa nifursa kwangu, baada ya kupata haka kamchongo nikasema maisha si ndio haya sasa ngoja nikomae kumbe nakomazwa kiakili na πŸ˜† πŸ˜„ Kiukweli kuna muda nilikuwa nakata tamaa ila najipa matumaini nikiangalia waliofanya ile kazi wapo vizuri na mimi najipa moyo ipo siku na maisha lazima yaendelee.

Sasa basi changamoto iliyokuja ni vihela vidogo vidogo vilivyokuwa vikipotea na kunifanya nikate tamaa zaidi maana ukizingatia Ofisini tupo wawili tu. Na anayeulizwa na anayetoa taarifa au report ni yule niliyemkuta kasheshe ndio ilipokuwa, ikitokea mimi nikiulizwa mbona kuna upotevu wa hela ndogondogo hauishi hapo? Nachojibu mimi sihusiki maana sina tabia hiyo ya wizi au udokozi.

Siku moja boss akaja Tawi letu kufunga hesabu sasa alipomaliza akaanza kuninanga na kuniambia maneno ambayo mpaka kesho au haitatokea siku nikayasahau maana ni maneno ambayo nilisema ni kama yananichochea kupambana zaidi ila ni vile sikusoma.

Baada ya hapo zikapita wiki 2 nikapata uhamisho nikapangiwa kituo kingine Mkoa wa Kigoma huko nilipoenda boss akaniambia unajua sikuile nilipokuwa huko niligundua kitu na kukuhamisha kwako kutoka pale, nataka nione hii tabia unayo??

Baada ya hapo boss aliniambia wewe fanya kazi, hayo mengine achana nayo familia inakutegemea na wewe unatafuta maisha, kwa hiyo katika utafutaji wako lazima utakutana na mitihani mingi hivyo usione ndio kikwazo cha kukukwamisha usisonge mbele.

Baada ya hapo siku zilienda ila mimi huwa siyo mtu wa kuambiwa maneno matamu nikaamini niliangalia yale mazito nikayapaki moyoni na nikaacha yale ambayo sioni yana madhara ila yale yakuchomo aloyoniambia nikiwa Maswa sikuyaachilia huko huko nilitembea nayo mpaka leo hii.

Kazi yangu Kigoma ilikuwa nzuri nilifanya kazi kwa bidii ila changamoto tena ikaja, mtu niliyempokea Maswa nimekuja kumkuta Kigoma akiwa hana muda kazini kanizidi mshahara na mimi niliyemtangulia niko chini yake ukizingatia hata kazi namzidi.

Baada ya miezi 2 baadae nikaja kupanda nikapata mshahara wangu wa Tsh 150,000 kwa mara ya kwanza hapo ni mwaka 2015 toka nimeanza kazi. Nilifurahi ila sikuwa na furaha kama mtu ambae alistahili kulipwa vile. Yule niliyemkuta aliongezewa na kufika 250,000 mimi nikiwa 150,000 sikuwa na kinyongo nilifanya kazi bado kwa bidii bila kushikwa na tamaa wala vishawishi vyovyote vile maana Ofisi ile ni ya hela muda wote unashika hela na kutoa hela ni kama bank tu.

Kwa hiyo tamaa ni nje nje unaweza pewe milioni 25 au hadi 30 peleka Bank kama ni mtu wa tamaa unapita nazo haijarishi ni ndugu unayemfanyia kazi au mtu baki ila ukiweza kuzuia tamaa wewe umekomaa katika utafutaji.

Baada ya mwaka na miezi 4 boss akatukalisha kikao mimi na yule jamaa tuliyekuwa tukifanya nae kazi, mada yake alikuwa anataka mtu mmoja kati yangu na yule jamaa ambae ataenda branch nyingine kuongeza nguvu maana huko anakotaka kumpeleka mmoja kati yetu aliyekuwepo ameiba kama milioni 2.5+ sasa anataka amtoe bila ya yeye kujua.

Sasa kikao chetu kikawa cha dakika kama 5 hadi 9 kujadili nani aondoke nani abaki, boss mwenyewe akasema wote najua utendaji wenu na mimi anajua zaidi utendaji wangu maana hata tuhuma zangu za kutoka Maswa nimebaini siyo za kweli akasema katika mitego yangu yote sijakunasa maana anasema alikuwa anaweka hela ya ziada kwenye droo akijua nikifunga hesabu na ile pesa isipozidi atajua fika huyu alikuwa anamchezo huo toka akiwa Maswa baada ya hapo akasema sijafanikiwa kubaini chochote kwa hiyo naomba unisamehe na mimi nilikuwa naambiwa na dada yangu hivyo nilivyokaa na wewe hapa karibu ndio nimegundua huna mkono wa wizi.

Hata hivyo akasema nashindwa kuteua kati yenu nani aenda Misungwi kwa sababu wote mnafanya kazi nzuri hivyo nawapa muda mjiteue nani aende Misungwi mkielewana nyie wenyewe mniambie nimkatie ticket kabisa kwa ajili ya safari ya siku inayofuata.

Baada ya hapo tulibakia wawili mimi na yule jamaa nikasema ngoja nienda ingawa niliona yule jamaa hakuwa amekubaliana yeye kutoka Kigoma kwa hiyo mimi ni kasema popote kambi ngoja niende.

Nilipofika kwa maelekezo niliyopewa niliyafanyia kazi, kiukweli nilikuta Ofisini iko taabani haikuwa na uongozi na wateja wanalipa wanavyotaka wengine wanadhurumu hawarudishi hela hivyo jukumu la kwanza nilifanya ofisi iheshimike na kingine nilikusanya madeni na kuiweka ofisi katika hali ya heshima.

Huo ulikuwa mwaka 2015 mwezi wa 4. Baada ya muda nikapanda dau nikapanda cheo kutoka accountants mpaka MenejaπŸ˜€ ila yule wakule sikuwa na mzidi Mshahara bado aliendelea kuwa juu yangu πŸ˜€.

Mshahara wa mwisho ulikuwa laki 530000 mwaka 2017 niliupokea kama miezi 3 hadi 4 nilikuwa nimejipanga sasa hapa nianze kujenga home sasa kwa haka kamsharaha πŸ˜€ kumbe nawaza huku mipango haiungani na mimi πŸ˜€ baadae shot ofisini haziishi mara mteja hela yake imepotea yaani ni vurugu tu. Kwa sababu mimi ndio mkubwa wa branch ile na nikimpa taarifa boss hanipi ushirikiano kwa sababu vijana niliokuwa nafanya nao kazi niligundua sio waaminifu, anasema hayo mimi siyajui daaah nikisikia hivyo nachoka kabisa. Ikawa kila nikitaka kufanya namna nitoke inashindikana.

Siku moja alikuja Misungwi mwezi 12 mwaka 2017

Alipokuja aliniambia anataka afungue Ofisi kama ile ila kwa sasabu ameona utendaji wangu hivyo hana wasiwasi juu yangu. Kampuni hiyo itatumia jina lingine kwa usajiri wa jina ambalo ataona linafaa. Nilikubali kwa sababu niliona kama huu ndio muda wa mimi kutoka sasa maana hapo toka nimefanya kazi ni miaka 5 sasa au 4 sina chochote.


Nilikuwa sina chochote kwa sababu, mimi kwetu ndio nimepata kazi na mimi kwetu ndio tegemeo mahitaji yote ya msingi niliona niyasimamie kwa sababu maisha yetu ya pale nyumbani mimi ndio ninayajua.

Nikikusimlia hapa huwezi amini kwa hii familia iliwezaje kuishi maisha yale na tulipona ponaje na mitihani ile? Kuna muda tulikula mabaki ya chakula cha ngurue ili kujinusuru na njaa na mengine siwezi kuyaongea yote hapa.

Hivyo baada ya kupata kazi niliona sitaweza kula mwenyewe, nitakula na mama yangu ili nae aone aliyemzaa hajasahau na hajamsahau mzaa chema.

Tuendelee...
Baada ya hapo boss alinipa ruhusa ya siku 4 hadi 7 maximum kama wiki hivi nikasavei sehemu ya kuweka Ofisi, safasi ya kwanza nilienda Muleba baadae nikaenda Biharamulo pale nilipata chumba na kulipia kabisa kwa mwaka mzima.

Baada ya hapo nikarudi Mwanza kwa boss tulipokutana kwake Mwanza tukaja nae moja kwa moja mpaka Misungwi, nikamkabidhi ofisi yake kila kitu tuliangalia kipo salama sina deni nae pesa yote kama milion 25 nikamhamishia kwenye Account yake na mimi sikuwa na mdai chochote, siku hiyo hiyo tukarudi nae Mwanza akanisaidia na kubebe na vilago vyangu πŸ˜€πŸ˜€

Baada ya kufika Biharamulo tukafungua ofisi, wiki ya kwanza mwezi hatuna mteja hata mmoja πŸ˜€πŸ˜€ ikabidi tuhamishe ofisi πŸ˜€ kwenda Bukoba mjini, hapa tulikuwa na mpwa wake na boss yaani mtoto wa dada yake na boss yeye ndio nilipewa nifanye nae kazi kamaliza shule kafeli uncle wake kaona ili mtoto wa dada yake asiteseke bora amfungukiee biashara.

Kumbuka dogo mwenyewe alikuwa mayai siyo mtoto aliyepitia shida wala hajui shida ilivyo. Nitakuja kukupa kisa baadae kwa nini nasema haya kwamba dogo ni mayai na hajui shida.

Baada ya kufika Bukoba tukapangisha chumba cha biashara maeneo ya Bank ya kaitaba kama ni mwenyeji Bukoba ukiwa Kituo cha police station kwa nyuma yake hapo. Ndio tulipokuwa na ofisi imeandikwa MJOMBA INVESTMENT COMPANY LIMITED.
IMG_20180416_184056.jpg

Hii pikipiki ni yetu na hapo ndio Ofisini, Nyuma ya kituo kikuu cha Police Bukoba.

Hilo jina au kampuni ya hili jina lilisajiliwa kwa sababu kulikuwa na wapwa wa boss wa wili mmoja wa kike mmoja wa kiume ambae tulikuwa nae wa kike alikuwa kwenye ofisi yake nyingine Kakonko. Tulitangulia sisi ili ofisi ikikomaa na yeye aje tuungane nae.

Tulipofika Bukoba hali haikuwa nzuri kama tulivyotarajia, maana biashara ilikuwa ngumu wateja hamna na ukizingatia tuna muda wa miezi si chini ya 5 hatujafanya mzunguko nikutumia hela tu.

Hali ikawa mbaya zaidi ni mwendo wa kujinyima ili tusipotumie hela vibaya, tulikula dagaa kwa upande wangu nilivimba miguu mashavu,
20170904_181406.jpg
kwenda kupima naambiwa nimezidisha madini ya chuma mwilini hivyo nijitahidi kula mboga za majani na kubadili mlo.

Hapo sasa, mimi ndio kama niko kwenye mtego nikisema nitumie pesa naitoa kwenye mtaji na mtaji wenyewe unajulikana hata ukitoa mia πŸ˜„ inaonekana ulifanya matumizi ikabidi nikomae hivyo hivyo.

Ila kwa kubadili tulikuwa tunanunua mchicha pori tuna mix na dagaa muda mwingine tunapila mchicha tu basi ili kuokoa gharama πŸ˜€πŸ™Œ

Kumbe bwana yule dogo mpwa wa boss ananirekodi kila nikilalamika kuwa life gumu anamtumia uncle wake siku ya siku nikaweka mtego wangu unajua unapoishi na mtu lazima uishi nae kwa akili bwana wee πŸ˜„ nikanasa sauti na chatting zake akiwa anawasiliana na bosi kuwa πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
IMG-20171124-WA0038.jpg

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
IMG-20171124-WA0036.jpg

Na message za ndugu yake ni hizi πŸ‘‡πŸ‘‡
IMG-20171124-WA0035.jpg

IMG-20171124-WA0022.jpg
IMG-20171124-WA0023.jpg


Yaani roho iliniuma nahangaika kote huku kumbe dogo hana shukrani kabisa πŸ€£πŸ€£πŸ™ŒπŸ™Œ acha kabisa hii dunia kuna watu wanapitia makubwa huenda yangu chamtoto 😁

Baada ya hapo Boss alipanga kuja kutuona na kuona amendeleo ya ofisi, baada ya kuja alijionea na mimi nikamwambia mwanzo mwisho alichokuwa anakikusudia kukifanya kwani mimi najua siyo mmiliki niko geresha ikiwezekana nisepe niwaache waendelee na ofisi yao maana naona kuna kila dalili mimi kuwepo kwangu hapa huenda ndio maana hatufanikiwi.

Boss alikataa nisitoke akasema anajua hii yote ni kukosa hela ndio maana wengine wanaanza kuchonganisha nililiacha lile lakini nilikaa na tahadhali kubwa huo ni mwaka 2018.

Baada ya hapo nikaanza harakati za kusajili rasmi kampuni na ikapata vibari vyote, tukaanza kazi nikiwa na mpwa wa boss, kumbuka mimi nipo geresha siyo mmiliki harali, nivile nimeaminiwa na boss ila wenye ofisi ni wapwa zake ila kwenye share boss aliniweka niwe kama mimi ndio mmiriki mwenye share kubwa kuliko wengine, mwanzo tulisota kidogo ila siyo mbaya ila baadae tulibadili biashara, ndio hapo tuliona biashara inaekelea kuwa nzuri.

Dogo akaanza wizi akienda kudai hela anaweka mfukoni hela zinapotea hela hazionekani, ndani ya muda mfupi tu tulikula ross ya million 17 πŸ€£πŸ€£πŸ™ŒπŸ™Œ boss kuona hivyo akasema kusanyeni madeni mfunge kila mtu asepe anakojua huo ni mwaka 2019 mwezi wa 3 πŸ€£πŸ€£πŸ™ŒπŸ™Œ

Nacheka kama mazuri ila ukweli ndio huo, baada ya kufunga biashara na kampuni kuifunga, nirudi home nimekaa kama mwezi hivi nikowa na fanilia yangu mke na mtoto mmoja wa miaka 2.

Siku moja boss akanipigia siku hapo nipo home sasa sina inshu naangalia namna nifanye niweze kuishi, simu ilipopiga nikapokea tukasalimiana akasema nimekutafutia kazi au umeisha pata nikamwambia hapana bado akasema sasa andika barua ya kuomba kazi kwa kutumia email ya kampuni uitume ukimaliza niambie.

Nilifanya hivyo nikaandika nikatuma nilipomaliza akaniambia Kuna mtu anakutunia hela hapo ya nauli kesho uondoke uende Kasulu.
Nikasema afadhali maisha ya kukaa bila kazi hata hapa home nitakuwa mzigo tena, bora nikahangaike kwa mara nyingine tena, hiyo ni 2019 mwezi kama wa 8


Baada ya kuondoka nikasema kwa sasa sitafanya makosa tena nikasema M/Mungu anisaidie πŸ™ miezi ikapita kama mitatu familia yangu ikaja nikaishi nayo maana huo ni mzigo wangu sina wakumuachia.

Ilikuwa kila nikipokea mshahara nilianza chini na mshahara wa 250,000 kila mwezi nilikuwa natuma laki 200,000 nyumbani kwa ajili ya ujenzi.
2020 nilipata ruhusa ya kuwa nje ya kituo cha kazi kwa wiki kama 2 hivyo ruhusa ile niliitunia kwa akiba niliyokuwa nimeiweka nikaona ninunue kiwanja na kumalizia kulipia mahali.

Mahali ndio ilikuwa ya kwanza kumalizia na baada ya hapo pesa iliyobaki nilipeleka kutafutia kiwanja.

Nilipanga nikanunue Geita ila kuna mtu akaniambia Geita pana maisha ambayo siyo rafiki kwa mtu mwenye kipato cha chini akanishauri nenda, Katoro akanipa ramani baada ya kufika Katoro nikafanya research yangu nikaona pako sawa pananifaa nikatafuta mwenyeji akanipa njia baada ya hapo tukaanza mizunguko sasa kama unavyojua kununua ardhi siyo kama nguo.

Baadae nikaona huyu mwenyeji kama ananizingua, katika pitapita zangu nikaona namba za dalali kwenye madaraja 🀣 nikasema hii namba itanipa kiwanja ngoja niitunze nikiona naelekea kushindwa naipigia.

Kweli bhana kila nikienda kucheli kiwanja kimoja baada ya kingine naona hapa napigwa kwa napelekwa site mbaya huduma hamna na kupitisha usafiri nishida hata kama umekata moto kuja kukufikisha kwako umetota 🀣🀣

Nikaona huu ndio muda wakumpigia dalali maana nimechemka πŸ˜€ kuna muda naona dalali ni miyeyusho ila muda mwingine wanasaidia kiasi chake.
Dalali yupo fasta akasema njoo, maeneo ya STAMICO kufika nikamwambia maeneo ninayotaka kiwanja tukaongozana siku hiyo hiyo nikaandikisha kila kitu kesho yake nikasepa kwenda Kahama. Kesho yake tarehe 06.09.2021 napata binti wa pili πŸ™

Siku iliyofuata nikarudi Kasulu kazi ikaendelea hapo nimeisha piga ndege 2 kwa jiwe moja.
1. Mahali
2. Kiwanja
Bonasi ikawa,
1. Kupokea baraka ya mtoto πŸ™

Mwaka 2021 nikamalizia kupaua nyumani na muda huo nikiwa napambania niweze kuanza ujenzi kwangu, kwa sababu mtoto amekaribia kuanza shule hivyo niliona siyo vizuri kuanzia shule kwa bibi yake au nikae nae wakati kazi yangu haitabiriki kuhama ni muda wowote.


Hivyo nitadhoofisha maeneleo yake na kukaa kwa bibi yake, niliona malezi ya bibi siyo mazuri kwa mtoto hivyo mara zote ukabebe mzigo wako wewe mwenyewe bibi wanamalezi ya kudekeza dekeza.

Mwaka 2021 nilianza ujenzi na kwangu hadi - 2023 nimefanikiwa kuwa na kwangu na nyumbani pamekamilika ingawa vitu vidogo vidogo bado ila siyo mbaya mama anaishi na mtoto anasomea kwao yaani kwangu kwa nguvu zangu πŸ™πŸ™

Yule dogo alirudishwa kazinibila akaiba tena akafukuzwa, akaajiliwa tena Geita uko nako ameiba amekamatwa yuko magereza mpaka sasa na boss ambae ni uncle wake amemkataa ahamjui watajuana huko huko na aliyemuajili hataki kumdamini 🀣🀣

Kiufupi story yangu ilikuwa nihii nimeona nikupe ujumbe na wewe unaweza kuambulia chochote,

Kitu ambacho kilimkost dogo nikwamba hakupitia hustle yeyote, kwanza kalelewa hajui mchicha unalimwaje, watu wanashidagani kwenye hizi familia, ni mtoto ambae amelelewa kiyai yai tu mpaka anamaliza shule na shule kasoma boarding ST.JAMES KIGOMA ila akatoka na Four kaja kitaa kakutana na maisha mengine kajichanganya anataka atoboe haraka haraka kuliko waliomtangulia.

Na hii muda mwingine vijana inabidi tujifunze, mimi mwenyewe nimetumia muda mwingi sana kufanya kazi za watu nivile sikuweka tamaa mbele na niliona hata kama nikijitegemea pesa yote niliyokuwa napata nilikuwa nakula na familia yangu hivyo ule muda wa kujitengenezea mazingira haukuwepo nimuda wa kutumia tu na matatizo kama mnavyoyajua kwenye familia zetu masikini tumezaliwa wazazi hawana kitu sisi ndio tuje tuikomboe familia mtihani tulionao hata wa shuleni haufikii hii inahitajika nguvu+akili na mengine ya kujiongeza kama Mayele akiwa na mpira karibu na gori.πŸ€£πŸ™Œ

Mimi yangu ni hayo asante kwa kupoteza muda wako kusoma ujumbe huu bado najitafuta, kwa nidhamu siyo shortcut za vijana wa kisasa Mungu atatenda muujiza ipo siku na mimi nitakuwa kama wengine wanaofurahia maisha kwa kujipata.
IMG-20180329-WA0007.jpg

Sitaki kuwa kijana mwenye kutanguliza tamaa mbele ndio maana niliporudi nyumbani boss aliniona umhimu wangu kwake na kwa kampuni yake nikarudi kwa mara nyingine.

Toka 2013 nipo kwenye kampuni moja hadi 2017 tukafungua kampuni ikafa 2018 nikarudi 2019 mpaka sasa nipo Mungu ni mwema nitafute mtaji nikae na familia yangu nitulize fuvu sasa. Usione mzee ametafuta kwa maisha yake yote bila kufanikiwa au kuwa na kitu chochote huyo siyo mjinga na wala siyo wakucheka. Maisha ni funzo kubwa sana na yana siri kubwa sana.

Imeandaliwa na Jumanne Mwita
Simu 0768966075
 

Attachments

  • IMG-20171124-WA0038.jpg
    IMG-20171124-WA0038.jpg
    69.7 KB · Views: 13
  • IMG-20171124-WA0036.jpg
    IMG-20171124-WA0036.jpg
    61.2 KB · Views: 16
  • IMG-20171124-WA0035.jpg
    IMG-20171124-WA0035.jpg
    51.2 KB · Views: 23
  • IMG-20171124-WA0035.jpg
    IMG-20171124-WA0035.jpg
    51.2 KB · Views: 12
  • 20170128_142334.jpg
    20170128_142334.jpg
    73.3 KB · Views: 12
Back
Top Bottom