Wabunge wa CCM mnawachezesha Watanzania "kwata" la akili!

Katika kile kinachoonekana kuwa wabunge wengi wa sisiemu wamechoka kufanywa mabwege leo katika kuhitimisha kipindi cha kwanza cha bunge mbunge huyo amesema wezi ni mawaziri waliowengi wala wizi hauko katika halmashauri kama inavyosemwa.lukuvi kama kawaida yake kasimama kupinga hilo tamko na akamuomba ndunga amuamuru filikunjombe atoe ushahidi kwa maandishi kwa kila waziri anaemtuhumu.

Hii ni ishara kua baadhi ya wabunge wamekwiva kutokana na sera za wabunge wa chadema kutokua waoga na kusima kidete na waziwazi bila uoga,kama ni mwizi aitwe mwizi hakuna kubana pua wala wala kumuangalia nyani usoni. Magamba kazi kweli kweli mwaka huu, sijui kama watatoboa mpaka 2015
 
Wabunge wa CCM ni wanafiki, na hayo ni mazingaombwe wamekuwa wanatuonyesha miaka yote! Leo wanasimama bila aibu bungeni kulalamikia serikali yao! Kweli? Kama kweli wana ushungu wa lolote kati ya hayo si waweke maslahi ya chama pembeni wachukue maamuzi magumu?!!!!! Waongo, wanafiki wakubwa, wao wanadhani hatujui kuwa wako pale kwa maslahi binafsi?

Kanuni zipo na wanzijua, miaka yooooooote CAg amekuwa antoa ripoti na hazifanyiwi kazi, tena siku hizi ni kwa uwazi kabisa bunge linadharauliwa na serkali, yako wapi maazimio ya saga la kujiuzuru kwa "ndanda kosovo" si yalikuwapo? wamefanya nini?

Hakika hili ni kwata la akili ambalo kwa ubinafsi wangu nakataa kulicheza, mazingaombwe matupu!!! Heri yake mkulu, yeye aahahaa swadkta yuko zake brasilia, anafanya shopping!!!
 
kipindi cha kujadili taarifa za kamati za ukaguzi mahesabu mbalimbali mbunge Filikunjombe amesema kuwa wizi haupo halmashuri pekee bali mawaziri wengi ni wezi na amesema yuko tayari kuleta ushahidi bungeni.Lukuvi ataka ushahidi uletwe,naibus spika hajasema lolote,wakati huohuo wabunge wambana naibu waziri Mwanri alete taarifa ya utekelezaji wa aliyoyasema na kuahidi bungeni.Zito amwambia hajatekeleza na ataka Hnsard isomwe alichoahidi kipindi kilichopita,watuhumiwa walaji wa fedha hawachukuliwi hatua kwa wakati.mmhm mambo yote jioni saa 11 bunge litakapoendelea.
source live bungeni tbc.
 
hapo kweli mmm umenena kwani yale yote ya huko nyuma mbona hayafanyiwi kazi,na bado wanaendelea kutuchezea akili,hawa ni wanafiki wakubwa!
 
Zitto huwa anaingia humu, mimi nampa ushauri, wawaumbue hao kasuku wa kijani na njano, kwa kuleta hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu, halafu utaona kama kasuku wao wataiunga mkono?
 
Kama kweli mna ubavu na uchungu mlioonyesha kwenye uchangiaji wenu wa report za kamati za Bunge ni wa kweli kutoka moyoni basi chukueni hatua madhubuti tuone kweli mko serious na mnacho lalamikia. Pigeni vote of no confidence to the government. Tumewazoea miaka yote kamati zinapo wasilisha taarifa zao mmekuwa mnatuletea usanii wa kuvunga mnalaumu mapungufu yaliyopo serikalini mwisho wa siku mnapulizia na kuunga hoja. Ya Jairo na kelele zenu yameishia wapi?

Tuna waangalieni tu na sidhani hata hiyo 2015 mtafika. Hatuto subiri kuingia barabarani tena kama mlivyozoea bali msituni. Tuone Jeshi letu ni la wananchi kama jina lao lilivyo au la mafisadi. Pamoja na uozo wote wa serikali wao wako kimya tu.. sasa tuna majeshi kweli au masanamu? Je, mnalinda wavamizi wasitoke nje ili walioko ndani watumalize vizuri? kuna tofauti gani ya kuvamiwa hapa? kwa mtindo huu wa magamba ni kama nchi imevamiwa tena kwa uvamizi wa aina mpya kutokea ndani wala siyo uasi kwa tafsiri halisi ya uasi, chukueni hatua. Msidhanie tunashindwa kupata silaha na kuzitumia. Kumbukeni wengine jeshini tulipitia tuna mshukuru hayati Nyerere kwa hilo. Tuna kuhesabieni siku tu..

Tulipo fikia kwa sasa serikali haiwezi tena kuchukua hatua na wala haina ubavu huo. Tuna mifano mingi ya mambo mazito ambapo wameshindwa kabisa kufanya lolote. Kilicho bakia kwa sasa ni majeshi kuingilia kati kama Guinea Bissau au kwa mara ya kwanza Tanzania iwe na waasi. Mapori tunayo mengi ya kuanzia front na vijana wasio na kazi watalianzisha. Mnapo sikia EL anawaambia vijana wasio kuwa na kazi ni bomu litakalo lipuka wakati wowote mnaona ni ndoto eh? subirini..
 
Wabunge wa ccm, cuf, tlp na udp walio wengi ni waongo, waoga, wanafiki na sio wa kuaminika.
 
Kama naota vile! Kumbe hata ccm wametambua peoples' power na hivyo wameanza kutetea maslahi ya taifa? Wasiwasi wngu ni kuwa wanafanya hivyo ili watetee maslahi yao kwenye uchaguzi ujao kwa kujisafisha mbele ya wapiga kura kupitia kwenye luninga. Time will tell!
 
Chadema kimesaidia sana kufanya watu kutokuwa waoga kwenye mambo ya msingi hasusan wabunge.

Zamani ulikuwa ukitoa madai kama haya ni mwisho wako wa kisiasa.Watakwambia udhibitishe ukishindwa watakulazimisha kuomba msamaha na kitakacho fuatia ni vikao vya CCM kublock jina lako kwenye jambo lolote lile na wanaccm wenzako kuanza kukutenga kwa kuogopa kuwatilia kitumbua chao mchanga.

Sasa hivi viongozi wa ccm wamekuwa ni waoga wanajua unaweza kuhama ccm na ukaretain nafasi yako
 
  • Thanks
Reactions: rom
Kwasasa imeshakuwa wazi kabisa ccm pekee hawawezi kufanya kazi. Kamati za bunge ambazo zinaongozwa na upinzani ndizo zinazofanya kazi mawaziri wengi wezi hakuna wanalofanya.
 
Kura ya kutokuwa na imani itatu cost sisi wananchi pia, inamaana bunge lote linavunjwa tunaanza moja. Hapana sikubaliani na hoja ila noana kuna haja rais avunje hii baraza abadilishe safu tena.

Mkuu kura ya kutokuwa na imani na serikali, itapelekea waziri mkuu kujiuzuru na rais ataunda baraza jipya? Ila kutokuwa na imani na rais ndo bunge litavunjwa!!

To me, hata ikifikia hatua tukasema rais hatuna imani naye ni sawa tu, mambo ya gharama haya-compliment demokrasia! Kwani hayo matrillioni yanayoliwa kila mwaka huwa tumeyatarajia? Ni bora tugharimie dekrasia mara mia!!
 
Kwanza wengi mnaoandika humu nanyi baadhi ni wanafiki na mashabiki tu, nilichojifunza badala ya kuelimishana na kupeana taarifa za maana mnaanza kushabikia na kuponda hata kama kitu kilichoongelewa ni cha kweli. Ikitokea mtu yeyote wa chadema hata akisema utumbo mnashabikia mpaka nashindwa kuelewa nyinyi nyote ni chadema au, pangetokea watu aina yangu ambao wanasiasa ninatofautiana nao tungeweza kujenga maada na kujadiliwa bila ushabiki ninaousoma kwenye comment zenu. Tubadilike jamani hawa wanasiasa sio wakweli hata siku moja na hao mnaowashabikia wakichukua dolla mtawachukia na kuanza kuwazomea japo hamtakubali lakini iko siku mtakubali maneno yangu, kumbukeni siasa ndiyo ajira yao na ili wawe wazuri ni kuongea maneno mazuri tu.
 
nawafananisha Wabunge wa CCM na huyu
the_best_green_dragon_picture_on_yellow_vectorized.png
 
Kwanza wengi mnaoandika humu nanyi baadhi ni wanafiki na mashabiki tu, nilichojifunza badala ya kuelimishana na kupeana taarifa za maana mnaanza kushabikia na kuponda hata kama kitu kilichoongelewa ni cha kweli. Ikitokea mtu yeyote wa chadema hata akisema utumbo mnashabikia mpaka nashindwa kuelewa nyinyi nyote ni chadema au, pangetokea watu aina yangu ambao wanasiasa ninatofautiana nao tungeweza kujenga maada na kujadiliwa bila ushabiki ninaousoma kwenye comment zenu. Tubadilike jamani hawa wanasiasa sio wakweli hata siku moja na hao mnaowashabikia wakichukua dolla mtawachukia na kuanza kuwazomea japo hamtakubali lakini iko siku mtakubali maneno yangu, kumbukeni siasa ndiyo ajira yao na ili wawe wazuri ni kuongea maneno mazuri tu.
Sisi CHADEMA,
Wewe ni nani??
270383_175684325826537_100001549126150_454565_5101192_n.jpg
 
Hawana ubavu wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na PM. Wote waoga wanajificha na kukimbia vivuli vyao wenyewe!
 
wengi wabungewa CCM wameingia uoga kuona sasa 2015 hata akipambanishwa na mtoto mdogo wataangushwa tu, watu wamechoka na ahadi za uongo zisizotekelezeka....... wizi wa waziwazi...... ITAKULA KWAO 2015.
 
Kwanza wengi mnaoandika humu nanyi baadhi ni wanafiki na mashabiki tu, nilichojifunza badala ya kuelimishana na kupeana taarifa za maana mnaanza kushabikia na kuponda hata kama kitu kilichoongelewa ni cha kweli.
Mkuu tunapenda wakiongea cha kweli ila tatizo ni unafiki leo wanasema hiki kesho kile, umesahau Anna Kilango alivyompaka Ngeleja mwaka jana alafu mwisho wa siku anatetea.., umesahau wizara ya nishati mwaka jana kila mtu anatoa mishipa alafu mwisho wa siku wanaunga mkono kwa ndio...


Ikitokea mtu yeyote wa chadema hata akisema utumbo mnashabikia mpaka nashindwa kuelewa nyinyi nyote ni chadema au, pangetokea watu aina yangu ambao wanasiasa ninatofautiana nao tungeweza kujenga maada na kujadiliwa bila ushabiki ninaousoma kwenye comment zenu.
Chadema ni wapinzani na kazi yao ni kupinga (na mpaka sasa wanaifanya kazi yao) wakianza kusifia chama tawala hapo taanza kuwaandama kwamba wameshindwa kazi


Tubadilike jamani hawa wanasiasa sio wakweli hata siku moja na hao mnaowashabikia wakichukua dolla mtawachukia na kuanza kuwazomea japo hamtakubali lakini iko siku mtakubali maneno yangu, kumbukeni siasa ndiyo ajira yao na ili wawe wazuri ni kuongea maneno mazuri tu.

Mkuu mimi ninaamini kwamba bila upinzani nchi haiwezi kwenda.., ndio maana nataka CCM ife au igawanyike katika vipande vingi vidogo vidogo ili kusiwe na chama chenye nguvu nyingi zaidi kuliko chama kingine.., na hawa wapinzani wakichukua dola wakichemsha bado kutakuwa na upinzani ambao tutaungana nao.., hapa hakuna ushabiki wa kama Simba na Yanga.., tunaangalia ni nani anafanya na nani hafanyi.., (na kwa miaka 50 hawa waliopo hawajafanya kitu) hatujui hawa wakiingia watafanya nini (ila uoga wa kutokujua usitufanye tubaki na uozo)
 
Back
Top Bottom