Upembuzi yakinifu kuhusu utofauti wa kozi za Computer engineering, computer science na Information Technology / Systems kwa kuzingatia mazingira ya TZ

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
copy paste fb ila muhimu

1655227699511.png

Wanafunzi wengi wenye ndoto za kusomea masuala ya Tehama huwa wanahangaika sana linapokuja suala la kufanya maamuzi juu ya kusomea kozi ipi kati ya hizo tatu.... ufuatao ni upembuzi yakinifu wa kuzitofautisha

1๏ธโƒฃ ๐™„๐™‰๐™๐™Š๐™๐™ˆ๐˜ผ๐™๐™„๐™Š๐™‰ ๐™๐™€๐˜พ๐™ƒ๐™‰๐™Š๐™‡๐™Š๐™‚๐™” / ๐™Ž๐™”๐™Ž๐™๐™€๐™ˆ๐™Ž & ๐™„๐˜พ๐™

๐Ÿ”น๐—œ๐—ป๐—ฎ๐—ต๐˜‚๐˜€๐˜‚ ๐—ป๐—ถ๐—ป๐—ถ

kozi hii imejikita zaidi katika kuyajua matumizi ya vitu vilivyomo kwenye computer kwajili ya matumizi rasmi na kuhakiisha vinafanya kazi kama inavyotakiwa.

Utajifunza matumizi ya software muhimu, kurekebisha matatizo yake, ku-configure settings za hardware, kufanya back ups, n.k. Yote hii ni kuhakikisha mifumo ya tehama kwenye shirika inakuwa inafanya kazi muda wote na watumiaji wake nao uwasaidie katika matumizi yake wapatapo shida.

Mambo ya kuijua computer kwa undani, kutengeneza system za computer, n.k huko ni computer science na computer engineering, wewe utajifunza zaidi kutumia vitu ambavyo vimeshatengenezwa kwajili ya matumizi rasmi, kazi yako ni kujua namna ya kuvitumia kwa hali ya juu

๐Ÿ”น๐—จ๐˜„๐—ฒ๐—ฝ๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐—ต๐—ฒ๐˜€๐—ฎ๐—ฏ๐˜‚: chache ๐Ÿ™‚

kozi hizi zina hesabu chache sana, ni zile hesabu za kawaida ambazo hata ukienda kusomea business administration, marketing, law, n. K hazikwepeki. Mnaweza soma somo 1 au labda mawili kati ya masomo zaidi ya 30 mtayosoma chuoni.

๐Ÿ”น๐—ช๐—ฎ๐˜๐˜‚ ๐˜„๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ฒ ๐—ฎ๐—ฑ๐˜ƒ๐—ฎ๐—ป๐˜๐—ฎ๐—ด๐—ฒ ๐—ธ๐˜‚๐—ถ๐˜€๐—ผ๐—บ๐—ฒ๐—ฎ

inakufaa zaidi mtu ambae una experience ya kutumia computer hata katika level walau ya kawaida, ukifika chuoni mambo mengi kwako itakuwa ni muendelezo, hutatumia nguvu nyingi sana kama wale ambao ni wageni kiasi kwaba hata kuwasha pc hawajui.

๐Ÿ”น๐— ๐—ณ๐—ฎ๐—ป๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐˜ƒ๐—ถ๐˜๐˜‚ ๐˜‚๐˜๐—ฎ๐˜ƒ๐˜†๐—ผ๐—ท๐—ถ๐—ณ๐˜‚๐—ป๐˜‡๐—ฎ

utajifunza namna ya kutumia programs muhimu kama microsoft access na mysql kwajili ya database, microsoft word kwajili ya kuandaa nyaraka, photoshop kwajili ya graphics, n.k.

Utajifunza kupiga window kwajili ya kuingiza operating system kwenye computer.

Utajifunza ku install programs na kuzi update.

Kwenye networking utajikita zaidi kujua namna ya ku install network, kuconfigugure na kuhakikisha zinafanya kazi kwa kutumia manuals na software ambazo zipo tayari.

Kwenye kutengeneza software utajikita zaidi kutumia software za compiler ili kutengeneza program / app, mambo ya kujua code hutahangaika nayo sana.

Kwenye kutengeneza website nako utatumia compilers kama dream weaver, mambo ya kuchapa code kama html, css, javascript, n.k utajifunza vile vitu basic ili uweze kutumia compiler.

Kwenye ulinzi utajikita zaidi kujua ku install na ku update anti virus.

Kwenye programming hutaingia ndani sana ila utajifunza lugha muhimu na nyepesi kama python ili ujue kutengeneza scripts.

Kwenye kurekebisha matatizo ya pc nako utajifunza zaidi kuyarekebisha kwa kutumia software ama ku trouble shoot kwa window, bila kusahau kutwanga window kwenye pc sugu.

๐Ÿ”น๐— ๐—ฎ๐˜‡๐—ถ๐—ป๐—ด๐—ถ๐—ฟ๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐˜‚๐—ณ๐˜‚๐—ป๐—ฑ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—ง๐—ญ

ni kozi ambayo hata kwa vyuo vya bongo inafundishika vizuri tu, masomo huwa ni machache nah ii itakupa muda mwingi wa kupumzika unaoweza kuutumia kujiendeleza na hobby za computer kama programming, website designing, kutengeneza apps, n. K. Hivi ni vitu ambavyo hata mwanasheria, muhasibu, doctor, n. K akivifanya kuwa hobby anakuwa deep kuzidi mtu anaesomea computer science au computer engineering ambae ni mgeni wa programming na ratiba imembana sana hata kujifunza kwa undani haya mambo.

๐Ÿ”น๐—”๐—ท๐—ถ๐—ฟ๐—ฎ:
ict support technician, help desk officer, pc support, technical support, chief information officer, database administrator, project manager system administrator, n.k

2๏ธโƒฃ ๐‚๐Ž๐Œ๐๐”๐“๐„๐‘ ๐’๐‚๐ˆ๐„๐๐‚๐„

๐Ÿ”น๐—œ๐—ป๐—ฎ๐—ต๐˜‚๐˜€๐˜‚ ๐—ป๐—ถ๐—ป๐—ถ

computer science imejikita zaidi kujua computation zaidi kuliko kuijua computer, computation itajikita zaidi kwenye upande wa kuijua mifumo ya system za software kwa undani zaidi na upana. Utajifunza comncepts za computer systems na jinsi zinavyotengenezwa na kufanya kazi. Mtafukua sana mambo ya programming, data structures, algorithm design. Software development.

๐Ÿ”น๐—จ๐˜„๐—ฒ๐—ฝ๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐—ต๐—ฒ๐˜€๐—ฎ๐—ฏ๐˜‚: Nyingi ๐Ÿฅธ

kwenye hii kozi kuna hesabu za kutosha tu, hivyo kama unazipenda hesabu na mambo ya programming, hapa patakufaa.

๐Ÿ”น๐—ช๐—ฎ๐˜๐˜‚ ๐˜„๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ฒ ๐—ฎ๐—ฑ๐˜ƒ๐—ฎ๐—ป๐˜๐—ฎ๐—ด๐—ฒ ๐—ธ๐˜‚๐—ถ๐˜€๐—ผ๐—บ๐—ฒ๐—ฎ

inakufaa zaidi mtu ambae una back ground ya coding, programming, n.k... Uwe angalau unazijua japo kwa mbali languages kama c++, java, python, pascal, css, javascript, n.k. Kiufupi usiwe mgeni sana lasivyo utatumia nguvu nyingi sana kujifunza mambo mapya. pia hakikish hesabu upo good.

๐Ÿ”น๐— ๐—ณ๐—ฎ๐—ป๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐˜ƒ๐—ถ๐˜๐˜‚ ๐˜‚๐˜๐—ฎ๐˜ƒ๐˜†๐—ผ๐—ท๐—ถ๐—ณ๐˜‚๐—ป๐˜‡๐—ฎ

web development, hapa mtajifunza lugha nyingi za kutengenezea websites kwa undani kama html, css, javascript, php, n.k.

Utajifunza vitu kama binary ambazo ni namba 1 na 0 zinavyotumika kufanya maamuzi, utajifunza logic gates zinazochukua hizo 1 na 0 ili kumpa mtumiaji matokeo kulingana na input.

programming, hapa mtajifunza lugha za programming kama java, c++, n.k ili kutengeneza system zainazofanya kazi

artificial intellingence

database mtaingia ndani zaidi kufukua database systems

networking mtachimba zaidi mambo ya ports, scanning, vulnerabilities, security, n. K.

Pia mtajifunza mambo ya ethical hacking, penetration testin, n.k. lengo likiwa kuzilinda systems.

๐Ÿ”น๐— ๐—ฎ๐˜‡๐—ถ๐—ป๐—ด๐—ถ๐—ฟ๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐˜‚๐—ณ๐˜‚๐—ป๐—ฑ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—ง๐—ญ

theory nyingi sana ndio tatizo hapa, walimu wengi nao wamefaulu vizuri kwenye vyeti vyao vilivyowapa ajira kwa kujbu mitihani vizuri kulingana na notes... Ratiba zilizobana ndani na nje ya darasa ili kuendana na shule ya haya mambo inafanya wengi wakose mda wa kujiendeleza kivyao kufanya projects au kujiendeleza na hobby zao kama programming.

๐Ÿ”น๐—”๐—ท๐—ถ๐—ฟ๐—ฎ:

Ajira karibia zote za waliosomea it/ is/ ict una sifa ya kuzifanya.

ajira za ziada ni kama Web developer, webmaster, app developer, programmer, software engineer, artificial intelligence engineer, n.k.

Kama unavyoziona hizo kazi za ziada kibongo bongo bado ni nadra sana, mwisho wa siku aliesomea hii fani ata apply kazi za it/is/ict. kwa target ya soko la ajira ni heri tu uchague kusomea it au computer engineering, hii kozi ya computer science kupata ajira zake pekee kwa hapa bongo ni ngumu.

๐Ÿ”น๐Ÿ”น๐—จ๐˜๐—ผ๐—ณ๐—ฎ๐˜‚๐˜๐—ถ ๐˜„๐—ฎ ๐—–๐—ผ๐—บ๐—ฝ๐˜‚๐˜๐—ฒ๐—ฟ ๐˜€๐—ฐ๐—ถ๐—ฒ๐—ป๐—ฐ๐—ฒ ๐—ป๐—ฎ ๐˜€๐—ผ๐—ณ๐˜๐˜„๐—ฎ๐—ฟ๐—ฒ ๐—˜๐—ป๐—ด๐—ถ๐—ป๐—ฒ๐—ฒ๐—ฟ๐—ถ๐—ป๐—ด

Software engineering ni tawi la computer science, imejikita zaidi na vipengere vya computer science vinavyohusu kudevelop software, umakini wote ni kuujua uwanja wa kutengeneza software, ku test software, ku deploy software, n.k. kitu ambacho kitaelekezwa kwenye computer science kama topic basi kinaweza kuwa ni somo kabisa linalojitegemea kwenye software engineering.

mwisho wa siku mtu aliesomea computer science ana uwanja mpana, anaweza kuwa software engineer au vitu vingine vya ziada alivyosomea tofauti na software engineer ambae kaweka focus kwenye kipengere kimoja cha computer science kinachohusu software. ila niweke mambo clear kwamba aliesomea software engineering ataweza kuumudu uwanja wake zaidi kuliko aliesomea comuter engineering, hii ni kwasababu ya advantage ya kuwekea umakini kitu kimoja.

Kibongo bongo wengi wanasoma ili kuja kuajiriwa, hivyo wanaangaliaga kozi yenye ajira nyingi, hii inapelekea kuwa nadra kukuta mtu kamua kusomea software engineering endapo anajua uhalisia utakuwaje baada ya kumaliza chuo kwenye soko la ajira.

3๏ธโƒฃ ๐‚๐Ž๐Œ๐๐”๐“๐„๐‘ ๐„๐๐†๐ˆ๐๐„๐„๐‘๐ˆ๐๐†

๐Ÿ”น๐—œ๐—ป๐—ฎ๐—ต๐˜‚๐˜€๐˜‚ ๐—ป๐—ถ๐—ป๐—ถ

computer engineering ni ndoa kati nusu ya computer science na nusu ya electronics engineering, inajumuisha 50% ya computer science kwenye mambo ya software na 50% ya electonics engineeing (uhandisi wa umeme) kwenye kujua umeme wa vifaa. Ni nusu software na nusu hardware

๐Ÿ”น๐—จ๐˜„๐—ฒ๐—ฝ๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐—ต๐—ฒ๐˜€๐—ฎ๐—ฏ๐˜‚: nyingi zaidi ๐Ÿ”ฅ

hesabu ni nyngi zaidi ya computer science maana humu kuna pande la electronics engineering

๐Ÿ”น๐—ช๐—ฎ๐˜๐˜‚ ๐˜„๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ฒ ๐—ฎ๐—ฑ๐˜ƒ๐—ฎ๐—ป๐˜๐—ฎ๐—ด๐—ฒ ๐—ธ๐˜‚๐—ถ๐˜€๐—ผ๐—บ๐—ฒ๐—ฎ

ni nzuri kama una background ya electronics, hasa ukiwa umesomea technic schools o-level na unaenda kusomea diploma ya haya mambo au uwe na diploma ya electronics na unaenda kusomea degree ya computer engineering..... coding nazo ukizijua kwa mbali si haba, Pia bila kusahau hakikisha hesabu kwako ni kama kucheza game.

๐Ÿ”น๐— ๐—ณ๐—ฎ๐—ป๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐˜ƒ๐—ถ๐˜๐˜‚ ๐˜‚๐˜๐—ฎ๐˜ƒ๐˜†๐—ผ๐—ท๐—ถ๐—ณ๐˜‚๐—ป๐˜‡๐—ฎ

Umeme - computer ni chombo kinachotumia umeme kwa hio lazima ujifunze vifaa vyake na mifumo yake ya umeme, utajifunza nje ndani vitu vya kwenye circuit kama capacitator, resistors na inductors. utajifunza volts, ohms, na mambo mengi zaidi ya umeme, hapa hata ukimaliza chuo unaweza kuwa fundi umeme.

-upande wa software utajifunza vitu takribani 50% vya computer science kwenye nyanja za software. Utajifunza vitu kama operating systems zinazounganisha hardware na software, hardware programming, robotics, automation, n.k.

-utajifunza kufungua na kuvirudishia vifaa vya computer, kuunda mother board na kupachika vifaa vyake, soldering, n.k.

๐Ÿ”น๐— ๐—ฎ๐˜‡๐—ถ๐—ป๐—ด๐—ถ๐—ฟ๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐˜‚๐—ณ๐˜‚๐—ป๐—ฑ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—ง๐—ญ

Again! Vyuo vingi tz hufundiha kwa theory wakati hii ni kozi ambayo inahitaji practicles nyingi sana, inafaa chuo kiwe na boards na components zake za kutosha ili mwanafunzi aweze kuunda na kutengeneza motherboards kwa sequence inayofata logic, theory pekee za darasani ni ngumu sana kupata elimu sahihi ya computer engineering. Kama una hela zako jipange ununue vifaa vya practices.

๐Ÿ”น๐—”๐—ฑ๐—ฑ๐—ฒ๐—ฑ ๐—”๐—ฑ๐˜ƒ๐—ฎ๐—ป๐˜๐—ฎ๐—ด๐—ฒ

ni taaluma ambayo inakuruhusu kusajiliwa na kutambulika kama engineer / muhandisi.. utawekewa salutation ya Eng (engineer) badala ya mr / mrs.

๐Ÿ”น๐—”๐—ท๐—ถ๐—ฟ๐—ฎ:

ajira nyingi za wenye it/is/ict + wenye computer science

ajira za ziada ni kama kuwa fundi wa minara, hardware engineer, electronics engineer, n.k.

Pia ni elimu nzuri sana kukuandaa kuwa fundi wa simu / laptops endapo umepata practicles za kutosha chuoni.

๐Ÿ”˜ ๐˜๐˜‚๐˜„๐—ฒ๐—ธ๐—ฒ ๐—บ๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ผ ๐˜€๐—ฎ๐˜„๐—ฎ,

kama umedhamiria kuwa programmer somea computer science ila hakikisha uwe na ka background kidogo kwenye programming.

๐Ÿ”น๐—ž๐˜‚๐˜€๐—ผ๐—บ๐—ฒ๐—ฎ ๐—ธ๐—ผ๐˜‡๐—ถ ๐˜€๐—ฝ๐—ฒ๐—ฐ๐—ถ๐—ฎ๐—น๐—ถ๐˜€๐—ฒ๐—ฑ ๐—ธ๐—ฎ๐—บ๐—ฎ ๐—ฐ๐˜†๐—ฏ๐—ฒ๐—ฟ ๐˜€๐—ฒ๐—ฐ๐˜‚๐—ฟ๐—ถ๐˜๐˜†, ๐˜€๐—ผ๐—ณ๐˜๐˜„๐—ฎ๐—ฟ๐—ฒ ๐—ฑ๐—ฒ๐˜ƒ๐—ฒ๐—น๐—ผ๐—ฝ๐—บ๐—ฒ๐—ป๐˜, ๐—ป.๐—ธ

Kwa ushauri wangu huku level za diploma na degree somea kozi pana kama I.t/is/ict, c.s, c.e, halafu kwenye masters ndio uka specialize (kubobea) kwenye Software development, Cyber security, n.k

๐Ÿ”˜๐˜พ๐™Š๐™‰๐˜พ๐™‡๐™๐™Ž๐™„๐™Š๐™‰

vyuo vyetu vya huku bongo vina lack sana kwenye practical, nguvu zote za ufundishaji karibia 98% ni theory ya kwenye notes na vitini na utapimwa uwezo wako kwa kujibu kitu kinachoendana na notes, uwanja wa mwanafunzi kuandaliwa practically ni mdogo mno, ndio maana si ajabu kumkuta mtu kamaliza degree electronics engineering lakini kaachwa mbali sana na fundi umeme au fundi radio wa mtaani.

Silaha kubwa ni kuhakikisha wewe kama wewe unaweza kujiendeleza na projects zako ama kujijengea uzoefu katika hobby flani ya kitu unachosomea, muda wa mwanafunzi kuwa huru ni muhimu sana ili apate muda wa kusakafia alichojifunza.

Katika soko la kazi nako sana sana ni kazi za IT / IS / ICT na computer engineering... ukisomea computer science ni ngumu sana kuwa na career specialised kwajili ya computer science, hivyo ni bora uchague usomee IT au Computer engineering hasa ukizingatia vyuo vyetu teory ni nyingi uisomea hio computer science.

unaweza kushare unacho kijua cha ziada, sio mbaya tukajifunza
 
copy paste fb ila muhimu

View attachment 2260898

Wanafunzi wengi wenye ndoto za kusomea masuala ya Tehama huwa wanahangaika sana linapokuja suala la kufanya maamuzi juu ya kusomea kozi ipi kati ya hizo tatu.... ufuatao ni upembuzi yakinifu wa kuzitofautisha

๐™„๐™‰๐™๐™Š๐™๐™ˆ๐˜ผ๐™๐™„๐™Š๐™‰ ๐™๐™€๐˜พ๐™ƒ๐™‰๐™Š๐™‡๐™Š๐™‚๐™” / ๐™Ž๐™”๐™Ž๐™๐™€๐™ˆ๐™Ž & ๐™„๐˜พ๐™

๐—œ๐—ป๐—ฎ๐—ต๐˜‚๐˜€๐˜‚ ๐—ป๐—ถ๐—ป๐—ถ
kozi hii imejikita zaidi katika kuyajua matumizi ya vitu vilivyomo kwenye computer kwajili ya matumizi rasmi na kuhakiisha vinafanya kazi kama inavyotakiwa.

Utajifunza matumizi ya software muhimu, kurekebisha matatizo yake, ku-configure settings za hardware, kufanya back ups, n.k. Yote hii ni kuhakikisha mifumo ya tehama kwenye shirika inakuwa inafanya kazi muda wote na watumiaji wake nao uwasaidie katika matumizi yake wapatapo shida.

Mambo ya kuijua computer kwa undani, kutengeneza system za computer, n.k huko ni computer science na computer engineering, wewe utajifunza zaidi kutumia vitu ambavyo vimeshatengenezwa kwajili ya matumizi rasmi, kazi yako ni kujua namna ya kuvitumia kwa hali ya juu

๐—จ๐˜„๐—ฒ๐—ฝ๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐—ต๐—ฒ๐˜€๐—ฎ๐—ฏ๐˜‚: chache

kozi hizi zina hesabu chache sana, ni zile hesabu za kawaida ambazo hata ukienda kusomea business administration, marketing, law, n. K hazikwepeki. Mnaweza soma somo 1 au labda mawili kati ya masomo zaidi ya 30 mtayosoma chuoni.

๐—ช๐—ฎ๐˜๐˜‚ ๐˜„๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ฒ ๐—ฎ๐—ฑ๐˜ƒ๐—ฎ๐—ป๐˜๐—ฎ๐—ด๐—ฒ ๐—ธ๐˜‚๐—ถ๐˜€๐—ผ๐—บ๐—ฒ๐—ฎ
inakufaa zaidi mtu ambae una experience ya kutumia computer hata katika level walau ya kawaida, ukifika chuoni mambo mengi kwako itakuwa ni muendelezo, hutatumia nguvu nyingi sana kama wale ambao ni wageni kiasi kwaba hata kuwasha pc hawajui.

๐— ๐—ณ๐—ฎ๐—ป๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐˜ƒ๐—ถ๐˜๐˜‚ ๐˜‚๐˜๐—ฎ๐˜ƒ๐˜†๐—ผ๐—ท๐—ถ๐—ณ๐˜‚๐—ป๐˜‡๐—ฎ
utajifunza namna ya kutumia programs muhimu kama microsoft access na mysql kwajili ya database, microsoft word kwajili ya kuandaa nyaraka, photoshop kwajili ya graphics, n.k.

Utajifunza kupiga window kwajili ya kuingiza operating system kwenye computer.

Utajifunza ku install programs na kuzi update.

Kwenye networking utajikita zaidi kujua namna ya ku install network, kuconfigugure na kuhakikisha zinafanya kazi kwa kutumia manuals na software ambazo zipo tayari.

Kwenye kutengeneza software utajikita zaidi kutumia software za compiler ili kutengeneza program / app, mambo ya kujua code hutahangaika nayo sana.

Kwenye kutengeneza website nako utatumia compilers kama dream weaver, mambo ya kuchapa code kama html, css, javascript, n.k utajifunza vile vitu basic ili uweze kutumia compiler.

Kwenye ulinzi utajikita zaidi kujua ku install na ku update anti virus.

Kwenye programming hutaingia ndani sana ila utajifunza lugha muhimu na nyepesi kama python ili ujue kutengeneza scripts.

Kwenye kurekebisha matatizo ya pc nako utajifunza zaidi kuyarekebisha kwa kutumia software ama ku trouble shoot kwa window, bila kusahau kutwanga window kwenye pc sugu.

๐— ๐—ฎ๐˜‡๐—ถ๐—ป๐—ด๐—ถ๐—ฟ๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐˜‚๐—ณ๐˜‚๐—ป๐—ฑ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—ง๐—ญ

ni kozi ambayo hata kwa vyuo vya bongo inafundishika vizuri tu, masomo huwa ni machache nah ii itakupa muda mwingi wa kupumzika unaoweza kuutumia kujiendeleza na hobby za computer kama programming, website designing, kutengeneza apps, n. K. Hivi ni vitu ambavyo hata mwanasheria, muhasibu, doctor, n. K akivifanya kuwa hobby anakuwa deep kuzidi mtu anaesomea computer science au computer engineering ambae ni mgeni wa programming na ratiba imembana sana hata kujifunza kwa undani haya mambo.

๐—”๐—ท๐—ถ๐—ฟ๐—ฎ:
ict support technician, help desk officer, pc support, technical support, chief information officer, database administrator, project manager system administrator, n.k

๐‚๐Ž๐Œ๐๐”๐“๐„๐‘ ๐’๐‚๐ˆ๐„๐๐‚๐„

๐—œ๐—ป๐—ฎ๐—ต๐˜‚๐˜€๐˜‚ ๐—ป๐—ถ๐—ป๐—ถ
computer science imejikita zaidi kwenye upande wa kuijua mifumo ya system za software kwa undani zaidi. Utajifunza comncepts za computer systems na jinsi zinavyotengenezwa na kufanya kazi. Mtafukua sana mambo ya programming, data structures, algorithm design. Software development.

๐—จ๐˜„๐—ฒ๐—ฝ๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐—ต๐—ฒ๐˜€๐—ฎ๐—ฏ๐˜‚: Nyingi
kwenye hii kozi kuna hesabu za kutosha tu, hivyo kama unazipenda hesabu na mambo ya programming, hapa patakufaa.

๐—ช๐—ฎ๐˜๐˜‚ ๐˜„๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ฒ ๐—ฎ๐—ฑ๐˜ƒ๐—ฎ๐—ป๐˜๐—ฎ๐—ด๐—ฒ ๐—ธ๐˜‚๐—ถ๐˜€๐—ผ๐—บ๐—ฒ๐—ฎ
inakufaa zaidi mtu ambae una back ground ya coding, programming, n.k... Uwe angalau unazijua japo kwa mbali languages kama c++, java, python, pascal, css, javascript, n.k. Kiufupi usiwe mgeni sana lasivyo utatumia nguvu nyingi sana kujifunza mambo mapya. pia hakikish hesabu upo good.

๐— ๐—ณ๐—ฎ๐—ป๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐˜ƒ๐—ถ๐˜๐˜‚ ๐˜‚๐˜๐—ฎ๐˜ƒ๐˜†๐—ผ๐—ท๐—ถ๐—ณ๐˜‚๐—ป๐˜‡๐—ฎ
web development, hapa mtajifunza lugha nyingi za kutengenezea websites kwa undani kama html, css, javascript, php, n.k.

Utajifunza vitu kama binary ambazo ni namba 1 na 0 zinavyotumika kufanya maamuzi, utajifunza logic gates zinazochukua hizo 1 na 0 ili kumpa mtumiaji matokeo kulingana na input.

programming, hapa mtajifunza lugha za programming kama java, c++, n.k ili kutengeneza system zainazofanya kazi

artificial intellingence

database mtaingia ndani zaidi kufukua database systems

networking mtachimba zaidi mambo ya ports, scanning, vulnerabilities, security, n. K.

Pia mtajifunza mambo ya ethical hacking, penetration testin, n.k. lengo likiwa kuzilinda systems.

๐— ๐—ฎ๐˜‡๐—ถ๐—ป๐—ด๐—ถ๐—ฟ๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐˜‚๐—ณ๐˜‚๐—ป๐—ฑ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—ง๐—ญ

theory nyingi sana ndio tatizo hapa, walimu wengi nao wamefaulu vizuri kwenye vyeti vyao vilivyowapa ajira kwa kujbu mitihani vizuri kulingana na notes... Ratiba zilizobana ndani na nje ya darasa ili kuendana na shule ya haya mambo inafanya wengi wakose mda wa kujiendeleza kivyao kufanya projects au kujiendeleza na hobby zao kama programming.

๐—”๐—ท๐—ถ๐—ฟ๐—ฎ:

Ajira karibia zote za waliosomea it/ is/ ict una sifa ya kuzifanya.

ajira za ziada ni kama Web developer, webmaster, app developer, programmer, software engineer, artificial intelligence engineer, n.k.

Kama unavyoziona hizo kazi za ziada kibongo bongo bado ni nadra sana, mwisho wa siku aliesomea hii fani ata apply kazi za it/is/ict. kwa target ya soko la ajira ni heri tu uchague kusomea it au computer engineering, hii kozi ya computer science kupata ajira zake pekee kwa hapa bongo ni ngumu.

๐‚๐Ž๐Œ๐๐”๐“๐„๐‘ ๐„๐๐†๐ˆ๐๐„๐„๐‘๐ˆ๐๐†

๐—œ๐—ป๐—ฎ๐—ต๐˜‚๐˜€๐˜‚ ๐—ป๐—ถ๐—ป๐—ถ
computer engineering ni ndoa kati nusu ya computer science na nusu ya electronics engineering, inajumuisha 50% ya computer science kwenye mambo ya software na 50% ya electonics engineeing (uhandisi wa umeme) kwenye kujua umeme wa vifaa. Ni nusu software na nusu hardware

๐—จ๐˜„๐—ฒ๐—ฝ๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐—ต๐—ฒ๐˜€๐—ฎ๐—ฏ๐˜‚: utitiri

hesabu ni nyngi zaidi ya computer science maana humu kuna pande la electronics engineering

๐—ช๐—ฎ๐˜๐˜‚ ๐˜„๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ฒ ๐—ฎ๐—ฑ๐˜ƒ๐—ฎ๐—ป๐˜๐—ฎ๐—ด๐—ฒ ๐—ธ๐˜‚๐—ถ๐˜€๐—ผ๐—บ๐—ฒ๐—ฎ
ni nzuri kama una background ya electronics, hasa ukiwa umesomea technic schools o-level na unaenda kusomea diploma ya haya mambo au uwe na diploma ya electronics na unaenda kusomea degree ya computer engineering..... coding nazo ukizijua kwa mbali si haba, Pia bila kusahau hakikisha hesabu kwako ni kama kucheza game.

๐— ๐—ณ๐—ฎ๐—ป๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐˜ƒ๐—ถ๐˜๐˜‚ ๐˜‚๐˜๐—ฎ๐˜ƒ๐˜†๐—ผ๐—ท๐—ถ๐—ณ๐˜‚๐—ป๐˜‡๐—ฎ

Umeme - computer ni chombo kinachotumia umeme kwa hio lazima ujifunze vifaa vyake na mifumo yake ya umeme, utajifunza nje ndani vitu vya kwenye circuit kama capacitator, resistors na inductors. utajifunza volts, ohms, na mambo mengi zaidi ya umeme, hapa hata ukimaliza chuo unaweza kuwa fundi umeme.

-upande wa software utajifunza vitu takribani 50% vya computer science kwenye nyanja za software. Utajifunza vitu kama operating systems zinazounganisha hardware na software.

-utajifunza kufungua na kuvirudishia vifaa vya computer, kuunda mother board na kupachika vifaa vyake, soldering, n.k.

๐— ๐—ฎ๐˜‡๐—ถ๐—ป๐—ด๐—ถ๐—ฟ๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐˜‚๐—ณ๐˜‚๐—ป๐—ฑ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—ง๐—ญ
Again! Vyuo vingi tz hufundiha kwa theory wakati hii ni kozi ambayo inahitaji practicles nyingi sana, inafaa chuo kiwe na boards na components zake za kutosha ili mwanafunzi aweze kuunda na kutengeneza motherboards kwa sequence inayofata logic, theory pekee za darasani ni ngumu sana kupata elimu sahihi ya computer engineering. Kama una hela zako jipange ununue vifaa vya practices.

๐—”๐—ฑ๐—ฑ๐—ฒ๐—ฑ ๐—”๐—ฑ๐˜ƒ๐—ฎ๐—ป๐˜๐—ฎ๐—ด๐—ฒ
ni taaluma ambayo inakuruhusu kusajiliwa na kutambulika kama engineer / muhandisi.. utawekewa salutation ya Eng (engineer) badala ya mr / mrs.

๐—”๐—ท๐—ถ๐—ฟ๐—ฎ:

ajira nyingi za wenye it/is/ict + wenye computer science

ajira za ziada ni kama kuwa fundi wa minara, hardware engineer, electronics engineer, n.k.

Pia ni elimu nzuri sana kukuandaa kuwa fundi wa simu / laptops endapo umepata practicles za kutosha chuoni.

๐˜๐˜‚๐˜„๐—ฒ๐—ธ๐—ฒ ๐—บ๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ผ ๐˜€๐—ฎ๐˜„๐—ฎ,
kama umedhamiria kuwa programmer somea computer science ila hakikisha uwe na ka background kidogo kwenye programming.

๐˜พ๐™Š๐™‰๐˜พ๐™‡๐™๐™Ž๐™„๐™Š๐™‰

vyuo vyetu vya huku bongo vina lack sana kwenye practical, nguvu zote za ufundishaji karibia 98% ni theory ya kwenye notes na vitini na utapimwa uwezo wako kwa kujibu kitu kinachoendana na notes, uwanja wa mwanafunzi kuandaliwa practically ni mdogo mno, ndio maana si ajabu kumkuta mtu kamaliza degree electronics engineering lakini kaachwa mbali sana na fundi umeme au fundi radio wa mtaani.

Silaha kubwa ni kuhakikisha wewe kama wewe unaweza kujiendeleza na projects zako ama kujijengea uzoefu katika hobby flani ya kitu unachosomea, muda wa mwanafunzi kuwa huru ni muhimu sana ili apate muda wa kusakafia alichojifunza.

Katika soko la kazi nako sana sana ni kazi za IT / IS / ICT na computer engineering... ukisomea computer science ni ngumu sana kuwa na career specialised kwajili ya computer science, hivyo ni bora uchague usomee IT au Computer engineering hasa ukizingatia vyuo vyetu teory ni nyingi uisomea hio computer science.
Ukiacha hzi kozi tatu ulizozizungumzia siku hizi vyuo vingi vinaibuka tu na kozi za ICT/Computer zenye majina ya ajabu ajabu kwa lengo tu la kuwa-confuse watu wadhani kuwa ni kitu kipya sana kumbe hamna lolote jipya tofauti na hzi kozi tatu. Nadhani bado hakujawa na standardized ICT/Computer course name ambazo zinatambulika rasmi sana kama ilivyo kwenye nyanja nyingine za taaluma.
 
Hii tabia ipo hasa udsm pale.... Degree ya computer engineering wao wameiita computer engineering and information technology

Diploma ya IT wanaiita computing and information technology

Pia computer science mbili pale udsm, kuna ambayo ni sahihi na inafahamika vyuo kibao duniani inaitwa Bachelor of science "in" computer science lakini wao wana ya ziada wanaiita bachelor of science "with" computer science, ni mambo ya ajabu tu.
 
Mwenye kufahamu bei ya hivi vitabu hapa Bongo jamani! Nimeanza kitambo kijisomesha mtandaoni nikaona Bora nitafute vitabu kabisa.
 
Attachments

  • 41VSIpPMJQS._AC_SY350_.jpg
    41VSIpPMJQS._AC_SY350_.jpg
    13.7 KB · Views: 73
  • 417bo-mCoBL._AC_SY350_.jpg
    417bo-mCoBL._AC_SY350_.jpg
    13.4 KB · Views: 62
  • 41X2i47NXUL._AC_SY780_.jpg
    41X2i47NXUL._AC_SY780_.jpg
    15 KB · Views: 76
Umeeleza vyema, lakini ninataka niweke sawa kwenye mambo machache.

Tukianza na hesabu kuwa chache upande wa IT labda inategemea na aina ya chuo na Mtaala wao.

Maana kwa uzoefu wangu kutoka certificate, diploma hadi degree na bahati nzuri nilisoma IT pekee nilikutana na mahesabu ya kutosha tena kwa bahati nzuri tulikuwa na wanafunzi wa CS kwa pamoja tulisoma na utofauti ulikuwa kwenye masomo machache sana ila katika hesabu tulikwenda sambamba na sio hesabu tu.

Pia hata kwa masomo ya programming isipokuwa java tu wadau wa CS walisoma advanced huku sisi tukibaki kupata elimu ya java ya kawaida huku tukifidia somo lililohusu IT. Hii ilikuwa kwa Degree. Huenda labda ni kutokana na asili ya chuo ni cha ufundi na mitaala yake imeelemea upande wa Engineering.

Kielelezo cha masomo ya IT

Kielelezo cha masomo ya CS

Nakumbuka hata nikiwa Diploma nilifanikiwa kupitia kwenye msitu wa hesabu. Hapa nakumbuka nilifundishwa na Mhadhiri ambaye pia alikuwa Mhadhiri katika programu ya ualimu wa hesabu katika level ya degree(BEDMATH)

Kwa upande wa certificate pekee nadhani hesabu ndio zilikuwa rahisi labda ni kutokana ni level ya chini kidogo. Nadhani hapa kozi zote haziwachoshi wanafunzi kwa mahesabu mazito.

Hivyo nadhani kusomea kitu fulani katika chuo fulani labda inategemea asili/misingi/utamaduni/nyenzo za chuo husika ndizo zinazoamua Mtaala/Mitaala ya Vyuo iweje. Mfano katika chuo nilichosoma kimekuwa na sifa zote za kufundishwa hesabu zilizotukuka.

Kwa ambaye anakwenda kusoma kwenye vyuo vya Engineering usitegemee kukuta mahesabu ambayo sio rahisi hata kama unasomea Kiswahili (*ni utani)
 
Kwa kuongezea, na kwa lugha rahisi,
1. information technology ni kada inayohusu usimamiaji na uendeshaji wa mifumo ya tehama kwa ujumla .

2. computer science ni kada inayohusu zaidi mifumo ya computer inavyofanya kazi, hapa ndio maana lazima ucheze na binary kidogo kuzidi ..I.T

3. na computer engineering....hii inahusu sana, designing, maintanance, repairing and making mifumo ya software na hardware...katika kada ya tehama
 
Msaada wadau, Kwa DSM, Je kuna chuo chochote wanachofundisha IT/computer science kwa level ya bachelor degree evening program? if yes please naomba unitajie
 
Back
Top Bottom