Sherehe za Kuzaliwa kwa CCM na Ujenzi wa Maabara za Masomo ya Sayansi Kwenye Sekondari za Musoma Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943

SHEREHE ZA KUZALIWA KWA CCM NA UJENZI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZA MUSOMA VIJIJINI

Sherehe za Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi zinaendelea kufana Musoma Vijijini.

Leo, sherehe hizo zimefanyika Kijijini Bwai Kumsoma, Kata ya Kiriba. Washiriki wa sherehe hizi wametembelea Bwai Sekondari na kushuhudia ukamilishaji wa ujenzi wa Mabara zake tatu za Masomo ya Sayansi (Physics, Chemistry & Biology). Hii ni sekondari ya pili ya Kata ya Kiriba.

Michango ya ujenzi wa Sekondari hii inatolewa na:
*Wananchi wa Kijiji cha Bwai Kumsoma
*Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo
*Serikali Kuu imechangia ujenzi wa Maabara 3 za Masomo ya Sayansi kwa kutoa Tsh Milioni 153.

Sherehe za kufungua rasmi shule hii iliyoanza kutoa elimu ya sekondari mwaka jana itanyika mwezi ujao.

Uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu Musoma Vijijini: Wanavijiji na Mbunge wao wa Jimbo wanashirikiana na Serikali yetu kwenye ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwenye sekondari zote za Jimbo la Musoma Vijijini.

Miaka 47 ya kuzaliwa kwa CCM: CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa - tafadhali pata ushuhuda uliotolewa na wanavijiji na viongozi wao Kijijini Bwai Kumsoma, Kata ya Kiriba.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumapili, 4.2.2024
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-02-05 at 00.09.40.mp4
    31.4 MB
Back
Top Bottom