Uzembe wa madaktari waua tena Hospitali ya DDH Bunda

Nakubaliana nawe kabisa ni lazima watu wawajibike kwa taaluma zao, mara nyingi wajenzi wamewekwa kitimoto na serikali, hata wafanyakazi wengine kama watumishi wa ardhi nao wamekumbwa na kadhia hii ya kushitakiwa kwa maamuzi mabovu.

Ifike mahali na madokta washtakiwe pia
Unaweza kuwahukumu/kuwashtaki. Ila sote tubadirike; yamkini hata anayelaumu angekuwa katika nafasi hiyohiyo angefanya vibaya. Yamkini anayelaumu naye ana shida zake kubwa kazini. Tubadirike
 
Kuwa mzembe hakuendani na chuo. Kama chuo ndiyo shida, basi hakuna aliyepona. Maana wote tumesoma vyuo hivyo hivyo.
Ni kweli sio wote ila kuna baadhi ya vyuo wauguzi wanaotoka huko wanakosa vitu vingi sana hasa vile basics tu sasa ethics ndio hakuna kabisa. Wakija field hua tunawaona na utendaji wao tunauona mkuu.
 
Sina hamu na Manesi kabisa maana nilimpoteza mama mdogo wangu, kaendaa kujifungulia hospitali ya Magu na baada ya kujifungua akakoswa huduma na kufariki dunia.
Mwishoni mwa mwaka jana 2015 mama mmoja amepelekwa kwenda kujifungua akakoswa huduma baada ya nesi wa zamu kutokuwepo mda wa kazi majira ya usiku na kupelekea mama huyo kufariki dunia.
Ngoja utakiwe kuthibitisha kimahakama ndio utaelewa kuwa siku hizi hata hao manesi mnaowatukana wanajua haki zao
 
Nilipasuliwa katika hospitali moja ya binafsi hapa Dar. Nakumbuka nilirudishwa wadini jioni baada ya Muda mfupi nilianza kutapika kila baada ya dakika kumi. Nilikuwa peke yangu room kwa hiyo nililazimika kumuita nesi aje anisaidie kwa kuwa nilikuwa siwezi kunyanyuka kwa kuwa miguu ilikuwa hainafahamu ganzi ilikuwa haijaisha. Lakini pamoja na hali hiyo kujirudiarudia wahudumiaji walikuwa mbali sikupata msaada hadi asubuhi ndo wakashangaa kuona hali hiyo ikijirudia.
Muda wa saa tano asubuhi alipita Daktari mmoja akanifahamu kumbe ni ndugu yangu. Nilipomuambia nilianza jana jioni akanichoma sindano nikatulia.

Kwa kweli huduma zetu bado haziridhishi.
 
Kwako ile huduma ya kupasuliwa sio huduma ya kuridhisha?

Ni kweli huduma hazijafikia kiwango kikubwa wanachotaka watu....lakini hatujiulizi hivi huyo muuguzi mmoja anahudumia wateja wangapi kwa siku na alitakiwa ahudumie wangapi?

Muuguzi mmoja wadi ya watu 50 unategemea upate huduma ya muuguzi mmoja kwa mgonjwa mmoja?

Je hiko unachotaka akifanye unakilipiaje???

Yaani unamuona professional wakati wa kutoa huduma tu lakini wakati wa kudai stahiki zake unamlinganisha na wafanyakazi wengine....
 
Naona jina laki linafanana na mawazo yako.

I nakuingia akilini mgonjwa kuita nesi nesi usiku kucha bila kupata msaada mpaka asubuhi ndo anajua kuna tatizo. Na linaendelea. Kama nawe ni nesi huendi kusikiliza shida za wagonjwa wakikuita uache hiyo ni tabia mbaya.
 
Kwako ile huduma ya kupasuliwa sio huduma ya kuridhisha?

Ni kweli huduma hazijafikia kiwango kikubwa wanachotaka watu....lakini hatujiulizi hivi huyo muuguzi mmoja anahudumia wateja wangapi kwa siku na alitakiwa ahudumie wangapi?

Muuguzi mmoja wadi ya watu 50 unategemea upate huduma ya muuguzi mmoja kwa mgonjwa mmoja?

Je hiko unachotaka akifanye unakilipiaje???

Yaani unamuona professional wakati wa kutoa huduma tu lakini wakati wa kudai stahiki zake unamlinganisha na wafanyakazi wengine....
 
Kwa hiyo ukimpasua mgonjwa inatosha? Complications zinazotokea baadaye hazikuhusu? Usiwe mvivu wa kufikiri, Soma uelewe
 
Jingalao

Si kila aliyeenda hospitali hana uwezo wa kulipia service na si kweli kuwa watu wote hawalipii.

Kama umesoma vizuri maelezo yangu ni kuwa ilikuwa ni hospitali binafsi na room ilikuwa ni ya mtu mmoja.
 
Imefikia wakati Wa Madaktari wetu kushtakiwa wanaposababisha Vifo vya watu kwa Makusudi au uzembe katika matumizi ya Taaluma yao.

Tunahitaji kuleta nidhamu katika matumizi ya Taaluma.Huwa tunapenda kukimbilia ni mapenzi ya Mungu hata kwa watu tuliowaharakishia mauti.

Sostenes Mitti Majira ya Saa kumi na Moja Jioni Jana tarehe 06 February 2016 Alijihisi vibaya akaondoka mwenyewe kwenda Hospital ya DDH Bunda kucheck Afya yake.Madaktari walimuattend na kumwekea Drip ya Maji kushusha Pressure,wakaendelea na shughuli zao wakimuacha ,mpaka marafiki walipokuja kumuona na kukuta amefariki ndipo wakawaita madaktari na wao kuanza kushangaa tu.Unawezaje kumwekea mgonjwa aliyeserious drip nawe ukaenda mbali.Kifo hiki kimeniumiza na naamini ni uzembe kwani kilichotokea kwa Mitti miaka miwili iliyopita nikiwa Bunda niliugua nikamwomba Mitti anisindikize,wakanilaza kwenye private ward zao hapo hospitalini kwao,wakanitundikia drip.Usiku akaja nesi mwanafunzi akabadilisha ile drip ya Quinine na kuongeza spidi ya follow,Akaondoka baada ya kama dakika kumi Hali yangu ilibadirika nikaita nesi nesi nesi hakukuwa na dalili ya MTU kuitikia.Nikampigia Sostenesi nikiwa siwezi kupumua vizuri,watafute uwezekano wa madaktari maana nimetelekezwa.

Hali ilizidi kuwa mbaya,nilichokumbuka nikuomba nakujua muda wangu umekwisha.Ndipo ghafla akaingia mama Mdogo ambaye ni daktari hospital hiyo hakuwa zamu,na hakujua kama nipo hospitalini pale alipigiwa simu na Mitti,akaja anakimbia akanikuta nimelowa na sina uwezo Wa kuongea kwa sauti,nikamwonyesha Drip akaona tatizo akaichomoa drip na kuleta oksjeni na kuniwekea baada ya kama nusu saa nikapata nafuu na akina Mitti walikuwa tayari wapo wamezunguka kitandani wasijue kinachotokea.

Niliwaeleza kilichotokea kuhusu Yule nesi alitafutwa hakupatikana kabisa.Tulifuatilia na Mitti,hakutokea na Daktari Wa zamu hakuweza kumtambua,.

Ninapoambiwa Sosteness katuacha katika Mazingira Yale Yale inaumiza sana.Tunahitaji kufuatilia kwa karibu utoaji huduma za Afya katika Hospital ya DDH ,Vinginevyo wananchi watakatiliwa Maisha kila kukicha.

Tangulia Mdogo wangu Mitti uliokoa maisha yangu,nimeshindwa kuwepo kukuokoa.Bwana alitoa na BWANA ametwaa.Jina la Mungu wetu lihimidiwe.
pole sana ndugu kwa musiba wa mdogo wako..Mungu wa Mbinguni akupeni moyo mkuu na kuwafariji ktk wakati huu wa majonzi wakuondokewa na mdogo wako.
 
Niliwauliza hili swali wakasema 'kwa kawaida' mgonjwa aliye hoi cha kwanza huwa ni drip ya sukari....kwahiyo kazi zinafanyika kwa mazoea
Wana dhambi hao, rafiki yangu alikuwa na kisukari (classmate) nikaambiwa kuwa alipelekwa hospital bila ya doctor wala nesi kuuliza ana maradhi yoyote wakatundikia drip ya glucose eti apate nguvu. Maskini ndio ikawa mwisho wa uhai wake so sad
 
Mkuu huwezi ukasema kwanini kwa sababu wagonjwa ni tofauti na watumishi wa afya wanaowatibu ni tofauti kitaaluma na uwezo. Hilo swali inatakiwa unamuuliza indication aliye order hizo fluids apewe mgonjwa, ili walau akupe sababu. Ila kwa uelewa wangu mdogo si kila mgonjwa anahitaji hayo maji yao.
Umesema kweli ila pia kwa taaluma ya doctor ni lazima aulize kwa undani huyo mgonjwa alikuwa anaumwa nini kabla ya hapo na uchunguzi lazima ufanyike sio wana assume tu.

Madokta wazoefu na kazi zao bila stress anakaa na kukuuliza believe me kama ulaya Dr anakuuliza mpaka wazazi au babu alikufa kwa maradhi au natural causes halafu anaanzia hapo hiyo ni baada ya kujiridhisha na vipimo na maswali kibao ndio anakupa dawa. Sio unatundikiwa halafu humuoni hata nurse akizunguka wodini
 
Wiki iliyopita waziri wa ofisi ya waziri mkuu or yeyote yule ambae anaeshughulikia maswala ya afya nayeye aliulizwa serikari imejiandaa vipi kuhakikisha wafanyakazi wa afya wanafanya kazi kwa tija na kuhakikisha wafanyakazi wanaoajiriwa are qualified bila ya kuwa na shaka. Jibu lake ni kwamba wao kama serikari wanahakikisha kila mfanyakazi cheti chake kinakaguliwa sasa basi we all know kuna vyeti vya ngono/kufanyiwa assignment and the likes ambazo mtu anaweza penya mpaka kupata cheti.

Kilichonishangaza katika hilo jibu ni kwamba siku sikia ya kuwa tuna national procedural frameworks ambazo kila mfanyakazi anatakiwa azifanye zinasimamiwa na hospitali husika, kuna appraisals za serikari kuhakikisha manesi na madaktari wanatoa huduma sahihi na wanavigezo vya uwezo na uelewa wa sera na taratibu za matibabu, kuongelea safeguarding practices in short majibu yake na swala zima la huduma bora lina majibu tofauti kabisa na aliyoyatoa waziri.

Kigwangala nayeye kuona asipitwe akasimama na kusema serikari inakaa sijui na bodi gani ya maadili kuhakikisha inasimamia wafanyakazi wanatumia maadili, Ummy Mwalimu na yeye akaja tunataka kila nesi awe na jina lake na tuna namba rasmi ya wizara ya malalamiko sasa unajiuliza yupi yupo karibu kurekebisha na kushugulikia matatizo ya raia wizara au taasisi inayotoa huduma ili kusimamia ubora wa huduma zake na hiyo management hapo hospitalini ina majukumu gani iwapo watumia huduma wap kwenye risks.

Unajua sasa ndio nawaelewa diaspora wengi kwanini wakirudi wanaishia private au kwenye NGO's kwa madai ya kuwa serikarini watu wana namna zao ukiwakosoa mabosi wanaona kama vile una challenge nafasi zao hila mtu anaona kabisa hapa siyo sahihi lakini hana jinsi ya kurekebisha na ushauri wake hakuna mwenye shida nao kuondoa frustration wanatimkia private isiwe tabu ina maana serikari inabakiza makapi tu sio best candidates.

Hayo matatizo ni ya muda mrefu hila kwa timu ya ungozi wa sasa kutatua hadithi isitoshe hapo wizarani halafu unaambiwa kuna kitengo cha quality management ya huduma za afya nationally haya mambo yanawezekana Tanzania tu kudhani watu wasiokuwa qualified wanaweza simamia kwa ufanisi technical sectors; wacha tu mweeh.
 
Imefikia wakati Wa Madaktari wetu kushtakiwa wanaposababisha Vifo vya watu kwa Makusudi au uzembe katika matumizi ya Taaluma yao.

Tunahitaji kuleta nidhamu katika matumizi ya Taaluma.Huwa tunapenda kukimbilia ni mapenzi ya Mungu hata kwa watu tuliowaharakishia mauti.

Sostenes Mitti Majira ya Saa kumi na Moja Jioni Jana tarehe 06 February 2016 Alijihisi vibaya akaondoka mwenyewe kwenda Hospital ya DDH Bunda kucheck Afya yake.Madaktari walimuattend na kumwekea Drip ya Maji kushusha Pressure,wakaendelea na shughuli zao wakimuacha ,mpaka marafiki walipokuja kumuona na kukuta amefariki ndipo wakawaita madaktari na wao kuanza kushangaa tu.Unawezaje kumwekea mgonjwa aliyeserious drip nawe ukaenda mbali.Kifo hiki kimeniumiza na naamini ni uzembe kwani kilichotokea kwa Mitti miaka miwili iliyopita nikiwa Bunda niliugua nikamwomba Mitti anisindikize,wakanilaza kwenye private ward zao hapo hospitalini kwao,wakanitundikia drip.Usiku akaja nesi mwanafunzi akabadilisha ile drip ya Quinine na kuongeza spidi ya follow,Akaondoka baada ya kama dakika kumi Hali yangu ilibadirika nikaita nesi nesi nesi hakukuwa na dalili ya MTU kuitikia.Nikampigia Sostenesi nikiwa siwezi kupumua vizuri,watafute uwezekano wa madaktari maana nimetelekezwa.

Hali ilizidi kuwa mbaya,nilichokumbuka nikuomba nakujua muda wangu umekwisha.Ndipo ghafla akaingia mama Mdogo ambaye ni daktari hospital hiyo hakuwa zamu,na hakujua kama nipo hospitalini pale alipigiwa simu na Mitti,akaja anakimbia akanikuta nimelowa na sina uwezo Wa kuongea kwa sauti,nikamwonyesha Drip akaona tatizo akaichomoa drip na kuleta oksjeni na kuniwekea baada ya kama nusu saa nikapata nafuu na akina Mitti walikuwa tayari wapo wamezunguka kitandani wasijue kinachotokea.

Niliwaeleza kilichotokea kuhusu Yule nesi alitafutwa hakupatikana kabisa.Tulifuatilia na Mitti,hakutokea na Daktari Wa zamu hakuweza kumtambua,.

Ninapoambiwa Sosteness katuacha katika Mazingira Yale Yale inaumiza sana.Tunahitaji kufuatilia kwa karibu utoaji huduma za Afya katika Hospital ya DDH ,Vinginevyo wananchi watakatiliwa Maisha kila kukicha.

Tangulia Mdogo wangu Mitti uliokoa maisha yangu,nimeshindwa kuwepo kukuokoa.Bwana alitoa na BWANA ametwaa.Jina la Mungu wetu lihimidiwe.

Kisheria muuguzi mwanafunzi haruhusiwi kutoa dawa, kushika drip, syringe drive wala kuchoma sindano na kama ikitokea akatoa dawa kwa mgonjwa ni lazima awe na muuguzi mfanyakazi anaemfundisha ambae atacheck aina ya dawa, doze ya dawa na expering date.
 
Nilimpeleka ndugu yangu ocean road hospital alikuwa na shida ya cancer. ..kufika Pale kuonekana yuko dhaifu saana akapewa drip ya sukari bila vipimo
Baadae doctor alipokuja kufanya vipimo akakuta sugar iko 32 normal ni 4-7 , wakastopisha ile drip haraka sana but it was too late alifariki siku ileile jioni...hii imetokea mwezi uliopita
Inasikitisha sana.
Na inasikitisha zaidi kuwa matukio haya yanaendelea kutokea pasipo hatua madhubuti kuchukuliwa.
 
Inasikitisha sana.
Na inasikitisha zaidi kuwa matukio haya yanaendelea kutokea pasipo hatua madhubuti kuchukuliwa.
Kuchukua hatua madhubuti inataka kuelewa jinsi ya kushape system nzima ya afya na people go to school to learn health management sio LLB or medical doctor; kwa mfano chukua hili takwa la kisheria kwa mujibu wa huyu mchangiaji

Kisheria muuguzi mwanafunzi haruhusiwi kutoa dawa, kushika drip, syringe drive wala kuchoma sindano na kama ikitokea akatoa dawa kwa mgonjwa ni lazima awe na muuguzi mfanyakazi anaemfundisha ambae atacheck aina ya dawa, doze ya dawa na expering date.

Ni nani anayesimamia hili zoezi kuhakikisha hakuna ata mara moja mambo hayafanyiki kinyume na taratibu hizi na inapotokea hatua gani za kinidhamu zipo kama adhabu kwa sasa.

Achilia mbali hao wanafunzi kila siku watu wanalalama kukosa vipimo sahihi mahospitalini ingawa wanakuwa wameshavilipia nani anajukumu la usimamizi huo usiku na mchana na muda gani umetengwa na serikari mtu akishapata vipimo hatua gani zichukuliwe maana wengine wanasema wamepata vipimo muda fulani lakini kumuona mtaalamu imewachukua siku na wamelala na drips ndio mambo kama haya kizembe kuna vifo unnecessary; tatizo ni uwezo wenyewe wa kujua kudhibiti sio kwamba awakati.
 
Poleni sana wafiwa, mshanajr na mwenzio. Unfortunately vifo vingi TZ vinatokea kutokana na uzembe. Iwe kwenye hospital au road accident. Nchi za wenzetu huyo nesi angetafutwa na kushtakiwa kwa kusababisha vifo. Magazeti yange andika habari hii na ku criticize sana. Lakini home magazeti yatashabikia Wema na Diamond na kuacha habari za muhimu kama hizi.
 
Kusema la haki haiwezekani eti nesi hajulikani how? Ni mjinga ndio atakubali uongo huo yaani shift hazijulikani au anehudumia hiyo ward hawawajui bull s@#
 
You knew about that DDH and why did you allow that to happen to your friend? Or you assumed things have changed? We should always not take chances

RIP Mitti
You sound like a staff member of Binds DDH hospital!!!!
 
Back
Top Bottom