USHAURI: Usije UDOM, kama umechaguliwa pale fanya taratibu za uhamisho haraka.

Hawa jamaa wnaongea tu na hizo hypothesis zao ambazo hazijafanyiwa research za kutosha....madogo mliochaguliwa UDOM kwanza nawapongeza na wala hamtajutia ila kinachohitajika ni kuvumilia changamoto za hapa na pale kwani hakuna sehemu isiyokuwa na changamoto kulinganisha chuo kimoja na kingine naona kama ni upuuzi tu cha msingi ni kupiga kitabu mambo yaende hayo mengine sijui ukiwa chuo fulani ajira hausumbuki ni uongo tu swala la ajira ni kama hesabu za probability tu...unajua wakati nipo form six haya maneno yalisemwa sana oooh chuo udom kibaya hakina walimu wataalam wenye uzoefu lakini baada ya kuingia pale ndipo nikaamini kuwa kuna watu wapo kwa ajili ya kupotosha raia katika kutafuta kile wanachokihitaji leo hii nipo pale na naenda kuhitimu mwaka wangu wa tatu na ninafurahi kuwa pale..na mkikae mkijua changamoto ni sehemu pia ya kufanikisha jambo fulani...
 
Mtu mwenye elimu yake huwezi kukaa na kushauri upumbavu kama huu...yaani ni utumbo wa maiti iliyooza kabisa.....
 
Hizo pia ni changamoto za elimu.
Nadhani kila chuo kina changamoto zake na hata wakihamia vyuo vingine watakutana na changamoto eidha zinafanana au tofauti na hilo.Watahama vingapi?
Chamsingi mtu akomae atoke mana cha msingi upate elimu.
 
Narudia Tena

Acha Ujinga

Na yule aliyeshindwa kumjibu mkulu Jana hapo Bandari alisoma UDOM ee?

Mungu Ibariki UDOM
 
UDOM kama hauna division one kozi za afya, engineering na education kwa upande wa arts hukanyagi utapasikia tu kwenye Radio.
UDOM YA SASA SI ILE YA ZAMANI.
Sikuhz UDSM NDO INACHUKUA WATU WENYE UFAULU MDOGO.
MFANO*kuna ndugu yangu alijaza education tupu alianza Udom chapili udsm ila kachaguliwa udsm education udom kakosa alipata one ya 9 HGL.
Inamaana one ya tisa ni ufaulu mdogo? ???
 
Hebu nipe kidogo changamoto za Transfer hasa Changamoto atazopata mtu mnufaika wa Mkopo baada ya kuhamia institution nyingine
Itakuchukua kama miezi isiyopungua mitatu ukiwa mfuatiliaji. Ila baada ya hapo ni mtiririko tu tena pesa yajo yote utapata. Ila inabidi uwe na akili ya kuwafuatilia hao loan board. ukizembea tu ishakula kwako.
 
Vyuo vingi Tanzania matatizo yapo naskia chuo kimoja sometimes mpaka maji taka yanatiririka majiani ni uchafu wa kiwango.
UDOM kule uhaba wa maji vyooni ni uchafu sana kichefuchefu naskia harufu ya vyoo inafika mpaka madarasani huko.

Elimu bora ni janga la kitaifa mfumo mbovu kuanzia mitaala na mbinu za ufundishaji hii kote uendako Tanzania huezi pata elimu bora sababu mfumo ni mmoja unaotumika kwa nchi nzima.
 
Nawakaribisha UDOM hasa first year kozi ya sheria. Kwa sasa tuna College na skuli yetu pande za bondeni humanities
 
Vyuo vingi Tanzania matatizo yapo naskia chuo kimoja sometimes mpaka maji taka yanatiririka majiani ni uchafu wa kiwango.
UDOM kule uhaba wa maji vyooni ni uchafu sana kichefuchefu naskia harufu ya vyoo inafika mpaka madarasani huko.

Elimu bora ni janga la kitaifa mfumo mbovu kuanzia mitaala na mbinu za ufundishaji hii kote uendako Tanzania huezi pata elimu bora sababu mfumo ni mmoja unaotumika kwa nchi nzima.
Nimekupata hapo..ila hiyo kusema kuwa harufu ya vyoo inafika mpaka madarasani kwa uliyesikia akisema basi ujue huyo anachuki binafsi na UDOM maana hakuna hicho kitu...
 
Back
Top Bottom