Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 121,947
- 95,237
Mkuu huo ni usanii kama kina jotiNi utaratibu usio sawa. Lakini umehalalishwa na serikali za CCM. Magari ya serikali kutumika katika shughuli binafsi haswa kwa viongozi waandamizi (mawaziri, wakuu wa wilaya na mkoa, DEDs, DASs, RASs, makatibu wakuu, wakurugenzi, makamishina, majaji n.k) ni matumizi mabaya ya mali za umma.
Siwezi kuongelea juu ya viongozi wakuu wa dola: Rais, Spika, Jaji Mkuu na Waziri Mkuu. Hawa wanastahili hiyo 'favour' ingawa ni vyema nao kuongozwa na sheria za namna ya kutumia mali za umma kwa mambo binafsi. Hapa mambo binafsi hayuhusiana na wao kuhudhuria sherehe za chama. Hili si sawa. Lakini wengine wote hawastahili kutumia mali za umma kwa matumizi binafsi.
Watu wa CCM uwa wanapenda sana kutoa mifano ya nchi zingine pale wanapohalalisha jambo lililo upande wao. Lakini ung'aka pale watu wanapotoa mifano ya nchi zingine kwa mambo wasiyoyataka. Utawasikia, "kila nchi inaamua mambo yake". Kwenye hili la matumizi ya mali za umma, serikali ya CCM ijifunze kwa nchi nyingine kama, Uingereza, Uswisi na nchi za Scandanavia.
NB: si Magufuli alisema ataachana na 'mashangingi'? Mbona bado yanatawala fleet ya serikali?!