Usipite polepole daraja la Kawe; kuna majambazi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,980
22,173
Ndugu wana JF.

Za asubuhi, mchana, jioni?

Wapendwa katika Bwana nimeona nishiriki nanyi kwa ushuhuda wa mwenyezi mungu alionisaidia jana

Nilikuwa nikienda kumshusha mchumba wangu Kawe, nikapitia bara bara ya Mama Rwakatare kuitafuta barabara ya Kawe, nilipokata kulia nikaona gari moja corolla 100 ilikuwa inakuja kwa mwendo wa kawaida gafla ikaongeza speed na katika kukimbia ikatoka nje ya barabara kidogo kabla ya kurudi barabarani.

Nilipoona nikasimama kwa shock; ghafla jamaa aliponiona nimesimama akapunguza mwendo nakutamka "FUNGA VIOO KUNA MAJAMBAZI DARAJANI"
Nilichofanya si kurudi nyuma nikaamua kwenda kwa speed na kupita pale darajani.. nilipopita kidogo shemeji yenu; wifi yenu akaniambia wale paale wanakimbilia porini....nilimshukuru Mungu nilipoona keep-left ya Kawe
nikawaza mbali sana ....jamani hawa watu nahisi kama awashiriki wanajeshi basi wanajeshi lazima wanawasaidia kwenye huu uhalifu....

Ndugu zanguni mh MWAMUNYANGE KABLA ya kuwa mkuu wa majeshi...alipitiwa na wataalam wa hapo hapo darajani.. siku ya pili yake wanajeshi wakaanza kushinda usiku pale mpaaka asubuhi....walikaa pale kwa muda kidogo....sasa nimeshindwa kuelewa ni nguvu ya soda ama ;
 
ndugu wanandugu ni vibaya kuamini lakini kwangu miimi naitajika kuamini hapa wanajeshi.....wanahusika na huu wizi...ndugu zanguni...sehemu wanayofanyia uhuni iko jeshini kabisa ,na leo nimepata mkasa mmoja kuna ndugu nae mwana JF alipita pale miezi sita iliopita...akatokea mtu na kudandia gari akakimbiza kwa speed alipofika karibuni jeshini akaruka.......,na hakuna mwanajeshi aliemfwatlia...mi nahisi hii kesi ya darajani aiitaji polisi tunaomba mwamunyange ajipange na wanajeshi wake waanze kukesha pale..na si mpaka alizwe mkubwa ama mtu wa jeshi ndio wakumbuke kuleta ulinzi pale..nyie wanajeshi kazi yenu kulinda wananchi na nyie ndio mnaamua kuigeukia amani..nani atulinde jamani???
 
Mna uhakika ni mandata au vibaka tu wa kawaida.Anyway patrol ni muhimu.
 
Sio kazi ya Mkuu wa majeshi bali Said mwema na wafuasi wake!
 
hili daraja kulikoni!? naelekea kuamini kuwa ni kweli hawa jamaa wenye dhamana ya kulinda nchi wanahusika! Hii sio incident ya kwanza, kwa mwaka huu peke yake nadhani inaweza kuwa ya tano au sita kati ya zilizoripotiwa katika hili hili daraja! nakumbuka pia alishawahi kuuawa mama mmoja wa kijapani katika daraja hili hili miaka ya nyuma! kulikoni????kama ni wezi/vibaka wa ukweli basi watakuwa na roho ya kijasiri mno ukizingatia lile ni eneo la jeshi, hali inazid kuwa mbaya licha ya kuwa limeongezwa daraja la pili kwenye hili eneo....
 
Vibaka kila kona, kama Zombe alikibaka hawa wengine si ndio watasisevia tuu kama wananawa.
 
Vibaka kila kona, kama Zombe alikibaka hawa wengine si ndio watasisevia tuu kama wananawa.

HASWAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
 
Eneo la kawe darajani ni kichaka kibaya cha majambazi,tunamuomba Kamanda kova atusaidie sisi wakazi wa mbezi beach,tegeta,na bunju,africana tunaotumia daraja hili na kurudi usiku kutoka makazini,tupatiwe askari wakulinda eneo hili jamani.

cha kusikitisha zaidi mahali pale ni karibu kabisa na kambi ya jeshi la kujenga taifa makao makuu,KULIKONI!
 
Ndugu wana JF.

Za asubuhi, mchana, jioni?

Wapendwa katika Bwana nimeona nishiriki nanyi kwa ushuhuda wa mwenyezi mungu alionisaidia jana

Nilikuwa nikienda kumshusha mchumba wangu Kawe, nikapitia bara bara ya Mama Rwakatare kuitafuta barabara ya Kawe, nilipokata kulia nikaona gari moja corolla 100 ilikuwa inakuja kwa mwendo wa kawaida gafla ikaongeza speed na katika kukimbia ikatoka nje ya barabara kidogo kabla ya kurudi barabarani.

Nilipoona nikasimama kwa shock; ghafla jamaa aliponiona nimesimama akapunguza mwendo nakutamka "FUNGA VIOO KUNA MAJAMBAZI DARAJANI"
Nilichofanya si kurudi nyuma nikaamua kwenda kwa speed na kupita pale darajani.. nilipopita kidogo shemeji yenu; wifi yenu akaniambia wale paale wanakimbilia porini....nilimshukuru Mungu nilipoona keep-left ya Kawe
nikawaza mbali sana ....jamani hawa watu nahisi kama awashiriki wanajeshi basi wanajeshi lazima wanawasaidia kwenye huu uhalifu....

Ndugu zanguni mh MWAMUNYANGE KABLA ya kuwa mkuu wa majeshi...alipitiwa na wataalam wa hapo hapo darajani.. siku ya pili yake wanajeshi wakaanza kushinda usiku pale mpaaka asubuhi....walikaa pale kwa muda kidogo....sasa nimeshindwa kuelewa ni nguvu ya soda ama ;

Tofautisha vibaka na majambazi ... usha sikia jambazi kaiba ucku?
 
Daraja livunjwe wanajeshi wachukue daraja leo halafu Tanroads walete daraja kubwa la magari 2 kila upande. Pale panachangia sana foleni
 
Hapo Darajani ni kambi ya Waheshimiwa wa NGUVU TISA AKILI MOJA bila shaka wakikosa kupora magari wanahamia maduka ya karibu na hapo na kupora na utashangaa hawakamatwi hata siku 1
 
Khaa!! Niliogopa kweli. Kumbe ni year 2009 wakati hata valentina kifua bado flat screen :)
 
Tatizo barabara zetu hazina taa! Sehemu kama ile ilihitaji mwangaza mkali pande zote na ikibidi kichaka kile kiondolewe ubaya kwetu tz uwajibikaji hakuna sijui halmashauri za manispaa zinafanya kazi gani? Nashanhaa jiji kubwa ka hili city centre hakuna street lights ni giza! Hii hatari sana
 
Juzi Stakishari Ukonga palikuwa pamewaka taa.
 
Duh bora mmetufahamisha na wengine japo habari yako nihatari unaweza jiku unang'olewa meno na plais
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom