Uteuzi wangu ni heshima kubwa kwa NCCR - Mbatia

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mwenyekiti wa NCCR James Mbatia amesema ameteuliwa kuwa mbunge na Rais kwa sababu chama chake hakiamini katika vurugu na kumwaga damu kama baadhi ya vyama vinavyofanya.

Mbatia amesema hiyo ndiyo sababu pekee iliyosababisha Rais kukipa heshima chama chake na wala sio kulipwa fadhila kama baadhi ya watu wanavyosema

Source: Mwananchi Jumamosi
 
Bora rais akupe na kadi mpya ya magamba kwani kazi yako ya kunafiki upinzani wa kweli umeifanya kwaumakini mkubwa.
 
Hongera nccm. Bado vyama njaa vingine. Tutaviona tu... Tlccm ipo njiani inakuja
 
Mwenyekiti wa NCCR James Mbatia amesema ameteuliwa kuwa mbunge na Rais kwa sababu chama chake hakiamini katika vurugu na kumwaga damu kama baadhi ya vyama vinavyofanya.
Mbatia amesema hiyo ndiyo sababu pekee iliyosababisha Rais kukipa heshima chama chake na wala sio kulipwa fadhila kama baadhi ya watu wanavyosema

Source:Mwananchi Jumamosi.

ndicho nilichokitegemea, kukataa kwamba hajalipwa fadhila...
 
Sasa nimegundua kwanini kafulila anautk uenyekiti wa NCCR,,huyu jamaa hajui anachokifanya na nini waxwax na uelewa wake kuhusu maana ya upinzani
 
Mwenyekiti wa NCCR James Mbatia amesema ameteuliwa kuwa mbunge na Rais kwa sababu chama chake hakiamini katika vurugu na kumwaga damu kama baadhi ya vyama vinavyofanya.
Mbatia amesema hiyo ndiyo sababu pekee iliyosababisha Rais kukipa heshima chama chake na wala sio kulipwa fadhila kama baadhi ya watu wanavyosema

Source:Mwananchi Jumamosi.

what a load of nonsense.....NCCR inakufa na ndio maana wanaanza kukimbilia ccm taratibu...this coming election ya 2015 tutaona nccr itapata wabunge wangapi....hata hao walionao sasa hivi 2015 wanapigwa chini...its the beginning of the end for nccr

Ndugu mbatia viongozi wa chadema wanaokatwa mapanga na kuchinjwa na wengine kutishiwa maisha yao...wanatishiwa na watu wa chama gani??!! Unaongea kama vile hujaenda shule...Njaa jamani kitu kibaya sana.:thinking:
 
Ningeweza kumhoji maswali live ningemuuliza 1. Chama cha upinzani kinachomwaga damu ni kipi? 2. Kwanini asifie ubunge wa kupewa na Rais(ccm) badala ya kupambana aupate kama wanaume [wenyeviti] wenzie walivyopambana 3. Atamlipa kikweti fadhila gani kwa ubunge aliompatia
 
Mwenyekiti wa NCCR James Mbatia amesema ameteuliwa kuwa mbunge na Rais kwa sababu chama chake hakiamini katika vurugu na kumwaga damu kama baadhi ya vyama vinavyofanya.
Mbatia amesema hiyo ndiyo sababu pekee iliyosababisha Rais kukipa heshima chama chake na wala sio kulipwa fadhila kama baadhi ya watu wanavyosema

Source:Mwananchi Jumamosi.
.....ningekuwa mbatia ningemalizia hivi....na ukizimgatia kipigo cha Halima Kawe namshukuru sana JK kwa kunibeba katika aibu
hii....ningejua ataniteua nisingegombea Kawe. Bravo JK
 
Heri ya chama kinachoamini katika kumwaga damu kuliko chama kinachomwaga damu kabisa. CCM imemwaga damu za makada wa CDM Igunga na Arumeru katika kulazimisha kuwatawala watu wasioitaka. Pia imemwaga damu za watanzania wasio na hatia Nyamongo, Songea na Arusha.
 
Mwenyekiti wa NCCR James Mbatia amesema ameteuliwa kuwa mbunge na Rais kwa sababu chama chake hakiamini katika vurugu na kumwaga damu kama baadhi ya vyama vinavyofanya.

Kwani anayemwaga damu ni nani kama sio CCM? Kilichotokea Arusha ni nani alimwaga damu? Kilichotokea Mwanza hivi karibuni ni nani wamefanya hayo? Nape ambaye siku zote anajinadi kama msemaji wa chama hajaesema chochote kuhusu la Mwanza. kilichotokea Arusha nacho vipi?

Kifupi amelipwa haki yake na sasa yuko tayari kuongeza nguvu Bungeni kwa kuungana na Mzee wa Kiraracha aliyemwachia jimbo enzi hizo. wote lao moja.
 
Mbatia anatakiwa akae kimya kabisa sitegemei Ukiwa M/Kiti wa chama Uteuliwe kuwa Mbunge ukubali hivi haoni kama amekidhalilisha chama chake na akiingia bungeni ikitokea hoja nzito sidhani kama ataweza kukutea taifa huyu naona kaenda kuchumia tumbo tu hatakuwa na jipya na NCCR ndiyo imekufa hivyo.
 
jamaa kaanza kazi kabla ya kuapishwa, atavuruga upinzani bungeni sana. ndo maana Kafulila aliona mbali na watu tukachukulia poa.
 
Back
Top Bottom