Uzinduzi rasmi wa JF Aprili 2010

Status
Not open for further replies.
Dah hili nalo neno kha!!
Mwendo mdundo karibia tunawapiga watu mabao ya kisigino.
Hongera wakulu wote wa JF.
 
Mkuu; tuna members zaidi ya 15,000/= na Premium Members ni 188 tu, nadhani hawa bado wanastahili pongezi kwa uamuzi wao wa walau kuchangia chochote walicho nacho kwa ajili ya ufanisi wa JF, tunaweza kufikiria kufanya unavyopendekeza siku za usoni lakini nadhani kwa sasa bado tuendelee kuwapa heshima kwa moyo wao wa kujitolea.

Nawaombeni wenzangu, tujitahidi kuiunga mkono JF kwa sisi tujitolee na kufika at least 7,000 within six moths to come!! This much invisible na crew watawezeshwa kwa hali ya juu.

Nawambieni hakuna sehemu unapata taarifa kuhusu nchi yangu na mustakabali wake kama hapa. We should be proud of this jamvi.

Big up the whole team.
 
Mkuu invisible hii kiboko sijawahi kuona Forum yoyote ya Kiswahili tangu niingie kwenye Mtandao wa internet inayopata Hits 45 Millioni itabidi muwe na Moderator wa kutosha Mkuu invisible poleni sana kwa kazi nzito

Kama ingekuwa kila HIT ni mtu mmoja, kwa mwaka JF inatembelewa na zaidi ya nusu ya wakazi wa bara la Afrika. Kwa upande mwingine ndani ya miaka 12 kuanzia mwaka huu idadi ya HITS itakuwa zaidi ya bilioni 6.48 ambayo ni zaidi ya wakazi wa dunia yetu kwa sasa.
 
Mkuu X-Paster, kupata moderator ni kazi ngumu, tushawahi kupokea maombi toka kwa members kadhaa wakitaka kuwa moderators, wengi tuliwachunguza kwanza na baadae kugundua ndio waporomosha matusi maarufu... Haikusaidia, kuna wawili wanaonekana wanafaa wakiwa trained vema, tunalifanyia kazi.

Moderators/Administrators wa JF ni hawa:

  1. Ab-Titchaz
  2. Brutus
  3. Silencer
  4. PainKiller
  5. Mtumishi
  6. Invisible
  7. Spiderman
  8. Farida
Si vibaya wakifika hata 10... Kama utaitaji msaada ni PM, nitajitolea.
 
Great achievement.. Congratulations...

Can you pls add gender button too... like blue for Gents and Pink for Ladies? sometimes it is confusing while discussing topic with member by just guessing their genders...

Thank you
 
Ni ukweli usiopingika kwamba wadau wengi wa JF wako dar,kwa mantiki hiyo ni bora uzinduzi huu,uambatane na kuwaalika wanachama wa Dar es Salaam, na wa mikoa jirani hii yaweza kusaidia kwa wanachama tutakaoukutana kuchangia na kujuana kiundani zaidi.
 
Job well done Invisible and your team
Staki kuongea sana as words are just mere bubbles.........
Jamani JF MEMBERS its high time kila mmoja wetu aone umuhimu wa kuchangia JF....kwa hali na mali.
we just enjoy the benefits huku tukisahau cost implications za kuiendesha JF!!!

tafadhali lets stand together as one....
 
Heshima zenu wakuu,

Baada ya kwikwi za hapa na pale (marekebisho ya nguvu), leo tumehitimisha kabisa sehemu ambazo tunaamini zilihitaji marekebisho ya nguvu (kwenye server). Tunasikitika kwa usumbufu uliojitokeza na kuwashukuru kwa uvumilivu wenu! Tunaamini kuna utofauti mtaugundua na mtaendelea kutupa ushirikiano huku tunakoelekea.

Tunatarajia rasmi kuizindua JF mpya mwezi Aprili, 2010 ikiwa na sura mpya na vitu vipya.

JF haijajitangaza na mlio wengi mmeifahamu kwa kuambizana aidha kwa njia ya barua pepe au kwa njia ya ku-search vitu kadhaa mtandaoni na mkajikuta mnaangukia humu, wengine mkachukua hatua ya kujisajili na kuwa wanachama kabisa. Tunawashukuru kwa uamuzi wenu wa busara na wa kiungwana.

Mpaka naandika hapa, tumefikia karibia asilimia 80 ya sura mpya ya JF. Tunaandaa pia version ya JF kwa wanaotumia simu za mikononi ili iweze kuwa ina-load kwa haraka kama inavyotokea kwa wanaotumia kompyuta.

Aidha, tumepokea maoni kadhaa na yafuatayo yametiliwa maanani kwenye JF mpya ijayo:

  1. JF ni ngumu kutumiwa, wengi wanashindwa kuelewa namna ya kutuma posts na namna ya kuanzisha topic/threads na wengine hata hawajui maana ya PM na baadhi ya maneno/vifupisho vitumikavyo JF. Wengine wanatamani kuichangia JF ili iweze kufanya vema zaidi lakini hawajui wafanyeje
    • Hili tumnekuwa tukijaribu kuwaelewesha wengi lakini imeonekana ni ngumu kwa version tuliyo nayo kuweza kueleweka. Ukisoma topic hii JamiiForums - How To inaeleza wazi namna ya kuitumia JF kirahisi na pengine majibu ya maswali haya yamewekwa. Katika version mpya ijayo tumejitahidi kurekebisha na kufanya mambo mengi yawe rahisi kwa mtu anayeitembelea JF kujifunza bila kuuliza sana. Bado tunasisitiza kwa wale ambao hawajui namna ya kufanya mambo kadhaa kuuliza kwa kutuma barua pepe (email) kwenda support@jamiiforums.com nasi tutawajibu ndani ya dakika 60 tangu barua pepe imepokelewa.
    • Ukiangalia kwenye topic hii utagundua kuwa maelezo yako wazi. Tunawashukuru wanachama ambao wamekuwa wakituchangia tangu 2009 mpaka sasa na kuwaomba waendelee kutupa ushirikiano tunakoelekea sasa. Katika version mpya tumeandaa njia rahisi ambayo itampa mhusika urahisi wa kutambua anawezaje kuwa Premium Member, anawezaje kuichangia JF na hata kufafanua juu ya ranking za JF zinavyokwenda.
  2. Matusi/pumba vimezidi JF, wahusika wachukuliwe hatua!
    • Hali hii tumeshaibaini, kutokana na kugubikwa na majukumu ya kuja na kitu cha maana zaidi tunajikuta tunashindwa kutekeleza kila kitu kama ambavyo tungependa kiwe. Lakini tunapenda kuwahakikishia kuwa hali itarejea kuwa sawa mwezi April na tutahakikisha tunasafisha jamvi na kuwafahamisha wote ambao watakuwa walienda visivyo juu ya makosa yao, tunasikitika hatutafungia mtu kwa makosa yaliyopita. Tunapenda kusisitiza wana JF kuzingatia Sheria na Kanuni za JF, tunakoelekea hatutawavumilia wachafuzi wa aina yoyote.
  3. Posts/Threads zinahamishwa bila kutoa taarifa:
    • Suala hili tumekuwa tukipata taarifa zake, tunafahamu inavyokera endapo mtu anaanzisha hoja anakuja kesho yake anakuta haipo na hajapewa maelezo. Baada ya Aprili mwaka huu, tutahakikisha kila hoja inayoondolewa mhusika (aloandika) anafahamishwa kwanini hoja yake imeondolewa na kuelezwa hoja ilipohamishiwa. Kila topic inapohamishwa huachwa redirection, kwa kipindi hiki tunaomba tuwieni radhi tukamilishe ngwe ya mwisho kisha tutafuata ambacho nimeeleza hapo juu.
    • JF moderation inazidi kuwa ngumu, JF inapata hits zaidi ya milioni 45 kwa mwezi na kila siku posts zaidi ya 1,200 zinatumwa. Tumefikiria kuongeza moderator mmoja na tutaendesha semina kwa moderators wote kuweza kukabiliana na hali halisi.
  4. Nataka kutangaza JF lakini sijui nifanyeje:
    • Katika toleo la JF lijalo tumeonelea ni vema kuweka gharama za matangazo katika JF pamoja na aina za matangazo na sehemu za kutangaza ndani ya JF. Tutaweka wazi gharama bila kificho ili kila anayetaka kutangaza biashara yake kupitia kwetu aamue ni eneo gani angependa kutangaza na kivipi.
    • Tunawashukuru Zain kwa kuwa wadau wa kwanza kuchukua fursa ya kutangaza kwenye Front Page, tunaamini baada ya uzinduzi wengi wataelewa gharama zikoje na wapi pa kuwasiliana nasi ili kuweza kuweka matangazo hapa JF
    • JF yenyewe itaanza kujitangaza kuanzia Aprili 2010.
  5. Harakisheni chat hapa JF!
    • Suala hili tumelifikiria kwa upana, linafanyiwa kazi lakini namna ya chat itakavyokuwa itakuwa na utofauti kidogo na wengi wanavyotarajia, bado itakuwa userfriendly lakini itakuwa ni baina ya mwanachama na mwanachama; wasiojisajili hawataweza.
  6. Nataka kuwa na blog yangu ndani ya JF
    • Tumelifikiria hili na linafanyiwa kazi kwenye JF mpya ijayo, aidha wale wenye blogs via blogspot na wordpress tunaweza kushirikiana nao katika kuzihamishia kwenye server yetu.
  7. JF Tv/Radio/News paper
    • Kimoja au viwili vya vitajwa hapo ki(vi)taanza karibuni, tunategemea ushirikiano kutoka kwenu!
  8. Kutakuwa na 24/7 Live support ambayo itakuwa na wasaidizi watano tofauti.
Aidha, kutakuwa na sehemu ya masoko (Market Place) na kwa wale mnaohitaji email via JF msisite kuwasiliana nasi via support@jamiiforums.com ili tuwatengenezee accounts zenu. Kwa wale waliosahau password zao na wana uhakika wamewahi kujisajili, pia wawasiliane nasi kwa anuani hiyo ili tuwakumbushie majina yao na password zao.

Logo ya JF itabadilika, mwonekano kwa ujumla! Kwa wale wenye kutaka kuchukua kumbukumbu za JF hii ya sasa mnaweza kuchukua screenshot ili siku za usoni mjikumbushe kabla ya mabadiliko tunayoyafanya JF ya sasa (up to April 2010) ilikuwa ina sura gani.

Kwa niaba ya wenzangu (wawili, mimi wa tatu) napenda kuwashukuru wote mliotuunga mkono tangu tunaanza na mnaoendelea kutuunga mkono tunakoelekea. Tunaamini katika ushirikiano mengi yanawezekana!

Tunakaribisha maoni, mapendekezo na ushauri wa nini kifanyike zaidi...
mkuu nimekusoma vilivyo.nimejikuta nagonga thnx kwa ghafla mno.
Keep it up !!
JF mbeleeX3333
 
Moderators/Administrators wa JF ni hawa:

  1. Ab-Titchaz
  2. Brutus
  3. Silencer
  4. PainKiller
  5. Mtumishi
  6. Invisible
  7. Spiderman
  8. Farida
Nilikuwa nahisi Mbu ni Moderator wa JF. Kwa jinsi alivyoandika katika "thread" fulani na kisha ikafungwa.
 
hongereni wakuu kwa kazi mnayofanya, na poleni kwa majukumu yote, hakuna jinsi ya kuwalipa kwa kazi mnayofanya lakini tutasaidiiana pale inapowezekana ili kufanikisha....mengi ya mapendekezo mumeyafanyia kazi inavyoonekana, kwangu suala la CHART room for online registered users ni muhimu sana, kama mumeliweka basi mtakuwa mumefanya kazi ya maana mno....kuhusu TV/redio/newspaper....mimi naona kutokana na jinsi hii forum inavyoendeshwa redio au gazeti ndio ideal, lakini wachangiaji wote wawe wanapeleka contact zao kwa JF (may be we call JF Media) na JF haitadiscslose hizo contacts isipokuwa pale itakapo hitaji kuwasialiana na mhusika katika kupata clarifications.....

otherwise Bravo!!!!
 
Siipatii picha JF TV sijui nayo itakuwa na anonymous system. All in all its a tough work to you all we understand and we do appreciate your efforts. Cheers
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom