Utii wa mwanamke ni dawa tosha ya nguvu za kiume

50 percent i agree but other percent the boy should use the altenative ways.Example VUNJA UKIMYA, VYAKUL, etc
 
Tukianza kuleteana mistari hapa hatutomaliza...tumeambiwa tupendane ila sio kila mtu ana uwezo wa kupenda...makosa kibao kwenye biblia tunambiwa tuadhibu kwa kuua ila hatufanyi hivyo...tunafundishwa kulipa visasi pia kutokufanya hivyo kwahiyo kila mtu anachagua kipi kinamfaa mle.As for me sina HITAJI la kutawaliwa though naweza nikawa NAPENDA ikitokea!

Exactly Lizzy!

Ukizingatia biblia iliandikwa na wanaume.

If this is the opinion then, we should demand a new Bible kama tunavyodai katiba mpya. Otherwise, sheria mama itaendelea kubakia:

"Hakika nitakuzidishia uchungu wa kuzaa na tamaa yako itakuwa kwa mwanaume naye atakutawala!" (Mwa. 3:16).
 
Naamini katika kutoku-challenge Hekima ya Mungu,Mungu Akisema Wanawake wawatii Waume zao ndiyo hivyohivyo,kuasi maagizo ya Mungu hutuletea MAUMIVU katika Maisha yetu!! Mungu anajua jinsi alivyomuumba Mwanaume in all aspects including mahusiano,anajua ile ahusiane vizuri na Mkewe Imempasa Mke Kushuku,huu si unyonge wala Ujinga ndiyo maana amefafanua "Kama kumtii Kristo" maana Kristo hawezi kumpa mtu maelekezo yasiyo na Maana!! Mwanamke ambaye ni Rebellious huujeruhi Moyo wa Mumewe na hufayafanya Mapenzi ya Mume kwa Mkewe KUSINYAA mithili ya Maua yaliyokosa Maji!! Mwanamke mwenye Utii hupendwa na Mumewe zaidi,viganja vyake humpapasa na kamwe havitotumika vinginevyo!!! Likewise,Waume nao imetupasa Kuwapenda Wake zetu!!! Cheers,No Hard Feelings!!!
 
Umejitahidi ila uliposema “maisha ya mwanamke yamejaa huzuni na mapungufu unless anatawaliwa somewhere“ umeangukia uso....yani naomba niseme umepotoka.Labda ungesema baadhi ungeleeweka zaidi na mimi ningekubaliana na wewe kwasababu najua wapo wanawake ndoa/mahusiano kwao ni zaidi ya HITAJI na SIO TAKWA‘!

Lizzy, Hapo kwenye Bold, ndo naona pamekukwaza sana, Mi naona ni sawa, hebu tupa nyongo.............
 
Jamani jamani bandugu bapenzi.....Ya Kaisari tumwachie huko kwake...na Muumba naye tumpe yake.

Siyo watu wote wenye ndoa wanaishi kwa katiba ya aina yoyote...ikiwemo biblia. Kwa hiyo si busara kutumia kitabu cha aina yoyote kuwa nyanyapaa au kuwalazimisha watu wengine mambo ambayo hawakubaliani nayo. Pia ukizingatia hakuna msaafu ambao unakubaliwa na watu wote katika dunia hii!!

Kwangu binafsi ndoa ni taifa huru (a sovereign state) ingawa mipaka yake siyo kama ya Tz, ZNZ au Kenya...Kwa hiyo mambo ya ndoa tuwaachie wahusika wenyewe...

Kuna ndoa wanaume wananyenyekeaa kuliko wanawake wakati ndoa nyingi wanawake wanaendeshwa kama magari mabovu...Tuwaache wenyewe waendeshi nchi zao (ndoa) labda wakiomba mediation ya aina yoyote ndio tuwape support!

Babu DC!
 
Ni kweli kabisa Dada, heshima na utii katika mahusiano ni suala la pande zote mbili, sawa sawa,
lakini hasa mwanamume anapaswa kumtii mke/mpenzi wake.
Vyenginevyo mke/mpenzi anaweza kulalamika na aibu ikamwangukia mwanamume.
Fikiria itakuwaje mke akilalamika "Mume wangu haniti.i"?
Iwe onyo kwa wanaume wasiowatii wake/wapenzi wao!

Hivi kutii ndo kufanyaje jamani?
 
JAMANI UTII NI SEHEMU YA UPENDO?,
sasa kwanini uwe unatolewa upande mmoja tu?,
kwa nini usitoke kila upande? na kwa nini utii uwe kwa kila jambo?,
kwani huyo mwanaume ni malaika? na siyo au binadamu?,
Binadamu huwezi kumtii kwa 100% kwa kila jambo alifanyalo, na kama
utamtii kwa kila jambo basi wewe ni sawa na boya, manake hata anapokosea wewe unamtii tu,
badala ya kumwelewesha na kumwambia kuwa anapotoka.

Kama utii ni sehemu ya upendo basi ni bora ukitolewa kwa kila upande, usiegemee upande mmoja,
na namuunga mkono aliyesema mambo ya ndoa hayana katiba bali yanaendeshwa jinsi wanandoa wenyewe,
wapendavyo kuiendesha ndoa yao, na hasa ukizingatia ndoa ni makubaliano ya watu wawili.
 
Hata hii umewapa?

avatar37304_2.gif

Toa avatar yako bana,haiendani na maadili ya JF

Hii avatar kwa kweli aaa,hapanaaa!
 
Inawezekana kuna ukweli flani ndani yake...
Ndoa nyingi ambazo wanawake wanawatii waume zao hudumu... tofauti na ndoa ambazo kila mtu anataka kuwa juu ya mwenzie!
Mwanaume anapenda kusikilizwa na kujiona yeye siku zote ndio muamuzi, yeye siku zote hana kosa, yeye siku zote ni wa kuombwa msamaha maana hakosei yeye...!
 
Inawezekana kuna ukweli flani ndani yake...Ndoa nyingi ambazo wanawake wanawatii waume zao hudumu... tofauti na ndoa ambazo kila mtu anataka kuwa juu ya mwenzie!Mwanaume anapenda kusikilizwa na kujiona yeye siku zote ndio muamuzi, yeye siku zote hana kosa, yeye siku zote ni wa kuombwa msamaha maana hakosei yeye...!
Eti hakosei....kawa malaika???Nadhani mngesema wanawake wakubali kuwa WATUMWA ili ndoa zao zidumu.Wakati huo huo wapo waliojitolea kwa moyo wote kua watumwa na wanachopata ni manyanyaso na ndoa za majina badala ya matendo!!
 
Malumbano yameonekana kinda sexity,wanaume tunachangia simply because we are men and the verses seems to be in our favour,and women including Lizzy are not supporting not simply because they are women and feel kinda being oppressed as they always think but they have a point to make..............as u know...
where fiords move,deep is the sea,
the dial stirs yet none perceives it move,
the turtles can not sing and yet they love,
and love is love as in kings is in slaves.
Mkuu, hatumshambulii Lizzy, tunabadilishana hoja ili tuweze kielewana.
 
Evergreen Umenena,

Hapa ndipo penye shida utii, alipewa mwanamke iweje mume amtii mke hali yeye alipewa kupenda, na kuishi kwa akili na mwanamke na kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu hivyo kuweni na akili kuishi nacho. Kuna wajibu watu walipewa hapa, na Mungu aliona kabisa shida iko wapi tena tangu pale bustani ya eden, ni kweli maneno yaliyomengi yaliandikwa na watu kulingana na mahali hapo, lakini ni sawa hata sasa, na biblia ya Yesu ilikuja kukamilisha tu ile ya mwanzo.

Wanaume kutokuwa na mapenzi na wake zao ni kwa sababu wanawake wanataka kushindana na wanaume (authority) (kichwa cha nyumba))wakati wao wamepewa kitu chao kuwa na mikono isiyobomoa nyumba zao (hekima/busara/maarifa).

Ukichinguza ndoa/wapenzi wenye furaha ni wale wanaotii agizo hilo, ambalo lina matunda ya upendo, furaha, upole, unyeyekevu, kiasi, heshima, mapenzi yatakuwepo, faraja itakuwepo, na Nguvu za kiume kama mmoja alivyosema itakuwepo, japo vyakula navyo vinachangia lakini kukiwa utii, hayo mtajadiri hata aina ya vyakula kwa ajili ya nguvu za kiume yatakuwepo, lakini wakati mwingine nguvu zakiume hazipo kwa sababu baba haheshimiwi nyumbani inambidi ahamie kule wanako mtii na ndiko anakomaliza hizo nguvu, kwa hakika nguvu hakuna nguvu inayotumika ikakaa kama ilivyo, hakuna nguvu itakayo kaa bure, lazima itumike, sasa mume wako mnalala mzungu wa pili/nne hiyo nguvu itapoteaje? sasa mama unataka nguvu kwa mtu usiyemtii itatokaje, usiyemjali, usiye mheshimu, usiye mpenda, na yeye anjua humpendi na unamtamkia kabisa...
Mwanake kauri mbaya, sauti ya juu kila siku, halafu unataka mashamsham na nguvu vitatoka wapi?

Pili, wanawake wakiwapata waume huwa wanadhani safari ndo imeisha, kujipenda kule kwa mwanzo kunaisha, kuvaa vizuri kunaisha, kukiss, kuhug, kutoa pole kwa wanaume zao hata kama wakati huo wao wote wanafanya kazi just do it for the sake of your marriage coz it is so, kama mwanaume wako anataka kuoga kabla ya kula fanya hivyo mpe maji kama hayako yale ya kisasa, kama taulo halipo bafuni fanay hivyo, kwa zile bafu zetu, kama chakula kipo mezani na pengine wewe hupendi kula jaribu kuwa naye mezani hata kama unajisikia taabu kufanya hivyo halafu ona kama huyu kiumbe dhaifu atabanduka hapo.

Mwanume anaweza akawa amekununulia hata gari, nyumba nzuri, kila kitu kizuri yet akakuacha unakula, unalala, unaendesha gari unafanya shopping, akaenda kula kwa mamashikaji nje tu kwasabau hakuna hizi herufi nne na kaneno ka UTII tu.

Na kama mwanamke anapaswa kutii, basi mwanamume amjali huyo anayemtii which is obviously kwa ka-research kangu nilikokafanya and the opposite is true.

Blessing Be Unto You !

Naamini katika kutoku-challenge Hekima ya Mungu,Mungu Akisema Wanawake wawatii Waume zao ndiyo hivyohivyo,kuasi maagizo ya Mungu hutuletea MAUMIVU katika Maisha yetu!! Mungu anajua jinsi alivyomuumba Mwanaume in all aspects including mahusiano,anajua ile ahusiane vizuri na Mkewe Imempasa Mke Kushuku,huu si unyonge wala Ujinga ndiyo maana amefafanua "Kama kumtii Kristo" maana Kristo hawezi kumpa mtu maelekezo yasiyo na Maana!! Mwanamke ambaye ni Rebellious huujeruhi Moyo wa Mumewe na hufayafanya Mapenzi ya Mume kwa Mkewe KUSINYAA mithili ya Maua yaliyokosa Maji!! Mwanamke mwenye Utii hupendwa na Mumewe zaidi,viganja vyake humpapasa na kamwe havitotumika vinginevyo!!! Likewise,Waume nao imetupasa Kuwapenda Wake zetu!!! Cheers,No Hard Feelings!!!
 
"Atamwacha baba na mamaye ataambatana na mumewe" ndani kabisa ya moyo wa mwnamke kuna ndoto ya kuchukuliwa na mwanaume mtanashati na mwenye kummiliki, vile vile maisha ya mwanamke mtawala mwanaume yamejaa huzuni,wasiwasi na mapungufu unless anatawaliwa somewhere..."Ukitii utakula mema ya nchi" .UTII wa mwanmke huifullfill nafsi ya mwanume na yeye kujisikia rijali na hivyo kitohitajika nguvu mbadala ktk mapenzi-sasa tunaona mke akipendwa sana, akienziwa na hata kubembelezwa..na ni wakati huu mme anapowajibika kwa familia yake. Mashindano,ubishi na hata kumlinganisha mwanaume ni sumu isiyo na simile ktk ndoa(impotance,ubaridi,kutojiamini na KUASI)..Nimefanya utafiti kidogo nimekutana na semi za wanaume ukioa mwmke mwenye elimu/fedha nyingi atakusumbua..Ewe msichana/mwnamke ni wakati wa kuikamata ndoa yako TII sasa kama agizo la BWANA

Enyi WAKE watiini waume zenu kama SARA alivyomtii Ibrahim hata akamwita Bwana. Enyi waume wamependeni wake zenu. Ni dhahiri kuwa Mwanamke anao wajibu wa kumtii mumewe hata kama hampendi naye Mwanaume anao wajibu wa kumpenda mkewe hata kama hamtii! Na chanzo cha nguvu za kiume ni ule upendo wa dhati kwa mwanamke, tatizo kubwa ni kwamba watu wanafanya mapenzi pasipo upendo, hii ni hatari kubwa sana hata jogoo linakuwa halina nguvu kwa vile upendo wa dhati umekosekana. Mwanaume anaweza kujisikia kuwa hana nguvu za kutosha kumbe jogoo limeingizwa mahali pasipotakiwa!
 
Kama issu ni responsibilities za nani kumtii nani au nani kumpenda nani (kama Mungu alivyosema!). Then vise versa is true, wanaume wanakiuka jukumu lao kubwa la uzalishaji. Wanawake walipewa reproduction role wakati Mungu alipomwambia eva kwamba kwa uchungu utazaa, na Adamu alipewa production role kwamba ardhi imelaaniwa juu yake na atakula kwa jasho. Sasa iweje watu humu jamvini hawaoni jinsi wanaume walivyowageuza wanawake 'mabuzi' wakati huo huo wanataka sisi tuendelee kushikilia zinazoitwa sheria za 'utii' kwa mwanaume, ikiwa wao mambo yamewashinda.
 
Kuna tofauti gani kati a upendo na utii ukizingatia ulivyoandika hapo kwenye bold. Nilivyokusoma inaelekea mwanamke anapaswa afanye vyote utii na upendo. Angalia nilipo bold. Mapenzi yanapaliliwa na pande zote mbili bwana ili yanoge. Kuna wamama nawajua ambao wakiona wame zao wanatetemeka which to me is more of utii na bado waume zao ni full vimada.

Evergreen Umenena,

Hapa ndipo penye shida utii, alipewa mwanamke iweje mume amtii mke hali yeye alipewa kupenda, na kuishi kwa akili na mwanamke na kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu hivyo kuweni na akili kuishi nacho. Kuna wajibu watu walipewa hapa, na Mungu aliona kabisa shida iko wapi tena tangu pale bustani ya eden, ni kweli maneno yaliyomengi yaliandikwa na watu kulingana na mahali hapo, lakini ni sawa hata sasa, na biblia ya Yesu ilikuja kukamilisha tu ile ya mwanzo.

Wanaume kutokuwa na mapenzi na wake zao ni kwa sababu wanawake wanataka kushindana na wanaume (authority) (kichwa cha nyumba))wakati wao wamepewa kitu chao kuwa na mikono isiyobomoa nyumba zao (hekima/busara/maarifa).

Ukichinguza ndoa/wapenzi wenye furaha ni wale wanaotii agizo hilo, ambalo lina matunda ya upendo, furaha, upole, unyeyekevu, kiasi, heshima, mapenzi yatakuwepo, faraja itakuwepo, na Nguvu za kiume kama mmoja alivyosema itakuwepo, japo vyakula navyo vinachangia lakini kukiwa utii, hayo mtajadiri hata aina ya vyakula kwa ajili ya nguvu za kiume yatakuwepo, lakini wakati mwingine nguvu zakiume hazipo kwa sababu baba haheshimiwi nyumbani inambidi ahamie kule wanako mtii na ndiko anakomaliza hizo nguvu, kwa hakika nguvu hakuna nguvu inayotumika ikakaa kama ilivyo, hakuna nguvu itakayo kaa bure, lazima itumike, sasa mume wako mnalala mzungu wa pili/nne hiyo nguvu itapoteaje? sasa mama unataka nguvu kwa mtu usiyemtii itatokaje, usiyemjali, usiye mheshimu, usiye mpenda, na yeye anjua humpendi na unamtamkia kabisa...
Mwanake kauri mbaya, sauti ya juu kila siku, halafu unataka mashamsham na nguvu vitatoka wapi?

Pili, wanawake wakiwapata waume huwa wanadhani safari ndo imeisha, kujipenda kule kwa mwanzo kunaisha, kuvaa vizuri kunaisha, kukiss, kuhug, kutoa pole kwa wanaume zao hata kama wakati huo wao wote wanafanya kazi just do it for the sake of your marriage coz it is so, kama mwanaume wako anataka kuoga kabla ya kula fanya hivyo mpe maji kama hayako yale ya kisasa, kama taulo halipo bafuni fanay hivyo, kwa zile bafu zetu, kama chakula kipo mezani na pengine wewe hupendi kula jaribu kuwa naye mezani hata kama unajisikia taabu kufanya hivyo halafu ona kama huyu kiumbe dhaifu atabanduka hapo.

Mwanume anaweza akawa amekununulia hata gari, nyumba nzuri, kila kitu kizuri yet akakuacha unakula, unalala, unaendesha gari unafanya shopping, akaenda kula kwa mamashikaji nje tu kwasabau hakuna hizi herufi nne na kaneno ka UTII tu.

Na kama mwanamke anapaswa kutii, basi mwanamume amjali huyo anayemtii which is obviously kwa ka-research kangu nilikokafanya and the opposite is true.

Blessing Be Unto You !
 
Una akili sana wewe! Machangudoa hunyenyekea sana wanaume (hata kama ni kwa hila) ndio maana wanajinyakulia waume za watu kiulaini na hawachomoki hata kwa dawa!

Katika biashara yoyote, mteja ni mfalme. Siyo ajabu ukaona changu anamnyenyekea mteja (mume wa mtu).Mahusiano ya kindoa hakuna uteja.Ni ubia wa kiwango cha juu kuliko ubia wa kawaida.

Nakubaliana nawe kuwa lazima mwanamke amuheshimu mumewe lakini pia lazima mume naye amheshimu mke.Heshima haiwezi kuwa ya upande mmoja tu.

Ogopa pia mnyenyekeo uliopitiliza maana "kutakua na agenda ya siri".Mruhusu mkeo awe yeye akiwa na wewe.Usimfanye awe na nidhamu ya woga.

Kwa kifupi kila mmoja wa wanandoa atekeleza wajibu wake ipasavyo na mambo yatakuwa mazuri tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom