SoC02 Afya ya uzazi: Upungufu wa nguvu za kiume

Stories of Change - 2022 Competition

Dr Yesaaya

Member
Jul 25, 2022
9
23
UKOSEFU AMA UPUNGUFU W NGUVU ZA KIUME

Mwandishi: DR. Yassayah M, 0752591744/0682080069 wa -Tegeta DSM

UTANGULIZI

Ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume kitaalam – Erectile Dysfunction ni hali ya uume kushindwa kuamka/kusimama au kuamka kwa muda mfupi kisha kushindwa kuendelea kusimama wakati mwanaume anaposhiriki tendo la ndoa. Hii ni tofauti na ugumba kwa wanaume yaan male infertility ambapo mwanaume hushindwa kutengeneza mbegu zenye ubora na nguvu kushindwa kurutubisha yai la mwanamke ili kumpa ujauzito. Hivyo mwanaume anaweza asiwe mgumba ila anaweza kuwa na upungufu tu wa nguvu za kiume. Ni tatizo linawakumba watu wa jamii na rangi zote duniani ikiwemo wazungu na watu weusi.

Tafiti iliyofanyika Dar Es Salaam, 2016 (Pallangyo et al) ilionesha asilimia 24% hadi 55% wanaume kati ya umri 18yrs na kuendelea wana tatizo la upungufu w a nguvu za kiume. Hata hivyo si suala kubwa kwa kijana wa kiume iwapo tatizo linatokea mara chache tu ila kama hutokea mara kwa mara ni suala nyeti na la kutafutia ufumbuzi maana huweza kuleta msongo wa mawazo (psychological stress), kupunguza kujiamini, na hata kuvuruga mahusiano ya ndoa au wapenzi. Tatizo hili linaweza kuwa ni dalili ya magonjwa mengine ndan ya mwili kama vile magonjwa ya moyo na kisukari. Mwanajamii usidharau.

Dalili zake
  • Kulegalega kwa uume kusimama imara wakati wa tendo la kujamiiana (trouble getting an erection)
  • Kushindwa kuendeleza hali ya uume kusimama yaan inasimama kisha inalala (trouble keeping an erection)
  • Kukosa hamu ya tendo (reduced sexual desire)
  • Kufika kileleni haraka sana (premature ejaculation) au kushindwa kabisa kufika mwisho/mshindo(delayed or failed ejaculation)
  • Kushindwa kumpa mwanamke ujauzito (male infertility) ni matokeo ya tatizo hili iwapo halikutibiwa kwa wakati
Sababu ya tatizo
  • Kupata hamu au nyege kwa mwanaume yaan kitaalamu tunaita male sexual arousal inahusisha vitu anuai – kama vile
  • Ubongo – ili uume usimame lazima ubono wa mwanume ulete taarifa kwa njia ya mifumo ya fahamu kwamba sasa ni muda wat endo hivyo vichocheo vizalishwe kwa wingi. Iwapo kuna shida katika ubongo uume hautosimama
  • homoni au vichocheo (testosterone) – hizi protini zinazozalishwa kwa wingi kijana anapobarehe hizi ndizo huchochea misuli ya uume ipelekewe damu na kusimama – unajiuliza uume hauna mfupa lakin husimama na luwa mgumu km fimbo – hilo ni sababu ya homoni hizi. Bila hizi homoni huwez kupata hamu ya tendo. Tafiti zinaonyesha Wanaume wenye homoni hii kwa wingi zaidi huwa na wanawake wengi na inahusishwa na suala la vinasaba au kurithi.
  • Hisia (emotions), - hizi huja kwa kuamrishwa tamaa ya macho na taarifa hufikia ubongo kisha homini kuzalishwa na kupelekea hamu ya tendo. Iwapo hisia haziko swa kama vile kutokumpenda mwenza au athari mambo mengine kama mazingira hatarishi, wivu wa mapenzi, magonjwa u=ya uke yaletayo harufu au maneno hasi kutoka kwa mwanamke hufubaza hisia za mwanaume na kupelekea kushindwa kusimamisha
  • mishipa ya fahamu (nerves), - changamoto za mishipa ya fahamu hupunguza taafa zinazotakiwa kufika kwenye uume. Magonjwa kama neuritis, periphero neropathy yaletwayo na kisuakali au ukosefu wa vitamin huathiri uwasilishwaji wa taarifa muhimu za kuamsha uume
  • misuli (muscles) – ulegevu wa misuli ya uume na ukosefu w protini muhimu huleta madhara katika usimamaji wa uume. Tafiti zinasema upigaji punyeto huweza kusababisha uzorotaji wa misuli hii lakin tafiti nyingi za kisayansi hupingana na hilo na kusema punyeto haina madhara kabsa kiafya. (nitazungumzia punyeto katika mada zijazo)
  • mishipa ya damu(blood vessels). Magonjwa kama vile vasculitis na shinikizo la juu au la chini la damu huathiri usafirishwaji wa damu kufikia kwenye uume.
  • Hivyp basi, Matatizo yoyote ktk maeneo hayo huweza kuleta upungufu wa nguvu za kiume na kuathiri ubora wat endo la ndoa.
  • Msongo w mawazo au matatizo y kisaikolojia yanayoiathiri akili ni rahisi kushindwa kusimamisha uume na hivyo kuathiri tendo la ndoa.
  • Hofu (anxiety) huzidisha tatizo hili maradufu.
  • Vilevile magonjwa ya moyo, mishipa ya damu kuziba, ongezeko la mafuta mwilini (high cholesterol), ugonjwa wa shinikizo la juu la damu (hypertension), ugonjwa wa kisukari(diabetes), na unene uliopitiliza(obesity) na kutokufanya mazoezi
  • Tena, uvutaji w sigara, unywaji pombe uliopitiliza, madawa ya kulevya, matatizo y kukosa usingizi, magonjwa ya tezi dume na tiba zake pia hupelekea tatizo hili
  • Masuala ya kisaikolojia kama vile msongo (depression) hofu, stress za maisha kifedha, changamoto za kimahusiano – ugomvi, makasiriko, kukosekana kwa mawasiliano mazuri baina ya wapenzi
  • Madawa ya hospitali kama vile dawa za mafua na miwasho (antihistamines), dawa za presha, dawa za kifafa huweza kuleta dalili za kupungua nguvu za kiume

Nini kifanyike kuzuia tatizo hili

Serikali kupitia wizara ya afya:-
Elimu kupitia mashirika na vyombo vya habari runinga, radio, magazeti na mitandaao ya kijamii,uelewa na elimu itolewe kwa jamii juu ya tatizo hili maana linaathiri furaha ya wanajamii hivyo kuchelewesha au kudumaza harakati za kimaendeleo.

wajibu wa Mwanajamii:
  • Fika kwa wataalamu eleza shida yako ili upimwe na kupewa ushauri kugundua sababu, kama ni sukari itibiwe, kama ni unene na ongezeko la mafuta pia litibiwe nakadharika
  • Jenga tabia ya kufanya uchunguzi wa afya yako angalau kila baada ya miezi 6 (mara mbili kwa mwaka)
  • Acha sigara, punguza au acha pombe. Acha dawa z akulevya
  • Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara, zinagtia mlo kamili epuka mafuta mengi katika chakula, kunywa maji ya kutosha, mboga za majani na matunda kwa wingi.
  • Chukuwa hatua za kupunguza mawazo(stress)
  • Tafuta msaada juu ya hofu (anxiety) uliyonayo, msongo wa mawazo na matatizo mengine ya kiakili
  • Shirikisha mpenzi au mkeo katika hili mtafute suluhisho mapema na kwa pamoja – wakati mwingine ni mkeo ndio anakusababishia kwa kukupa stress au kwa kutokukuandaa kwa ajili ya mechi au makasiriko ya mara kwa mara kukukaripia, au harufu mbaya inayotoka katika uke wake au matatizo mengine yalio upande wake.
Matibabu
Inaposhindikana njia zilizotajwa hapo juu basi sasa dawa za kitaalamu hutumika kama vile sildenafil, tadalafil nakadharika. Angalizo usitumie dawa hizi bila ushauri wa daktari. Dawa hizi zinaweza kuleta matokeo hasi (side effects) kama vile mafua, kicha kuuma, matatizo ya tumbo, kushuka kwa msukumo w damu(low blood pressure).

Ushauri w kisaikolojia ni tiba

Source: Davidson textbook, mayoclinic. Wikipedia, researches, medical books
 
Back
Top Bottom