Unazuia sherehe za Uhuru, unaadhimisha birthday ya CCM

Naona mmeshindwa kujua kwanin mwanzisha thread anatokwa povu pa1 na wote wanaomsupport sio kwamba uwezo wao ni mdogo la hasha ni hivi yeye hajui lini chama chake cha cdm kiliasisiwa ama kuzaliwa ili naye walau angetamani hata kwa siku moja ktk maisha yake wafanye sherehe, mi naona ni muda mzuri kwa yy kumuuliza mtukufu mbowe ni lin waadhimishe ili taifa na media zipambwe na mbwembwe zao,ni hilo tu maana hawana jipya
 
Siku hizi ujinga umegeuzwa kuwa hekima na busara!

Kuna baadhi ya watu hawafahamu kama ni wajinga!

He who knows not and knows not that he knows not is a fool!

Hufahamu hata maana/tofauti ya sherehe za chama na taifa.

Kasome kwanza civics!

Mambo kama haya hata mtu mwenye common sense ambaye halifahamu hata darasa atafahamu tofauti ya sherehe za chama na kitaifa,
sasa povu jingi bila kutoa binafsi,..
mtoa uzi anasemaaaa viongozi weameenda singida kwa kutumia fedha gani????
magari walioenda kule yametumia mafuta gani na gharama gani?????ni serikali
ni viongozi wangapi wametumia magali ya Government?????
wale police waliotumika kuescort wametumia gari gani????na mafuta je?????
jumla ni how much fedha za serikali zilizotumika ktk hiyo sherehe ya majuha????
WAKATI MASHINE ZA WAgonjwa muhimbili wanahamisha kutoka dodoma,...
 
Kwa hiyo mleta mada unashauri Sherehe za Uhuru Zingefanyika kwa sababu chama kimefanya Sherehe. Na hata kama zote zingekuwa halali kufanya moja na nyingine ukawasaidia wananchi tatizo ni nini????? Vyovyote iwavyo kuna unafuu kuliko tulipotoka.
no mkuu,..
labda nikuingilie kidogo mkuu,..
swala ni hivi sherehe za kipuuzi kwanini serikali iingiie gharama kias hikoooo
wakati huduma za afya mbovu,maendeleo hovyo hovyo.,.,.,.,zile za uhuru zilitumika ktk barabara ya moroko
na hizo za viongoz zilizotumika jana zingewekwa ktk maendeleo mengine
 
Nadhani unataka kujifanya kuwa ni mwelewa sana, lakini ww hujui chochote yani ni sawa na debe tupu, Makufuri ndo mwenyeki wa ccm? ccm ina miradi yake na taratibu zake, Magu ni Rais wa nchi na alizuia zile serehe kwani zilikuwa ndani ya uwezo wake, wakati mwingine muwe mnafikiri kwanza kabla ya kukurupuka, haya twambie hizo sherehe zimetumia bei gani hapo Singida? acha mambo ya kukaririshwa mambo!
Me sikushangai wala siwezi kufikiria juu ya uwezo wako wa kufikiri kwa sababu ulichoandika tu kinatoa mwanga ww ni mtu wa aina gani!! Bandiko km hili linahitaji uwezo mkubwa wa kufikiri...! Hapa tunamzungumzia Rais wa nchi ambae aligoma hata kuhudhuria kikao cha wakuu nchi za africa kwa sababu msafala wake ni hasara kwa taifa. Hicho ndo tunachopigia kelele hapa,sherehe za ccm zinahusisha serikali nzima. Me naamini wewe shule ni ndogo lkn hata kuelewa kwamba ccm hawawezi kuwagharamia hao viongozi nalo mpaka uwe umesoma!!?? Ni kweli sherehe ni za ccm hakuna anayekataa. Labda lingine kwa kukusaidia Rais anayetokana na ccm ni mjumbe wa kamati kuu kutokana cheo chake. Kauli zenu kwamba Rais anakaribishwa nadhani ni kwa sababu hamjui. Ndo maana sisi wengine tunahoji km kweli dhamira ya kubana matumizi ipo! Kumbuka watumishi wote wa umma hawaruhusiwi kusafiri kwenda nje ya nchi bila kutoka ikulu hata km wanatumia fedha zao.

Kumbuka pia Rais alizuia sherehe za wabunge na kuna pesa zilitangazwa zimeokolewa,bunge ni mhimili unaojitegemea kwa mujibu wa katiba na hizo pesa hazikuwa za serikali. Tulitaka tuone akishawishi hata ndani ya chama chake kubana matumizi...! Rais ni mkuu wa nchi anaushawishi mkubwa kuliko hata huyo m/kiti ndani ya ccm..
 
Sidhani kma kuna kosa la ccm kufanya sherehe ya chama chao hivyo mleta mada liangalie kwa jicho la tatu coz hiyo ni isue ya chama na si ya kitaifa na mh raisi si mwenyekiti wa chama hivyo awezi kuzuia sherehe hiyo tumsubiri atakavyokuwa mwenyekiti kama na uko atabana matumiz ya chama chake au la
 
Naona mmeshindwa kujua kwanin mwanzisha thread anatokwa povu pa1 na wote wanaomsupport sio kwamba uwezo wao ni mdogo la hasha ni hivi yeye hajui lini chama chake cha cdm kiliasisiwa ama kuzaliwa ili naye walau angetamani hata kwa siku moja ktk maisha yake wafanye sherehe, mi naona ni muda mzuri kwa yy kumuuliza mtukufu mbowe ni lin waadhimishe ili taifa na media zipambwe na mbwembwe zao,ni hilo tu maana hawana jipya
Mkuu umemaliza
 
Wanabodi
Salaam;

Serikali ya awamu ya 5 inajinasibu kubana matumizi na kufuta baadhi ya sherehe za kitaifa kwa lengo hilo la kuzuia matumizi yasiyo ya lazima.

Kichekesho kimeonekana leo baada ya serikali nzima kuhamia Singinda kwenye sherehe za birthday ya CCM ya kutimiza miaka 39.

Huko nyuma tulishuhudia sherehe za uhuru zikipigwa kumbo, sherehe za wabunge zikapigwa ban, baadae TBC nayo ikapigwa ban kwa lengo hilo hilo la kubana matumizi. Cha kushangaza Rais na serikali nzima walikuwa kwenye birthday hiyo ya CCM kwa ajili ya kutoa hotuba za mipasho!!

Kweli hii nchi ngumu sana aisee!
"CCM Baba aliotuzaa wana Tanzania...." nyimbo maarufu ya makada wa CCM.... JPM hana ubavu nacho na pesa si za serikali
 
You mean unasema kuwa chadema, ACT, Nccr, Tadea, Chaumma wakitaka kufanya sherehe zao magufuli aingilie??

Sherehe za CCM sio za kitaifa, sherehe ya uhuru ni ya kitaifa

sherehe ya ccm ni ya kichama, ya uhuru ni ya serikali

acha upuuzi
Ana matatizo huyo
 
Poleni sana kwa kazi nzito ya kuwaelimisha hawa watoto---hawa watoto msiwachoke akili zao bado ndogo hawana uwezo wa kuchambua mambo wanahitaji kusaidiwa.
 
Sidhani kama tupo sawa kwenye jambo husika,tofautisha mimi na wewe,hilo gari ni mali ya umma na kwa kuwa tumeridhia kufuata mfumo wa siasa wa vyama vingi na huyo rais anajipambanua kuwa ni msafi na mchukia ufisadi ilibidi atumie gari lake binfsi

Unachoshindwa kuelewa Maguruli ni Rais hana madaraka yoyote ndani ya chama, amealikwa kwenye sherehe za CCM kama Rais. Akaeleze nini serikali inafanya katika utekelezaji wa Ilani ya CCM, sasa isijui ulitaka Rais afikaje kwenye shughuli hiyo. Angalikuwa amealikwa kama Mwenyekiti wa Chama ungalikuwa na sababu ya kuchupalia jambo hili, lakini kwa sasa hana cheo chochote ndani ya chama ni kiongozi wa serikali
 
Wakati mwingine ni vyema ukafikiri na kutafakari kwa makini kitu unachotaka kuandika kabla kuandika. Rais amefuta sherehe ya Uhuru ambayo ni sherehe ya kitaifa kwa lengo la kubana matumizi ili fedha hizo zilizotengwa kwa ajili ya sherehe ziweze kutumika katika shughuli nyingine za msingi za kujenga Taifa letu.

Lakini hajafuta sherehe za CCM na wala hawezi kuzifuta kwa sababu kwanza sio sherehe za kitaifa, pili fedha zinazotumika kufanya sherehe hizo hazitoki serikalini bali zinatoka kwenye mfuko wa chama na tatu yeye sio kiongozi wa chama hicho hivyo hana mamlaka ya kuzuia sherehe za chama hicho.
Sawa, you have point lakini hamuoni ingekuwa ni busara kuonesha kwamba wapo serious kwa suala la kubana matumizi hata ndani ya chama? Ikiwa Magufuli aliamrisha michango ya watu binafsi ipelekwe Muhimbili what about pesa za CCM kwanini zisingepelekwa sehemu sawa na Muhimbili? Hivi pesa ya wafanyabiashara binafsi na pesa ya CCM ni ipi hasa ilitakiwa kuwa diverted to public interest? CCM wana mashule wanayomaliki kwa jina la shule za wazazi na ni moja ya shule ambazo ni wazalishaji wazuri wa division 5 hapa nchini! Sasa kwanini hizo pesa wasingeelekeza kwenye uboreshaji wa shule zao kwa maslahi mapana ya taifa? Ikiwa shule zao ni bora zaidi kwanini wasingetumia hizo pesa kujenga shule zingine bora zaidi? Kwanini hizo pesa wasingetumia kununua stationary na kusambaza kwenye wenyeviti watendaji wao waliojaa kila kona ya nchi ili biashara ya kuchomoa buku buku toka kwa wanaotaka barua za utambulisho ikome?
 
Wanabodi
Salaam;

Serikali ya awamu ya 5 inajinasibu kubana matumizi na kufuta baadhi ya sherehe za kitaifa kwa lengo hilo la kuzuia matumizi yasiyo ya lazima.

Kichekesho kimeonekana leo baada ya serikali nzima kuhamia Singinda kwenye sherehe za birthday ya CCM ya kutimiza miaka 39.

Huko nyuma tulishuhudia sherehe za uhuru zikipigwa kumbo, sherehe za wabunge zikapigwa ban, baadae TBC nayo ikapigwa ban kwa lengo hilo hilo la kubana matumizi. Cha kushangaza Rais na serikali nzima walikuwa kwenye birthday hiyo ya CCM kwa ajili ya kutoa hotuba za mipasho!!

Kweli hii nchi ngumu sana aisee!
Hivi kweli inahitaji elimu ya darasa la saba kutambua kwamba hiki ulicho andika ni pumba?? Au tunahitaji mfumo tofauti wa watu kama wewe!
 
Humu ndani viwango vya uelewa tunaziadiana kwa lengo moja tu kulinda masilahi fulani. Lakini niseme kitu kimoja Kama mchango wangu kwa watanzania, Ccm ndicho chama dola, kilipoamua kupunguza matumizi ya serikali kwa kuzuia sherehe za kitaifa (Uhuru) tulipongeza sana. Kwa mantiki hiyohiyo ccm Kama chama dola kilipaswa kutangaza mojakwa moja kwamba mwaka huu hakutakuwa na sherehe za kuzaliwa kwa chama badala yake pesa zote zilizotengwa zipelekwe serikalini ili kumsaidia rais Dr .JPM kupunguza deni la walimu na elimu bure izidi kunoga kwa kuwawezesha walimu.

Huwezi kutenganisha chama cha Mapinduzi na serikali ni kujidanganya! Tofauti ya serikali ni kwamba Magufuri na Majaliwa hawavai ile sare ya kijani tu, lakini ndani yao ile sare ya kijani inakuwa imevaliwa kwa ndani ila kwa macho ya nyama ya uso wako huwezi kuona ila wao wanaona hiyo sare. Hivyo kubeza bandiko la mleta mada eti sherehe za chama ni tofauti na zile za serikali katika kujenga uchumi na kutumbua majipu ni kulidanganya taifa mchana kweupe. Kwa maana hiyo basi nashauri chama kiendani na kasi ya rais katika kurudisha heshima iliyopotea kwa muda mrefu kwa taifa letu. Pesa walizotumia Ccm kwenye sherehe zao ni pesa za walipa kodi!
 
You mean unasema kuwa chadema, ACT, Nccr, Tadea, Chaumma wakitaka kufanya sherehe zao magufuli aingilie??

Sherehe za CCM sio za kitaifa, sherehe ya uhuru ni ya kitaifa

sherehe ya ccm ni ya kichama, ya uhuru ni ya serikali

acha upuuzi

Sa kwani hizo si ni pesa za chama chao ama?

Tatizo kuu la Nchi yetu kwa sasa ni upeo mdogo wa Watu wetu kama huyu mleta mada! Mtu mzima hataki kushughulisha akili (kama anayo)! CHADEMA na hii "Mizwazwa" ni mzigo kwa Taifa! Mtu hajui hata tofauti kati ya shughuli za Chama na Serikali! Mwisho itasema Rais Magufuli kazuia harusi za watu binafsi ili kubana matumizi ya Serikali! Haya ndo huandaa maandamano kwenda Ikulu kwa Rais ili kuona TV live! Michovu kila mahali!

Siku hizi ujinga umegeuzwa kuwa hekima na busara!

Kuna baadhi ya watu hawafahamu kama ni wajinga!

He who knows not and knows not that he knows not is a fool!

Hufahamu hata maana/tofauti ya sherehe za chama na taifa.

Kasome kwanza civics!

Mambo kama haya hata mtu mwenye common sense ambaye halifahamu hata darasa atafahamu tofauti ya sherehe za chama na kitaifa,
Nyie mkiangalia ccm walivyo wapumbavu wanaweza kutoa ela zao mfukoni na kugharamia sherehe zao?
 
Tangu jana kikwete aliposema vijana wa mtandaoni serikali iwafikirie,naona mko busy kutetea kila upuuzi! Me naweza kuwa sina ushahidi wa takwimu lkn ushahidi wa mazingira upo wazi. Rais alienda na msafara na magari ya umma,waziri mkuu,mawaziri,wakuu wa mikoa na wilaya. Hawa wote walitumia kodi zetu. Ambacho niliona kwa macho ni cha ccm,ni mashati tu ya kijani. Acheni kujitoa ufahamu!

"One man's meat is another man's poison"
 
You mean unasema kuwa chadema, ACT, Nccr, Tadea, Chaumma wakitaka kufanya sherehe zao magufuli aingilie??

Sherehe za CCM sio za kitaifa, sherehe ya uhuru ni ya kitaifa

sherehe ya ccm ni ya kichama, ya uhuru ni ya serikali

acha upuuzi
Ofcourse hata pesa inayotumika ni ya chama si serikali ila kuna ukakasi kimtindo
 
Hawa jamaa kuna wakati nawaona UKAWA inawatesa sana kwenye akili zao. Yaani wasipotafuta sababu za kuiongelea UKAWA au CHADEMA wanakuwa hawana furaha kabisa! Wanaacha kuongea mambo ya maana yanayohusu mipango na maendeleo ya nchi, wanakalia mipasho ya ukawa/CDM au Lowassa tu. Nashangaa sana. Chama kiko madarakani kwa zaidi ya miaka 40, kwa nini kinaendelea kuwa na kiwewe na na chama cha upinzani ambacho (kwa mujibu wao), siyo popular kwa wananchi?
 
Sawa, you have point lakini hamuoni ingekuwa ni busara kuonesha kwamba wapo serious kwa suala la kubana matumizi hata ndani ya chama? Ikiwa Magufuli aliamrisha michango ya watu binafsi ipelekwe Muhimbili what about pesa za CCM kwanini zisingepelekwa sehemu sawa na Muhimbili? Hivi pesa ya wafanyabiashara binafsi na pesa ya CCM ni ipi hasa ilitakiwa kuwa diverted to public interest? CCM wana mashule wanayomaliki kwa jina la shule za wazazi na ni moja ya shule ambazo ni wazalishaji wazuri wa division 5 hapa nchini! Sasa kwanini hizo pesa wasingeelekeza kwenye uboreshaji wa shule zao kwa maslahi mapana ya taifa? Ikiwa shule zao ni bora zaidi kwanini wasingetumia hizo pesa kujenga shule zingine bora zaidi? Kwanini hizo pesa wasingetumia kununua stationary na kusambaza kwenye wenyeviti watendaji wao waliojaa kila kona ya nchi ili biashara ya kuchomoa buku buku toka kwa wanaotaka barua za utambulisho ikome?

Wazo la kubana matumizi ni la Magufuli na sio CCM na wala halipo katika ilani ya CCM na ndio maana CCM hawabani matumizi. Labda hilo litawezekana endapo Magufuli atachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM lakini sio vinginevyo.
 
Back
Top Bottom