Wabunge wa CCM wote ni wasanii. Zikipelekwa hoja za kuziba mianya ya ufisadi, wanakuwa wa kwanza kuzipiga mawe. Juzi wote tumeona jinsi walivyoikataa hoja ya JJ Mnyika ya kutaka kuthibiti ufisadi kwenye mashirika ya umma.
Mbunge Erasto Zambi anasema, "Twende kwenye kikao cha wabunge wa CCM tukafanye uamuzi. Maana hapa Bungeni hatuwezi kumaliza". Sasa kama swala lina maslahi kwa Taifa kwanini lisimalizwe hapo Bungeni? Hata Richmond ilimalizwa kisanii hivi hivi huko kwenye vikao vya wabunge wa CCM pembeni, mjadala ukafungwa bila serikali kutekeleza maazimio ya Bunge.
Serukamba anasema, "watumie kanuni za kuwabana mawaziri wasiowajibika na wanaopindisha mambo bila ridhaa ya Bunge". Mawaziri wangapi mpaka leo hii ambao wametakiwa na Bunge wajiuzulu na hawajafanya hivyo? Kama wanataka Baraza Jipya, wapige kura ya kutokuwa na imani. Bado hata hiyo siyo suluhisho la ufisadi unaoendelea.
CCM wamekuwa wakipitisha sheria za ajabu ambazo zimejaa discretion za watendaji na hivyo kuwapa mianya ya kufanya madudu kwa jinsi wanavyojisikia na hakuna lolote linalofanyika.
Kwa hiyo wabunge wa CCM ndio ambao wamekuwa wakiilea serikali yao ambayo inajifanyia mambo yake jinsi inavyopenda na wabunge wa CCM wamebaki kuwa wacheza sarakasi. Sasa hivi tutaona sarakasi nyingi kuelekea 2015.
Chaguzi ndogo za kati ya 2006 na 2010 waliwatumia sana hawa wabunge wanaojiita wapiganaji ili ku-neutralize hoja za ufisadi. Sasa hivi wamejaribu kuwatumia Kirumba, Kiwira na Arumeru, kote huko imekula kwao. Sasa wameanza sarakasi na mazingaombwe ya kuandaa timu mpya ya "wapiganaji" kuelekea 2015 na ndio maana wamekuwa wakii-refer mara kwa mara baada ya kugundua ile timu ya mwanzo ama imepoteza mvuto au watu wameanza kuamka.
Kinachonisikitisha ni kwamba wakati mwingine watanzania ni wepesi sana wa kuwa carried away na hizi sarakasi za CCM, yaani juzi tu tumeona jamaa wanakomaa na hoja ya Mnyika, leo tayari tunasema Bungeni kumewaka moto. Hata siku ya Richmond moto uliwaka, watu tukajua sasa serikali itashikishwa adabu, matokeo yake tunajua. Baada ya hapo, kila kinachoendelea Bungeni huwa ninaona ni sanaa na mazingaombwe ya kuendelea kuwaibia watanzania ili wawe na imani na wabunge wa CCM na hivyo uchaguzi ujao CCM irejeshwe madarakani na mambo yanaendelea kama kawa.