Unazuia sherehe za Uhuru, unaadhimisha birthday ya CCM

Mshana jr mtendee haki mtoa mada, usiendelee kumjaza ujinga. Ninafahamu wewe una uelewa zaidi kuhusu tofauti ya sherehe za vyama na serikali.

Waziri Mkuu alipoenda Arusha kwenye sherehe ya kusimikwa Askofu Mkuu KKKT Frederick Shoo unadhani kanisa la KKKT lilimlipia pesa za mafuta ya magari na walinzi wake?

Nimekuambia nenda shule ukajifunze civics!
Chama ni muhimu kuliko Taif?
 
Hili suala wachieni viongozi wa UKAWA walifuatie na walizungumzie, wao wanamadaraka ya kufuatia kila jambo ili kuhakikisha mali ya umma untumika ipasavyo. Sana sana sasa hivi tuna tumia enegy nyingi tu ya kutoa maini na matusi wakati wakina LOWASA wamekaa kimyaa
Mkuu tanzania ni yetu sote na husitegemee kiongozi fulani aje aanzishe vita ya ukombozi wako pekee yake unaaza wewe
 
hivi katika viongozi wakuu wa ccm magufuli yupo, je ana mamlaka gani ndani ya ccm , je ana uwezo wa kuzuia maamuzi yoyote ya CHAMA..?

MSIKURUPUKE TU KULAUMU
 
Mmawia trust me yule kwangu ni maji mafupi
Teeeeeeeeh teeeeeeeeh teeeeeeeeeh, wenyewe wana muamini na unakumbuka kabla ya uchaguzi alipo rudi toka india kwenye matibabu akakuta hali ya hewa kisiasa jimboni kwake inamwendea vibaya akawatishia wapiga kura wake,eti sasa nitafanya maamuzi magumu!!!!!!!!!
 
Kurusha Birthday ya ccm Live Azam Tv siyo gali lakini kuonyesha Bunge lenye maslai mapana na nchi tena kwenye chombo chenyekutumia kodi za haohao wananchi ni gali sana
Mkuu hiyo ndiyo serikali yetu sikivu inayo wajali wananchi wake
 
Ni zao kweli kabisa, lakini hizo hela pesa siwangenunulia maskini na wahitaji chakula.
Mkuu huoni sasa huko ni kumpangia mtu matumizi ya pesa zake. Vipi kwa upande wako unasherekeaga idd el fitr au xmass au pasaka? Kama ndio kwanini hiyo pesa ya kusherekea hizo sikukuu zako usisaidie maskini?
 
Wanabodi
Salaam;

Serikali ya awamu ya 5 inajinasibu kubana matumizi na kufuta baadhi ya sherehe za kitaifa kwa lengo hilo la kuzuia matumizi yasiyo ya lazima.

Kichekesho kimeonekana leo baada ya serikali nzima kuhamia singinda kwenye sherehe za birthday ya ccm ya kutimiza miaka 39.

Huko nyuma tulishuhudia sherehe za uhuru zikipigwa kumbo,sherehe za wabunge zikapigwa ban,baadae tbc nayo ikapigwa ban kwa lengo hilo hilo la kubana matumizi. Cha kushangaza Rais na serikali nzima walikuwa kwenye birthday hiyo ya ccm kwa ajili ya kutoa hotuba za mipasho!!

Kweli hii nchi ngumu sana aisee!
Tujitahidi kuwa na uelewa mpana wa kutofautisha sherehe za chama na zile za serikali.
 
You mean unasema kuwa chadema, ACT, Nccr, Tadea, Chaumma wakitaka kufanya sherehe zao magufuli aingilie??

Sherehe za CCM sio za kitaifa, sherehe ya uhuru ni ya kitaifa

sherehe ya ccm ni ya kichama, ya uhuru ni ya serikali
Acha upuuzi wako raisi alienda kama nani he alitumia kodi ya CHAMA au serikali na he alitumia msafara au alipanda gari LA CHAMA ukipata majibu utakuwa umeacha upuuzi
acha upuuzi
 
You mean unasema kuwa chadema, ACT, Nccr, Tadea, Chaumma wakitaka kufanya sherehe zao magufuli aingilie??

Sherehe za CCM sio za kitaifa, sherehe ya uhuru ni ya kitaifa

sherehe ya ccm ni ya kichama, ya uhuru ni ya serikali

acha upuuzi
Wew nd mpuuzi unataka kutufanya sisi sote ni wajinga sana hatujui kuchambua mambo eee?? jinga sana wewe acha kuandika kama hujui kujenga hoja ambayo inaweza kuleta hoja yenye tija,,, unataka kutuaminisha uongo wako kwamba ccm ndo wamelipa gharama za viongozi hao wote waliohudhuria birthday ya ccm Singida? jibu ni hakuna tuonyeshe vocha ya masurufu na gharama za kugharamia misafara ya Raisi,Makamu na Wazir Mkuu kama zimelipwa na ccm??, misafara ya polisi mpaka masikini ya watu wamekufa wakilinda na kuongoza msafara wa Raisi Magufuli tunataka utuletee hapa vielelezo vyakuthibitisha malipo ya gharama zote zimegharimiwa na ccm ndo tutakuamini na vimaneno vyako visivyo na ukweli wowote zaidi ya kuingiza ushabiki wa kichama..acheni kudanganya watanzania... ukiamua kuacha kula nyama..acha kabisa kula aina yoyote ya nyama kula mboga za majani tu kama wahindi wajiitao vegeterian hawali nyama kabisa maisha yao yote hivyo Raisi Magufuli hakupaswa kwenda kuhudhuria sherehe hizo angetafuta ofisi yoyote ya ccm ilipo na kwenda na kopo la rangi kupaka rangi jengo hapo tungemuona kweli anadhibiti matumizi ya pesa, pili angewaachia wenye chama washangilie wenyewe na watu wao sisi hatukubali kwenda kwake singida ni moja ya ufujaji wa pesa za umma kupitia mgongo wa ccm..... tuleteeni vocha zinazoonyesha malipo ya misafara yooootetteeeee......
 
Kama ambavyo wachangiaji wengi wameshakwisha sema. Sherehe za ccm (chini ya kikwete) singida jana hazina uhusiano wowote na serikali (chini ya magufuli). Katika hili, magufuli asilaumiwe hata kidogo kwani hana uwezo wala mamlaka ya kuzuia zisifanyike.

Sherehe za Uhuru ni za kitaifa na zinagharamiwa na serikali (kodi zetu) wakati za jana zilikuwa za kichama na zinagharamiwa na chama.

Hongera CCM kwa kutimiza miaka 39. Lakini kauli za vijembe kutoka viongozi wakuu zilizotolewa kwenye sherehe hizo, zinakipaka chama matope na haziendani na madai kwmba ccm ni chama kikongwe na chenye sura ya kitaifa. Kina sura ya kitaifa wakati watu wa taifa hilo hilo wanadhihakiwa na kubaguliwa na chama hicho hicho kwa misingi ya tofauti ya kisiasa? Sura ya kitaifa ipi? Mbona kati ya viongoz waliozungumza hapo hakuna aliyethubutu kukemea na kulaani tukio la bango la kibaguzi tulilolishuhudia huko visiwani? Sura ya kitaifa, ipi? Au wana maana ya sura za watu?
 
Ugumu ni justifucation kuwa hakuna hata Tsh50,000/ ya mlipa kodi ilitumika au justification kuwa kuna angalau Tsh 50,000/- ya mlipa kodi haikutumika ni ngumu kuipata!
 
Ugumu ni justifucation kuwa hakuna hata Tsh50,000/ ya mlipa kodi ilitumika au justification kuwa kuna angalau Tsh 50,000/- ya mlipa kodi haikutumika ni ngumu kuipata!
Kuhusu ugumu hiyo ni sawa kabisa. Lakini pengine watalaam wa utawala na sheria watusaidie hapa; hivi ni safari zipi za kiongozi wa nchi zinazopaswa kulipiwa na kodi na ni zipi atajilipia mwenyewe. Je, akienda kusalimia kwao anajigharamia mwenyewe? Akienda kwenye sherehe za kidini kama juzi waziri mkuu alivyoalikwa KKKT ni gharama ya nani? Je, tumzuie rais kwenda kushiriki shughuli za chama chake?
 
kama ametumia gharama za serikali sio vizuri na inastahili kukemewa ila kama ni za chama sawa tu,tutofautishe mambo ya chama na ya serikali hata mimi naweza acha party yoyote ofisini kwangu nikaenda kusheherekea birthday ya mwanangu
Msafara wa raisi ni full gharama za serikali!
Alipaswa atumie chopa za chama!
Na ni vigumu kutofautisha pesa za umma na za ccm!
Lkn discipline huwa haina mipaka, the same principle ya kubana matumizi serikalini, ilipaswa ku apply kwa chama kwa kuwa wao nao wanatumia ruzuku tu au mapato ya viwanja etc ambavyo kimsingi ni pesa ya umma!
 
Hii ni sawa na kuambiwa ongea tujue uwezo wako wa kufikiri.
Sina nia ya kumdharau mtu yeyote aliyechangia humu,ila napenda kusema kwamba kuna watu ni kama wanapenda utani vile,unamwona mwenzako hajui kitu badala ya kumsaidia akielewe wewe unamsapport ili azidi kutokukielewa zaidi.
 
Back
Top Bottom