Vicent Nyerere (CHADEMA) amwaga luninga sokoni

Ha ha haa NYINYIEMU........Hapa unabomu FLANAZ

1+(2).jpg
yaani nimecheka sana tena kwa sauti sasa hapo nepi anashangaa kichina mpaka kakunya uso tehtehetehte
 
Kwanini hizo million 9 asitoe waboreshe hiyo miundombinu ya soko kama mifereji na mapaa! mwisho wa siku mtakuja kuambiwa TV alizonunua mbunge zimenyeshewa na mvua kwa kuwa paa bovu,
soko lenyewe hoi kama sisi kwa sisi manzese!
 
duu!!! yaani ndo kaona ni kipaumbele kununua T.V nakuziweka sokoni ,huyu kamanda mbaya, yaani ni noma!! waekee na pooltable mzee.....usisahau mahospitalini maana wagonjwa na wao wanahitaji mahabari ya kutwa nzima huku wakiwa ktk dozi zao......ila bora wewe kuliko kamanda mwenzio wa ARUSHA yeye huwa anawanunulia viroba baadhi ya wapiga kura wake!!! ...........hii ndo chadema bana!!!
 
duu!!! yaani ndo kaona ni kipaumbele kununua T.V nakuziweka sokoni ,huyu kamanda mbaya, yaani ni noma!! waekee na pooltable mzee.....usisahau mahospitalini maana wagonjwa na wao wanahitaji mahabari ya kutwa nzima huku wakiwa ktk dozi zao......ila bora wewe kuliko kamanda mwenzio wa ARUSHA yeye huwa anawanunulia viroba baadhi ya wapiga kura wake!!! ...........hii ndo chadema bana!!!
View attachment 67228Bora ya huyu.
attachment.php
 
Hivi tatizo la wananchi wa Musoma Mjini ni runinga.
 
Hongera Vicent japo nahisi hukufanya tafiti ya kutosha kujua mahitaji ya kina ya watu wako. Mfanyabiashara haitaji TV tena katika eneo la soko hilo ambalo vibaka wa kumwaga.Hawezi kuuza nyanya zake ama vitungunguu kwa kutizama TV huku akihitajika kurudisha chenji na kumkaribisha mteja. Radio kwa maana ya mawasiliano ni muhimu kwa kazi zao maadam taarifa za habari nyingi katika TV ni nyakati za usiku na huwa majumbani .Hapa umuhimu wa TV ni mdogo sana na hasara yake ni kubwa hasa kuibiwa huku akishangalia vipindi vya TV.

Soko linavuja hasa nyakati za mvua, ungetumia nguvu hiyo ya milioni 9 kwa kuhamasisha wananchi nao kuchangia ungekuwa umefanya la maana sana tena la kihistoria. Wasi wasi wangu ni hizo TV kunyeshewa hatimaye kufa (e-waste production) ama kuibiwa na vibaka kisha kuzua tafrani humo sokoni.

Ni kazi nzuri lakini issue ya TV kwa sasa tena 9 sokoni kwa kazi gani? Hapo mjini na maduka hayo TV kibao .Hii ni mis-use of resource kwenye project ambazo hazina impact kubwa kwa jamii.Hongera kwa kuthubutu japo next time unawezakufanya makubwa zaidi japo kwa fedha ndogo uliyonayo. Ni heri kuliko wale "wahongaji" kupata vyeo tena nyakati za uchaguzi.
 
IJUMAA, OCTOBA 05, 2012 05:55 NA DOROTHY CHAGULA, MUSOMA

MBUNGE wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (CHADEMA), amekabidhi runinga 10 kwa wafanyabiashara wa soko kuu la Musoma mkoani Mara. Mbunge huyo alikabidhi runinga hizo jana, zenye thamani ya Sh milioni 9, katika eneo la ndani ya soko hilo lenye wafanyabiashara wengi.

Nyerere alisema kuwa, wafanyabiashara wa sokoni wamekuwa wakikosa haki ya kupata habari za uhakika, kutokana na kushinda kutwa nzima sokoni.

“Wafanyabiashara wa sokoni ni watu wa kuhangaika, hawana televisheni katika maeneo yao ya kazi na wanaporudi nyumbani, hupata habari za kusikia kwa watu,” alisema.

Amesema runinga hizo zitawasaidia kupata habari za mambo mbalimbali yanayoendelea nchini, ikiwa ni pamoja na uendeshwaji wa vikao vya Bunge.

“Wanapitwa na mambo mengi, vikao vya Bunge huanza asubuhi muda ambao wafanyabiashara hawa wapo sokoni, wanakosa haki ya kupata habari,” alisema.

Akipokea runinga hizo kwa niaba ya wafanyabiashara, Ofisa Biashara wa Manispaa ya Musoma, God Machumu, alimpongeza mbunge huyo kwa kutimiza ahadi yake kwa wananchi.

Mbali ya kupokea runinga hizo, wafanyabiashara hao walimweleza mbunge huyo changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika soko hilo.

Miongoni mwa changamoto hizo, ni pamoja na usumbufu nyakati za masika, kutokana na soko hilo kujaa maji, hali inayosababishwa na soko hilo kukosa mitaro ya maji.

Tatizo la ulinzi katika soko hilo limeelezwa kuwa, kikwazo katika maendeleo ya wafanyabiashara hao kwa madai kuwa, wamekuwa wakiibiwa mali zao kutokana na kutokuwepo kwa ulinzi wa kuaminika.


Inapendeza sana kwani hiyo ndiyo njia nyingine rahisi zaidi ya kufikisha majibu/habari kwa wapiga kura wako. VIVA Nyerere.
 
Wacha uongo hizo bei za Sony ndio kanunua Vicent Nyerere, bei yake bongo milioni 1.2 hawezi kununua, amenunua kachala za China Sony Sh300,000 kila runinga moja.
Sasa unawashwa nini? Si uende mahakamani?
 
Tv kumi za kichina eti amwaga,heading ya sredi haiendani kabisa na kontenti iliyomo
 
Hivi tatizo la wananchi wa Musoma Mjini ni runinga.
Je, maisha bora kwa kila Mtz yataondolewa na kupewa kofia na kanga au elimu kwanza?! Sometimes Mzee wa nywere nyeupe yupo sahihi anapoipinga propaganda ya mtoto wa mkulima ya kilimo kwanza. Kumbuka habari ni elimu tosha ya kupiga hatua.
 
Wacha uongo hizo bei za Sony ndio kanunua Vicent Nyerere, bei yake bongo milioni 1.2 hawezi kununua, amenunua kachala za China Sony Sh300,000 kila runinga moja.

Ritz mbona hata kidogo kinachofanya na makamanda hau-appreciate? Wakati hao jamaa zako hata kidogo kama hicho wameshindwa kukifanya?
 
Mambo ya kugawa TV, Jezi, mipira ya football/netball, ni dalili mbaya kwa chama chenye kutaka kufanya mabadiliko!
 
Wacha uongo hizo bei za Sony ndio kanunua Vicent Nyerere, bei yake bongo milioni 1.2 hawezi kununua, amenunua kachala za China Sony Sh300,000 kila runinga moja.

Rizt kwa hesabu za kawaida tu , kama Vicent amenunua "kachala" za china ambazo ni Tshs 300,000 kila moja , basi kwa TV kumi ingekuwa ni Tshs million tatu ( 3,000,000) na sio million TISA! so kwa pesa hiyo TV moja amenunua kwa Tshs 900,000 which is not far from 1.2 million! inaonesha alipata punguzo dukani! Bravo Vicent!
 
Back
Top Bottom