Kampeni za Uchaguzi wa Diwani Kata ya Magubike Kilosa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,899
944

MBUNGE NORAH MZERU ASHIRIKI UZINDUZI WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA MAGUBIKE WILAYA YA KILOSA​

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Mhe. Norah Waziri Mzeru ameshiriki katika kampeni zinazoendelea za uchaguzi wa Diwani Kata ya Magubike Wilaya ya Kilosa.

"Nimesimama hapa kumuombea kura Ndugu Abuu Msofe kwa unyenyekevu mkubwa naomba msikiangushe Chama chetu, Chama Cha Mapinduzi (CCM) - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Kuanzia Rais awamu ya kwanza mpaka sasa awamu ya sita tumepata jemedari Mama Samia Suluhu Hassan, anatekeleza Ilani ya CCM 2020-2025 kwa kasi kubwa. Miradi mikubwa ya kimkakati inaendelea kutekelezwa kwa kasi kubwa nchini" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Rais Samia ameleta mageuzi makubwa nchini katika sekta zote. Ujenzi wa Shule na madarasa, Elimu bure mpaka kidato cha sita. Amemtua ndoo mama kichwani, Utalii, Umeme, Madini. Nchi imefunguka" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Nimesimama hapa kwa heshima na taadhima kukiombea kura Chama Cha Mapinduzi, ninaomba mumchague Ndugu Abuu Msofe awe Diwani wetu Kata ya Magubike" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro
 

Attachments

  • IMG_9038.JPG
    IMG_9038.JPG
    47.5 KB · Views: 6
  • maxresdefaultmnbvyut.jpg
    maxresdefaultmnbvyut.jpg
    106.6 KB · Views: 4
Back
Top Bottom