tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,240
- 4,466
Tuwajibike wote maeneo yetu ya kazi. Si afya tu.Ndio maana wengine wanakimbilia kwa waganga tu.....
Ila tatizo ni kukosa uwajibikaji
Na manesi kwenye hospitali za serikali ni majanga sana
Tuwajibike wote maeneo yetu ya kazi. Si afya tu.Ndio maana wengine wanakimbilia kwa waganga tu.....
Ila tatizo ni kukosa uwajibikaji
Na manesi kwenye hospitali za serikali ni majanga sana
Mimi mkuu katika masuala yanayohusu roho ya mtu sina huruma na masihara....huyo jamaa ni mzembe kwa kushuhudia kifo cha mwanae kwa uzembe wa nesi....alafu unamuacha nesi atambe kwa kauli ya bahati mbaya huku wewe umeshapoteza mtoto huku akipokea mshahara kama kawaida....Basi mwaka 1996 nilipeleka mwanagu hapo Bunda DDH alikuwa anaumwa homa Kali sana.nikaonana na Dkt nikaandikiwa vipimo nikaenda maabara mtoto akapimwa nikapewa majibu kuwa ana homa Kali sana lakini hana Maji kabisa muda wowote anaweza kufa.
Ikabidi Dkt aache watu wako mwenye foleni akaondoka na mgonjwa wangu mpaka hodini akamwambia nesi mwekee huyu mtoto drip sasa hivi Fanya haraka.nesi kaleta drip yule Dkt akaondoka akawahi wagonjwa aliowaacho foleni.
Alipoondoka tu nesi akaning'iniza chupa ya Maji mwenye stand bila kumwekea mtoto ,nesi akaenda kukaa kwenye kichumba chao akatutelekeza
Hapo.kila nikimfata ananijibu kwa hasira INA maana unatufundisha kazi.
Kikaona hapa nikizubaa mwanangu anakufa basi nikamfata nesi kwa hasira nikamukwida nimpe vibao ,ghafula Dkt mkuu WA hospt Dkt Sweya akatokea alikuwa anatembea hodini anasalimia wagonjwa ,akaona nilivyo mkwida akaja nikamweleza kila kitu nesi akakoromewa akatolewa akaletwa mwingine mwanangu Dkt sweya akamwekea drip.
Ajabu hata nesi aliyeletwa nae ni jipu Muda kidogo kitanda nilicholazwa akaletwa mtoto mmoja toka kijiji kung'ombe ameishiwa damu ,wakamtoa babaake damu ,ikaletwa ikatundikwa kwenye stand ikatelekezwa hapo .
Nikawa namsihi baba MTU nenda wafate anaogopa .zaidi ya SAA moja hajawekewa damu yule mtoto akafa.nesi akachukua ile CHUPA ya damu akaondoka nayo sijui alienda kuiuza.
Ukifikiria utadhani hawa manesi wana mkataba na kuzimu WA kuchomoa roho zetu.hawana huruma
Tuanze na afya kwanza mengine yatafuata........Tusisahau kutokujali hakuko afya tu, hata benki, ardhi, polisi, simu n.k. Tusiwalaumu sana hawa watu. Kila mtu awajibike eneo lake.
Mimi sitaweza kuvumilia kumpoteza mpendwa wangu kwa uzembe wa mtu mwenye jukumu la kuokoa maisha ya mpendwa wangu na analipwa kwa kazi hiyo......wakati home wanapanga mazishi na wao kwao lazima wapange mazishi na nitakuwa naendelea na kesi ya kuua kwa bahati mbaya.....
Hizi kesi zimekuwa nyingi sana acha zile zisizo ripotiwa na wahusika wamekuwa wakitoa maelezo kama kwamba waliopoteza maisha ni midoli tu nasio binaadamu...
Nakumbuka kisa kimoja cha mtu fulani aliyekuwa amelazwa kwenye kituo fulani cha afya.....
Nesi alipomkuta kazimia akawaambia ndugu zake kuwa amefariki na ndugu wakaanza kuangua kilio.....ikawa wanaandaa mipango ya mazishi na maiti wakaipeleka nyumbani.....wakati wanamuaandaa maiti kwa ajili ya mazishi mara ghafla marehemu akazinduka na kuwashangaa wao....
Sasa jiulize kesi kama hizo zipo ngapi....??na ni wangapi wanazikwa hai....kama jamaa asingezinduka si ndio angefukiwa moja kwa moja.......???
Halafu hatuko makini na post mortam(spelling sijui kama ni sahihi)Pole sana mkuu. Hii Africa yetu bado ni majanga sana aisee. Ebu imagine mgonjwa anawekewa dripu ya sukari bila ya kipimo kwanza cha haraka. Yani muuguzi (sijuwi ndo nesi) anakisia tu na kufanya maamuzi afanye hiki. Hapo hakuna tofauti na ramli.
Unabunia tu na kumuwekea mtu dripu ya sukari ilihali kumbe mwili wake hauhitaji hicho kitu, then kwa uzembe huo mgonjwa anakufa! Afu eti ooh bahati mbaya, ooh mipango ya Mungu, and blah blah! Inaumiza sana walahi.
Ifike mahala watu waanze kushtakiwa kwa kosa la 'professional negligence' kama nchi zilizoendelea. Otherwise watu hawatakuwa makini wala kufuata guidelines za profession zao ktk kuhudumia watu.
Ndo maana mimi binafsi huwa naamini kwamba majanga na vifo vingi hapa Africa ni kutokana na UZEMBE (negligence/recklessness) tu, wala hakunaga bahati mbaya!! Na hii 'bahati mbaya' ndo ishakuwa utetezi wetu wa kila siku.
Poleni sana
Niliwauliza hili swali wakasema 'kwa kawaida' mgonjwa aliye hoi cha kwanza huwa ni drip ya sukari....kwahiyo kazi zinafanyika kwa mazoeaMungu amlaze pema, jambo la kushangaza kwanini hospital za tz kila mgonjwa anatundikiwa drip tu kila akionekana yuko hoi?
Ni ajabu sana kiasi unaongea doc anaandika utumbo
Hahahaaaa. Huwezi sema utaanza afya tu, unadhani kwingine kusipobadirika wao watabadirika? Changes zinaanza ulipo. Endelea kusubiri.Tuanze na afya kwanza mengine yatafuata........
Ardhi inatafutwa maisha ya mtu yanatafutiwa wapi???
Unashutumu vipi chuo wakati hujui waliomhudumia wana elimu gani?Ndio matatizo ya kusajili vyuo vingi vya afya na kushindwa kusimamia ipasavyo ethics zinazotolewa hapo chuoni kwa wahitimu. Wauguzi wengi ni graduates wa vyuo private ambavyo hata hao walimu wao ni wababaishaji tu.
Hizo elimu zao wamezitoa wapi kama sio vyuoni mkuu?Unashutumu vipi chuo wakati hujui waliomhudumia wana elimu gani?
Hizo elimu zao wamezitoa wapi kama sio vyuoni mkuu?
Nakubaliana nawe kabisa ni lazima watu wawajibike kwa taaluma zao, mara nyingi wajenzi wamewekwa kitimoto na serikali, hata wafanyakazi wengine kama watumishi wa ardhi nao wamekumbwa na kadhia hii ya kushitakiwa kwa maamuzi mabovu.Tusisahau kutokujali hakuko afya tu, hata benki, ardhi, polisi, simu n.k. Tusiwalaumu sana hawa watu. Kila mtu awajibike eneo lake.
Kuwa mzembe hakuendani na chuo. Kama chuo ndiyo shida, basi hakuna aliyepona. Maana wote tumesoma vyuo hivyo hivyo.Hizo elimu zao wamezitoa wapi kama sio vyuoni mkuu?