Halmashauri ya Kigoma Ujiji Iache Kusumbua Wafanyabiashara Wadogo

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Kusumbuliwa kwa wafanyabiashara wadogo soko la Mwanga Kaskazini Kigoma.

Chama cha ACT Wazalendo kimesikitishwa na kinapinga vikali maamuzi ya Halmashauri ya Kigoma Ujiji ya kubadilisha utaratibu wa shughuli za Wafanyabiashara ndogondogo wa soko la Malungu kata ya Mwanga Kaskazini.

Utaratibu mpya ulioanzishwa unalazimisha biashara zifunguliwe kuanzia saa 12:30 jioni badala ya saa 10:00 jioni. Pili, wafanyabiashara wanalazimishwa kuondoa meza zao kila siku na kuzipeleka nyumbani. ACT Wazalendo tunaona uamuzi huu ni kurudisha nyuma jitahada za kuwawezesha Wafanyabiashara wadogo ili kukuza kipato chao na kufanya biashara bila bughudha.

Aidha, utekelezaji wa uamuzi wa Halmashauri ya Kigoma Ujiji umesababisha manyanyaso, bughusha, usumbufu na matumizi ya nguvu kutoka kwa Mgambo wa Halmashauri kwa kuvamia mara kwa mara eneo hilo la soko na kupora bidhaa, kuwapiga wananchi na kuvunja meza za Wafanyabiashara wadogo wakiwa kwenye maadalizi ya kufungua biashara zao.

Ikumbukwe kuwa Halmashauri hii iliyoongozwa na ACT Wazalendo 2015-2020 ndiyo ilianzisha soko hilo la jioni ili kuwapa nafasi na muda wa kutosha wafanyabiashara wadogo pamoja na wananchi kupata mahitaji na kipato katika soko hilo maalum kama hatua ya kuhakikisha tunajenga miji ya wote kwa maslahi ya wote. Kwa kuruhusu shughuli za uzalishaji na huduma ili watu waweze kujipatia kipato chao na kukomesha manyanyaso.

ACT Wazalendo tunaitaka Halmashauri ya Kigoma Ujiji isitishe mara moja utaratibu mbovu ulioanzishwa ili kutoa nafasi ya wananchi hao kuendelea na shughuli zao kwa uhuru na amani.

Pili, tunawataka Madiwani wote wa Kigoma Ujiji kurejea maamuzi yao na kufuta Azimio hilo dhalimu ili kuondoa manyanyaso na vilio vya wananchi.

Imetolewa na;
Naibu Waziri Kivuli TAMISEMI
Ndg. Hussein Juma Ruhava

Na
Naibu Waziri Viwanda na Biashara
Ndg. Julius J. Massabo

09 Januari 2024
 
Uchuuzi unapaswa kupigwa vita nchi nzima,Biashara za uchuuzi ni chaka la wanasiasa kutafuta kura,ila yakunaFaida kwa nchi,Hakuna nchi Duniani inahamasisha uchuuzi zaidi ya Tanzania
 
Back
Top Bottom