Wachina hawafungui maduka leo huruma

ameacha mtoto wa miaka sita.mmewe ndo mwenyekiti wa wachina tanzania.na ndiye msimamizi wa kampuni ya t-better pikipiki.mumewe kalia sana.baba yake na mwanamke aliye uwawa alikuwepo.alikuwa anakaa na mkwewe.aliyekufa anaitwa (hanchwin) sijui inavyo andikwa lakini ndivyo walikuwa wanaitamka.mi nlijua watazika,lakini nilipoulizwa watazika wapi nikaambiwa mwili wataenda kuuchoma kwa maandamano.maandamano yao yameanza saa sita mchana.
R.I.P.
mia
 
Jamani eeh,kama nyie hamtafuti maisha nje mjue kuna jamaa zenu kibao nchi za watu ! Isitoshe asilimia kubwa ya watz ni illegal immigrants huko mbele ,hizo kauli zenu za kibaguzi tena wa kijinga pasina utu wala soni mziache!
 
Pole kwa wachina wote lakini Jamani kwani watanzania wangapi wameuawa kwa staili hii?embu watulie bwana, kila siku watu wanafanyiwa haya wazawa,sa wao wanajiona special kisa wachina,suala lingekuwa wameuliwa wachina kisa wapo nchini kweli,sa wanataka polisi wafanyaje zaidi ya kupeleleza?
 
Kwani wasirudi kwao kama wanaona hali ya kiusalama sio nzuri Tanzania. Au wametenda maovu huko kwao ndio wakaamua kukimbilia Tanzania?

Hivi wewe unafikiri Serikali ya China ikisimamisha biashara na Tz japo kwa week moja uta survive?
Au wakisitisha kutoa Viza kwa watanzania unafikiri Uchumi utaenda?
Usiongee na kutota kauli zisizo na msingi, Chinese wanagombaniwa na mataifia makubwa, ni sisi Tanzania ndio tunaona hawafai.

Nenda kamuulize Obama, Cameron or Waziri mkuu wa Japan ndio watakueleza umuhimu wa Wachina.

We need to protect wageni, ili nao watuheshimu. Lakini tukiendelea na fikira zile za zamani wa huyu mweupe au mchina basi tuwadhulumu au kuwanyayasa, tutaachwa na kuendelea na porojo zetu za umasikini.
Mimi Napinga na kulaani kabisa haya yaliyotokea! Lazima tuwaheshimu na kuwashukuru wachina mana wamesaidia kuleta maisha rahisi, unafikiri bila wao leo hee watanzania wangapi wangekuwa na uwezo wa kuwa na computers, simu etc? mana bei zake zingekuwa hazishikiki...Japo tunaona quality hazifai lakini wachina wanasaidia maisha yanaendelea!
 
we mzalendo, umesoma mpaka darasa la ngapi!?
Unajua ubalozi wa china uko sehemu gani hapa nchini?
Unajua ni Watanzania wangapi wako China (wengine wakigharamiwa na serikali ya China?

watz waliopo china na wachna waliopo tz hawalingani kiidadi!so hata kama watz wapo china,lakin mara nying wachina wamekua wakiwanyanyasa sana watz!
 
RIP marehemu, poleni wafiwa. Lakini mi naamin kuwa matukio haya yataiangusha hii serikali hii ambayo ujamabazi, uharifu na wizi unapangwa na kutekelezwa na walinda amani.
 
RIP marehemu, poleni wafiwa. Lakini mi naamin kuwa matukio haya yataiangusha hii serikali hii ambayo ujamabazi, uharifu na wizi unapangwa na kutekelezwa na walinda amani.

Tena ingetakiwa iwaangushe haraka sana. Serikali legelege ndiyo faida yake.
 
RIP marehemu, poleni wafiwa. Lakini mi naamin kuwa matukio haya yataiangusha hii serikali hii ambayo ujamabazi, uharifu na wizi unapangwa na kutekelezwa na walinda amani.

Bila kusahau majangili ya Al Shabab yataanza kufanyiza bongo nzima na Kenya nzima sooner or later
 
Hii siku nasikia Mchina alipigwa risasi ya kichwa usipime mwanangu.....Kichwa fumu jamaa wakakimbilia maeneo ya TMK wakiwa na kiroba mmoja mwarabu mwingine anaongea kama Mpemba hv niligongana nao maeneo ya mitaa ya kitomondo tmk nilikuwa sifahamu baada ya muda ndio nikaona askari nikagundua kumbe wale kima mapanja soo mwana.....
 
habari za kusikitisha leo tar 17ock 2011 wachina katka vipepelush vyao walivyobandika ktk maduka yao yote kariakoo na kwingineko wanasema "leo tar hatutafumgua maduka kuomboleza kifo cha mchina mwenzetu aliyeuawa na majambazi na tunasikitishwa na hali ya usalama mdogo wa raia pamoja na wageni tanzania" jamani hili la majambazi serikali wanalionaje?

Mh! Wewe unashangaa hilo! Mbona waziri Chami amehamishwa nyumbani kwake na majambazi na wametishia kumwua Mama yake na wamevamia mfululizo siku mbili tena kwa mfuatano? Polisi na serikali wameona bora wamhamishe maana huyo Jambazi ni noma! Hii ndiyo Bongo bwana! Mimi nimeamua kujifunza kila aina ya mapigano kuanzia Karete, judo, Taek-wondo na kubeba michuma maana mjini lazima uwe na ulinzi. Japo mlinzi namba moja ni Mungu. Karibu Tz
 
Kwanini wasirudi kwao kwenye usalama zaidi? Hivi serikali ina data kujua wanalipa kodi kiasi gani? Je, wote hao wana vibali halali vya kuishi na kufanya biashara Tanzania?
 
Barubaru,
Hii si kauli sahihi!
Ukisema hivyo unafuta kauli isemayo Dunia ni Kijiji!...warudi kwao wapi?..na je Watz waliozagaa China na mataifa mengine wakirudishwa wote utafurahia?
Kwa namna yoyote ile Usalama wa raia ni jukumu la serikali, na si kulaumu wageni!

Umesema Vyema niliona bora nisiseme chochote kwa BARUBARU, kauli aliyotoa si sahihi kabisa ni jukumu la serkali husika kulinda usalama wa wageni ambao umewakaribisha kwako, tuna watoto wetu nje ya nchi yetu wanaishi salama kabisa iweje wageni wetu tuwatake waondoke kisa wameomba usalama wao!!
 
Kwanini wasirudi kwao kwenye usalama zaidi? Hivi serikali ina data kujua wanalipa kodi kiasi gani? Je, wote hao wana vibali halali vya kuishi na kufanya biashara Tanzania?

Ndugu yangu kuwa na kibali au kutokuwa nacho hakuhalalishi mauji yoyote, ni watanzania wengi sana wako nje ya nchi hawana vibali lakini wanaishi salama, tunatakiwa kupigania DUNIA iliyosalama bila vitisho. kama wanafanya biashara bila kibali ni jukumu letu kusimamia lakini sio kuacha waovu watende maovu kisa waliotendewa wanaishi kinyume cha sheria!! huko china kuna watanzania wengi sana wanaishi bila vibali wako salama na hawanyanyashwi kabisa.
 
Barubaru,
Hii si kauli sahihi!
Ukisema hivyo unafuta kauli isemayo Dunia ni Kijiji!...warudi kwao wapi?..na je Watz waliozagaa China na mataifa mengine wakirudishwa wote utafurahia?
Kwa namna yoyote ile Usalama wa raia ni jukumu la serikali, na si kulaumu wageni!

Mkuu basi wawe wanaandamana pia kuwashinikiza Wachina wenzao kila mara Wachina wanapowapiga Watanzania na hata mapolisi na kila Mtanzania anayeuawawa popote pale walipo Wachina nchini basi waandamane kupinga mauaji hayo.

Hawa jamaa wanajiona wao ni watu wa maana sana na pia wengi wao wanaishi nchini kuharamu, kama Serikali ingekuwa inafuatilia kuhakikisha sheria zakw dhidi ya uhamiaji nchini zinafuatwa basi wengi wao wasingestahili kuwepo nchini.

Siungi mkono kabisa kitendo cha kuua raia yoyote yule nchini hata kama anaishi kiharamu lakini wana Ubalozi wao ambao wanaweza kuutumia ili kufikisha malalamiko yao Serikalini. Leo kauwawa mchina, maandamano, kesho kauwawa mhindi nao wanafanya maandamano, kesho kutwa kauwawa mzungu nao waandamane!!! Tutafika kweli Mkuu!? Watumie balozi zao ili kufikisha malalamiko yao kwamba hawaridhishwi na hali ya usalama nchini ambayo pia inawakabili Watanzania katika kila kona nchini.
 
Tatizo la Wachina na Wajapani na watu wengine waasia ni UBAHILI. Inabidi wajifunze kwa wageni wenzao hususan wazungu jinsi wanavoekeza heavily kwene ulinzi, wao kudadeki wanasubiri serikali ichukue kodi zetu na polisi wetu ili ziwalinde wao. Hiyo itakuwa sio haki kwa sisi wazawa ambao inabidi at times kutoa hela ya usafiri ili watuhumiwa wetu wakamatwe. These mchinaz wanatuletea mabidhaa feki, hawana vibali vya ukazi wala ajira/biashara na ultimately hawalipi kodi inayostahili halafu wanataka kuleta demands za ajabu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom