fiksiman
JF-Expert Member
- May 17, 2008
- 402
- 104
Jamani sina nia ya kumtusi mtu ila tuache tabia ya kuweka picha zinazofanana na zeutamu....nimekuwa nikitalii kwenye thread mbalimbali lakini kikubwa si kupata maoni bali kuona namna wanaJF wanavyoshindana kuweka vibwengo kwenye profile picha zao. Kuna zingine zinamwelekeo wa kuwavunjia watu tena wazito heshima zao...kwa mfano nimekutana na picha ya komrade mugabe, bush, obama na wengine wakiwa katika mazingira tata.
Cha kushangaza hata hao wanaojiita masenior na premiure wa JF nao ndo kabisa aibu tupu...kwa mfano kuna mdau mmoja kaweka picha nyani ana gitaa, njiwa anasoma kitabu yaani nisiseme mengi. Ila kiukweli inatoa burudani kusoma post huku kibwengo kikitia mbwembwe...siku nilijisahau na kuanza kufuta scree ya laptop yangu nikidhani kimdudu kinatembea kumbe picha ya mdau wa JF.
Nimeonelea nitoe angalizo hili hasa kwa kile kilichotokea hivi karibuni kwenye ile blog chafu ya zeutamu....asiyeijua imekula kwake. JF ni jukwaa lenye heshima kubwa na kila anaetaka kuingia humu anajua kuwa ameingia kwenye ulimwengu mwingine yaani ukikosea unapewa adhabu na ukizubaa unakumbushwa sasa chonde chonde hili jamvi liendelee kuwa la heshima badala ya kutegana na picha zenu za ajabu ajabu..ooops nitaitoa ile ya kwangu pia..tehethehtehe