Wabunge wa CCM mnawachezesha Watanzania "kwata" la akili!

Vasco daggama atakuja lini? Mimi nawashauri ikulu wamweekee recording ya leo bungeni ili na yeye asikilize
 
Tatizo kubwa la wabunge wa CCM ni 'Wbunge-Masilahi', wengi wanaangalia je bunge lijalo CCM itaniteua kugombea jimbo langu?, na kwa kuwa wamezoea kuwa ukiwa mgombea wa CCM ni mshindi wa uchaguzi mkuu by dafault. Yaliyotokea Arumeru East, Nyamagana et al yamewatisha sana. Wanajua fika kuwa 2015 wananchi watalinda kura zao kama ilivyofanyika sehemu hizo na kuwalazimisha kinyume chake ni kuliingiza taifa kwenye mgogoro usio wa lazima.

Wameona kuwa njia pekee ya kupata kura halali za wananchi ni kuanza na 'Ada ka dabra' za kuwaonesha wananchi kuwa wapo bungeni kwa ajili yao. Kwa Lugha nyingine wanataka kujitenga na serikali pamoja na chama kilicho unpopular kwa wananchi wakati huo huo wakiendelea kupitisha yale yale wanayoyakemea. Yaani hii ni sawa na kusema 'Nguruwe haramu ila supu yake tamu'.

Kama kweli wanataka tahafifu 2015 wawe huru kujiamulia siyo kupelekeshwa na kina Wassira et al. wakubali kuanza na katiba mpya ya watanzania isiyokuwa na upendeleo kwa CCM maana ndiye wanayemlalamikia. Walipoteza fursa hiyo toka mwanzo ila wanaweza itumia kwenye sheria zilizobaki. Ule usemi wa masilahi ya chama kwanza uwe ni taboo badala ya wimbo wa kuoneshana nani kada mzuri.

Vyovyote watakavyofanya kwa kawaida kutokana na hali ya uchumi na maisha ya watu ni lazima washindwe uchaguzi na kama matokeo yatakuwa tofauti yatakuwa haya-reflect voters demands.
 
Kwata la CCM ni chafu kwa wananchi, mkumbuke tume ya uchaguzi( wote) ni usalama wa taifa, waandishi wengi wa habari, viongozi wengi wa dini, waalimu wengi-mara nyingi ni mawakala wakati wa chaguzi, viongozi wa halmashauri, mahakimu na wengi kwa kila taasisi ya serikali. Iko siku kwani Kenya nayo si ilikuwa na mfumo kama Tanzania kwenye chaguzi. Eee Mwenyezi mungu tusikilize waja wako.
 
Hii ya leo ya wabunge wa ccm ni purely dalili za mfa maji,, au ile siku ya kufa nyani.
Tatizo hawataki kumvika paka kengele na kusema ukweli ulio wazi kuwa uongozi wa chama chao kwa sasa ni dhaifu mno! Mwenyekiti mzururaji, Katibu mkuu ni kilaza na mzee anayekula pensheni hivyo hajishugulishi na kazi za presha. Sekretarieti imeoza, Nape hayuko secured anaishi kama popo kulala mchana usiku mahangaiko, Mwigulu yuko kimaslahi zaidi, January yuko busy anachanga karata akijua future yake kisiasa ni ngumu baada ya 2015. Ukija kwa Lusinde ni kichaa, wapambanaji wa ufisadi wamekataliwa na wananchi katika chaguzi za juzi, je wapi chama kitajishika? Jibu no, kinachungulia kaburi
 
Wabunge wa CCM ni Wanafiki hadi wanakinaisha. Dawa yao ni ndogo sana.

Ninaomba Wabunge wa Chadema wamuwekee KURA YA KUTOKUWA NA IMANI Waziri wa Fedha na Afya na sijui nani na tuone kama CCM watapiga kura kuwaondoa au laah.

Wakipiga kura ya HAPANA, Chadema iende kuwashitaki kwa wananchi wao kuwa Wabunge wao wanajifanya wakali bungeni lakini hakuna lolote kwani ikija kwenye kumsulubu mtu, wanaUFYATA.

1a1a1a1a1a1asweet-girl-scar.jpg

Na hapo Chadema wataonyesha kuwa ni Watetezi kwelikweli. Watakuwa ni kile kishoka kidogoo kilichonolewa vizuri sana tayari kuufyekelea mbali ule mti Mkubwaa (Bob Marley - Small axe).
 
Mimi nimekereka sana tena si kidogo, kwani niliamua kuzima runinga lakini nilipokwenda twitter nikakuta vichwa pasi wakihenyeshwa kuaminishwa kuwa bunge la ccm leo limekuwa bunge la wananchi,

Imeniwia vigumu sana kuamini na kamwe sijaamini kama kweli watu wa pale twitter na hapa jf ninao waamini ktk hoja zenyemafaa leo wanashangilia mazingaombwe ya bunge!

Wabunge walewale hupitisha miswaada mibovu mpaka hata rais huwashangaa, leo haohao wanashtushwa na matokeo ya uabunuasi wao!

Mimi nitakuwa wa mwisho kabisa kuliamini bunge hili lenye kila akanyagae mlango wa bunge ni MWIZI!
 
hawawezi kumpigia kura waziri mmoja kutokuwa na imani naye; kama tatizo lao ni serikali njia pekee - na ndio NJIA PEKEE - ni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu (ndiye mwakilishi wa serikali). Tuone haw wabunge wa CCM kama watapiga kura hiyo.
 
Kuna yule mbunge mweupe flani hivi, Somebody Kessy Mohamed, jamaa anaongea kwa hisia kali sana!
 
hapa tunaibiwa mchana kweupe eti lukuvi naye anatetea upuuzi eti wazirii wa fedha yupo washington DC

Kila unapojaribu kuitetea ccm kwa sasa ndio unaiangamiza!! Bora ukubaliane tu na wanaodai haki!
 
hawawezi kumpigia kura waziri mmoja kutokuwa na imani naye; kama tatizo lao ni serikali njia pekee - na ndio NJIA PEKEE - ni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu (ndiye mwakilishi wa serikali). Tuone haw wabunge wa CCM kama watapiga kura hiyo.
from the look of thing and if Joni woKa hata ingilia, basi upepo wa kus unavuma kama utani

the damage is too big and PM is incompetent and tactic-less
 
on a serious note....

Mwanakijiji, kuna tofauti gani kati ya sisi tuliosapoti session ya leo na wewe uliyemsapoti william kwenye eala????
 
Kwa waliofuatilia bunge jana jioni watakuwa wamesikia kilio cha wabunge wakidai mafisadi wanaojinufaisha kwa raslimali za Taifa hili wanyongwe tena ikiwezekana pole pole ili wasife haraka. Na mmoja akaomba wapigwe risasi hadharani!

Lililo kubwa zaidi ni pale Magamba walipotangaza rasmi 2015 hawana chao! Maana pamoja na kwamba kauli ya Zambi siyo ya Msemaji wa Chama ila kwa maneno yake kwamba tusishangae 2015 CCM ikapoteza utawala ni ishara kwamba tayari Nguvu ya Umma inaanza kueleweka vizuri!

Wadau sasa ni wakati muafaka kuendeleza mapambano! Ukisikia Mh. Selukamba anadai Bunge halijawahi kufanya kazi yake na hata Raisi hawezi kuwatimua kazi Mawaziri wazembe! Tunasubiri nini kama si kueneza elimu ya Uraia ili 2015 mageuzi ya kweli yapatikane!

Imagine deni la Taifa leo ni 14Trilioni bajeti ni 13Trilion. Uchumi unakuwa kwa 6% wakati deni linakuwa kwa 36%! Mh. Keissy anadai wanetu na hapa nadhani hata wale walioko viunoni nao wakitoka wanadaiwa!

Enough is enough! Lets be part of change! Its now time for change! M4C

Naomba kuwasilisha!

Source: Bunge tarehe 18.04.2012 kama lilivyorushwa live na TBC baada ya kipinddi cha maswali na majibu!
 
Elimu ielekezwe vijijini Kwa nguvu na umakini, na lengo lisiwe kuiondoa CCM Bali lengo liwe kuuondoa udhalim popote ulipo, iwe ndani ya chama kinachotawala AMA vyama vinavyopigania kutawala kuna.
 
Nashangaa sana watu kukejeli hii hoja badala ya kuishabikia. Ikipigiwa kelele inawezekana.
 
Well said MM, Wnahitaji fikra mbadala; najua wanatamani kutoka tunduni lakini wanashindwa waanze vipi, tunahitaji kuwapa ushauri na kuwaonyesha njia; sio kuwakandya na kuwa dharau.
 
Back
Top Bottom