Wabunge wa CCM mnawachezesha Watanzania "kwata" la akili!

Nakipenda chama cha mapinduzi lakini siwapendi baadhi ya wanachama na hasa viongozi wake kwa kuwa wamejaa unafiki tu.
Inashangaza na hadi nashindwa elewa kama kuna mtu anaejua nini hasa majukumu yake na nguvu alizonazo kwenye nafasi anayoiongoza.
Wewe ni mbunge kazi yako ni kulalamika tuuu bila kuchukua hatua za kurekebisha matatizo yanayowakabili wananchi.
Nashangaa wabunge wameletewa taarifa ya ubadhirifu wa serikali na wao wanaanza kupiga kelele tu bila kuchukua hatua.
Ina maana hawajui wapo bungeni kufanya nini?
Au wanakuwa kama nyumbu,akisimama wa kwanza kulalamika na wao wanafuata mkumbo tu.
Taarifa za ubadhirifu kwenye ripoti ya CAG zinatoka kila mwaka.na hatua "kali" zaidi kuchukuliwa ni watu kuhamishwa kituo tena unatolewa kishapu unaadhibiwa kwa kupelekwa rombo kwa cheo kile kile....kuna mtu mwenye akili timamu hapa?
mwananchi akisoma taarifa hii atalalamika...
Na mshangao wa mwaka hata viongozi nao wanalalamika tuuu.
OTIS
 
Wamekamatwa pabaya mkuu,hawana la kufanya zaidi ya kubaki kupapasa tu gizani,come 2015 wataipata hukumu yao
 
hawawezi kumpigia kura waziri mmoja kutokuwa na imani naye; kama tatizo lao ni serikali njia pekee - na ndio NJIA PEKEE - ni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu (ndiye mwakilishi wa serikali). Tuone haw wabunge wa CCM kama watapiga kura hiyo.

Walau Mh. Tundu Lissu, ameligusia hili bungeni. Wasiwasi wangu, ni kwenye uungwaji mkono kama hoja ikiwasilishwa kwan kura nyingi zipo kwa wabunge wa CCM kutokana na wingi wao
 
Sisemi haya sababu ya chuki au sitafurahia hawa ndugu zetu wakianza uzalendo, (baada ya issue ya Ngeleja mwaka jana, baada ya watu kuja juu afukuzwe alafu mwisho wa siku wanamtetea), nadhani ni busara kujiuliza…., Je hawa ndugu zetu ?:-

Wamebadilika: Uzalendo umewaingia ghafla
Wanaogopa: Kwamba wakifanya mchezo 2015 hatutawaona tena (hili sio baya sababu mwisho wa siku tunachojali ni means to an end)
Unafiki: Wanajifanya kutetea ila nyuma ya mgongo ni business as usual
Changa la Macho: Wanajifanya kuja juu (kwamba watu wanyongwe) ila mwisho wa siku wanajificha kwenye kelele za Ndiooooo (sababu hatuwezi kujua nani kasema ndio au hapana)

Hivyo ndugu zangu inabidi tusisikilize tu bali tuangalie kwa matendo yao, kama mwisho wa siku wataendelea kusema ndio na kupinga hoja za kutengua sheria bila msingi (hawa jamaa watakuwa bado ni wale wale tu…)
wisdomeyes1024%20.jpg
 
Hamna kitu mpaka siku wakimpigia kura yakutokuwa na imani na kiongozi mkuu wa serikali wa shughuli za Bunge Kwa maana ya Waziri Mkuu hapo ndipo tutasema kweli wana nia vinginevyo ni daganya toto

Mi nadhani hata hapo wanaweza wakawa bado wasanii (hawa jamaa hakuna wanachoogopa kama maslahi yao, kutokurudi bungeni, hivyo hata wakibadilisha waziri mkuu (atapewa kazi nyingine ya kupeta / au watamwomba ajiuzulu) alafu atakuja mwingine (business as usual)

Mimi naona dawa ni kuwapunguza tu hawa jamaa hata iwe 50 / 50 yaani wapinzani nusu na chama tawala nusu, hapo Ndiooo zao zitakuwa hazina maana.
 
hawana lolote wanatoka povu ili tuone kune kitu wanaonge,tuwaulize ripoti za kamati zinazosimamiwa na wabunge wa ccm ziko wapi?
 
The threat and/or more CCM leaders crossing to CDM ... The More the Power shift ... from top CCM leaders to normal CCM members and hence the MPs empowerment!!! ... You touch anyone of them ..? Next day you know where to find HIM!!

AND honestly CCM must not toy around with this it can cost them great deal!!!!
 
jana serukamba alisema eti wabunge wakiongea sana bungeni, mawaziri wanasema wamajipigia debe kutafuta umaarufu
 
Kama nimemuelewa vizuri Mh Tundu Lissu .kama wabunge walio wengi wa ccm wangekuwa waadilifu na wanavyoongea wabunge wa CCM kwa hisi na uchungu wa nchi yao basi walishapiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.mimi naona wabunge wengi wa ccm ni wanafiki nawanaotaka kuonekana katika tv tuu.
 
jana serukamba alisema eti wabunge wakiongea sana bungeni, mawaziri wanasema wamajipigia debe kutafuta umaarufu

Nisingeona shida ya kupiga hilo debe kama kweli wapo genuine, lakini shida baada ya muda wanaanza kutetea tena polepole.., tumeyaona haya mwaka jana katika issue ya Anna Kilango na Ngeleja.., (ila nadhani sasa wamejifunza, wanapiga kelele alafu huenda wasitetee ila wakajificha kwenye kura za Ndioooo, sababu hapo hatuwezi kujua ni nani kasema ndiooo,

Nadhani ifike wakati kuwe na (button ili mtu akisema ndio, tujue ni nani kasema na nani amekataa)
 
Mbunge yoyote wa CCM simuamini hata kidogo hata angekua ndugu yangu wa damu haaamini, hawana msimamo kama 'indi
viduals' kila kitu mpaka chama..,wako hivyo ni afadhali ya kinyonga..wakishakutanishwa kwenye hiyo caucaus yao basi watarudi kikao kijacho wadogo utadhani sio hawa leo wanaotoka povu eti wanamuonea uchungu mkulima maskini wa nchi hii...walishapata nafasi nyingi za kuonesha makucha hawkufanya hivyo badala yake mwishoni hawahudhurii vikao afu waliobaki wanapitisha kwa ma-ndioo yao..

Ni imani yangu kama alivyoombea Zambi,2015 kisirudi madarakani kwa miaka mingine 500..nchi itakuwa imestabilize na machungu ya ulafi na kutowajibika kwao..!
 
hapo umenena kweli mkuu,kwani siku zote hawaoni kuwa serikali hii haiwasikilizi?,kila kukicha ni ufisadi tu.
 
Hao Wabunge wa CCM ni kama yule mdudu washawasha akikupata hakuachii,wamejiumbua sana, wao wanaingia kwenye vikao vya halmashauri kwa sababu na wao wanakuwa kama madiwani wanapohamishia kesi kwa mawaziri wakaacha wenyeviti wa halmashauri na mameya hapo mimi naona ni unafiki wa hali ya juu
 
Back
Top Bottom