Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,900
- 3,206
Siwafahamu kiundani,.lakini nina uhakika vyombo vya dola vinawafahamu vizuri zaidi na ndio maana vikapeleka majina yao kwa Mh. Rais kwa nafasi za Ukuu wa Wilaya.
Sasa kinachoonekana kwa sasa ni kwamba, hawa viongozi wa walimu, wanaandamwa kwa sababu ya kugomea uteuzi wa Mh. Rais!
Kama kweli walikuwa na kashifa za ufisadi, mbona hawakushughulikiwa hapo kabla?
Ina maana kukataa uteuzi wa Mh. Rais ni kosa?!
Nimejisikia kuongelea hilo kwa maana kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na changamoto sana kwa wale wanaoonekana kutokubaliana na Mh. Rais, kuibuliwa kwa vikwazo vingi.
Hili la viongozi wa CWT, nalifananisha na kile kilichotokea kwa kiongozi wa chama cha NCCR-Mageuzi, Mh. James Mbatia, ambaye baada ya kugoma kuitikia wito wa Mh. Rais wa kwenda Ikulu kufanya maridhiano, vikwazo vikaanza kuibuka kwa viongozi wenzake waandamizi!
Kama Mtanzania, nimeona niliongelee hili, maana kinachotokea kwa viongozi wa walimu, binafsi naona ni kwa sababu ya "kukataa" uteuzi na wala si vinginevyo.
Asalaam Aleykum.