Kaveli
JF-Expert Member
- Dec 4, 2012
- 5,120
- 8,140
Nilimpeleka ndugu yangu ocean road hospital alikuwa na shida ya cancer. ..kufika Pale kuonekana yuko dhaifu saana akapewa drip ya sukari bila vipimo
Baadae doctor alipokuja kufanya vipimo akakuta sugar iko 32 normal ni 4-7 , wakastopisha ile drip haraka sana but it was too late alifariki siku ileile jioni...hii imetokea mwezi uliopita
Pole sana mkuu. Hii Africa yetu bado ni majanga sana aisee. Ebu imagine mgonjwa anawekewa dripu ya sukari bila ya kipimo kwanza cha haraka. Yani muuguzi (sijuwi ndo nesi) anakisia tu na kufanya maamuzi afanye hiki. Hapo hakuna tofauti na ramli.
Unabunia tu na kumuwekea mtu dripu ya sukari ilihali kumbe mwili wake hauhitaji hicho kitu, then kwa uzembe huo mgonjwa anakufa! Afu eti ooh bahati mbaya, ooh mipango ya Mungu, and blah blah! Inaumiza sana walahi.
Ifike mahala watu waanze kushtakiwa kwa kosa la 'professional negligence' kama nchi zilizoendelea. Otherwise watu hawatakuwa makini wala kufuata guidelines za profession zao ktk kuhudumia watu.
Ndo maana mimi binafsi huwa naamini kwamba majanga na vifo vingi hapa Africa ni kutokana na UZEMBE (negligence/recklessness) tu, wala hakunaga bahati mbaya!! Na hii 'bahati mbaya' ndo ishakuwa utetezi wetu wa kila siku.
Poleni sana