Viongozi wa serikali, taasisi futurisheni kipindi cha mfungo wa Kwaresma

Mtuturas

JF-Expert Member
Apr 18, 2017
458
859
Imekuwa kawaida kipindi cha Mfungo wa ramadhani viongozi wa serikali, taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kufuturisha.

Sasa basi ili kuondoa dhana ya upendeleo au double standard ni vyema basi katika kipindi hiki cha Mfungo wa Kwaresma basi futari ikaandaliwa pia na taasisi hizo.

Ni vyema Ikulu ikaandaa kitu kama hiki nakumbuka Rais Magufuli pamoja ni mkristu alifuturisha Ikulu. Mawaziri, Ma RC na Ma DC na nyie pia muandae futari ya namna hii Kwa wadau wenu ili kuboresha mahusiano Kwa kutumia Mfungo wa Kwaresma.

Na nyie maaskofu ie TEC andaeni futari kipindi hiki muwaalike viongozi wenzenu wa kiserikali au Waislamu mjumuike pamoja kwenye futari. Kama Bakwata wanavyowaalika kwenye futari wanazoanda kipindi cha Mfungo wa Ramadhani.

Na taasisi nyingine kama voda, tbl muandae futari kipindi hiki cha Kwaresma kama mnavyofanya kipindi cha Ramadhani.

Mwisho nawatakia Mfungo mwema wa Kwaresma wakristu wote.
 
Mbona humu leo mmefungua Uzi.mmeambiwa na padri nyinyi hamuna maswala ya futari hapa naona mnataka kufuturishwa tena

Kweli kazi ipo.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Huyo padri atakuwa amepotosha kimsingi suala la kufunga Kula kuanzia asubuhi na mchana na kufungulia Jioni lipo kipindi hiki cha kwaresma , yaani ni kama vile ndugu zetu waislamu.
Kwa hiyo tunatakiwa tutendeane haki Kwa sie tunaofunga .
 
Wakristo hatuhitaji kufutulishwa na mtu. Maana uwezo wa kufutulu wenyewe na kwa wakati wetu; tunao.
 
Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.

Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;

ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi
 
Vitu vingine si muhimu sana,then funga ya wakristo siyo ya show off kama ya Waislam muda wote wanavizia adhana jioni.......so haina haja huo ushauri kifanyiwa kazi
 
Huyo padri atakuwa amepotosha kimsingi suala la kufunga Kula kuanzia asubuhi na mchana na kufungulia Jioni lipo kipindi hiki cha kwaresma , yaani ni kama vile ndugu zetu waislamu.
Kwa hiyo tunatakiwa tutendeane haki Kwa sie tunaofunga .
Nashukuru maana nashangaa hapa haohao walio kua wanasapoti ule uzi wameanza tena kuusapoti na huu

Ngoja ninyamaze tu niwatakie kwaresma ya Amani

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.

Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;

ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi
Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;..

Lugha ya Biblia ni ngumu sana.
 
Back
Top Bottom