Ving'amuzi (speed limit) "ilikuwa" mradi wa kundi dogo la watu (CCM)

Siku mbili nyuma nilipanda Eicher kutoka Mpanda kwenda Uvinza, kwa kipande kile cha lami cha kilomita kama 30 hivi alikua anatembea above 90km/hr..... Mkuu mbona ni rahisi sana kujua!?

January hii iliyoisha Kuna mabasi ya Dar kwenda Mbeya yamepita Makambako saa kumi kasoro au na dakika chache....

Sauli &Goldeer kuingia Mbeya saa 12 ama 11 imekuwa kawaida yao.
 
Navyofahamu, ni gari zote za abiria hata hizi Coaster za mazishi zimewekwa vithibiti mwendo. Mimi binafsi ni mpenzi wa spidi kwa kuzingatia usalama lakini sijawahi panda bus linalokimbia zaidi ya 89kmh. Natamani unachosema iwe kweli. Nakumbuka miaka ile safqri ya Dar/Moro ilikuwa si zaidi ya saa 3 siku hizi hutoboi chini ya masaa 4.
huyu mleta mada kafanya utafiti wa gari moja tu, magari mengi mno yamefungwa hivyo vifaa, na syo jukumu la madereva bali wenye magari wenyewe maana hata wao wanakosa amani magari yao yanapokuwa hayana hivyo vifaa.
 
Siku hizi madereva wanatumia radar detector, ile bar ikianza kujaa kuonesha tochi ipo karibu ndio wanapunguza mwendo..radar nazo zimekua majanga
 
Naomba ku-declare interest kuwa Mimi ni mdau WA safari (abiria) WA mara Kwa mara 75% nikiwa natumia bus.

Niliwahi kuandika kuhusu "uhuni" wa kile kinachoitwa ving'amuzi kwenye mabasi.

Leo hii mabasi mengi yaliyosajiliwa kuanzia 2020 hayajafungwa ving'amuzi au vipo na havifanyi kazi! Mabasi ambayo hizo speed limit zinafanya kazi ni Yale ya maskini TU. .

Kwa mfano, Ajali ya Bus la Kampuni ya Frester, hakuna popote pale taarifa inayoonyesha mwendo aliokua anaendesha dereva. Narudia HAKUNA!

Wiki iliyopita nilielekea maeneo ya Nzega, nilirekodi speed ya mabasi kadhaa ikiwa ni above 90km/hr hadi 130km/hr. December 2022 mara tano kwa mwezi huo nilisafiri kwenda Tanga kutoka Dar, mara mbili Kwa gari binafsi na mara tatu Kwa bus!

Hakuna bus hata Moja, yote yanatoka Mbezi asubuhi kupitia Bagamoyo Road, hakuna bus lililokua linatembea chin ya speed 100km/hr.

Sasa unajiuliza, hivi ving'amuzi vililetwa kwa ajili ya akina nani? Kama tumeshindwa kusimamia basi tuseme kwa uwazi.

Muda huu ni 01:20 usiku, basi nililopo Lina speed governor (Yale ya zamani) Kuna mabasi kadhaa yametupita utadhani tumesimama!

Mamlaka husika zitoe tamko RASMI la kuondoshwa Kwa speed limit ili wachache wasiwe waathirika.
Kawaida hiyo,hivyo vimiradi hutayalishwa Ili wakubwa wapige,Kuna ile tender ya kuweka biometric devices kwenye vituo vya polisi,ile alipewa mkwe wa Kikwete,Lugumi,jamaa alipewa mpunga wote hata kabla hajaleta kifaa chochote,pesa akapiga,Jiwe alimuweka ndsni,alipokufa tu,jamaa akaachiwa,
 
huyu mleta mada kafanya utafiti wa gari moja tu, magari mengi mno yamefungwa hivyo vifaa, na syo jukumu la madereva bali wenye magari wenyewe maana hata wao wanakosa amani magari yao yanapokuwa hayana hivyo vifaa.
Hebu rudia kusoma nilichoandika tafadhali, soma kwa utulivu!
 
Kawaida hiyo,hivyo vimiradi hutayalishwa Ili wakubwa wapige,Kuna ile tender ya kuweka biometric devices kwenye vituo vya polisi,ile alipewa mkwe wa Kikwete,Lugumi,jamaa alipewa mpunga wote hata kabla hajaleta kifaa chochote,pesa akapiga,Jiwe alimuweka ndsni,alipokufa tu,jamaa akaachiwa,
Hahahaahaha this life buana
 
Nakubaliana na wewe mkuu, kuna siku nimepanda MM8 tokea moro kwenda Mbeya aisee jamaa wanatembea 130km/hr kwa muda mrefu tu.

Bila shaka huenda hivyo vifaa vinachezewa baada ya kuwa vimefungwa.
Asante sana
 
Ninayo hiyo app huitumia kila ninapohisi basi linaenda kasi. At least hiyo screenshot uliyotuonyesha jamaa yupo within speed limit.

Update: Nimeona hio screenshot ingine kweli jamaa wako above speed limit.
Naipataje /naitafuta kwa jina gani hiyo app boss?
 
Navyofahamu, ni gari zote za abiria hata hizi Coaster za mazishi zimewekwa vithibiti mwendo. Mimi binafsi ni mpenzi wa spidi kwa kuzingatia usalama lakini sijawahi panda bus linalokimbia zaidi ya 89kmh. Natamani unachosema iwe kweli. Nakumbuka miaka ile safqri ya Dar/Moro ilikuwa si zaidi ya saa 3 siku hizi hutoboi chini ya masaa 4.
UNa ishi nchi gan w jamaa
 
Ushahidi mwingine ni ile ajali ya Bus la Mbeya to Tanga, iliyoua watu wa kutosha TU, ilikuja kuwa confirmed kuwa mara ya mwisho king'amuzi kilikua kinafanya KAZI kama one hour ago before disaster na hapo pia ilikua above 100km/hr.

Ushahidi mwingine ni thread ambayo nilianzisha humu kwa evidence pia nikiwa natoka Dodoma kwenda Njombe ambapo nilirekodi speed ya bus kuwa kati ya 135km/hr hadi 140km/hr kuanzia Makambako hadi Njombe usiku wa saa saba
Duh ! Huyo alikuwa ni dereva chinjachinja !!
 
Naomba ku-declare interest kuwa mimi ni mdau wa safari (abiria) wa mara kwa mara 75% nikiwa natumia bus.

Niliwahi kuandika kuhusu "uhuni" wa kile kinachoitwa ving'amuzi kwenye mabasi.

Leo hii mabasi mengi yaliyosajiliwa kuanzia 2020 hayajafungwa ving'amuzi au vipo na havifanyi kazi! Mabasi ambayo hizo speed limit zinafanya kazi ni yale ya maskini tu.

Kwa mfano, ajali ya bus la kampuni ya Frester, hakuna popote pale taarifa inayoonyesha mwendo aliokua anaendesha dereva. Narudia HAKUNA!

Wiki iliyopita nilielekea maeneo ya Nzega, nilirekodi speed ya mabasi kadhaa ikiwa ni above 90km/hr hadi 130km/hr. December 2022 mara tano kwa mwezi huo nilisafiri kwenda Tanga kutoka Dar, mara mbili kwa gari binafsi na mara tatu kwa bus.

Hakuna bus hata moja, yote yanatoka Mbezi asubuhi kupitia Bagamoyo Road, hakuna bus lililokua linatembea chin ya speed 100km/hr.

Sasa unajiuliza, hivi ving'amuzi vililetwa kwa ajili ya akina nani? Kama tumeshindwa kusimamia basi tuseme kwa uwazi.

Muda huu ni 01:20 usiku, basi nililopo lina speed governor (yale ya zamani), kuna mabasi kadhaa yametupita utadhani tumesimama!

Mamlaka husika zitoe tamko rasmi la kuondoshwa kwa speed limit ili wachache wasiwe waathirika.
Una hoja lakini huna taarifa
Hakuna speed governer kwenye mabasi kwa sasa , bali kuna gps module ambayo inafanya kazi kama vehicle tracking sytem, controler wa mfumo huu ni Latra,
Next time ukiona basi linakimbia hovyo , jua kuwa wadau wana maelekezo ya hao hao latra officials , ni rushwa .
 
Asante kwa kunirekebisha Lugha!
 
Una hoja lakini huna taarifa
Hakuna speed governer kwenye mabasi kwa sasa , bali kuna gps module ambayo inafanya kazi kama vehicle tracking sytem, controler wa mfumo huu ni Latra,
Next time ukiona basi linakimbia hovyo , jua kuwa wadau wana maelekezo ya hao hao latra officials , ni rushwa .
Umetumia neno zuri sana MAELEKEZO

Leo nilikuwa nasafiri kwenye basi moja hivi wakawa wakipitwa na wenzao wanasema hilo basi lina MAELEKEZO hivyo halikamatwi.

Mchana kutwa nikawa najiuliza haya MAELEKEZO yanatolewa na nani? Yanaenda kwa nani? What if Askari mmoja akaenda kinyume na MAELEKEZO akakamata moja ya hayo mabasi? Kiukweli we have a rotten system
 
Bro
Ukisikia "Maelekezo" , ni notoruously vicious cycle! Normally controller anakuwa wa kwanza kuona basi linalo over speed , pili kuna ground crews , hawa wana manual timetable na wanakaa kwenye vituo vya mabasi, wao pia kama basi lililimbia mahala wanajua kwa sababi ni lazima litawahi kufika kwenye kutuo,, then kuna askari, kiufupi basi lenye maelekezo linatoboa kwenye uangalizi wa makundi yote hayo.
It is a very expensive hobby too! Maana mzunguko inabidi uhusishe kundi kubwa la watu,
 
Navyofahamu, ni gari zote za abiria hata hizi Coaster za mazishi zimewekwa vithibiti mwendo. Mimi binafsi ni mpenzi wa spidi kwa kuzingatia usalama lakini sijawahi panda bus linalokimbia zaidi ya 89kmh. Natamani unachosema iwe kweli. Nakumbuka miaka ile safqri ya Dar/Moro ilikuwa si zaidi ya saa 3 siku hizi hutoboi chini ya masaa 4.
Coaster nyingi dash yake Inaishia 80km/hr hiyo speed governor wanaweka ya nn...alafu jamaa yangu atofautishe
kati ya speed na velocity..gari zaweza kuwa ata the same speed but in different velocity
 
Back
Top Bottom