Uzinduzi wa kampeni za CCM Arumeru now...

Mkuu tunakutegemea kwa update, nipo hapa corner nirobi nimekutana na lori na cruisers zikitokea Monduli kuelekea Arumeru. Watu waliobebwa kwenye Lori wanaonekana wamechoka sana.

Nina wasiwasi watu hawa wanaobebwa na malori ndio huwa badae wanakuja pia kupiga kura bila kustahili wafuatiliwe
 
Hata mi ningekuwepo ningekuja kuburudika na bongo fleva na ukizingatia ubwabwa upo ningebeba na marafiki zangu baada ya hapo chademaaaaaaa
 
clip_image002.jpg
Sumari Juuuu
 
kama picha zinavyosema hapo juu....pamedoda kweli na hawajiamini kabisa
 
Asante kwa picha mkuu; hakika hali ni mbaya mno hapa

Mkuu hapo italuwa ni barabarani na sii uwanjani kwenyewe. Ivi wewe unadhani mpaka viongozi wa chadema wamehama mji unafikiri umati ulioko pale ni wa kitoto?
 
Sasa thred iko sawa, asante mkuu crashwise. endelea ukipata picha za motomoto kabla hazijakaa muda mrefu uzipakue humu.
 
Sina shaka kuwa kwa matamasha ya waimbaji watu watekwenda wengi kushudia hao Waburudishaji, ukiongeza na wanaosombwa na magari hilo halina ubishi.
Kazi ni kuhakikisha hao watu hawaondoki baada ya muziki. Au kuna Maaskari wa kuwazuia?
Kingine nachotabiri nia CCM kuanza kuvunja sheria na kanuni za uchaguzi, kwa uzoefu nilionao, CCM hawatakubali kuhitimisha mkutano wao saa 12.00 jioni kama walivofanya CDM jumamosi.
 
Mambo yanazidi kuwa mambo hapa USA river wakati mji wote ukiwa umepambwa kwa rangi za kijani na manjano.
Hali ilivyosasa
(1) Buruduni ya wasanii wa Bongofleva, maigizo na kundi la TOT tarabu zinaendelea katika eneo la tukio
(2) Wananchi wanafurahia burudani huku vijana wakiserubuka na Bongofleva yap CCM inawapa raha
(3) Mamia ya Rai na Wasio Rai wanaendelea kumiminika kotoka sehemu mbalimbali za Mji wa Arumeru na Wengine kutoka Arusha na Moshi
(4) Watu ni wengi haijawahi kutokea Tanzania yaani Arumeru ni full shangwe
(5) Viongozi wa Chadema wakimbia mji kwa muda kuepuka aibu ya kuzomewa
(6) Kiongozi wajuu kabisa wa CCM kuzindua kampeni hizi leo
(7) wanawake na binti ni wengi kuliko unavyofikiri
(8) maandamano yanatarajiwa kuanza kutoka sehemu kuu nne ikiwa upande Kaskazini yataongozwa na Samweli SITTA,Kusini Chenge, Mashariki Chiligati na Magharibi ni Nape na Rostamu

Tutaendelea kuwajuza yatakayokuwa yanaendelea kila dakika kutoka hapa USA River stay tuned usitoke

Mkuu unaonekana umeingilia frequency!! Kwa nini usiwaachie CCM wenyewe wakatuletea updates mkuu. Huo ndio uungwana wa kipinzani. Unaonekana kuupotosha umma! Ila nimecheka baada ya kuona viongozi watakaoongoza maandamano.
 
Back
Top Bottom