Serikali yapiga marufuku mazao ya uhandisijeni(GMOs) nchini

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,882
20,734
Nov 21, 2018

KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO AITAKA TARI KUSITISHA MAJARIBIO YA GMO

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe leo tarehe 21 Novemba 2018 ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kusitisha mara moja utafiti na majaribio ya uhandisijeni (Genetic Modified Organisms(GMO) yanayofanyika kwenye vituo vyake vya utafiti.

Aidha, Katibu Mkuu ameilekeza Taasisi hiyo ya TARI kuwa mabaki yote ya majaribio ya Uhandisijeni yateketezwe mara moja.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Taasisi hiyo kuanza kutoa matokeo ya utafiti bila kupata idhini ya serikali.

Siku za hivi karibuni Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kupitia kituo cha Makutupora imekuwa inaalika watu mbalimbali kwenda kuona matokeo ya utafiti wakati serikali haijaruhusu matumizi ya uhandisijeni nchini.

For the English Audience
The Tanzanian government has ordered The Agricultural Research Institute(TARI) to stop all Genetic Engineering (Genetic Modified Organisms-GMO) research and testing in all its centers.

This is to be followed by destroying all of what remains of the GMO testing materials.

Recently the Institute without the consent of the Government, had started to disseminate and exhibit research results at one of its centers.

Zaidi, soma >> Nimeona wabunge wakishangilia ujio wa mbegu za GMO. Je, hawajui madhara yake kwa binadamu? - JamiiForums

Kwa wale wageni kwenye swala la GMOs,mada ifuatayo itasaidia kwa kiasi fulani kuonyesha hatari kubwa iliyopo mbele yetu.

Barua ya wazi kwa Rais Joseph Pombe Magufuli kuhusu GMOs.

areafiftyone
JF-Expert Member

Nov 5, 2018.

Mazao ya uhandisijeni(GMOs) ni janga la dunia,pamoja na sisi tulioko JamiiForums.
Mwenzetu Dr Richard Mbunda ambaye anakerwa na GMOs pamoja na mimi, labda na wengine,
amemuandikia Rais barua ya wazi akieleza kwa kina ubaya wa GMOs na kueleza wazi kwa nini anaamini GMOs kama zitaruhusiwa kulimwa nchini,zitaleta adhari kubwa kwa mazingira yetu,uchumi wetu, hasa wa wakulima wadogo wadogo na afya za Watanzania.Kwa vile janga la GMOs ni letu sote,tusome barua ya Dr.Richard Mbunda kwa makini halafu totoe mawazo yetu kama JF.Naomba baada ya hilo angalizo, sasa niombe moderators wasitoe uzi huu, ili watu waweze kutoa mawazo yao.Michango itakayotolewa hapa ina maana kubwa kwa kizazi hiki na vizazi vingi vijavyo.

Barua ya Wazi kwa Rais wa Tanzania: Je, GMOs ni Sera ya Serikali?

Na Dkt. Richard Mbunda (UDSM)

Mheshimiwa Rais,

Heri ya siku ya kuzaliwa!

Kwa heshima na taadhima, niruhusu mimi mtoto wa mkulima mdogo na mwananchi wa nchi yetu tukufu nikusalimu. Hali yangu mimi na wanafamilia wenzangu, ambao ni wakulima wadogo nchini, si njema kabisa. Mheshimiwa Rais, kama ujuavyo, sisi ni takribani asilimia zaidi ya 70 ya wananchi wote wa Tanzania, na naamini kuna ndugu zako wa damu ambao ni sehemu ya jamii hii ya watanzania.

Ukulima mdogo ndiyo uhalisia wetu. Hatuwezi kuukataa kwa sasa, japo wengi tuna matumaini ya kupiga hatua, kama serikali itatuwekea misingi thabiti. Lakini hali yetu ni ile, Waswahili wanasema ‘bora ya jana kuliko leo.’ Mikakati ya kumkwamua mkulima mdogo nitaieleza katika kitabu changu, lakini kwa leo niruhusu tu nikuulize swali la kisera.

Mheshimiwa Rais, tarehe 28 Septemba, 2018 Jijini Geneva, Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ilipitisha Azimio la Haki za Wakulima Wadogo. Azimio hili ni ushindi kwa wakulima wadogo duniani dhidi ya Makampuni hodhi katika sekta ya kilimo katika mapambano yaliyochukua zaidi ya miaka 17. Azimio hili linazungumzia haki za ARDHI, MBEGU, BAIOANUAI (Biodiversity) na SOKO LA NDANI LISINAJISIWE NA BIDHAA KUTOKA NJE.

Kimsingi haki hizi zinaendana na Uhuru wa Chakula (Food Sovereignty) kwa nchi maskini, ambao ndiyo uhuru pekee tuliobaki nao. Kinachonishangaza Mheshimiwa Rais, ni kuwa, pamoja na kuwa na idadi kubwa ya wakulima wadogo nchini, Tanzania haikuwakilishwa katika Azimio hili muhimu. Jumla ya nchi 34 zilikubali Azimio, nchi 11 zilikaa(abstain) na kama ilivyotegemewa, nchi zilizoendelea zilipinga Azimio hili. Mheshimiwa Rais, tulipitwa au hatujali? Namshukuru Mungu wa wanyonge, Azimio limepita.

Lakini Mheshimiwa Rais, mienendo ya Serikali inatupa mashaka makubwa zaidi sisi familia ya wakulima wadogo. Naliongea hili kwa ujasiri kwa kuwa nimekulia kilimo na naishi na wakulima wadogo. Hata utafiti wangu wa uzamivu uliwalenga wakulima wadogo na unahusu Uhuru wa Chakula Tanzania.

Mheshimiwa Rais, serikali imekuwa ikipigia chapuo teknolojia ya uhandisijeni wa mazao ya GMOs nchini. Tumeliona hilo katika Programu ya ASDP II uliyoizindua hivi karibuni, ambayo inatamka wazi mwelekeo wa kilimo chetu kwa matumizi ya GMOs, siyo tu katika mimea, bali hata wanyama (ikanifanya niwaze majaliwa ya ng’ombe za rafiki zangu Wamasai). Angalau basi tukusikie kwa maneno yako, je, wewe ni shabiki wa teknolojia hiyo na kwamba ni mdau wa mradi ya GMOs katika utafiti unaoendelea Makutupora, ambayo sasa inahalalishwa hapa nchini kupitia vyombo vya habari?

Barua yafaa iwe fupi ili isomeke kwa haraka na kueleweka kirahisi. Hivyo, Mheshimiwa Rais, nitaandika kwa uchache kuhusu sababu kwa nini Tanzania haihitaji GMOs. Lakini ninazo makala ndefu za kitaaluma zinazohusu jambo hili.

Sababu mojawapo ya kukataliwa GMOs inatokana na athari zake katika mazingira. Kwa mfano, katika utafiti uliofanywa na Mwanazuoni John Paul na kuchapishwa mwaka huu wa 2018, ikiwa na kichwa Genetically Modified Organisms (GMOs) as Invasive Species unaonesha kuwa GMOs ni viumbe vamizi. Huharibu mazao asilia, mimea mingine, wanyama na kuleta athari katika mazingira ya viumbe hai.

Hata katika elimu ndogo ya Kilimo tuliyojifunza sekondari, Mheshimiwa Rais, mahindi huzaa kwa uchavushaji. Kama mahindi ya GMOs na ya kawaida yatapandwa pamoja tutegemee nini? Kimsingi mahindi ya mbegu zisizo za GMOs yakiingiliana na ya GMOs yatapotea na kutuletea balaa kubwa la utegemezi huko mbeleni. Izingatiwe kuwa mbegu za GMOs hazirudiwi kupandwa zikatoa mazao.

Mheshimiwa Rais, napenda kujua kama hayo majaribio ya Makutupora yanajibu wasiwasi huu. Kwamba mbegu zao za GMOs hazitaathiri mbegu zetu, mimea mingine na mazingira kwa ujumla! Au ni utafiti unaoonesha tu kuwa GMOs zitastawi nchini? Mheshimiwa Rais unisamehe kwa kusema hili, hata bangi, ule mmea tunaoupiga vita, bado unastawi katika nchi yetu tukufu, tena vizuri mno.

Kupotea kwa mbegu zetu [kutokana na kuingiliana na mbegu za GMOs] kutatufanya tuwe watumwa wa makampuni ya mbegu. Mheshimiwa Rais, naamini umefuatilia habari kuhusu kampuni ya Monsanto, ambayo sasa imenunuliwa na kampuni ya Bayer ya Ujerumani kwa zaidi ya shilingi trilion 120 (USD 62 bn). Monsanto imekuwa ikipigwa vita hasa Amerika ya Kusini kwa namna ilivyotaka kuwafanya watu wake watumwa wa chakula. Pale ambapo tutapoteza mbegu zetu za asili, au tulizoziendeleza muda mrefu kupitia taasisi zetu za utafiti, tutakuwa tumekubali kuwa mateka.

Mheshimiwa Rais, wewe umekuwa ukipinga ubeberu kwa nguvu zako zote, na nisingependa hili la utumwa wa mbegu litokee katika utawala wako. Afrika Kusini, ambako waliruhusu GMOs tangu miaka ya 90, sasa zaidi ya asilimia 90 ya mahindi ni GMOs na wakulima wanalazimika kulipa ziada ya ada ya teknolojia kwa Monsanto. Pamoja na kubeparisha kilimo chao, bado Afrika Kusini hawajaweza kutokomeza njaa.

Suala la utamaduni wa chakula ni muhimu pia liongelewe katika muktadha huu. Kuna ladha, harufu nzuri na uasili wa chakula. Kama ujuavyo, Mheshimiwa Rais, hizi ni sifa pekee zinazotofautisha chakula chetu. Na tunapaswa kuvitunza vyakula hivi kwa choyo kubwa - hasa kwa kuwa sisi ni kitovu cha utalii Afrika.

Tukisoma baadhi ya makabrasha na shuhuda za wageni, tunaona watalii wanakizungumzia chakula chetu katika namna ya sifa ya pekee. Mheshimiwa Rais, pengine unakumbuka kuwa, mmoja kati ya watetezi wa GMOs Robert Paarlberg aliwahi kusema mwaka 2009 kuwa “chakula kilichozalishwa kiasili (organically) kina ladha na harufu ya kuvutia zaidi kuliko vyakula vya GMOs ndiyo maana nchi za Ulaya hazitaki GMOs" lakini "masikini wa Afrika hawapaswi kuwa na uchaguzi” Je, ni kweli tumefika sehemu ambayo hatupaswi kuwa na uchaguzi kwa kuwa sisi ni maskini?

Mheshimiwa Rais, katika makala yenye kichwa "No Scientific Consensus on GMO Safety," iliyochapisha wa wanasayansi 15 kwa pamoja katika Jarida la Environmental Sciences Europe mwaka 2015, tunaelezwa kwamba japo kumekuwa na jitihada za kuuaminisha ulimwengu kuwa GMOs ni salama kwa afya, lakini kimsingi hakujawa na muafaka wa usalama wa GMOs. Na kuna baadhi ya tafiti zilizoenda mbele kueleza kuwa GMOs zina madhara kiafya. Baadhi ya madhara ya afya yanayotajwa ni pamoja na uzio na saratani. Je, utafiti unaofanyika Makutupora unalenga kuleta majibu ya wasiwasi wa madhara ya afya yatokanayo na GMOs?

Monsanto imeshtakiwa zaidi ya mara hamsini huko Marekani na hivi karibuni ilipatikana na hatia, wananchi wakiilalamikia bidhaa zao kuwaleatea saratani. Kuhusu chakula cha GMO, jibu la kampuni hiyo limekuwa hilo hilo kuwa hawalazimiki kisheria kudhibitisha kuwa vyakula vyao havina madhara. Wanaojiita wanasayansi wetu nchini hawatuambii ukweli, labda kwa maslahi yao binafsi. Lakini katika majadiliano tuliyofanya HakiArdhi hivi karibuni, mmoja wa wanasayansi hao, baada ya kubanwa na wakulima, alikiri kuwa uangalifu unahitajika hasa katika mimea iliyobadilishwa kuzalisha sumu ili kuua wadudu.

Mheshimiwa Rais, Takwimu za Wizara ya Kilimo zinaonesha kuwa Tanzania bado hatujafikia hata asilimia 30 ya matumizi ya mbegu bora, mbolea na viuatilifu. Bado tumekuwa tukizalisha zaidi ya asilimia 120 ya chakula kinachohitajika nchini. Wiki tatu zilizopita nilikuwa Mkoa wa Rukwa (Sumbawanga) na nilikutana na Wazalishaji wanaolalamikia soko la mahindi na siyo changamoto za uzalishaji. Tena kuna waliovuna mahindi ya kutosha bila hata kutumia mbolea.

Lakini watu wa GMOs wanatuletea taarifa kuwa kuna uzalishaji mdogo sana na mahindi yanashambuliwa sana na wadudu. Kimsingi wanatangaza Hali ya Hatari (National Emergency) kwa jinsi wanavyotuonesha wadudu wala mahindi katika video zao. Mheshimiwa Rais, ni kweli tumefikia huko? Kama ni kweli mbona hujatutangazia hali ya hatari ili basi GMOs tuipokee kama hatua yetu ya kupunguza kifo cha haraka? Na kama siyo kweli, kwa nini tunalazimishwa kuruka kutoka kutumia mbegu za asili kwa asilimia 80 za sasa hadi GMOs, teknolojia ya juu kabisa wakati hatujaweza kuvuna tija itokanayo na mbegu bora za OPVs na Hybrid?

Kuna agenda gani hapo? Tunakimbilia wapi? Tunapitwa na nini?

Mheshimiwa Rais, sipendi nikuchose sana. Naomba niulize swali moja la mwisho. Ubora tulio nao kama nchi ukilinganisha na nchi zingine (Comparative Advantage) wanaouongelea wachumi au kile wasomi wa fani ya Biashara wanachokiiita eneo la ubora (niche) wetu lipo katika nini? Sidhani kama tunaweza kushindana na Marekani katika kuzalisha mahindi ya GMOs, chakula chenye unyanyapaa duniani kote. Sisi tunapaswa kuwa msingi wa chakula salama Afrika Mashariki na kwingineko duniani. Wakulima wetu wanapaswa kuwa msingi wa kuzalisha chakula hiki na kunufaika kama ilivyo sasa, ambapo soko bado si la uhakika.

Katika utafiti wangu nilitembelea vituo vya utafiti wa kilimo. Nikiri kuwa ni taasisi nyeti na zina wataalam (japo wametelekezwa) wanaoweza kutusaidia katika kuboresha mbegu zetu za asili kama wakiwezeshwa. Sote tunajua mbegu bora siyo lazima ziwe za GMO.

Mheshimiwa Rais, tukumbuke kuwa wakati wa Utawala wa Rais Dkt. Jakaya Kikwete, mradi wa GMO wa WEMA haukuanza nchini japo ulipaswa kuanza 2008. Hii ilitokana na kifungu kinachohusiana na dhamana ya uharibifu kijulikanacho kwa Kiingereza kama ‘strict liability’ kilichopo katika kanuni zetu za usalama wa viumbe na uhai (Biosafety). Kifungu hiki kilisema mtu atakeyeingiza GMOs nchini atawajibika moja kwa moja kwa madhara yoyote yatakayotokana na GMOs kiafya, kimazingira na kiuchumi.

Hiki kifungu kiliwachelewesha watu hawa wa WEMA kuanza utafiti mpaka mwaka 2016 Serikali ilipolegeza masharti na kuweka kifungu kinachosema ‘strict liability’haitatumika katika utafiti. Kama GMOs ni kitu chema kama WEMA unavyodai na ni ukombozi wetu, waliogopa nini kuanza 2008 hadi wakashawishi kanuni zibadilike? Hata sasa wanadai sheria zetu zinawabana wanataka tulegeze zaidi watuletee balaa tushindwe pa kuwabana.

Walaji wa chakula kinacholimwa na wakulima wadogo hawapo salama pia. Muda si mrefu tutaanza kuona maduka makubwa (supermarkets) za vyakula vya asili (organic food) ambavyo watu wa kada ya juu tu ndio pekee watamudu kununua. Wameshaanza na madogo madogo. Tunaendelea kutengeneza matabaka kwa maslahi ya mwekezaji.

Mheshimiwa Rais, huenda barua hii haitakupendeza. Najua pia barua hii haitawapendeza wadau na watunga sera wanaopigania GMOs izidi kutamalaki nchini. Hakika itaichukiza kampuni husika inayowekeza katika mradi wa WEMA huko Makutupora.

Wanatudhihaki kuwa sisi tunapinga sayansi. Lakini ni sayansi zipi tumezipinga hapa nchini? Kama alivyowahi kusema mwanazuoni nguli Karl Polanyi mwaka 1944, hatuwezi kuiruhusu teknolojia ya kinyonyaji na inayokusudia kunufaika na majanga ya watu itamalaki.

Mheshimiwa Rais, nakushukuru kwa kusoma hii barua. Hatimaye nimetimiza wajibu wangu. Nimesema ukweli na sina haja ya kujificha.
 
Hili ni la kupongezwa maana hizo mbegu pamoja na mazao yake zina athari kwa afya, mbegu za asili zina uhai kwa maana ukiipanda ikatoa zao na bado ukachukua kwa ajili ya kupanda tena wakati mwingine

Lakini mbegu za GMO japo zinatoa mavuno makubwa lkn huwezi kutumia mazao yake kama mbegu tena kwa maana nyingine ni mfu miche yake haitoi mbegu

MWA. :1:29
Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;

Mbegu za asili japo nazo sasa hivi ni za kutafuta kwa manati lakini hizo ndizo zifaazo kwa chakula na afya njema kwa binadamu hizi za GMO ni hatari kama ambavyo zenyewe hazina uhai zinaweza kubadili mfumo wetu wa reproduction nao kufa na hivyo kuathiri uzalianaji wetu hapo hujazungumzia magonjwa mengine kama kansa, obesity nk
 
Hapa kwakweli nahitaji elimu zaidi kuelewa kitu chenyewe... maana wenzetu wanapromote sana research na innovations
 
Sasa si ufanyike kipi ni bora, kama zinazaa zaidi, hazina madhara kwetu sisi na mazingira na hazina gharama vs mbegu za asili.
 
Ni kweli huu ni ushindi mkubwa kwa watanzania. Nina imani na nchi nyingine za Afrika zitaiga ili katika kulinda afya ya walaji na vizazi vyao kutoka kwenye 'makucha'! Hongera watanzania...

Shukrani sana viongozi wa serikali kwa kuendelea kutambua umuhimu wa kulinda Watanzania katika nyanja zote.
 
Hili ni la kupongezwa maana hizo mbegu pamoja na mazao yake zina athari kwa afya, mbegu za asili zina uhai kwa maana ukiipanda ikatoa zao na bado ukachukua kwa ajili ya kupanda tena wakati mwingine

Lakini mbegu za GMO japo zinatoa mavuno makubwa lkn huwezi kutumia mazao yake kama mbegu tena kwa maana nyingine ni mfu miche yake haitoi mbegu

MWA. :1:29
Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;

Mbegu za asili japo nazo sasa hivi ni za kutafuta kwa manati lakini hizo ndizo zifaazo kwa chakula na afya njema kwa binadamu hizi za GMO ni hatari kama ambavyo zenyewe hazina uhai zinaweza kubadili mfumo wetu wa reproduction nao kufa na hivyo kuathiri uzalianaji wetu
Unaongea nini wewe unajua ulimwengu uliko sasa katika technology ya kilimo?. Mbona huwa mnaongea pumba tu. Unafikiri Ulaya, America, Asia wote hao wanakula chakula cha asili.

The matter here is TBS and TFDA mzee. Nikupe mfano unafikili nyanya zinazolimwa na kupigwa madawa yasiyo na uwiano sahihi ni salama Kwa matumizi ya binadamu?.

Haupo salama Kama unavyofikili, kuna asali ya kutoka Tabora tena wanaitwa ni ya asili ilifanyiwa analysis majubi yake haifai Kwa matumizi ya binadamu Kwa sababu imeasiliwa na dawa za kupulizia tumbaku.

Msishangilie Kila kitu jiulizeni Kwanini wazungu wanatumia Sana chemical food bado Maisha yao no marefu kuliko tuaojiita walaji wa vyakula vya asili. Baba TBS ni mhimu Kwa vyakula.
 
Jamani mnatuchanganya na hizi taarifa. Jana imeripotiwa humu JF wabunge wameshangilia kuletwa GMO. Leo mnasema GMO zimesitishwa.
Wabunge sio wataalam mkuu,ndio maana walishangilia.Serikali naamini imepitia ushahidi uliopo wa kisayansi kuhusu GMOs na imeona kwamba mazao hayo hayafai kutumiwa na wanadamu.Nimekuwa naleta mada nyingi humu kuhusu ubaya wa GMOs,ila kwa bahati mbaya watu wengi walikuwa wanakimbilia mada za udaku.Ifike mahali Watanzania tujali mambo ya msingi,kuliko kukimbilia mambo yasiyokuwa na faida kwetu.
 
Sasa si ufanyike kipi ni bora, kama zinazaa zaidi, hazina madhara kwetu sisi na mazingira na hazina gharama vs mbegu za asili.
Serikali imepitia taarifa za kitalaamu na imeona kwamba mazao ya uhandisijeni (GMOs) hayafai kwa matumizi ya wanadamu,kwa maana kwamba yana athari kwa afya zetu,uchumi wetu na mazingira.Kwa hili serikali haina budi kupongezwa sana.
 
Unaongea nini wewe unajua ulimwengu uliko sasa katika technology ya kilimo?. Mbona huwa mnaongea pumba tu. Unafikiri Ulaya, America, Asia wote hao wanakula chakula cha asili. The matter here is TBS and TFDA mzee. Nikupe mfano unafikili nyanya zinazolimwa na kupigwa madawa yasiyo na uwiano sahihi ni salama Kwa matumizi ya binadamu?. Haupo salama Kama unavyofikili, kunaasali ya kutoka Tabora tena wanaitwa ni ya asili ilifanyiwa analysis majubi yake haifai Kwa matumizi ya binadamu Kwa sababu imeasiliwa na dawa za kupulizia tumbaku. Msishangilie Kila kitu jiulizeni Kwa nini wazungu wanatumia Sana chemical food bado Maisha yao no marefu kuliko tuaojiita walaji wa vyakula vya asili. Baba TBS ni mhimu Kwa vyakula.
Wewe sio mtaalamu obviously,you are working on hearsay.Mimi ni mtaalamu na nimepigania sana mazao ya uhandisijeni yapigwe marufuku nchini.Najua yote yanayoendelea
duniani kuhusu GMOs,kwa hiyo serikali iko sahihi kabisa katika uamuzi wake.Nimekuwa naleta mada mbali mbali humu kuhusu ubaya wa GMOs.Tatizo la Watanzania tulio wengi ni kwamba tunakimbilia udaku na mambo yasiyo ya msingi na manufaa katika maisha yetu,tubadilike.
 
Unaongea nini wewe unajua ulimwengu uliko sasa katika technology ya kilimo?. Mbona huwa mnaongea pumba tu. Unafikiri Ulaya, America, Asia wote hao wanakula chakula cha asili. The matter here is TBS and TFDA mzee. Nikupe mfano unafikili nyanya zinazolimwa na kupigwa madawa yasiyo na uwiano sahihi ni salama Kwa matumizi ya binadamu?. Haupo salama Kama unavyofikili, kunaasali ya kutoka Tabora tena wanaitwa ni ya asili ilifanyiwa analysis majubi yake haifai Kwa matumizi ya binadamu Kwa sababu imeasiliwa na dawa za kupulizia tumbaku. Msishangilie Kila kitu jiulizeni Kwa nini wazungu wanatumia Sana chemical food bado Maisha yao no marefu kuliko tuaojiita walaji wa vyakula vya asili. Baba TBS ni mhimu Kwa vyakula.
Uelewa wako wewe kwenye maswala ya GMO ni mdogo sana. Nakushauri kaa kimya tu wakufundishe wanaojua. Si lazima kuchangia hata kama hujui.
 
Nov 21, 2018

KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO AITAKA TARI KUSITISHA MAJARIBIO YA GMO

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe leo tarehe 21 Novemba 2018 ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kusitisha mara moja utafiti na majaribio ya uhandisijeni (Genetic Modified Organism-GMO) yanayofanyika kwenye vituo vyake vya utafiti.

Aidha, Katibu Mkuu ameilekeza Taasisi hiyo ya TARI kuwa mabaki yote ya majaribio ya Uhandisijeni yateketezwe mara moja.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Taasisi hiyo kuanza kutoa matokeo ya utafiti bila kupata idhini ya serikali.

Siku za hivi karibuni Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kupitia kituo cha Makutupora imekuwa inaalika watu mbalimbali kwenda kuona matokeo ya utafiti wakati serikali haijaruhusu matumizi ya uhandisijeni nchini.
Tena wachome moto kabisa, wazungu wenyewe hawataki kusikia GMOs, na ni sheria kuonesha GMO product in case kama ipo. Nimefurahia sana huu uamuzi, kweli Tz tumezinduka
 
Hili ni la kupongezwa maana hizo mbegu pamoja na mazao yake zina athari kwa afya, mbegu za asili zina uhai kwa maana ukiipanda ikatoa zao na bado ukachukua kwa ajili ya kupanda tena wakati mwingine

Lakini mbegu za GMO japo zinatoa mavuno makubwa lkn huwezi kutumia mazao yake kama mbegu tena kwa maana nyingine ni mfu miche yake haitoi mbegu

MWA. :1:29
Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;

Mbegu za asili japo nazo sasa hivi ni za kutafuta kwa manati lakini hizo ndizo zifaazo kwa chakula na afya njema kwa binadamu hizi za GMO ni hatari kama ambavyo zenyewe hazina uhai zinaweza kubadili mfumo wetu wa reproduction nao kufa na hivyo kuathiri uzalianaji wetu
Ina maana mbegu za mahindi wanazotumia wakulima nowdays nazo ni gmo?

Mbona niliskia wanaziita hybrid/chotara

Nazo ukizipanda mara ya pili hazioti
 
Wabunge sio wataalam mkuu,ndio maana walishangilia.Serikali naamini imepitia ushahidi uliopo wa kisayansi kuhusu GMOs na imeona kwamba mazao hayo hayafai kutumiwa na wanadamu.Nimekuwa naleta mada nyingi humu kuhusu ubaya wa GMOs,ila kwa bahati mbaya watu wengi walikuwa wanakimbilia mada za udaku.Ifike mahali Watanzania tujali mambo ya msingi,kuliko kukimbilia mambo yasiyokuwa na faida kwetu.
Katika ulimwengu wa fake news, sijui nimwamini yupi: Katibu Mkuu au Bunge
 
Ni kweli huu ni ushindi mkubwa kwa watanzania. Nina imani na nchi nyingine za Afrika zitaiga ili katika kulinda afya ya walaji na vizazi vyao kutoka kwenye 'makucha'! Hongera watanzania...

Shukrani sana viongozi wa serikali kwa kuendelea kutambua umuhimu wa kulinda Watanzania katika nyanja zote.
Ni jambo la maana sana amefanya waziri.
 
Back
Top Bottom