Urio kimiroI
Senior Member
- Jan 2, 2016
- 146
- 74
Imefikia wakati Wa Madaktari wetu kushtakiwa wanaposababisha Vifo vya watu kwa Makusudi au uzembe katika matumizi ya Taaluma yao.
Tunahitaji kuleta nidhamu katika matumizi ya Taaluma.Huwa tunapenda kukimbilia ni mapenzi ya Mungu hata kwa watu tuliowaharakishia mauti.
Sostenes Mitti Majira ya Saa kumi na Moja Jioni Jana tarehe 06 February 2016 Alijihisi vibaya akaondoka mwenyewe kwenda Hospital ya DDH Bunda kucheck Afya yake.Madaktari walimuattend na kumwekea Drip ya Maji kushusha Pressure,wakaendelea na shughuli zao wakimuacha ,mpaka marafiki walipokuja kumuona na kukuta amefariki ndipo wakawaita madaktari na wao kuanza kushangaa tu.Unawezaje kumwekea mgonjwa aliyeserious drip nawe ukaenda mbali.Kifo hiki kimeniumiza na naamini ni uzembe kwani kilichotokea kwa Mitti miaka miwili iliyopita nikiwa Bunda niliugua nikamwomba Mitti anisindikize,wakanilaza kwenye private ward zao hapo hospitalini kwao,wakanitundikia drip.Usiku akaja nesi mwanafunzi akabadilisha ile drip ya Quinine na kuongeza spidi ya follow,Akaondoka baada ya kama dakika kumi Hali yangu ilibadirika nikaita nesi nesi nesi hakukuwa na dalili ya MTU kuitikia.Nikampigia Sostenesi nikiwa siwezi kupumua vizuri,watafute uwezekano wa madaktari maana nimetelekezwa.
Hali ilizidi kuwa mbaya,nilichokumbuka nikuomba nakujua muda wangu umekwisha.Ndipo ghafla akaingia mama Mdogo ambaye ni daktari hospital hiyo hakuwa zamu,na hakujua kama nipo hospitalini pale alipigiwa simu na Mitti,akaja anakimbia akanikuta nimelowa na sina uwezo Wa kuongea kwa sauti,nikamwonyesha Drip akaona tatizo akaichomoa drip na kuleta oksjeni na kuniwekea baada ya kama nusu saa nikapata nafuu na akina Mitti walikuwa tayari wapo wamezunguka kitandani wasijue kinachotokea.
Niliwaeleza kilichotokea kuhusu Yule nesi alitafutwa hakupatikana kabisa.Tulifuatilia na Mitti,hakutokea na Daktari Wa zamu hakuweza kumtambua,.
Ninapoambiwa Sosteness katuacha katika Mazingira Yale Yale inaumiza sana.Tunahitaji kufuatilia kwa karibu utoaji huduma za Afya katika Hospital ya DDH ,Vinginevyo wananchi watakatiliwa Maisha kila kukicha.
Tangulia Mdogo wangu Mitti uliokoa maisha yangu,nimeshindwa kuwepo kukuokoa.Bwana alitoa na BWANA ametwaa.Jina la Mungu wetu lihimidiwe.