USHAURI: Usije UDOM, kama umechaguliwa pale fanya taratibu za uhamisho haraka.

Huyu mtoa mada inaonekana ala disco isee...
Nilimwambia mdogo wangu ajifelishe ili tumpeleke chuo kingine, aliandika madudu sana lakini cha ajabu matokeo yanatoka ana GPA ya 4.2,, Acha uongo mkuu hapo UDOM hata ukiamua kufeli hauwezi.
 
Nilimwambia mdogo wangu ajifelishe ili tumpeleke chuo kingine, aliandika madudu sana lakini cha ajabu matokeo yanatoka ana GPA ya 4.2,, Acha uongo mkuu hapo UDOM hata ukiamua kufeli hauwezi.
Acha uongo wewe. Humu sio wodi ya vichaa.... umepotea. Humu tunajielewa.
 
Pole sana ndugu yangu, Inaonyesha kuna pesa hukuzipata na bado utazilipa tu bodi.. Hayo matatizo kwa UDOM ni kawaida sana na hakuna anayejali, sio Uongozi, walimu wala serikali ya wanafunzi.
ni deni na nitalipa no way out....maana Bodi walijifanya hawajui kama wanafunzi huwa wanasaini kwanza frdha ndiyo wanawekewa kwenye akaunti zao, walisema tu ikiwa zimesainiwa basi ulilipwa...!!!!!!!!!!!
 
h
Haya kama ni kweli ni uzembe na kutowajibika kwa wahusika na serikali inatakiwa kuangalia haya uongozi wa chuo na hata huko bodi.
hauamini...au unataka kukitetea chuo ambacho chenyewe ni aibu hata kujitetea kwa hili??? mie nilikuwa college ya Social Science, Mkurugenzi wa idara ya wanafunzi niliyokuwepo alikuwa anafahamu suala langu hadi mwisho waliponiingiza mjini na loan officer wake miaka ile....na nafahamu waliopatwa na haya wanaweza wakawa wengi zaidi. labda kama kondoo mwenye madoamadoa pale UDOM alishagastaafu ila kama bado yupo................
 
Kachukue statement benki kwa muda huo. Uonyeshe. Tulifanya hivyo tukafanikiwa
its long time now brother, and so far ni kama kuna mambo mengine huwa ni ya kupotezeana muda sana na nilighairi kwa sababu hata Bodi makao makuu alikuwepo yule jamaa kama mmasai aliyetumbuliwa alikuwa anaboa sana mbaya zaidi ni kama kulikuwa na networking...ukienda kwa jamaa aliyekuwa anashughulika na UDOM anajifanya ana majibu hata kabla hujamaliza kueleza shida yako na unapigwa kalenda!!! au unaambiwa andika barua tutakujibu kwa e-mail n.k
 
Poleni sana wadogo zangu na kipindi hiki kigumu kwenu katika kufuatilia mustakabali wa elimu yenu ya chuo kikuu.

Ushauri wangu kwenu ni kwamba jitahidini kadri ya uwezo wenu kutafuta elimu bora na sio bora elimu kwani itakua ni msaada mkubwa baada ya wewe kumaliza chuo huku mtaani hata kama utakosa ajira.

Elimu bora hupatikani Katika mazingira mazuri ikiwemo uongozi na walimu lakini haya mawili hayapo Udom licha ya majengo mazuri yenye uhaba wa maji.

Uongozi ni tatizo pale Udom hasa katika college ya COES na NATURAL SCIENCE , mfano kupata hela ya mkopo kutoka bodi kama bum na pesa ya PT ni kama kubahatisha kwa mwanafunzi wa pale. Hadi kufikia sasa kuna kundi kubwa la wanafunzi wa COES na NATURAL SCIENCE ambao hawajapata pesa ya Field na Special faculty na hakuna sababu yoyote ya msingi inayotolewa zaidi ya ukiuliza utatishiwa kufukuzwa chuo tu.

Kifupi Kuna ombwe kubwa sana la uongozi chuoni pale hasa college ya COES na NATURAL SCIENCE kwani wakuu wake wamekua waoga sana na kukosa maamuzi.

Yangu ni hayo tu, usiponielewa hapa nenda mwenyewe ukajionee miaka mitatu au minne utakavyoiona kama muongo mmoja hapo Dodoma.
kwa first year group la whatsupp udom mtafute 0657604167 kwa information nying za chuo unapata
 
Sasa unabisha nini na unakubali nini?? Mara nyingi uongozi wa Udom hawajali kabisa swala la pesa za wanafunzi, huwezi mpa mwanafunzi kilicho bora wakati ana njaa ndio sababu vyuo vingine hutilia mkazo sana swala la mikopo ya wanafunzi wao.
Chuo gani kinachotilia mkazo swala la mikopo ya wanafunzi wao?!
Waulize NIT, UoB wanafunzi wanavyolia kufatilia mikopo yao.
Ishu ya mkopo ni mkataba kati ya mwanafunzi na heslb, chuo kina'play role ya kuziunganisha hizi pande mbili. Inapotokea kuna matatizo kwenye taarifa za mwanafunzi, mwanafunzi mwenyewe anatakiwa awe mtu wa kwanza kufatilia badala ya kuuchia uongozi wa chuo peke yake.
 
Mwenye admission letter iliyotoka kwa 1st year atuonyeshe lini chuo kinafunguliwa.
 
Poleni sana wadogo zangu na kipindi hiki kigumu kwenu katika kufuatilia mustakabali wa elimu yenu ya chuo kikuu.

Ushauri wangu kwenu ni kwamba jitahidini kadri ya uwezo wenu kutafuta elimu bora na sio bora elimu kwani itakua ni msaada mkubwa baada ya wewe kumaliza chuo huku mtaani hata kama utakosa ajira.

Elimu bora hupatikani Katika mazingira mazuri ikiwemo uongozi na walimu lakini haya mawili hayapo Udom licha ya majengo mazuri yenye uhaba wa maji.

Uongozi ni tatizo pale Udom hasa katika college ya COES na NATURAL SCIENCE , mfano kupata hela ya mkopo kutoka bodi kama bum na pesa ya PT ni kama kubahatisha kwa mwanafunzi wa pale. Hadi kufikia sasa kuna kundi kubwa la wanafunzi wa COES na NATURAL SCIENCE ambao hawajapata pesa ya Field na Special faculty na hakuna sababu yoyote ya msingi inayotolewa zaidi ya ukiuliza utatishiwa kufukuzwa chuo tu.

Kifupi Kuna ombwe kubwa sana la uongozi chuoni pale hasa college ya COES na NATURAL SCIENCE kwani wakuu wake wamekua waoga sana na kukosa maamuzi.

Yangu ni hayo tu, usiponielewa hapa nenda mwenyewe ukajionee miaka mitatu au minne utakavyoiona kama muongo mmoja hapo Dodoma.
Kaka angu sijui ni dada, katika maisha hakuna formula Rafik angu, unachokishindwa wewe siyo wote watakishindwa. Kila mtu Ana bahati yake, unavyoidhalau udom Leo, kuna mwingine anaisifu kwamba imemfanya ale matunda mema. Na pia njia uliyoitumia si sahihi kabisa hata kidogo, usilifanye tatizo liliokusumbua wewe kuligeneralise kuwa ni LA wote. Japo sijui nini adhima ya kuandika haya, sijui ni hasira, kutokuelewa au basi tu makusudi,lakini nafikiri kama msomi as you have said, hukupaswa kuliadress hili kwa jinsi hii. You would at least just adress it as one of the challenge so people have to see how to handle while they're in the process, lakini siyo kuwaambia wasiende. Wewe siyo Mungu wa kuwapangia watu maisha yao, mafanikio ya mtu anayeyajua ni Mungu tu. Wewe unaweza kufeli udom Lakin mwingine akatoka vizur Sana na akapata kazi nzur ya maana Sana na hata kuwa raisi wa baadaye. Yote huja kwa mipango ya mwenyezi Mungu na si mwanadam.

Wadogo zangu, mliochaguliwa chuo cha udom na vyuo vingine, niwatie moyo na niwaambie hivi, Nendeni chuoni mkasome,. Msisikilize maneno ya watu wala hakuna haja ya kukata tamaa. Eleweni ya kuwa, siku zote Katika maisha si wote watakutia moyo, kuna wengine watakuvunja moyo ili tu mafanikio yako yasitimie na katika hao shetani naye huingilia ili kubomoa kusudi la Mungu, usiogope ndugu yangu, wewe simama na songa mbele kwa ujasiri huku ukiweka Nia ya kufanikiwa kwa hali yeyote itakayokuwa, hakika utakuwa mshindi na nakuona ukiwa tayari umeyashika mafanikio yako. Elewa pia kuwa watu wanaokuvunja moyo ni kipimo cha ustahimilivu na ujasiri wako katika kutetea ndoto zako, jinsi utakavyopigwa mawe na kusemwa vibaya Lakin bado ukasimama na kwa ujasiri ukasonga mbele ndipo utakavyokuwa thabiti katika kuyafikia mafanikio yako. Mtu asikutishe, weka malengo yako, weka strategies na weka Nia ya kufikia ndoto zako, kamwe usiruhusu mwanadamu akaharibu ndoto zako, ni Mungu pekee ndiyo Ana nafasi hiyo palipo na sababu, yeye mwenyewe atakuepusha.

Mimi mwenyewe ni zao la udom, siongei kusifia chuo changu ila naongea ili kuwasaidien wadogo zangu na kuwapatieni ujasiri maana yapo mengi Sana yatasemwa ambayo yanawezawakatisha tamaa mkajikuta mnapoteza malengo yenu kwa sababu ya Bure. Natambua chuo cha udom kina mapungufu yake kama ambavyo vyuo vingine vinayo pia, kikubwa wadogo zangu ni kuvumilia na kuwa jasir kwa kuweka Nia na malengo yenu mbele. Hakuna sehemu yeyote duniani ambayo haina changamoto, kwenye ndoa, makazini, masomoni, makanisani poote ni changamoto, vivyo hivyo hata Katika vyuo wanavyoviita sijui vikubwa bado nako kuna full of challenges, yaan kwa kiufupi challenges are everywhere to ensure you stand strong and the more challenges you get faced, the more harder stronger you become. Jifunzeni kuzipokea changamoto na kuzifanya kuwa opportunities, kwa mnaonielewa na kufanya, mtafika mbali sana. Weka nia mbele, Kisha songa mbele, with positive attitude, all will be easy.

Uzuri sasa hivi hakuna mtu anaajiliwa eti kwakuwa alisoma chuo fulani. Umahiri wako na uelewa wako wa mambo ndo utakupa chance to compete in market. Haijalishi umesoma ruco, sijui udsm, tumaini, udom, teofilo whatever the college, your compitent and ability of your understanding, hard working and commitment is what matters now in the market. Kwahyo wewe acha wakuseme na wakucheke, usjali wala usipoteze muda, komaaa mdogo wangu, toka na GPA yako Safi isiyo na doa, kuwa competent na jitambue, naamini kuna siku watakupigia saluti!!!!

Namalizia kwa kusema tena mliochaguliwa udom na vyuo vingine, nendeni shule kwa ujasiri. Anayejua maisha yako na mwenye uwezo wa kuyaona mafanikio yako ni Mungu pekee na si mwanadam. Msikate tamaa kuweni jasir mkiweka nia na malengo yenu mbele, huku mkimtanguliza Mungu katika yote, nami nawaombea baraka kwa Mungu, awaguse na kuwapa ufahamu ya kuwa ni yeye tu ndio mpangaji wa maisha yenu na kwahivyo awaongoze vyema mzifikie ndoto zenu ili kesho muwe chachu ya taifa na dunia kwa ujumla. Amina
 
Back
Top Bottom