Vicent Nyerere (CHADEMA) amwaga luninga sokoni

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
IJUMAA, OCTOBA 05, 2012 05:55 NA DOROTHY CHAGULA, MUSOMA

MBUNGE wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (CHADEMA), amekabidhi runinga 10 kwa wafanyabiashara wa soko kuu la Musoma mkoani Mara. Mbunge huyo alikabidhi runinga hizo jana, zenye thamani ya Sh milioni 9, katika eneo la ndani ya soko hilo lenye wafanyabiashara wengi.

Nyerere alisema kuwa, wafanyabiashara wa sokoni wamekuwa wakikosa haki ya kupata habari za uhakika, kutokana na kushinda kutwa nzima sokoni.

“Wafanyabiashara wa sokoni ni watu wa kuhangaika, hawana televisheni katika maeneo yao ya kazi na wanaporudi nyumbani, hupata habari za kusikia kwa watu,” alisema.

Amesema runinga hizo zitawasaidia kupata habari za mambo mbalimbali yanayoendelea nchini, ikiwa ni pamoja na uendeshwaji wa vikao vya Bunge.

“Wanapitwa na mambo mengi, vikao vya Bunge huanza asubuhi muda ambao wafanyabiashara hawa wapo sokoni, wanakosa haki ya kupata habari,” alisema.

Akipokea runinga hizo kwa niaba ya wafanyabiashara, Ofisa Biashara wa Manispaa ya Musoma, God Machumu, alimpongeza mbunge huyo kwa kutimiza ahadi yake kwa wananchi.

Mbali ya kupokea runinga hizo, wafanyabiashara hao walimweleza mbunge huyo changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika soko hilo.

Miongoni mwa changamoto hizo, ni pamoja na usumbufu nyakati za masika, kutokana na soko hilo kujaa maji, hali inayosababishwa na soko hilo kukosa mitaro ya maji.

Tatizo la ulinzi katika soko hilo limeelezwa kuwa, kikwazo katika maendeleo ya wafanyabiashara hao kwa madai kuwa, wamekuwa wakiibiwa mali zao kutokana na kutokuwepo kwa ulinzi wa kuaminika.

 
mpaka kufikia mwaka 2015 tutajua nani yuko kwaajiri ya tumbo lake au yuko kwa ajili ya wananchi..
 
hayo ndio maendeleo wala sio maneno tu. tunataka wabunge wenye vision kama huyu maana anaona mbali sana
 
Runinga 10 milioni 9? Kweli wanasiasa mmezidi sasa,tv zenyewe za china halafu mwatudaganya kitoto hv?
 
Kwa mbunge mchapa usingizi hawezi thubutu kufanya hivyo. Hongera sana V. Nyerere, hakika hawa wafanyabiashara watafanya maamuzi yenye uhakika zaidi hapo 2015. Maana wataona watatafakari na watachukua hatua (kufanya maamuzi).
 
Runinga 10 milioni 9? Kweli wanasiasa mmezidi sasa,tv zenyewe za china halafu mwatudaganya kitoto hv?
Nenda pale duka la Game- Mlimani City ukaangalie, ndio utajua unadanganywa kitoto ama kikubwa, siyo unatoa povu!
 
Hongera kwa uliyoyafanya

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Bravo..............................................

Mungu mkuu wa israel akubariki vicent nyerere.
 
Angekuwa analala bungeni asingetoa,tungoje wassira nae atoe Bunda nawapenda CHADEMA wakati wenzao wanapiga domo wao wanachapa kazi na kutimiza ahadi,
 
hongera mheshimiwa,ngoja tuendelee kujiliwaza wakati tukisubiria kuchukua nchi 2015.!
 
hongera mheshimiwa,ngoja tuendelee kujiliwaza wakati tukisubiria kuchukua nchi 2015.!

Hamuwezi kuchukua nchi 2015,labda kilimanjaro ijitangazie uhuru wake na kuitwa nchi,chadema ni chama cha wachaga.Over
 
Tumia busara wakati mwingine.......



[More Details]
Bravia LCD TV
Model : KLV40BX450

Bravia Engine 3
Full HD
Bravia Sync
MPEG Noise Reduction
HDMI X 2
Advanced Contrast Enhancer


Retail Price USD Approx. 558.63/- in Dubai

Wacha uongo hizo bei za Sony ndio kanunua Vicent Nyerere, bei yake bongo milioni 1.2 hawezi kununua, amenunua kachala za China Sony Sh300,000 kila runinga moja.
 
Back
Top Bottom