Uzinduzi rasmi wa JF Aprili 2010

Status
Not open for further replies.
Hongera JF team Mungu awape nguvu na hekima kwasababu kazi mnayoifanya ni ngumu lakini yenye manufaa makubwa kwa Tanzania kama nchi na wananchi wake kwa ujumla.
 
Nimefurahishwa kwa mara nyingine tena kujua kuwa JF inazidi kushika kasi kwa kwenda mbele. Keep it up moderators, tuko pamoja.
 
Hongereni sana wakuu,

Nimefurahishwa na mambo mengi aliyoyaongelea Invissible, JF mpya itatupa nafasi nzuri ya kuweza kushiriki katika mambo mbalimbali,

Ushauri
TV na Radio iwe na kazi mbili tu, kutuletea habari za ndugu zetu wanaonyang'anywa haki zao huko maeneo ya vijijini na ya pili ni kuwapongeza kwa dhati au niseme kutambua utendaji wa mawaziri wanaofanya kazi zao kwa maslahi ya watanzania na siyo kwa masilahi ya chama, binafsi au malengo ya kisiasa zaidi. Hawa watu hawana mitandao ya vyombo vya habari vya kuwasemea, na kwa maana hiyo wanabaki hawana support yoyote kutoka kwenye jamii wanayoitumikia.

Heshima wakuu.
 
Wakuu wa JF kwanza hongereni kwa kazi. Wengi tumepata sehem ya kuongelea, ila isiwe pumba.

Kuna suala moja nilipendekeza, nalo linahusu kutambua na kupewa taarifa ni thread gani ulichangia, maana yaweza kuwa umetuma post nyingi kwa topic tofauti. Pia inawezekana kuna mdau aliuliza swali likataka jibu na ww hujaingia kwenye topik iliyouliziwa swali. Angalau nimeeleweka kidogo
 
mweee !!! poleni kwa kazi wajukuu zangu na hongereni sana.Kuna siku tutawavisha nishani ya utumishi uliotukuka..hasa wewe Invisible
 
Si vibaya wakifika hata 10... Kama utaitaji msaada ni PM, nitajitolea.

You will be considered, utakaribishwa kwenye semina kwa moderators, huenda ukawa na uamuzi wa kuwa ndani ya kundi au kutokuwemo, tutakuarifu tarehe ya semina hiyo siku si nyingi.

Great achievement.. Congratulations...

Can you pls add gender button too... like blue for Gents and Pink for Ladies? sometimes it is confusing while discussing topic with member by just guessing their genders...

Thank you

Mkuu hili ombi lako gumu kidogo kulitekeleza... Nadhani issue ya gender ibakie ilivyo, yeyote anaweza kudanganya juu ya gender yake na si rahisi mtu ku-verify kuwa alichosema ni sahihi. Muhimu ni kuangalia hoja yake zaidi bila kujali jinsia au nafasi yake katika jamii.

Ni ukweli usiopingika kwamba wadau wengi wa JF wako dar,kwa mantiki hiyo ni bora uzinduzi huu,uambatane na kuwaalika wanachama wa Dar es Salaam, na wa mikoa jirani hii yaweza kusaidia kwa wanachama tutakaoukutana kuchangia na kujuana kiundani zaidi.
Ni pendekezo jema, litafanyiwa kazi haraka!

Where is Ole & Mbu

Nilikuwa nahisi Mbu ni Moderator wa JF. Kwa jinsi alivyoandika katika "thread" fulani na kisha ikafungwa.
He once was a moderator (Mbu) but not now. Ole pia aliwahi kuwa moderator lakini kwa sasa si moderator tena.

....mimi naona kutokana na jinsi hii forum inavyoendeshwa redio au gazeti ndio ideal, lakini wachangiaji wote wawe wanapeleka contact zao kwa JF (may be we call JF Media) na JF haitadiscslose hizo contacts isipokuwa pale itakapo hitaji kuwasialiana na mhusika katika kupata clarifications.....

otherwise Bravo!!!!
Katika Media nadhani zote kuna kitu kimoja almost ni common; kulinda source ya info kwa kila hali. Kila anayefikisha ujumbe lazima alindwe na kuhakikisha kuwa hatasumbuliwa kwa namna yoyote iwayo. Ndio maana sometimes unaona naweka data kadhaa hapa, hizi si kuwa nakuwa nazo mimi binafsi, ni watanzania wanaziwasilisha kwetu, tunazi-review kisha kuona zinafaa kushirikishwa kwa wana JF na watanzania kwa ujumla au vipi.

Kuna suala moja nilipendekeza, nalo linahusu kutambua na kupewa taarifa ni thread gani ulichangia, maana yaweza kuwa umetuma post nyingi kwa topic tofauti. Pia inawezekana kuna mdau aliuliza swali likataka jibu na ww hujaingia kwenye topik iliyouliziwa swali. Angalau nimeeleweka kidogo
Mkuu Kingi, bonyeza Username yangu utajikuta umeenda link hii: https://www.jamiiforums.com/members/invisible.html

Sasa basi, chini kwenye hiyo link utakuta kuna sehemu imeandikwa STATISTICS hapo ndipo pana maelezo yote:

Find all posts by Invisible
Find all threads started by Invisible

Kwa njia hiyo mimi binafsi nitaweza ku-recall wapi nimeandika na ukifanya vilevile kwa username yako utapata kitu kilekile!
 
Mkuu Kingi, bonyeza Username yangu utajikuta umeenda link hii: https://www.jamiiforums.com/members/invisible.html

Sasa basi, chini kwenye hiyo link utakuta kuna sehemu imeandikwa STATISTICS hapo ndipo pana maelezo yote:

Find all posts by Invisible
Find all threads started by Invisible

Kwa njia hiyo mimi binafsi nitaweza ku-recall wapi nimeandika na ukifanya vilevile kwa username yako utapata kitu kilekile!

mkuu nashukuru kwa maelezo hayo. Hope yatawasaidia wengi
 
Hongera wote mnaofanikisha JF iweze kuwa live...!!!

ila tunavyooelekea...au tulipofikia Invisible hata kuwa tena invisible ktk maana ile ya Awali...!!!
 
Hongera wote mnaofanikisha JF iweze kuwa live...!!!

ila tunavyooelekea...au tulipofikia Invisible hata kuwa tena invisible ktk maana ile ya Awali...!!!

mbona umepotea sana Mkuu.........?
 
Big up man tunatarajia JF mpya yenye malengo mazuri kwa jamii ya kitanzania.
 
Hongera kwa kazi nzuri mkuu je michango lazima iwe ni pesa tu? hakuwezekani kukawa na utaratibu wa kupokea hata mali?
 
Dah...nimepitwa na hii lakini kwa kusoma kuanzia mwanzo, nadhani Invisible and Co mnaelewa ni support kiasi gani mliyo nayo from us members..na at large tunawawakilisha wale wato ambao hawawezi kuwa hapa kama sisi

hili linapeleka ujumbe mmoja tu: kwamba JF ina ujumbe maalum unaoonekana kufika katika jamii kwa namna ya pekee

So imekuwa ni jukumu na wajibu wenu, ambao mmeubeba kwa uvumilivu mkubwa over the years, kuifanya JF iwe hivi

hili linanipa mimi na wengineo sababu ya kuwapongeza kwa dhati kwa hatua hii mpya, huku mkiwa mnategemea support yetu!

keep it up
 
Mkuu Invisible na timu nzima,

Asante kwa kazi yenu nzuri. Kwa wengine JF imekuwa ni kama mtu nanvyokaa sebuleni kwake.Kila baada ya nusu saa lazima niingie JF kuona kuna jipi lipya.

Naunga mkono kuendesha kampeni ya nguvu juu ya uchangiaji kabla ya uzinduzi rasmi. Mimi mwenyewe naahidi kuchangia Tshs. 100,000 ifikapo mwishoni mwa mwezi wa nne.

Tiba
 
asante sana uongozi wa jf.

pendekezo langu kwa vile April ndio uzinduzi rasmi unafanyika,mnaonaje mwezi mzima wa April tutembeze harambee ya changia JF kwa chochote kile mtu alichokuwa nacho wanachama wote kwa ujumla na wageni ? Harambee hiwe inakumbushwa kila siku mpaka mwezi utakapomalizika.

ni wazo tu kama itawezekani na najua hipo thread ya kuchangia lakini kampeni kama hizi huwa zinasaidia mda mwingine huku tukiwa tunaendelea na michango ya kawaida.

Wazo zuri sana...mzee...hii ni good move...web zingine kwa miaka mingi zimekuwa rigid hazitaki mabadiliko...wamekuwa wakucuba..

Thanks.
 
Poleni na kazi nzito, hongereni mods kwa mabadiliko yajayo April pia kutilia manani maoni ya wanaJF ktk kuboresha JF na pia iendelee kupiga stepu zaidi!.. IDUMU JF!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom