Kassim Majaliwa: Bangi ya 'Cha Arusha' pamoja na 'Skanka' inafanya watumiaji kuwa vichaa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,817
11,993
Fuatilia kinachojiri kwenye Sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, leo Aprili 2, 2024 ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ni Mgeni rasmi.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wananchi kwenda kuhakiki majina yao kabla uchaguzi wa Serikali za Mitaa haujaanza kwani zoezi la kuhakiki wapiga kura kwenye daftari la kudumu tayari umeshaanza.

Amesema kila mtanzania anayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa, na wale wanaokusudia kufanya hivyo mwezi wa 10 ni fursa yao.

Kuhusu suala la lishe, Waziri Majaliwa amesema Serikali inapambana na kutokomeza utapiamlo wa aina zote kwa kuimarisha sera, kanuni na miongozo ya kuwezesha watanzania kupata lishe bora.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2022, hali ya lishe nchini bado siyo ya kuridhisha ambapo 30% ya watoto chini ya miaka 5 wanakabiliwa na tatizo la udumavu na 12% wana uzito pungufu na 3% wana ukondefu na mikoa inayoongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha udumavu na ukondefu wa watoto kwa zaidi ya wastani wa kitaifa ni Iringa, Njombe, Rukwa, Geita, Ruvuma, Kagera, Simiyu, Tabora, Katavi, Manyara, Songwe na Mbeya.

Aidha, 42% ya wanawake wenye umri wa kuzaa wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa damu, pia tatizo la kiribatumbo na uzito uliozidi unataka kuwa janga la taifa.

Akizungumzia suala la Rushwa nchini, Waziri Kassim Majaliwa amesema mbio za mwenge za mwaka huu zitaendelea kusisitiza umuhimu wa kupambana na rushwa na kwa mujibu wa tafiti, Tanzania inafanya vizuri katika kupambana na rushwa.

Hivi karibuni imeibuka aina mpya ya bangi yenye kiasi kikubwa cha kilevi inayofahamika kama 'Cha Arusha' pamoja na 'Skanka'. Aina hii ya bangi yenye sumu nyingi huchanganywa kwenye sigara na wanaoitumia hubadilika kuwa kichaa. Ni wakati mzuri kwa vijana kuacha ili kunusuru maisha yao.

Pia soma:

Bangi ihalalishwe, Sheria zinazotumika kuhusu Bangi. Ziende kudhibiti Ushoga

Kamishna wa Kudhibiti dawa za Kulevya: Bangi ya Tanzania haifai kwenye Masoko ya Kimataifa

Serikali iruhusu kilimo cha bangi na ipunguze masharti ya uingizaji wa fedha nchini ili kukabili uhaba wa dola
 
Sasa mbona sijaelewa lengo la mwenge. Bado ubadhirifu unazidi uzembe na ubinafsi ndio usiseme. Mbali na kuligharimu taifa je umuhimu wake niupi
 
Mwenge dhumuni mojawapo ilkua ni kumulika na kuwafichua wala rushwa lakini leo hii wala rushwa na mafisadi ndio mawaziri waliokalia ofisi za serikali kazi kubwa ni kuhamishwa wizara. Mwenge umepoteza maana nashauri uwashwe ukaachwe huko juu ya mlima kilimanjaro ukiisha mafuta usiwashwe tena.
 
HIIIZI SIKU WATOTOO WADOGO WANAPIGWAHA MITI HATAREE USIKU NILIYAONA MARA NKAOGOPA
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Taifa Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) wakiwa katika Sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mkoani Kilimanjaro tarehe 02 Aprili, 2024.

#UWTImara
#JeshiLaMamaSamia
#KaziIendelee

IMG-20240402-WA0024.jpg
 
Haya mambo yanatupoteea muda....

Ehe budget huko mmetumia tsh ngapi

Ova
 
Fuatilia kinachojiri kwenye Sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, leo Aprili 2, 2024 ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ni Mgeni rasmi.

Kuhusu suala la lishe, Waziri Majaliwa amesema Serikali inapambana na kutokomeza utapiamlo wa aina zote kwa kuimarisha sera, kanuni na miongozo ya kuwezesha watanzania kupata lishe bora.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2022, hali ya lishe nchini bado siyo ya kuridhisha ambapo 30% ya watoto chini ya miaka 5 wanakabiliwa na tatizo la udumavu na 12% wana uzito pungufu na 3% wana ukondefu na mikoa inayoongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha udumavu na ukondefu wa watoto kwa zaidi ya wastani wa kitaifa ni Iringa, Njombe, Rukwa, Geita, Ruvuma, Kagera, Simiyu, Tabora, Katavi, Manyara, Songwe na Mbeya.

Hii aione ChoiceVariable
 
Back
Top Bottom