Pumzika Sanctus Mtsimbe, Kazi Umekamilisha, Mwendo Umeumaliza. Asante Kutuachia Hazina Kubwa ya Maarifa Humu JF Tutakuishi Milele!. Pumzika

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,605
Wanabodi,
Hili ni bandiko mwendelezo wa bandiko hili Tribute to Sanctus Mtsimbe: Sio tu ni smart kwa mavazi na muonekano, pia ni smart kwa mawazo, maneno, na matendo, na very smart upstairs!

20240317_101058.jpg


View: https://www.youtube.com/live/rZNj5GiWTQQ?si=n_v1QK5KOlYRkOhc
Leo ndio tuna mpumisha Mtanzania mwenzetu kwa Sanctus Mtsimbe kwenye nyuma yake ya milele!. Misime ambaye japo ni Mtanzania wa kawaida tuu, lakini ni mwanachama wa mtandao wa Jamiiforums na japo yeye ametangulia, huku nyuma ametuachia hazina kubwa ya maarifa kwa maandishi na video zake humu jf.

Taarifa ya msiba huu, ilitolewa na Mkuu wa Jamiiforums, Maxence Melo
"Wakuu,

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024.

Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, SimbaNet na makampuni mengine, pia alikuwa Mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi na Mjumbe wa Bodi na taasisi kadhaa za umma na binafsi. Alipenda sana sanaa.

Ndg. Mtsimbe alikuwa ni Mwanazuoni mzuri, mbobezi, mbunifu na Mzalendo wa kweli kwa nchi yetu.
Sanctus alikuwa patner wangu kwenye baadhi ya projects zake.

Huyu ndie aliongoza ile kampeni ya Kumuenzi Regia Mtema kwa kumuandikia kitabu. Huyu ndie alimbeba mwanachama mwingine wa JF, Le Mutuz pale ofisinini kwake!, pia mimi alinikaribisha ofisini kwake na kuitumia studio yake wakati wowote.

Kuna baadhi ya vitu mimi na Sanctus Mtsimbe tulifanana na kuna vingine tulitofautiana, tulifanana kupenda vitu vizuri,gari zuri, suti nzuri, suti kali,na kushirikiana na watu wazuri, wakiwemo wasanii maarufu.

Kufahamiana na Sanctus.
Mimi japo ni Msukuma, na sisi Wasukuma tunasifika sana kwa ushamba, mimi naomba kukiri kuwa japo mimi ni Msukuma wa mjini, niliyezaliwa mjini, nikasomea mjini, ila ushamba wa Kisukuma wa kuchanganyikiwa na "vitu vyeupe" nakiri ni mshamba.

2007, kuna event fulani pale British Council, Sanctus alikuwa anafanya presentations fulani kuhusu Simba Net, mimi nikachangia kitu, wakati wa tunatoka Sanctus aniuliza Kiti Moto kimefia wapi?!, tuonane tukifufue. Tukaagana, nilipomuangalia, akavuka barabara amepaki Range Sport pale CRDB, Holland House!. Nilisimama nikimkodolea macho mpaka anaishia!.

Toka hapo tukaanza urafiki, akanikaribisha Simba Net, tukaa chini kuanzisha studio, akaanzisha Jason Production, alinikaribisha studio yake niliitumia bure pale Tancot House wakati mimi nikiwa Mtaa wa Mkwepu,

Wakati wa kipindi kile cha kukaza kwa vyuma, mimi vilinikazia sana hadi vikaumana, hivyo kulazimika kufunga ofisi ya Mkwepu, huyu jamaa alinibeba kwa muda pale ofisini kwake, ndipo nikagundua kumbe yale makeke yote na ma babez ya Le Mutuz, jeuri ile huyu jamaa ndio mfadhili na mhifadhi Mkuu wa LE MUTUZ SUPER BRAND.

Tukakutana JF msiba wa Regia Mtema, akaongoza kampeni ya kumuandikia kitabu.

Tenda ya Publicity ya DSE Wekeza Inalipa

Sanctus ni Lobbyist mzuri, alishinda tenda ya publicity ya DSE, kupitia kampeni iitwayo, wekeza inalipa, hivyo akanikaribisha tuka join forces to execute it. Mimi ndio nilikuwa presenter, akanipa kazi ya kuwafundisha utangazaji warembo, kiukweli ilikuwa mtihani!.

Sanctus Mtsimbe na Pasco Mayalla, Compare and Contrast
Kwenye hiyo tenda ya DSE mimi ndio nilikuwa mtangazaji kiongozi, nikapewa jukumu la kwanza kuwa train watangazaji wasaidizi. Watangazaji hao ni mabinti 5 mastaa wa Bongo Movies. Hao mabinti wote walikuwa single, halafu mwalimu mwenyewe family inaishi US!, ilikuwa mitihani mkubwa kwangu, lakini kwa Mtsimbe alikuwa ni mtu muadilifu wa hali ya juu.

Kitendo cha kunifanya Mwalimu wa warembo 5 single, ni kama kumpa fisi kazi ya kulinda bucha ya mbuzi!. Mimi pia ni binadamu, na sio malaika!, ila darasa nikaliendesha vema.

Baada ya project ya DSE kukamilika akafungua TV yake.

Sanctus Mtsimbe na JF.

Ni Mtsimbe aliasisi JF get together na kunifanya mimi kuwa MC. Pia ndie alikuwa President of TPN. Sanctus Mtsimbe alikuwa ni Mwalimu.

1. Kwanza alisisitiza connectivity, watu wawe connected, ni kupitia connections na connectivity aliamini kila mtu unaweza kufanya kila kitu kwa kujiunga na wengine kuunganisha uwezo na kutenda. Hivyo pale ofisini kwake alisaidia wengi kushinda tenders.

2. Alisisitiza Afya Bora, ili ufanikiwe ni lazima uwe na uwezo wa kufanya kazi hivyo alisisitiza sana afya bora, alikuwa hali ovyo ovyo, hanywi pombe, havuti sigara, na ile starehe nyingine... yeye wala, ni kazi tuu!, akaandika kitabu cha jinsi ya kuondoa kitambi

3. Alichukia umasikini na kusisitiza utajiri hivyo ametuachia makala nyingi za kuondoa umasikini na kupata utajiri.

4. Alipenda vitu vizuri, wakiwemo warembo. Kuna wanaume na mababa wengi wanapenda warembo, kumbe ukweli hao watu sio wanawapenda hao warembo ili wawasaidie, wanawapenda hao warembo ili wawatumie hivyo wanazuga kuwapenda!, lakini Sanctus Mtsimbe aliwapenda warembo kwa dhati ili kuwasaidia na sio ili kuwatumia!, na kiukweli amewasaidia wengi.

RIP Comred Santus Mtsimbe.

Umepigana vita vilivyo Vitakatifu,

Mwendo Umeumaliza, Imani umeilinda.

Bwana Ameleta, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.

Paskali
 
Wewe ndio ulichangia kuiharibu tamthilia ya siri za familia, wakati inaanza ilikuwa na mabinti wa warembo wanaojua kuigiza ila baadae ukashauri wachukuliwe mabinti hata wasiojua kuigiza ili mradi tu upate warembo, mtu mbaya sana wewe.
 
RIp mtsimbe,, huyu Bwana ni mara ya kwanza kumsikia ,lakini katika wasifu wa kaka #pmayalla na wanamajumui wengine humu jukwaani imenifunza mambo yafuatayo.......
(1). Die empty
Tumia vipawa vyote Mungu aliyokujaalia Kwa kugusa maisha ya wengine ,Kwa kufanya hivyo hata kama ukilala ule usingizi isio ndoto bado sayarini utaendelea kuishi kama taasisi.
"It's better to be born alone but after death persist as an institute"
2. Gusa maisha ya wengine na waache na tabasamu.
Hii inasaidia sana maombi ya waja kukujaalia mwendo mwema mbele ya kiti Cha maanani.

(3).Kutumia taaluma vizuri Kwa waliojaaliwa umbuji katika maeneo mbalimbali ya kitaaluma.
=> Kwenye eneo hili inaonesha marehemu aliweza kugusa maisha ya watu wengi,, kama aliweza kuandika kitabu Kwa ajili ya mbunge wa viti maalumu(CHADEMA) hakika alipenda mawazo ya mwanaharakati na falisafa zake ziweze kuendelea kuishi.
Hii inanikumbusha maneno ya wahenga wa kibantu kuwa...." In order to get whatever you want ,make sure that you make others to get enough for what they want,then you can have abundance to use"

RIp comrade,,
I will walk some of your best steps in life.
 
Kitendo cha kunifanya Mwalimu wa warembo 5 single, ni kama kumpa fisi kazi ya kulinda bucha ya mbuzi!. Mimi pia ni binadamu, na sio malaika!, ila darasa nikaliendesha vema.

Tukimaliza Msiba Pascal uje utudadavulie hiyo point hapo ulipiga pigaje....
 
4. Alipenda vitu vizuri, wakiwemo warembo. Kuna wanaume na mababa wengi wanapenda warembo, kumbe ukweli hao watu sio wanawapenda hao warembo ili wawasaidie, wanawapenda hao warembo ili wawatumie hivyo wanazuga kuwapenda!, lakini Sanctus Mtsimbe aliwapenda warembo kwa dhati ili kuwasaidia na sio ili kuwatumia!, na kiukweli amewasaidia wengi.
Hapo mtihani mkubwa ni sawa na kusema fisi na mbuzi wote unawaweka Buchani pamoja na kuwafungia na kuwaambia waheshimiane.Kama aliushinda huo mtihani heri yake lakino eneo kama hilo hatarishi wengi hawakosi kudaka ukimwi na kuondoka
 
Back
Top Bottom