Fatma Karume amshauri Bashe kutotatua shida ya Sukari kipindi cha mfungo Ramadhani

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Kufuatia Sekeseke la udini baada ya Waziri wa kilimo Hussein Bashe kusema Kufikia Ramadhani sukari itakuwepo, Mwanasheria na mwanaharakati Fatma Karume amemshauri Bashe kutotatua uhaba wa sukari nchini.

Kauli hiyo ameitoa kwenye ukurasa wake wa "X",

"Ushauri wangu kwa Bashe: “Kifo cha wengi harusi!”.

Hakikisha hakuna SUKARI mwezi wa Ramadhan ili kuwe na HARUSI wa UHABA!

Nchi ina VIUMBE hii. No logic whatsoever." - Fatma Karume

Screenshot_20240223-114302.jpg

Fatma ameitoa kauli hiyo baada ya waumini wa Dini ya Kikristo kutofurahishwa na uwepo wa Sukari kipindi cha mfungo wa Ramadhani ilhali Kwaresma hakuna sukari inayotosheleza.

Nini maoni yako?

Written by Mjanja M1 ✍️
 
Hali kwakweli ni changamoto hivi kweli hatu wizara yenye dhamana na masuala haya kweli?
 
Bora angesema sukari itakuwepo kuanzia mwezi machi kuliko kutaja neno ramadhan, inaleta hisia za kidini kwamba wengine dini yao mambo yake yanathaminiwa na serikali huku dini zingine mambo yake yakipuuzwa
Naomba nitofautiane na wewe kidogo. Ni ivi:
1. Ramadhani inaambatana na kula/vyakula. Ni sehemu ya Ibada kula vyakula vingi wakati wa Ramadhani.
2. Matumizi ya sukari ( na vyakula vingine) yanakuwa makubwa kwa vile inatumika sana kwenye uji, chai, na mapishi mengine yahusuyo mfungo.
3 Hivyo kuwahakikishai kuwa itakuwepo sukari si vibaya maana ni sehemu ya Ibada ya waislamu.
4. Kwaresima hawafungi vyakula kama Ramadhani, hivyo si hitaji muhimu Kwaresma.
 
Hamna mambo ya kwaresma wala ramadhani sukari inatakiwa iwepo.
 
Mkuu kula ni ibada kwa kila mtu sio waislamu tu, hata wapagani. Kusema utaleta sukari wakati wa ibada ya watu fulani ni kuwadharau wengine na ibada zao za kula.
 
Uko sawa kabisa, more than uko sawa: sasa kuna uhaba, sukari haipo. Kuna tukio muhimu la Ibada linakuja,. Unafanyaje kunusuru ibada? Unaweza kulegeza masharti ya uingizaji etc etc etc. Waislamu linpokuja suala la ramadhani wanataka sana kutimiza ibada........kuwapa kipa umbele sioni tatizo...
 
Mkuu kula ni ibada kwa kila mtu sio waislamu tu, hata wapagani. Kusema utaleta sukari wakati wa ibada ya watu fulani ni kuwadharau wengine na ibada zao za kula.
Kwaresima hatuna ibada ya kula. hatuna kabisa! ILA kila mmoja anataka sukari. Kuwapa kipaumbel waislamu na ramadhani, sioni tatizo
 
Back
Top Bottom